Sakata la Kashfa ya Richmond: The Facts

Mkandara, jambo moja ambalo Waziri amesema na sijui ni nini naona wanacheza na muda kuwa kwa kadiri muda unavyoongezwa basi RDC wata deliver. Maana aliniuliza "kwani unajua mkataba unasema ni lazima wakamilishe lini?" ukweli ni kuwa sijui mkataba unasema nini only RDC. Tanesco na Waziri ndo wanajua..

Sasa hivi naanza kuhisi kuwa katika mkataba huo kuna kipengele kinachotoa perpertual flexibility ya kutekeleza mkataba huo pasipo kikomo na hivyo kufanya mkataba huo kuwa vigumu kuvunjika.
 
Mzee mwanakijiji,
Hilo swali la kukuuliza wewe kama tunajua mkataba unatakiwa ukamilishwe lini? ni swali moja la kijinga sana. Kwa sababu hiyo When wameiweka wao hawakutuuliza wananchi mnataka mkataba huu wa dharura uwe na terms zipi? Na wala sii kazi yetu tunachotaka sisi ni umeme sasa hivi.
Wameweka wao muda bila kutazama umuhimu wa huu umeme kwa wakati huu.
Yaani hiyo short term contract wameivuta hadi ionekane kama ni long term, wakati huohuo hawa hawa viongozi wanatuambia kuwa mkataba wa RDC ni wa kipindi kifupi tu kama miaka miwili maana serikali imeisha nunua mashine zake toka Finland na zimeisha fanyiwa majaribisho!... Then why kutoka mwanzo wasijaribu kampuni hiyo hiyo ama za Ki- Finland kwa hiyo short term wakati tukisubiri matokeo.
Hii ndio njia pekee ndio inaleta maana kwa sababu kama hawa Finland wameisha leta baadhi ya mashine zao kwa majaribio kwa nini serikali itumie mtu mwingine kabisa nje ya watu ambao tunataka kuwatumia ktk long term! badala yake tunaingia mkataba na kampuni ambayo imeleta mashine bomu zilizochoka na pili sasa tunavumbua kuwa haziendani na mali ghafi yetu..
No wonder, bei yao ilikuwa chini zaidi hawakupiga mahesabu kuwa gas ile ilitakiwa kusafishwa kwanza. Hii ni sawa na sisi tufikiri kuwa tunaponunua mafuta toka Arabuni basi tutegemee mafuta hayo yatakuwa tayari yameisha safishwa tayari kutumika ktk magari yetu.
Hii ina maana baada ya mkataba wataanza kung'oa hizo generator na kuzitafutia mteja mpya. Na trust me, RDC watapeleka mashine zao mikoani kwa contract za serikali yaani hatakosa kazi na mashine zake bomu.

Mzee Mwanakijiji, muda aliousema waziri ni April 2007, na kuna wadanganyika walimpigia makofi kuona kuwa RDC wamepewa muda wa mwisho hiyo April wakati nchi nzima haina Umeme. Na toka mkutano ule nadhani huyu waziri alipewa kipozeo cha watu ktk kujibu hoja hizi.
 
kwa marais wa africa na nchi nyingine aina hii ,rais hata augue kipindupindu kinachoua haraka hawezi kukubali kuachia ngazi [kipindu pindu cha ubongo ni more worse!!]
angalia rais mwanawasa alipata stroke pale na kama si kuwahishwa london angeweza kuwa bubu,lakini akagombea second term na kashinda,hakuna aliyeombwa ajaribu kupimwa ubongo.
angalia bob wa zimbabwe he is 82 now set to retire in 2008 he will be almost 85 by that time ,ni juzi tu wamemuongezea two years .au wanataka afe akiwa rais ,uzee wa rais ni mbaya but huwanufaisha wanaomzunguka na ndio huhakikisha anaendelea kwa sababu rais mzee hutegemea sana wasaidizi kuongoza,,na wao hapohapo wanakula sasa tunasubiri kuona wanafikia uzee kama wa jomo kenyatta ambaye alizeeka hadi akawa muda wote anautumia working holiday mombasa,walikua muda mwingi wanamtoa kuangalia kwaya hadi anasinzia then wanambeba wasaidizi na kumwingiza ndani,,,nchi ikibaki chini ya wasaidizi vijana kama moi,njonjo na wengine kama ina paul ngei wakitamba...
na hivyo ndivyo itakuwa kwa mugabe [msisahau ana mke kijana]sijui kama kaka yetu museeni naye atataka kuwa hivyo....
 
imeandikwa 'you work with the type of people you have'. Viongozi wetu wafanye nini tena maadamu wameshatuona sisi ni wadanganyika! Lakini bado nina matumaini kuna siku watu wataanza kudai uwajibakaji kwa viongozi wetu. Cha kuomba tu ni kwamba tusichelewe sana!
 
Mzee ES,

Lete mambo mzee wangu. Huyo aliyeporwa alikuwa mke au hawara? Kama mke
hiyo ni mbaya sana lakini kama hawara basi labda ni kuzidiana ujanja.

Humu ndani watu kwa data, huwawezi. Sasa DC kakimbia na madeni ya credit cards, huyo kweli hawezi kukimbia na pesa za wananchi huko wilayani?
 
Mwanasiasa,

Kusema kweli mzee, maneno yako safi kabisa na upande mwingine inasikitisha. Sasa kweli tutawahi vipi ikiwa hata Freeman katuweka ubaoni hali hapa hakuna utendaji kazi isipokuwa hoja tu?

I mean, kama alijua hawezi kuwa na nafasi basi usiwape wananchi ahadi na tumaini hali ametingwa!.. na kama kaamua kujikata basi bora atuambie kwani Freeman sio Mkandara ni mtu anayegombea nafasi ya juu serikalini. Utekelezaji wa maneno na ahadi zake ni moja ya vielelezo vya who he is!
Haya haya yanafanywa na JJ Mnyika, kila anapokuja hutuachia Ugali mkavu bila kitoweo, inabidi watu tuanze kumchora samaki ukutani...
Shibe haipatikani namna hii, bora kutoweka kitu mezani kabisaaa tujue kila mtu ki vyake!
 
Mzee Mbongo,

Waziri amechukua au kupora mke wa kiongozi mwenziwe, kwa maneno mengine mali ya mwananchi mwenziwe, sasa itakapokuja mali ya taifa itakuwaje? alikuwa ni mke wake jamaa na watoto watatu!

Halafu hao jamaa zangu wengne kina Mongella, aibu hata kusema, eti wanaweza kuwa wakurugenzi au wakuu wa wilaya, I find it to be incredible, only in bongo!

Hawa kule India na US, wameacha aibu tupu za madeni, wallahi only in bongo!
 
Mkandara: usiwe na wasiwasi sisi wawakilishi wake tupo hapa. Huyo JJ inabidi apotee, si unaona majibu yake yanavyokuwa marefu na ya kina, inabidi aingie shule kwanza ndo aje kujibu hoja hapa! Mtu makini huyo!
 

Katika kumpa mtu madaraka ni lazima rais awe anafanya background check ya kina, ikiwa ni pamoja kumtathmini mtu uwezo wa kujiongoza mwenywe kabla ya kumpa madarakla ya kuongoza watu. Mtu anyetmuia krediti kadi zaidi ya anavyoweza kulipa ana upungufu wa kujiongoza na hastahili kuongoza watu. Mtu anayechukua wake za watu pia ana upungufu wa kujiongoza kwa vile hatofautishi matendo mema na mabaya, hastahili kuongoza watu pia.
 
Mwanasiasa,

Majibu mengi umeyaacha wazi kwa kuwasubiri hawa jamaa. Na wao wameingia mitini hadi hapo mji huu utakapo kosa kabisa Umeme. Mvua (hoja) ndio zinaanza kwisha hivi kilichobaki tunakula kizani ugali (hoja) kwa samaki wa kuchora ukutani (bila majibu).
Ebu twambie imekuwaje Free kaingia mitini?... kwa sababu ya Chinga au?..
Well, kama hapa anapaona sii pahala pake kwa nini katupa tumaini toka mwanzo hali akifahamu wapo akina Mwanasiasa, wanachama na sio viongozi.
Hii mnanifanya nianze kuamini kuwa Chinga had valid questions ingawa wengi wetu hatukuona umuhimu wake..valid in a sense kwamba kuingia hapa ni suicide kwake kisiasa.
mwambie tupo wazee wa baraza tutamlinda pale inapohitajika, muhimu tupate picha kamili kupitia nguvu za hoja.
 
Mzee Kichuguu,

Hiyo ya background check inalelekea kwenye current government ni kama haipo, matokeo yake ndio tunakuwa na naibu waziri ambao wako kwenye payroll ya serikali ya Botswana
 
Richmond ni mzigo mzito kwa Tanesco

MKATABA baina ya Tanesco na Kampuni ya Richmond Corporation (RDC) huenda ukaiingiza Tanesco katika mzigo wa madeni makubwa, JamboForums.com imeelezwa.

Hali hii imethibitika kutokana na undani na maelezo ya kina kuhusu mkataba huo ambao JamboForums.com imeelezwa na kuona, kwamba inaiingiza tanesco katika madeni mengine makubwa.

Vyanzo vyetu vimeeleza kwamba ingawa Richmond walieleza wakati wa majadiliano walikuwa wamekwisha kupata watu wa kuwapatia mitambo ya kuzalisha megawati 100 kwa mujibu wa mkataba, mara baada ya kusainiwa kwa mkataba huo juni 23 mwaka huu, ilithibitika kwamba hawakuwa na uwezo huo.

Ukweli huu umethibitisha kwamba Timu hiyo ya maofisa wa serikali haikufanya udadisi wa kina ( Due Diligence), kuhusu Richmond kama kampuni ila tu ilijihusisha na masuala ya kitaalamu kuhusu mitambo.

Hadi sasa Richmond imekwisha kuingiza nchini, kufunga na kujaribu mitambo yenye uwezo wa kuzalisha megawati 20 tu za umeme na mitambo ya kuzalisha kiasi kingine cha megawati 80 ikiwa haijulikani hatima yake.

Uchunguzi wa muda ambao umekuwa ukifanywa na timu ya waandishi wa gazeti hili, umegundua kwamba mkataba wa Richmond hauna nafuu yoyote ya maana kwa Tanesco kwani inafanana kwa karibu kabisa na ile ya IPTL na Songas.

Tanesco kwa gharama zake huipatia IPTL dizeli ya kuendeshea mitambo na vivyo hivyo hununua gesi kwa ajili ya kuendeshea mitambo ya Songas na Aggreko na itaendelea kununua gesi (kwa gharama zake) na kuipa Richmond ili izalishe umeme na kisha Tanesco iununue umeme wa kampuni hizo kwa ajili ya kuingiza kwenye gridi ya taifa.

Kwa mujibu wa Nyaraka ambazo tumeziona na kuelezwa na vyanzo mbalimbali, Tanesco itawajibika kulipa kodi ya ongezeko la thamani (Vat) na kodi zote za forodha kwa vifaa ambavyo vitaingizwa na kupelekwa nje ya nchi na Richmond.

Mkataba huo unaiweka Tanesco katika wakati mgumu zaidi wa fedha katika kipindi chote cha miaka miwili cha uhai wake. Ulisainiwa Juni 23, mwaka huu na kuanza kufanya kazi Oktoba 5 , mwaka huu.

Mkataba huu utaiongezea Tanesco mzigo wa kulipa gharama ya kukodi mitambo ya Richmond kwa Sh 4.7 bilioni kwa mwezi tayari inalipa IPTL ya Sh 3.3 bilioni kwa mwezi na Songas Sh. 5.8 bilioni kwa mwezi.

Taarifa zilizopo zinaonyesha kuwa Tanesco inauziwa umeme wa Songas kwa senti za Marekani 5.5, wa IPTL senti 11, wa Richmond senti 4.5 na Aggreko senti 4.99.
Ikiweka kando gharama za mkataba huu, udharura wa Richmond uliokusudiwa haupo tena hasa ikizingatiwa kwamba sasa ni takribani miezi sita imepita, lakini bado imeshindwa kuingiza kwenye gridi ya taifa walau megawati moja ya Nishati hiyo iliyokuwa adimu sana sana nchini kwa zaidi ya miezi tisa sasa.

Tayari kuna habari kwamba hali ya upatikanaji wa maji katika mabwawa makubwa ya kuzalisha umeme imekuwa nzuri, na hivyo kupunguza kwa kiwango kikubwa ulazima wa Richmond katika hatua ya sasa na hasa ikizingatiwa kwamba mwenendo wake mzima umekuwa ni wa kutiliwa shaka na kila mwananchi.

Wakati Richmond ikizidi kuchechemea ikitoa sababu nyingi za kushindwa kutimiza mkataba wake kama ilivyokubaliana na Tanesco, kuanzia Desemba 5, mwaka huu, siku 60 baada ya kupewa hata ya dhamana (letter of credit – LC) na serikali, inaelekea kukumbwa na matatizo zaidi kuliko mafanikio katika utekelezaji wa mkataba wake.

Kutokana na upungufu huo, sasa Tanesco itawajibika kuidai Richmond dola za Marekani 10,000 kwa kila siku tangu Desemba 5 hadi siku itakayoweza kuzalisha umeme huo na kuunganishwa kwenye gridi ya taifa.

Kwa hali hiyo, Richmond hadi kufikia leo inatakiwa kuilipa Tanesco Sh 156 bilioni kwa kipindi cha siku 12 ambacho haijaweza kuwasha umeme wake, kama Tanesco itaamua kung'ang'ania utekelezaji wa mkataba kifungu kwa kifungu.

Tanesco ili kujinusuru na madeni na ukata, imewasilisha maombi yake ya kutaka kupandisha bili za Nishati hiyo kwa asilimia sita kwa Mamlaka ya Uthibiti wa Huduma za Maji na Nishati (EWURA). Wadau wametakiwa kutoa maoni yao kabla maombi ya Tanesco hayajajibiwa
 
MAAFISA waliohusika na majadiliano ya kuandaa mkataba kati ya shirika la Umeme nchini (Tanesco) na Kampuni ya Richmond Development Corporation (RDC) wamejulikana, JamboForums.com imeweza kubaini.

Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya habari ambavyo mtandao huu limeelezwa na kuona, maofisa wa serikali walioshiriki wanatoka Wizara ya Fedha, Wizara ya Madini na Nishati, Tanesco, Chama cha Wenye Viwanda Tanzania (CTI) na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AGC).

Pia wamo wajumbe kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT), na Kampuni ya Lahmeyer International, wote hawa walikaa pamoja na wawakilishi wa RDC, ambao walitoka na mkataba ambao ulisainiwa Juni 23, mwaka huu na kutoa muda wa siku 150 kwa umeme wa megawati 100 kupatikana kulingana na siku ambayo hati ya dhamana (letter of credit – LC) itakapotolewa na Tanesco.

Vyanzo vya habari vinasema kwamba timu hiyo ya majadiliano ilikaa katika mkutano kwa siku saba, kuanzia Juni 8-15 na ulifanyika katika moja ya kumbi za kituo cha kimataifa cha mikutano cha Dar es Salaam (DICC).

Kulingana na vyanzo vyetu katika orodha ya maofisa wa umma walioshiriki majadiliano na Richmond yumo SIngi R. Madata kutoka Wizara ya Fedha, na anaelezwa kwamba alikuwa mwenyekiti wa Timu ya Serikali iliyoingia katika majadiliano hayo.

Mwakilishi wa Wizara ya Nishati na Madini ni Theophillo Bwakea pamoja na Julius Sarota anayeelezwa kwamba alikuwa kwenye sekretariati.

Wawakilishi wa Tanesco katika mazungumzo hayo ni Stephen Mabada; Mohamed Saleh; Godson Makia; James Mtei na Wangwe Mwita aliyekuwa kwenye sekretariati.

Kampuni ya Lahmeyer International iliwakilishwa na Klaus-Uwe Huhnke na Wolfgang Pauly; mwanasheria Mkuu wa Serikali aliwakilishwa na Donald L. Chidowu na CTI iliwakilishwa na Gideon Nasari.

Kwa upande wa RDC vyanzo vyetu vinasema kwamba kulikuwa na Mohamed Gire na Naeem Gire; Gary Borges na Cuthbert Tenga.

Vyanzo vya habari vinasema kwamba timu ya serikali ilikuwa na udhaifu mkubwa kwani ilijihusisha tu na masuala ya kiufundi ya mtambo wa kuzalisha umeme wa megawati 100.

Uchunguzi wa muda mrefu baada ya kusainiwa kwa mkataba huo, umethibitisha kwamba udadisi wa kina (due diligence) Juu ya uwezo na nguvu za Richmond haukufanyika.

Hali hii ndiyo imesababishwa matatizo makubwa kuibuka baada ya mkataba kusainiwa kwamba Richmond walishindwa kutimiza wajibu wao wa kuwasilisha nchini mashine za kuzalisha umeme ilipotimu Oktoba 8, mwaka huu.

Kulingana na vyanzo vya habari hata kabla ya Timu ya Serikali ya majadiliano na Richmond kumaliza mazungumzo, Richmond ilithibitisha kwamba tayari ilikuwa imekwisha kupata kampuni ya kuipatia mitambo yote kwa pamoja yenye uwezo wa kuzalisha migawati 100.

Richmond kwa kauli yao wenyewe waliweza kueleza wazi kwamba upatikanaji wa mitambo hiyo, yaani yenye uwezo wa kuzalisha megawati 100 ni wa asilimia 95, jambo ambalo lilikubaliwa na Timu ya mashauriano bila hata Mjumbe mmoja kuonyesha kuhoji uthabiti wa kauli hiyo ama kwa kupata taarifa mbadala juu ya kampuni hiyo iliyoonyesha kila kitu kikiwa rahisi kabisa.

Hata hivyo, baadaye ilikuja kuthibitika kinyume chake kwani hadi sasa Richmond wameweza tu kuwasilisha nchini mashine zenye uwezo wa kuzalisha megawati 20 na hizo nyingine 80 inadaiwa na vyanzo mbalimbali kwamba zinatafutwa nchini Afrika Kusini.

Mashine za awali zilipatikana nchini Marekani ambako Richmond ina makao yake makuu, katika jiji la Houston, jimboni Texas.

Katika mazungumzo ya Richmond na Timu ya serikali iliweza kujenga hoja ambayo ilikubalika kwamba wangeweza kutekeleza kazi hiyo kwa mpango wa kuingiza nchini majenereta yenye uwezo wa kuzalisha megawati 25 kwa mikupuo minne.

Mkupuo wa kwanza kulingana na makubaliano hato, ni kwamba Richmond baada ya kupata LC, ingewasilisha mtambo wa kwanza katika kipindi cha siku 60 kama ingetumia ndege au siku 90 kama ingetumia usafiri wa meli; mejenereta ya awamu ya pili yangeingia katika kipindi hicho hicho cha siku 60 baada ya za kwanza au siku 120 tangu utekelezaji wa mkataba uanze.

Majenererta ya awamu ya tatu na nne yangeingia nchini na kuanza kuzalisha umeme katika kipindi cha siku 30 baada ya awamu ya pili, hivyo kufanya utekelezaji wa mradi wote; yaani kusafirisha, kufunga na kuwasha majenereta hayo yenye uwezo wa kuzalisha megawati 100 kutimia katika kipindi cha siku 150 tangu tarehe ya kupatikana kwa LC.

Vyanzo vyetu vinasema kwamba awali ilikubalika kwamba LC ingetolewa siku saba baada ya mkataba kusainiwa, yaani juni 30, 2006.

Hata hivyo baadaye hisia ziliibuka serikalini kwamba Richmond haikuwa ni kampuni yenye nguvu na uwezo kama ilivyokuwa imejitangaza na kuthibitisha yenyewe katika majadiliano, na hivyo serikali ilivuta sana miguu kuruhusu kutolewa kwa dhamana hiyo, ambayo kimsingi ni mzigo wa serikali kwamba inajitoa kuiwekea kifua kampuni husika ili iweze kupata fedha za kuendesha shughuli zake na ikitokea la kutokea ingeweza kuwajibika kwa benki husika.

Hofu hii ndiyo ilisababisha LC kupigwa danadana kuanzia Juni 30, hadi Oktoba 5, 2006 siku inayodaiwa ndiyo ilipatikana na kukubaliwa na moja ya benki.

Danadana ya LC hiyo ilielezwa kurushwa kutoka Agosti 24, 2006, ikaenda Septemba 9, 2006; ikarushwa tena Septemba 18, 2006; ikafutwa na kutolewa nyingine ya Septemba 25, 2006; nayo ikafutwa ikitolewa nyingine ya Oktoba 3, 2006; ikanyofolewa pia na mwisho ikitolewa ya Oktoba 5, 2006 ambayo ndiyo inafanya kazi.

Kwa maana hiyo utekelezwaji wa mradi wa Richmond unahesabika kuanzia Oktoba 5, mwaka huu
 
I doubt na procurement practice iliyotumika ktk ku-solicit huyu RDC. nina uhakika kama ingefuata taratibu zote kihalali tusingeona ubabaishaji huu.

kama taratibu zote za procurement zilifanyika kumpata RDC, basi tuna MATATIZO MAKUBWA ya procurement staff and evaluation team walio award hiyo contract.
 
JeiKei,

Uchambuzi mzuri sana. Kinachotakiwa TZ kwasasa ni kureview baadhi ya hiyo mikataba na watu walio nje ya system na kisha kujifunza. Inaelekea tunarudia makosa yale yale kila siku na hii ni dalili kwamba hiyo mikataba huwa haipitiwi tena kuangalia sababu za kwanini imeshindwa au kwanini kulikuwa na matatizo.

Kwa dunia ya sasa hao RDC walitakiwa waonyeshe documents na ambazo zingetakiwa kuthibitishwa kwamba tayari wana kampuni ambayo ita supply hiyo mitambo. Mbali ya hiyo pia kwenye kamati ya RDC ilitakiwa kuwe na mafundi (Engineers) kutoka huko wanakotoa hiyo mitambo ili kusaidia kujibu
maswali ya kitaaluma.

Ninapoangalia watu waliokuwepo kwenye hiyo kamati kwa upande wa RDC naona ni ma middlemen tu na mwanasheria wao. Je waliwezaje kutoa ufafanuzi
kwenye mambo ya kiufundi?

Inaelekea serikali ina kamati zake za ku review hiyo mikataba lakini mara nyingi huwezi kupata jibu sahihi kwa kamati kama hizo maana kuna kulindana. Ni muhimu mno watu wanao review hiyo mikataba kuwa huru na kufanya uchambuzi wa kina kwa faida ya nchi huko mbele
 
Jamani naomba ufafanuzi! Huyu Cuthbert Tenga wa RDC ndio yule yule wa Bro.Ukiwaona Ramadhani Mwinshehe Ditopile Mzuzuri? Jamani kama ndio hivyo mbona mimi naishiwa nguvu!
 
Binafsi nimeshashiriki sana ktk shughuli kama hizi za ku-procure, ku-review mikataba katika stages mbali mbali, na kukutana na Contractors/developers mbali mbali for negotiations.
Wakati wa negotiations Contractors wana tabia ya kuleta wazungumzaji wazuri sana sana na wanasheria wao wakali, sasa kama wawakilishi wa Client ni wababaishaji na in most cases unakuta ma-client ni ama wavivu kusoma mikataba ama ni kickbacks huwa hawazungumzi lolote wanabaki yes yes yes yes, yah yah yah yah.

Kinachonisumbua mimi ni ile njia inayotumika kumpata huyu Contractor, hapa ndipo kwenye tatizo SUGU, kwani huko kwenye negotiations Client reps mara nyingi hujikuta wakiwa ma-ruber stamps in so many ways
 
Sijaelewa statement ya Waziri, watakaoadhibiwa ni Watanzania waliotuingiza kwenye mkataba huo au wale anakina-Rich. Maana nijuavyo huwezi kumuadhibu mtu asiye ndani ya mamlaka yako. Jamani nisomesheni !!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…