Kijana wa Ifoza
JF-Expert Member
- Oct 31, 2025
- 1,180
- 2,302
Heshima yenu wakuu na wanafamilia wote wa JamiiForums. Imekuwa ni desturi yetu kukutana hapa jukwaani kubadilishana mawazo, kutafakari, na kuweka mambo sawa pale tunapoona mustakabali wa taifa letu unahitaji jicho la ziada.
Leo nimeona si vibaya tukaweka mezani mada inayotikisa kwa sasa katika sekta ya michezo nchini. Hii ni kufuatia hatua ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, kuukosoa hadharani mkataba wa mzabuni wa jezi mpya za Timu ya Taifa (Taifa Stars), kampuni ya Sandaland, pamoja na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF). Mzozo huu unaibua maswali mapana kuhusu usimamizi wa rasilimali za umma, mikataba ya kibiashara, na mipaka ya mamlaka ya viongozi wa kisiasa katika taasisi zinazojiongoza kisheria. Naomba tuchambue sakata hili kwa nyanja kuu nne:
1. Ubora wa Jezi na Maslahi ya Umma vs. Utawala wa Sheria
Waziri Makonda amesimama kwenye hoja kuwa jezi zilizozinduliwa hazina ubora unaoakisi chapa na hadhi ya Tanzania, huku akibainisha uwepo wa mapungufu ya kisheria na kikodi kwenye mkataba wa mzabuni huo. Kwa upande mmoja, hoja hii ina mashiko ya kiwajibikaji; Taifa Stars ni nembo ya nchi inayogharamiwa kwa kiasi kijubwa na kodi za wananchi kupitia Serikali. Ni wajibu wa Wizara kuhakikisha rasilimali na chapa ya nchi hazitumiwi kwa maslahi binafsi au chini ya viwango.
Hata hivyo, upande wa pili wa sarafu unaibua wasiwasi wa kiutawala. TFF ni taasisi inayojiongoza (autonomous body) chini ya misingi ya katiba yake na kanuni za mashirikisho ya kimataifa kama FIFA na CAF, ambayo yanapiga marufuku uingiliaji wa kisiasa au kiserikali katika masuala ya soka. Hatua yoyote inayokiuka taratibu hizi inaweza kuhatarisha nafasi ya Tanzania katika ramani ya soka duniani, hasa tunapoelekea kuwa wenyeji wa AFCON.
Changamoto ya Usimamizi wa Mikataba: Kosa liko wapi?
Sakata hili limefichua upungufu mkubwa katika uandishi na usimamizi wa mikataba ya michezo nchini. Kama mkataba una makosa ya kiufundi kama vile kutotaja vizuri wajibu wa kodi au mkanganyiko wa tarehe, lawama kuu hubaki kwa TFF. TFF ndiyo yenye dhamana ya kusimamia timu na kisheria ndiyo iliyoweka saini kwenye makubaliano hayo na mzabuni.
Kwa upande mmoja, msambazaji (Sandaland) anasimama kwenye mkataba halali wa kisheria waliomsainiana na TFF. Kosa lao linaweza kuwa ni kutozingatia uzito wa kisiasa na kijamii wa bidhaa wanayoizalisha—timu ya taifa si klabu ya kawaida ya mtaani, inahitaji ushirikishwaji mpana wa wadau wakuu, ikiwemo Serikali, kabla ya uzinduzi wa kihistoria.
3. Mipaka ya Mamlaka ya Waziri: Wapi Alipolenga na Wapi Alipokosea?
Kisheria, Waziri ana mamlaka makubwa ya usimamizi na udhibiti wa sekta (Regulatory & Oversight Powers). Ana haki kamili ya kuhoji matumizi ya fedha za umma, kulinda nembo za nchi, na hata kuunda kamati za uchunguzi pale anapoona maslahi ya taifa yanachezewa.
Pamoja na uwepo wa madaraka hayo ya kisheria, kiutawala na kiweledi, Waziri alikosea kumshambulia msambazaji (mtengenezaji wa jezi) hadharani. Mzabuni si idara iliyo chini ya Wizara, bali ni mfanyabiashara binafsi aliyefuata mchakato uliowekwa na TFF. Waziri alitakiwa kuishughulikia (ku-deal na) TFF—taasisi ambayo ipo chini ya mwavuli wa Wizara yake na ambayo Serikali inaipa fedha na ruzuku. Malumbano ya hadharani dhidi ya sekta binafsi yanaweza kutuma ishara hasi kwa wawekezaji na wadhamini wanaotaka kuingiza mitaji yao kwenye michezo hapa nchini.
4. Mtazamo Wangu: Je, Ukali Huu Mbona Hauonekani Kwenye Mikataba ya DPP na Ripoti za CAG?
Kama kijana wa Ifoza, ninatazama sakata hili kwa jicho la ziada la kiuhasibu na kiuwajibikaji wa kitaifa. Ningefurahi sana kuona nguvu na ukali huu mkubwa anaouonyesha Waziri Makonda dhidi ya mkataba wa Sandaland, angefanya hivyohivyo kwenye vikao vyao vya Baraza la Mawaziri wakiwa na Boss wao mkuu.
Inakuwaje mawaziri wetu wanakuwa kimya na hawakosoi mikataba mingi mikubwa ambayo wananchi wanaipigia kelele kila siku—kama vile sakata la mikataba ya bandari (DP World)—lakini wanakuwa wakali mno kwenye mkataba wa jezi za mpira? Swali linaloumiza kichwa ni hili: Je, kwenye mkataba huu wa Sandaland watu wamekosa ule usemi wa '10%' ndiyo maana kelele zimekuwa nyingi hivi hadi mitaani?
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kila mwaka anatoa ripoti zenye madudu, ubadhirifu, na upotevu wa mabilioni ya fedha za umma kwenye taasisi za Serikali, lakini hatujawahi kuona kina Makonda wakishupalia maeneo hayo kwa staili hii ya "kushuka mitaani".
Walio karibu na Waziri Makonda wamstue na kumkumbusha kuwa, pengine Boss wao alishabariki mambo haya, au labda amesahau ule msemo maarufu wa Mama yao unaosema: "Watu wale kufuatana na urefu wa kamba zao?" Kama kamba ya TFF ndiyo imeishia hapo kwenye Sandaland, kelele hizi zote za nini wakati kamba ndefu zaidi za ubadhirifu serikalini zikiachwa zizubae?
Asanteni na nawasilisha kwenu wakuu, jukwaa ni lenu sasa kwa michango zaidi.
Ndimi ndugu yenu kutoka Lumemo Kimero. Niwaache saa hizi ni jioni ni saa za kuandaa kukaanga ngarange tayari kwa biashara ya jioni Soko Mjinga V60 na Kwa Churu