Sakata la Fei toto likiisha itachukua muda Fei kurudi kwenye kiwango chake

HOPEfull

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2021
Posts
1,882
Reaction score
2,313
Salamu humu.

Michuano ya kimataifa inayoendelea sasa hivi kwa Simba na Yanga ambayo inaangaliwa na afrika nzima ilikuwa ni sehemu muhimu Sana kwa dogo Fei kuonyesha dunia kiwango chake na kujipima yeye mwenyewe je anaweza kwenda kucheza kimataifa au abaki humu matopeni.

Sijajua alikuwa na haraka gani kwa nn hakusubiri mkataba wake uishe ndio alizue Jambo.

Sasa ona muda aliokaa benchi ni lazima kiwango kitachuja kwa sababu mwili unaathirika kiakili na kisaikolojia hakuna mazoezi huna mechi unayocheza hata Kama kila siku utaenda beach kujifua ni lazima upate dimba la kukutana na wenzako.

Kama Mungu akimjalia kurudi katika kiwango chake basi liwe ni fundisho.Sikuona haja ya Fei kutoka Yanga na kutafuta tena kucheza humu humu ndani.

Ilitakiwa awe na mahesabu ya kwenda mbele zaidi ya hapa kwa kiwango chake na akumbuke kuwa unapoona kiwango chako kinakua kuna wenzako wanakuwezesha sio kwamba unacheza peke yako ni muhimu kuwaheshimu.

Sasa bahati mbaya ndio hiyo michuano ya kimataifa ameikosa kwa time yake ya Yanga kutokana na haraka yake au kutokupata ushauri mzuri.

Pamoja na pesa lkn Kuna haja ya kutulia katika kufanya maamuzi kwa mustakabali wa maisha ya baadae.
 
Fei alikua na uhakika wa mechi sita za confederation ambazo Kwa kiwango alicho kua amefikia upo uwezekano wa kupata timu ndani au nje ya Africa, kwakua Yanga imefika robo alikua ameongeza platform ya mechi mbili.
Tukisema Hana bahati sikweli ila watu wame mrubuni na kumharibia kabisa.

Kwasasa hayupo sawa kisaikolojia ni Bora alivyoitwa Timu ya Taifa angalau Kwa izo siku chache itampunguzia Msongo wa mawazo na kupata usingizi kwakua anacheza na marafikizake atapata furaha Kwa muda na kichwa chake kupumua.

Ata yuda alipo kamilisha zoezi la kumsaliti Yesu, Alipata fedha nyingi sana Kwa wakati uo lakini baadae aligumdua amekosa furaha na Amani na mwishowe alijinyonga Kwa kujiona yeye si kitu na amekosea sana.
 
Sidhani kama Fei alijichukulia maamuzi,wanaomrubuni yule kijana nafikiri ndo wanaharibu career yake,hata ile kauri ya kwamba Fei hana tena mapenzi na Yanga ni kumfunga ili hata ikitokea akahitaji kurudi Yanga basi shabiki wasiwe na imani Naye tena..katika maisha chunga sana watu unaowaweka pembeni na kuwaita washauri
 
Mbona msuva alikaa mda mrefu bila kucheza lakini ilikuwa anakiwasha yanga acheni roho mbaya mwacheni dogo akatafute riziki sehemu nyingine.
 
Timu ya taifa nayo ni shida tu yaani mtu unaweza ukafikiri umelogwa.
 
Salamu humu.

Michuano ya kimataifa inayoendelea sasa hivi kwa Simba na Yanga ambayo inaangaliwa na afrika nzima ilikuwa ni sehemu muhimu Sana kwa dogo Fei kuonyesha dunia kiwango chake na kujipima yeye mwenyewe je anaweza kwenda kucheza kimataifa au abaki humu matopeni.

Sijajua alikuwa na haraka gani kwa nn hakusubiri mkataba wake uishe ndio alizue Jambo.

Sasa ona muda aliokaa benchi ni lazima kiwango kitachuja kwa sababu mwili unaathirika kiakili na kisaikolojia hakuna mazoezi huna mechi unayocheza hata Kama kila siku utaenda beach kujifua ni lazima upate dimba la kukutana na wenzako.

Kama Mungu akimjalia kurudi katika kiwango chake basi liwe ni fundisho.Sikuona haja ya Fei kutoka Yanga na kutafuta tena kucheza humu humu ndani.

Ilitakiwa awe na mahesabu ya kwenda mbele zaidi ya hapa kwa kiwango chake na akumbuke kuwa unapoona kiwango chako kinakua kuna wenzako wanakuwezesha sio kwamba unacheza peke yako ni muhimu kuwaheshimu.

Sasa bahati mbaya ndio hiyo michuano ya kimataifa ameikosa kwa time yake ya Yanga kutokana na haraka yake au kutokupata ushauri mzuri.

Pamoja na pesa lkn Kuna haja ya kutulia katika kufanya maamuzi kwa mustakabali wa maisha ya baadae.
sidhani kama atarudi kabisa
 
Huyu dogo sijui kwa nini wanapenda kumnyanyasa 🤣😂🤣 Mimi nilimshauri asiende kule ona sasa.

20230323_202201.jpg
 
Back
Top Bottom