PreGE2025 Sakata la Gongo latikisa bungeni, Mbunge ahoji Serikali kusambaza mitambo yakutengenezea

PreGE2025 Sakata la Gongo latikisa bungeni, Mbunge ahoji Serikali kusambaza mitambo yakutengenezea

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Bungeni leo Aprili 14, 2025, Mbunge wa Momba (CCM), Condester Sichalwe amehoji kuhusu hatua za Serikali kudhibiti pombe kali zinazoingizwa nchini ambazo kwa kiasi kikubwa zinachangia kuharibu afya na maadili ya vijana.

Sichalwe amesema:

"Kuna pombe nyingi sana zinaingizwa ambazo ni kali na zinaendelea kuharibu vijana na nguvu kazi ya Taifa. Vijana wengi wanaendelea kuharibikiwa kwa kunywa hizo pombe kali. Je, ikiwa hizo pombe kali zinaweza kuingizwa zikiwa zimetengenezwa kutoka nchi nyingine, kwa nini Serikali ishindwe kuwafundisha wananchi wetu kutengeneza pombe kama gongo kwa usalama zaidi, kwani gongo bado inatumika na inapendwa?"

Ametaka Serikali kutafuta njia mbadala ya kusaidia wananchi wa kawaida walioko vijijini kwa kuwapa maarifa ya uzalishaji salama, kama hatua ya kudhibiti madhara yanayosababishwa na pombe zisizosimamiwa vizuri.




 
Karine ya 21 bado Bunge wana discus ujinga
Bac acha ujinga na upuuzi. Punguza ujuaji na lugha za kujidhalilisha.

Hizo pombe zote unazo ziona kokote duniani ni aina fulani ya gongo.

Gongo ni nini?

Unapiga rungu Neno?
 
Back
Top Bottom