Sakata la Interview za Air Tanzania leo tarehe 31 January 2026

Damaso

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
6,236
Reaction score
10,774
Kama kuna siku vijana wamejisikia kama wako kwenye onyesho la futuhi—lakini lisilo na kicheko chochote—basi ni siku ya usahili wa ajira wa Air Tanzania leo pale DUCE. Kilichotarajiwa kuwa zoezi la kitaalamu, la haki na la kutoa matumaini, kimegeuka kuwa kilio chenye maswali mengi kuliko majibu, na dhihaka nyingi kuliko haki.
images - 2026-01-31T160442.078.jpeg

Hebu tuanze na hoja ya kwanza: sifa. Inadaiwa kuwa mhitimu wa Bachelor of Science in Accountancy and Finance hana sifa za kufanya mtihani wa kada ya Accountancy upo hapo?
tz-graduate.webp

Kwa mantiki hiyo hiyo, mhitimu wa Bachelor of Computer Science anaambiwa hana uhusiano wowote na Information Technology. Kwa maneno mengine, Computer Science haina uhusiano wowote na “computer” wala “technology”. Hapa mtu anaweza kujiuliza: je, waliopanga zoezi hili walitazama mitaala au walitupa tu karata mezani? Kama wanabet?
images - 2026-01-31T160541.678.jpeg

Kama hilo halitoshi, kuna vijana waliorejeshwa nyumbani kwa sababu kitambulisho cha Mpiga Kura hakifanani kwa asilimia 100 na Kitambulisho cha Taifa, licha ya majina ya vyeti na NIDA kuwa yale yale.
images - 2026-01-31T160609.652.jpeg

Inaonekana hapa si ajira, ni shindano la “Tafuta tofauti tano kwenye picha”. Ukikosea, rudi nyumbani—hata kama umetoka Tunduma, Mtwara au Mwanza.
images - 2026-01-31T160619.714.jpeg

Na ndipo tunafika kwenye safari za mateso. Vijana wametoka Iringa, Mbeya, Mwanza, Mtwara—wengine kwa nauli ya kukopa, wengine kwa kuuza ndizi au simu.
images - 2026-01-31T160629.048.jpeg

Wanapowasili Dar es Salaam, wanakaa kwenye foleni ndefu, halafu wanapewa majibu mepesi kama SMS ya salio: “Huna sifa”, yaani unapewa taarifa kirahisi kabsa. Hapo hakuna hata “samahani kwa usumbufu”, wala maji ya kunywa. Ni kama umefika airport, ukaambiwa ndege imeondoka jana asubuhi.
tz-graduate.webp

Cha kushangaza zaidi ni mazingira ya usalama. Vijana wakianza kuuliza maswali ya msingi, ghafla polisi wanaonekana kusogea na kufoka utadhani vijana wanataka kuandamana. Swali linabaki: je, usahili huu ulikuwa dhidi ya majambazi au wahitimu wa vyuo vikuu? Kwani tangu lini kuuliza haki yako imekuwa tishio la usalama wa taifa? Serious
images - 2026-01-31T160442.078.jpeg

Kuna kipengele kingine kinachotia shaka: idadi ya waombaji. Kuna kada zinahitaji mtu mmoja, lakini wanaoingia kwenye mtihani ni zaidi ya 100. Hapa mtu anaweza kudhani labda wanatafuta mtu wa ziada wa kushika foleni. Au pengine shughuli ilikuwa kama sherehe ya harusi—watu wengi, lakini bwana harusi ni mmoja na mke mmoja.
 
Kama hilo halitoshi, kuna vijana waliorejeshwa nyumbani kwa sababu kitambulisho cha Mpiga Kura hakifanani kwa asilimia 100 na Kitambulisho cha Taifa, licha ya majina ya vyeti na NIDA kuwa yale yale.
Hapa panahitaji ufafanuzi tangazo likiwataka waende na vitambuli vyote viwili NIDA na cha Kura?? (Hapa kuna mashaka) Ila kama kuna tofauti za majina kati ya NIDA na Cheti chochote Hapa hakuna wakumlaumu ni kawaida na imewakuta wengi.

Cha kushangaza zaidi ni mazingira ya usalama. Vijana wakianza kuuliza maswali ya msingi, ghafla polisi wanaonekana kusogea
Kwenye hizi saili Polisi na TISS hua wapo kwa ajili ya usalama.... So kwa viashiria vyovyote lazima wasogee mana mwisho wa siku wataandika report ikiwemo za matukio swali ni Je.. maswali gani ya msingi unayaongelea hapa?? Tupe mfano wa swali na je mazingira ya kuuliza hayo maswali yalikuaje? Mlikusanywa mkaambiwa muulize, mlianza kuropoka mkiwa mnauliza??? Fafanua hapa.
idadi ya waombaji. Kuna kada zinahitaji mtu mmoja, lakini wanaoingia kwenye mtihani ni zaidi ya 100. Hapa mtu anaweza kudhani labda wanatafuta mtu wa ziada wa kushika foleni.
Kaka inaweza kuwa ni usaili wako wa kwanza na hoja hii inaonesha kabisa mihemko ya kuiona mitandao kama suluhu ya mambo yote. Ivi saili za walimu na madaktari ushawahi kuziona?? Za TRA VIP Ulishawahi kuzifuatilia??? Hii hoja haina msingi kwenye ushindani wa ajira.

Nb. Umezalisha hoja zisizo na ushahidi na zenye mashaka juu ya ukweli wake. Hoja zako zinaibua zaidi maswali kuliko majibu. Next time jiandae. Kagua vyeti, hakikisha una kitambulisho na soma tangazo na ulielewe. Kuna ajira zinataka elimu ya kada fulani tu na sio zinazofanana na hizo. (Other related)
 
Tz kila kitu ni connection, undugunaizesheni na kujuana... hizo nafasi tayari zina watu...

Mmeitwa tu kutimiza takwa la kisheria kwamba kulikuwa na uwazi !

Haya piga simu nyumbani wauze ng'ombe uweze kurudi ! sio kwa matani, inauma sana lakini hakuna namna! Ndipo tulipofikia !

Tushike jembe tukalime mwanetu
 
Ndugu,

Tafadhali rejea tangazo letu la kazi ya Afisa Rasilimali Watu Daraja la II (Human Resource Officer II) lililotolewa tarehe 30 Desemba, 2025 pamoja na barua yako ya maombi ya kazi uliyoiwasilisha.

Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) inapenda kukualika kwenye usaili wa Kuandika(written interview) ambao umepangwa kufanyika siku ya Jumamosi ya tarehe 31 Januari,2026 katika Dar es Salaam University College of Education (DUCE) Dar es salaam kuanzia saa moja na nusu asubuhi (07:30 AM) utakao tanguliwa na usajili wa kila mtahiniwa pamoja na ukaguzi wa vyeti. Aidha, unatakiwa kufika ukiwa na vitu vifuatavyo;

Kitambulisho cha Taifa (NIDA) au Kitambulisho cha Mpiga Kura au Passport ya Kusafiria;
Cheti Halisi cha Kuzaliwa;
Vyeti vyote (halisi) vya taaluma vinavyohusiana na nafasi uliyoomba kwa mujibu wa sifa zilizobainishwa kwenye tangazo. Cheti cha Sekondari (Kidato cha nne au/na Kidato cha Sita) na cheti cha shahada ni lazima."
Mtahiniwa atakayechelewa kufika kwenye eneo la kufanyia usaili baada ya muda uliotajwa hataruhusiwa kushiriki.

Ninakutakia uzingatiaji mwema.
 
Tuwe wakweli kipindi cha Magufuli mtu wa nje ya taasisi walikuwa wanaheshimika na kuogopewa sana. Kwa sasa nchi iko Autopilot
 
Hivi watu waliopo ofisini huwa hawawazi ata n kwa namna Gani vijana wanahumia mpaka anafikia hyo hatua ya kufika eneo la usaili?
 
Kama kuna siku vijana wamejisikia kama wako kwenye onyesho la futuhi—lakini lisilo na kicheko chochote—basi ni siku ya usahili wa ajira wa Air Tanzania leo pale DUCE. Kilichotarajiwa kuwa zoezi la kitaalamu, la haki na la kutoa matumaini, kimegeuka kuwa kilio chenye maswali mengi kuliko majibu, na dhihaka nyingi kuliko haki.
View attachment 3537001
Hebu tuanze na hoja ya kwanza: sifa. Inadaiwa kuwa mhitimu wa Bachelor of Science in Accountancy and Finance hana sifa za kufanya mtihani wa kada ya Accountancy upo hapo?
View attachment 3537002
Kwa mantiki hiyo hiyo, mhitimu wa Bachelor of Computer Science anaambiwa hana uhusiano wowote na Information Technology. Kwa maneno mengine, Computer Science haina uhusiano wowote na “computer” wala “technology”. Hapa mtu anaweza kujiuliza: je, waliopanga zoezi hili walitazama mitaala au walitupa tu karata mezani? Kama wanabet?
View attachment 3537003
Kama hilo halitoshi, kuna vijana waliorejeshwa nyumbani kwa sababu kitambulisho cha Mpiga Kura hakifanani kwa asilimia 100 na Kitambulisho cha Taifa, licha ya majina ya vyeti na NIDA kuwa yale yale.
View attachment 3537004
Inaonekana hapa si ajira, ni shindano la “Tafuta tofauti tano kwenye picha”. Ukikosea, rudi nyumbani—hata kama umetoka Tunduma, Mtwara au Mwanza.
View attachment 3537005
Na ndipo tunafika kwenye safari za mateso. Vijana wametoka Iringa, Mbeya, Mwanza, Mtwara—wengine kwa nauli ya kukopa, wengine kwa kuuza ndizi au simu.
View attachment 3537006
Wanapowasili Dar es Salaam, wanakaa kwenye foleni ndefu, halafu wanapewa majibu mepesi kama SMS ya salio: “Huna sifa”, yaani unapewa taarifa kirahisi kabsa. Hapo hakuna hata “samahani kwa usumbufu”, wala maji ya kunywa. Ni kama umefika airport, ukaambiwa ndege imeondoka jana asubuhi.
View attachment 3537002
Cha kushangaza zaidi ni mazingira ya usalama. Vijana wakianza kuuliza maswali ya msingi, ghafla polisi wanaonekana kusogea na kufoka utadhani vijana wanataka kuandamana. Swali linabaki: je, usahili huu ulikuwa dhidi ya majambazi au wahitimu wa vyuo vikuu? Kwani tangu lini kuuliza haki yako imekuwa tishio la usalama wa taifa? Serious
View attachment 3537001
Kuna kipengele kingine kinachotia shaka: idadi ya waombaji. Kuna kada zinahitaji mtu mmoja, lakini wanaoingia kwenye mtihani ni zaidi ya 100. Hapa mtu anaweza kudhani labda wanatafuta mtu wa ziada wa kushika foleni. Au pengine shughuli ilikuwa kama sherehe ya harusi—watu wengi, lakini bwana harusi ni mmoja na mke mmoja.
Ndio Nchi yetu, nani anajali?
 
Hivi watu waliopo ofisini huwa hawawazi ata n kwa namna Gani vijana wanahumia mpaka anafikia hyo hatua ya kufika eneo la usaili?
Hawajali muda wala gharama za watz wenzao, ktk hali ya kutaka kuonesha kutoa nafasi sawa kwa wote, ni vichekesho
 
Ndugu,

Tafadhali rejea tangazo letu la kazi ya Afisa Rasilimali Watu Daraja la II (Human Resource Officer II) lililotolewa tarehe 30 Desemba, 2025 pamoja na barua yako ya maombi ya kazi uliyoiwasilisha.

Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) inapenda kukualika kwenye usaili wa Kuandika(written interview) ambao umepangwa kufanyika siku ya Jumamosi ya tarehe 31 Januari,2026 katika Dar es Salaam University College of Education (DUCE) Dar es salaam kuanzia saa moja na nusu asubuhi (07:30 AM) utakao tanguliwa na usajili wa kila mtahiniwa pamoja na ukaguzi wa vyeti. Aidha, unatakiwa kufika ukiwa na vitu vifuatavyo;

Kitambulisho cha Taifa (NIDA) au Kitambulisho cha Mpiga Kura au Passport ya Kusafiria;
Cheti Halisi cha Kuzaliwa;
Vyeti vyote (halisi) vya taaluma vinavyohusiana na nafasi uliyoomba kwa mujibu wa sifa zilizobainishwa kwenye tangazo. Cheti cha Sekondari (Kidato cha nne au/na Kidato cha Sita) na cheti cha shahada ni lazima."
Mtahiniwa atakayechelewa kufika kwenye eneo la kufanyia usaili baada ya muda uliotajwa hataruhusiwa kushiriki.

Ninakutakia uzingatiaji mwema.
SAGUDA 47 ata-survive kweli bila connections?

Magufuli tusaidie.
 
Back
Top Bottom