Sakata la Interview za Air Tanzania leo tarehe 31 January 2026

Duh,
Hakika samaki huoza kuanzia kichwani. Hao wanafuata nyayo za mabosi wao - watawala.
Ukute ajira walishagawana hayo yalikuwa maigizo tu
 
Duh,
Hakika samaki huoza kuanzia kichwani. Hao wanafuata nyayo za mabosi wao - watawala.
Ukute ajira walishagawana hayo yalikuwa maigizo tu
Yaani mtu kasoma Procurement and Supply Chain Management halafu wamekatalia asiende kwenye paper la Procurement.
 
VIJANA WASOMI SIKIENI HILI👇
✍️.....Acha kupoteza muda wako kuhangaika na hayo maajira ya bahasha na upuuzi wa mainterview yasiyojali UTU wako.

Inawezekana vipi msomi uliyehitimu chuo kikuu kwa Marks nzuri kabisa, unajua kabisa kazi zimetangazwa mahala fulani, wanahitajika idadi fulani ktk mahitaji ya hiyo kazi, alafu unaona kabisa kuna ushindani wa waombaji mara 10x, 20x au hata mara elfu zaidi ya wahitajika,

let say ajira inahitaji watu 10 tu lkn watuma maombi wapo zaidi ya 100, wewe msomi ambaye unga unga mwana kwenu life gumu hata sabuni ya kuogea shida, unapata wapi ujasiri wa kuchoma pesa zako za mawazo kwenda kupoteza muda kushindana mahala ambapo washindi wameshachaguliwa?, Na hata Kama hawajachaguliwa bado, chance ya kushinda ni 1% out of 100%?, yaani wewe na anae bet mnatofauti gani?.

Shida yangu si hao watoa ajira bali hawa wapumbavu ambao wanaamini kwenye bahati na kutotumia akili kujiongeza.

Ukishatangaziwa ajira na unaona kutoboa ni ngumu achana nayo, ukiona ajira imetangazwa mbali na eneo lako, na hata nauli na mambo ya msingi ya kukufanya usurvive ukiwa huko hauna mpaka uombe kwa watu, acha huo upuuzi, kwani mnaamini kwenye ajira tu?, hivyo vyuo vyenu vya kipuuzi mlifundishwa ili muajiriwe tu?.
Mbinu moja wapo ktk maisha ni ku abort the mission na kuchagua mambo mapya, acha kung'ang'ana na jambo moja litakutoa roho ewe kijana msomi mpumbavu usiye na akili timamu.

Elimu ya Tz bado ni TAKATAKA iliundwa na mkoloni kwaajili ya kumsaidia kupata vibaraka kwa kufanya mambo yake kwa ujira mdogo, nashangaa serikali za Afrika bado zinaendeleza huu mfumo haramu wa elimu hii TAKATAKA.

Pia ningependa hawa viongozi maana najua wanapitia humu, wajifunze kwa wenzenu nchi zilizofanikiwa, elimu ya Tanzania imelemaza vijana, hawataki kujifunza fursa mpya, hawataki kusoma mambo magumu yanayohitaji kujitoa nje ya mfumo waliouzoea, hawataki kujua nini dunia inataka ndio hawa wanaochoma nauli kutoka mpanda vijijini mpaka dar kisa kuomba kazi ambayo tangu anapanda bus anajua kabisa kazi hiyo kuipata ni ngumu.

Vijana wa aina hii ni kuwakomboa kifikra, hizo nauli zenu fungueni hata magenge muuze nyanya, nafaka, nguo, spair za simu/Tv/laptop mtaingiza chochote kitu, kuliko kubet kwenye ajira za wachache

Wake up guys.
 
Sijui kwanini hawa vijana wajinga hawaupendi huu ukweli mchungu kuwa kwa sasa nchi hii ajira zimeingiliwa na mfumo wa ubinafsi, ni ngumu kwa kapuku choka mbaya kutoboa bila kutoa chochote kitu.

Kuna namna inafika unamuonea huruma kijana anapambana kutumia gharama kubwa kisa ajira ambayo hana uhakika wa kuipata.

Hizi nguvu wangewekeza hata kujifunza ufundi, upishi, online jobs/Freelancing(trading, network marketing, contents creating, editing/graphics designing, researching n.k) wangekua mbali sana.

Vijana amkeni, kwanini mnasumbua wazazi wenu hamtaki kazi, hamtaki kujiajiri mnataka mtelezo serikalini mkakwapue mamilioni ya fedha, alafu akina mwigulu na ndugu zake wakale wapi?.
 
Sio ajira Wala interview Mimi nilipeleka barua ya field mara tatu Kwa unyenyekevu walikataa kupokea
Tangia siku hiyo hata Mimi niliwaona takataka
 
Sio ajira Wala interview Mimi nilipeleka barua ya field mara tatu Kwa unyenyekevu walikataa kupokea
Tangia siku hiyo hata Mimi niliwaona takataka
Wanakataaje barua maana wanatakiwa waipokee harafu wakujibu hiyo barua yako maana anaekataa sio anaejibu sema Tanzania watu wana roho mbaya hatari ukiwaona sasa mtaani kwa kufake kuwa sio wao wenye roho korosho utakataa.
 
Marehemu Mtei Ali soma BA ya arts akawa gavana bank kuu.

Ukiona mtu kasoma bachelor of something with jua ana wigo mpana SANAAAAAA.

NB. Vijana wanakosa guru, connection, mentor wazurii Tanzania pesa ipo.. umaskini ninaukimbiza mbali kwa kweriiiii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…