Sakata la Fei Toto

hometown

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2016
Posts
939
Reaction score
1,311
Anaandika Wakili Msomi simon.esq, Mkurugenzi wa sheria wa Yanga Sc

_____________

Kwa ridhaa ya timu ya Yanga (klabu ya Wananchi) napenda kuongelea kwa mara ya mwisho sakata la mdogo wetu Feisal Salum na kilichotokea jana.

Mdogo wetu kwa mara nyingine tena aliandika barua ya kutaka kuvunja mkataba na klabu ya Yanga na akaipeleka TFF akiwataka wao ndio wavunje mkataba.

Sisi kama klabu tuliitwa TFF na Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji, ambacho ni chombo chenye hadhi ya kimahakama. Yanga tuliweka mapingamizi manne kuhusu maombi ya Feisal;

1. Shauri linalohusu uvunjifu wa mkataba “Contract termination“ lilishasikilizwa na kutolewa maamuzi na kamati kwenye maamuzi ya kwanza na maamuzi ya rejea (review). Hivyo kamati ileile haiwezi kusikiliza shauri lilelile na kwa muktadha uleule (Res judicata).

2. Kwakuwa suala hili limeshasikilizwa na kutolewa maamuzi hapo awali, hivyo mikono ya kamati imeshafungwa na sheria (Functus officio).

3. Kwa kuwa kisheria mikono ya kamati imeshafungwa, hivyo basi Kamati haina tena mamlaka (Jurisdiction) ya kusikiliza suala hili. (The committee lacks any power to re-examine decision).

4. Mkataba unaotaka kuvunjwa ni kati ya Yanga na Feisal, hivyo basi wao ndio wenye uwezo wa kuuvunja, na sio TFF kwa sababu TFF sio wahusika wa mkataba huo. Kisheria inaitwa "Privity of Contract" yani huwezi kuvunja mkataba ambao wewe sio sehemu yake.

Hivyo basi TFF hawana mamlaka yoyote kisheria kuvunja mkataba wakati wahusika wa mkataba, hawajakaa kwa ajili ya kuvunja mkataba wakashindwana.

Hoja hujibiwa kwa hoja (argumentum per argumentum). Mambo ya sijui mimi namwakilisha Drogba hayatuhusu. Hata kama ungekuwa unamwakilisha Messi na Ronaldo, dakika 10 ni nyingi sana kujibu hoja.

Mwisho; Feisal ni mdogo wetu na ni ndugu yetu. Anakaribishwa muda wowote kuja Yanga kuleta maombi ya kuvunja mkataba na atapewa baraka zote na klabu. Na huu ndio msimamo rasmi wa Yanga.

Jumaa Mubarak [emoji1545]
Simon.esq
Mkurugenzi wa Sheria - Yanga Sc
 
Aisee, kwa hiyo alipewa ridhaa na klabu atoe mipasho hiyo!
 
Aende sasa akakae na timu yake avunje mkataba. Siyo aendelee kujificha kama digidigi. Aachane pia na hao wapuuzi wake wanaompotezea muda na fedha zake.

Mambo ya kusema mimi ni wakili wa Drogba! Sijui nilisimamia mkataba wa Emmanuel Eboue, Simon Msuva, nk. Unaihusu nini klabu ya Yanga na mchezaji wake?
 
Dogo Fei kashikwa pabaya hafurukuti,kadri anavyojitikisa ndivyo anavyojibana na kujiumiza zaidi.

Namshauri arudi tu Yanga aombe msamaha awaombe radhi viongozi na wachezaji wenzake na mashabiki kuwa amekosea basi arudi klabuni maisha mengine yaendeee.

Kuendelea kutunishiana misuli na Yanga ambao kwa sasa wapo vizuri kila idara ni kuendelea kupoteza muda wake bure pasi na sababu zozote za msingi.

Werevu husema kufanya jambo hilo hilo kwa njia hiyo hiyo ukitegemea kupata majibu tofauti ni utaahira.abadilishe njia za namna ya kudai anazoita haki zake.Muda haumsubiri mtu mana Yanga inaonekana wanataka tu kumkomoa mana hawana kazi nae tena.
 

Sikuwahi kufikiri Fatuma ana akili ndogo kwa kiwangi hiki, analeta hisia za Huruma kwenye mambo ya sheria? Mbona hii iko clear sana?
 
Hatimae Wakili kapata pakupanulia domo lake, baada ya kugalagazwa sana kisheria kwa kesi rukuki hapo Yanga,,.

Anapata jeuri hiyo baada ya Tff kupokea maelekezo ya wanasiasa kwamba fei aminywe mpaka atoke damu.. Baada ya wanasiasa,viongozi wa hapo klabun kumpigia magoti Fei arudi klabun na kugoma wameona wamkomoe,.

Nachoamini Feisal atacheza mpira msimu ujao, na hatoichezea Yanga, sheria zipo zinawalinda wachezaji

Ma Tycon wa Sheria za soka tunaingia Front Sasa subilini kifinyo huko mbele
 
Mdogo wetu Feisal anaua kipaji yake
 
Hoja mufilisi.
 
Jinga lingine hili.... Huko mbele wapi?, Nenda kamsaidie saizi. Mnaleta utahira kwenye Mambo ya sheria pumbavu kabisa.
 
Subilini ndio nini?
Huna uanasheria wowote wala uzee wa baraza
 
Mwanasheria hujui kutofautisha kati ya R na L utashinda kesi gani?
 
Mwanasheria wa yanga bhana kidogo kwenye hii kesi anaonyesha kauhai na ni kwa sababu hii kesi inachezwa na upande mmoja....... la sivyo huyo ni hamnazo kabisa... rejea kesi za akina morisoni, okwi....
 
Kwa nn asiende CAS kila siku anarudi tff
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…