Sakata la Kashfa ya Richmond: The Facts

Tanzania Imefungwa Magori Mengi Ndio Kosa Hapo Imefungwa Magoli 6 Na Ndio Timu Iliyofungwa Magori Mengi Katika Kundi Hili Kwahiyo Tatizo Liko Hapo

Ahsante
 
Dowans suffers 3bn/- penalty
Daily News Reporter

Soma hapa


Je hizo hesabu ni sahihi kutoka siku waliyoahidi kutimiza malengo? Je wameweza kufanikisha mkataba?
 
hesabu siyo sahihi kwani 234 x 10,000 ni sawa na 2,340,000 na siyo 2,430,000!
 
Sasa kama wanashindwa hesabu ya kitoto namna hii tutawaamini vipi? Ndio sababu Richmondulian hakujibu swali la mwanafunzi wa secondary.
 
ina maana Richmond bado hawajaanza kuzalisha huo umeme au labda sielewi
 
Koba.. fikiria hili for your entertainment....

- Richmond wanaingia mkataba na Tanesco kuzalisha umeme baada ya kuleta majenereta (say kwa gharama ya Sh. 200 Bilioni)
- Baada ya porojo nyingi, Richmond wanaona hawataweza kutimizisha masharti ya mkataba huo hivyo wanaamua kuuza mkataba huo kwa kampuni nyingine (tenda ilitangazwa lini kati yao.. sijui)
- Dowans inajitokeza na kusema "tuuzieni huo mkataba".
- Kwa vile hili ni suala la biashara itakuwa ni ukichaa kama Richmond watauuza kwa hasara.
- Hivyo wanauuza kwa bei ya chini kidogo wakihamishia madeni yao na kila kitu kwa Dowans... say Sh. Bilioni 30 tu.

Hivyo:

- Dowans wanaingia kwenye mifuko yao na hazina yao wanachota bilioni 30 na kuwalipa Richmond.
- Hadi hapo RDC hawajalipwa na serikali hata "senti moja" kwa mujibu wa kamanda mkuu wa kupambana na rushwa.
- Dowans wanaanza vibweka vyao na wanawaambia Tanesco tutautimiza mkataba huu na tunahitaji kiasi cha Sh bilioni 50 hivi kuweza kukamilisha, kiasi hicho tutakikata kwenye malipo ya mbeleni hivyo waheshimiwa serikali tunaomba advance payment ya kutuwezesha kuwaletea umeme.
- Sasa Dowans iliyokuwa na deni la Sh bilioni 30, inajikuta imejilipia deni hilo kwa fedha za serikali na kubakiwa na Shi. Bilioni 20 mfukoni kwa ajili ya shughuli zao.

Sasa:

- Kwa vile mvua imeshaanza kunyesha na mabwaya yamejaa hivyo umeme wa Dowans hauna haraka, hivyo wanaamua kuziingiza fedha hizo zilizosalia kwenye mambo yao mengine na kuzizalisha kidogo huku wakifunga funga spana.

- Kwa vile mambo yametengemaa licha ya kuchelewa wanaanza kuzalisha umeme na kuuzia Tanesco kwa bei ya juu kidogo ukilinganisha makampuni mengine.

- Serikali inasema kuwa wamechelewa kuleta umeme hivyo wataadhibiwa. Hawataadhibiwa kwa kuwataka walipe fedha zaidi bali kwa kuwanyima fedha za mbeleni (ambazo hazikuwa mfukoni mwao).

- Dowans wamepiga mahesabu na kuona kuwa hata wakinyimwa tufweza huto bado watatengeneza faida. HIvyo hawalalamii na mambo yanakuwa mdundo.

Kati haya yote, watu wanasahau kuwa Richmond Development imelipwa na serikali kwa kutumia mazingaombwe ya Dowans..

So, Hosea anaposema RDC haikulipwa na serikali anasema kweli, tatizo ni kuwa hasemi kuwa fedha za serikali zimeishia kwa RDC kwa kupitia mkono wa Dowans!
 
Do you guys really think that Hosea is a person Tanzanians can count on? Do you really think anaweza kuwakatama watu wanaohujumu Taifa? HAIWEZEKANI, unless wawe mahakimu wadogo wadogo. Lakini for sure JK au EL wakitaka aondoke madarakani ataondoka tu. Nadhani kumtegemea Hosea kwenye issue ya Richmonduli is wastage of time. PCCB is toothless dog, ilianzishwa kuwaliwaza donor community, it is a useless institution, kama alivyosema member mmoja, it makes no difference to have it or not to have it.
 
Viini macho vya Takukuru vitaendelea mpaka lini bwana Hosea? kama wanakuongoza vibaya na wewe kushindwa kufanya kazi yako basi JIUZULU MKUU, utakuwa shujaa wetu!
 
Richmond hidden truth

 
kesi ya Liji-Nyani, Ngedere atoe hukumu? what do u expect? PCCB hawana jipya kwa watanzania.... hizi transparent reports zitaendelea kuwasha moto na kufunua uozo uliotanda ktk utendaji mzima wa viongozi wetu ...

well done n keep on guys..
 
..Hosea credibility ni zero na sasa naona amejikita kukusanya shilingi mbili mbili za TANESCO kutoka kwa walalahoi walioshindwa kulipa bills zao,huyu mtu anatuchezea akili tuu na wala hana mpya bora aachie ngazi tuu kuliko kufanya mambo ya aibu kama anayoyafanya sasa hivi maana ni kashfa baada ya kashfa na kazi yake kila akifungua mdomo...OUR INVESTIGATION blah blah blah CLEAN!
 
Hii nchi kila kukicha nazidi kugundua ilivyo na viongozi wachafu. Hivi ndo kusema hakuna kitu kinachoweza kufanywa bila kona? Hawa kina EL mbona ni matajiri sana already, si wapumzike basi kuwakamua wananchi hata damu walizobaki nazo? watakufa tu wote na hiyo mimali mtaiacha tu. Na PPCB si ifutwe tu, haina kazi, wamebaki kuwashika mahakimu wanaoomba vi 20000 vya rushwa, hao samaki wakubwa hawaguswi. Iko siku.
 
PCB na HOSEA waliwahi kusema wana ushahidi wa kutosha kumkamata Rugemalira lakini mpaka leo jamaa anatanua tu. Mpaka hapo watakapomkamata Rugemalila ndio walau naweza kuanza kuwa na imani na PCB, PCB is a useless instutuions. Hata siku moja haiwezi kumwajibisha aliyeiweka ilipo(Serikali). PCB ilianzishwa kuwapumbaza donror community
 
PCCB hakuna kitu kabisa, kile ni kiini macho tu halafu na huyo Hosea ni maneno mengi matupu.
 
Hebu angalieni hawa THISDAY wanatonesa vidonda!!!!!!!!!!!!!!

http://www.thisday.co.tz/News/2874.html

 
tuliuliza maswali yale 10 miezi kadhaa iliyopita.. lakini kwa vile "hakukuwa na rushwa" basi atakalo kiongozi maarufu, mahiri, shujaa na aliyetamba Bungeni analipata!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…