Aljazeera,
Thanx a million bob, maanake hata mimi nimejaribu kufuatilia hilo lakini hadi sasa hivi mtupu!...
Hawa wahindi na viongozi wanatuona sisi vipi lakini?....I mean wamefanikiwa kutudanganya mara ya kwanza, leo hii wanafanya kuwa ibada! hata baada ya wananchi kuamuka!...
Mwanagenzi,
Nadhani jibu la maswali yako yote hapo juu yamekamilika vizuri!... kwanza kumbuka tu kuwa Dowans wanapoingia wameomba muda zaidi.. kwa hiyo tarehe ya kuanza kazi imekuwa extended kuwapa muda zaidi. Pili, TIME brother time matters!
Hakuna shirika ambalo linaweza kununua contract bila kuangalia faida na hasara zake...Which means RDC wameisha nunua mitambo ya hizo 20 ambazo RDC wameuza kwa Dowans bila sisi kupata umeme bado. hakuna kati yetu anayefahamu RDC imeuzwa kwa kiasi gani, meaning wameweka kijifaida baada ya Dowans kuridhika na mkataba kuwa wataweza kuendesha kwa faida mbali na ununuzi wa hii kampuni.
Hivyo basi, wakati biashara hii inatembea sisi tupo kizani..na uzalishaji umesimama, wawekeshaji wengine wameisha funga virago kuhamia Kenya!.. Je, unafahamu ni kiasi gani cha fedha tanzania hupoteza kila siku Umeme unapotatika?...Now, ukishapata hesabu zidisha kwa muda wote ambao tumekuwa tukipigwa chenga na hawa RDC. Hata kama Umeme utarudi kuwa kawaida, Tanzania imelala kiuchumi vibaya sana kwa muda wa hiyo miezi. Hii peke yake ni scandal kubwa sana ambayo inatakiwa kuzungumziwa bungeni na hata watafutwe wale waliohusika...Kifupi wote wahusika wanatakiwa kulipa hasara zote za Umeme.
Nimefurahi sana kuona Tanecso wanaanza kudindisha, na itakuwa balaa kwa RDC na hao Dowans wa Kuchonga!