Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mzee ES, Mkjj na wengineo, nimeiona na kuisoma hiyo report ya PCB (sikuimaliza kwa kukosa muda mwafaka). Sikuruhusiwa kutengeneza nakala kama nilivyotaka. Kitu kimoja kilichoni-strike ni kuwa apart from the Gires, Mohammed (m-Pakistan) wa Houston na PM mwenyewe, wahusika wengine wa kutoka wizara na taasisi zingine zote hawakutajwa majina hata kidogo. Siyo tu ndani ya report hata kwenye references za report.
Jamaa aliyenionyesha report alisema kuwa hiyo itakuwa imefanywa kwa makusudi kwani aidha wahusika hao hawakuhojiwa na TAKURU au maelezo yao yanaweza kugongana na yale yaliyotolewa na TAKURU.
Kwa hiyo jiulize, ikiwa TAKURU inaona ugumu kutaja kuwa fulani na fulani toka Tanesco, fulani na fulani toka Nishati, ...nk, how credible is the findings and the report itself?
Sitashangaa kama ni jamaa mmoja au wawili tu wa TAKURU walipewa kazi ya kutayarisha report na wakajifungia ndani na magazeti na kutoa report. Tuliokuwa serikalini tunajua haya yanafanyika kila leo.
Ukiambiwa lete report, suala la kwanza unauliza 'ya kurasa ngapi, mzee'. Mengine yote ni mapishi tu.
Matatizo ya Dowans yaelezwa
Mwandishi Wetu
HabariLeo; Wednesday,May 30, 2007 @00:03
KUCHELEWAkupata leseni ya kuiuzia Tanesco umeme wa megawati 100 kunatokana
na kampuni Richmond kubadilisha majina yake mara kwa mara, imefahamika.
Habari kutoka ndani ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), zinasema
kuwa kubadilisha majina kutoka Richmond, Dowans Holdings na sasa Dowans Tanzania ltd, kuliifanya mamlaka hiyo ikawie kutoa leseni.
Mkurugenzi wa Umeme wa Ewura, Anastas Mbawala aliiambia HabariLeo juzi kuwa kampuni ya
Richmond iliomba leseni ya biashara mwaka jana lakini baada ya mabadiliko hayo mamlaka ikabidi isubiri.
Mbawala alisema wao hawakuwa na taarifa kama kampuni hiyo ya Dowans Holdings pia
ilibadilika hadi ilipopeleka maombi ya leseni ofisini kwake na ndipo wao wakaenda kuthibitisha Brela kama Dowans Tanzania imesajiliwa kwa halali.
Alisema kwa mujibu wa maelezo ya viongozi Dowans Holdings, Dowans Tanzania ltd ilianzishwa kutokana na mkataba kati ya Tanesco na Dowans Holdings kwamba kampuni
nyingine isajiliwe kwa ajili ya kuendesha kazi hiyo ya kuuza umeme.
Kutokana na kuchelewa huko kupata leseni kampuni hiyo mpya ya Dowans sasa imepeleka maombi mapya Ewura ikiomba ipewe leseni ya miaka miwili kufanya kazi ya kuuza umeme.
Hata hivyo kampuni hiyo inakabiliwa na wakati mgumu wa kupata leseni hiyo katika kipindi kifupi baada ya Ewura kutoa matangazo yanayowataka wananchi kutoa maoni yao kama kampuni hiyo ipewe au isipewe leseni.
Endapo wananchi watapinga kampuni hiyo isipewe leseni basi kunauwezekano mkubwa uamuzi wa kutoa au kutotoa leseni utachukua muda mrefu na hivyo umeme huo kuendelea kusubiri kwani kisheria hawaruhusiwi kuuza umeme bila leseni.
Mbawala alisema maoni ya wananchi yatachukuliwa na yatafanyiwa kazi na kama yatakuwa
na hoja za msingi basi bodi ya Ewura itatoa uamuzi.
Kichuguu,
Habari hii niliipata kijiweni nikiwa Bongo ndio maana nimeuliza kama hao TARUKU wamefanya uchunguzi wa kampuni hii ya Dowans!...
Ilongo,
Maneno yako naanza kuona hekima za JK!... yawezekana kabisa kuna kila haja ya kufanya hivyo... Utamwamini nani ikiwa wasomi wetu ndio hawaaa!
A corrupt parent will obvioulsly bring up a corrupt child.
Kitu gani hasa kilichosukuma tender hii?
.....Inaendelea.......!
Hata hivyo pamoja na ripoti hiyo kukiri kuwa Ofisi ya Waziri Mkuu ndiyo iliyoamua kubatilisha uamuzi wa kutafuta kampuni kwa njia ya kutangaza Zabuni kimataifa, bado imeshindwa kutoa tathmini iwapo uamuzi huo ulikuwa wa manufaaa kwa taifa au la! Na ilipata mamlaka hayo toka kifungu gani cha sheria za Jamhuri yetu!
Nani aliipa Mamlaka ofisi hiyo ya Waziri mkuu, kuingilia kati masuala ya tenda za serikali, bila ya kuwa na jambo la msingi kufanya hivyo iwapo kanuni za ununuzi na sheria yake (Government Procurement Act) ziko wazi? Ofisi hiyo iliogopa nini kutangaza iwapo sheria zote ziko wazi kuwa shughuli kama hiyo ni lazima itangazwe kwenye gazeti la (Government Gazette), inapotokea kukawa na udhuru?
TAKURU, hawalelezi vyanzo huru vya ushaidi wao, maana hata waliotoa ushaidi huo hawajulikani ni kina nani? Na waliochunguzwa ni kina nani? Zaidi tu ya kuisemea na kuihami serikali! Kusema kweli, hii ni danganya toto, ukweli bado kuwekwa hadharani. TAKURU, hawaelezi walifanya uchunguzi kutokana na shutuma toka kwa wananchi, serikali, au wabunge? Je ni nani aliyekuwa akituhumiwa? na wapi ikiwa ni kwa mambo gani? Ukweli ni kwamba hii kesi ni ya upande mmoja ambapo kinachoonekana ni hakimu kuwa mwendesha mashitaka, mshitakiwa, shahidi na baadaye mtoa hukumu! Kwa mtu anayejua jinsi watwala wetu wanavyosema tofauti na wanavyofanya au kufanya tofauti,
na inavyosemwa, hawezi kuamini ripoti ya TAKURU, hata chembe! Na inatukumbusha wakati wa mchakato wa ununuzi wa Radar, mtakumbuka rais mstaafu Mkapa, alivyotuhakikishia kuwa dili lote la Radar, halikuwa na harufu ya rushwa hata chembe, kuachilia mbali rushwa yenyewe!
Tunachoelewa sasa, ni kwamba rushwa zaidi ya shilingi billioni 16, zilitumika kwenye dili hilo la Radar, wanachi tulipotaka kumkaba shati Mkapa, atueleze kulikoni kutudanganya, Rais Kikwete, akamkingia kifua na kutuonya kuwa tusimbughudhi na tumuache apumzike kwa amani! Na ni hivi karibuni, ili kumsafisha Mkapa na dili hilo la Radar, utafanyika uchunguzi mwingine wa TAKURU, acheni kucheza ma masilahi ya wananchi jamani!
Ukienda kwenye uuuzaji wa NBC, tulikuwa tumeaminishwa kuwa hakukuwa na rushwa hata kidogo na kwamba Mkapa ni Mr. Clean! Lakini wenye akili walikataa na kuamua kuhoji anyway! Bahati nzuri wakati huo Mwalimu alikuwepo bado hai, na aliamua kuwatolea uvivu kina "Uza Uza" hadi kuzuia baadhi miradi muhimu kuuzwa kama Kiwanda Cha Nguo cha Urafiki, Mzee wetu Mwalimu alipiga kiguuuu mpaka U-China, na kumleta muwekezaji ambaye anaingia akilini, na mpaka leo hatujasikia mauza uza ya Richmond, huko Urafiki!
.............Itaendelea..........!
... Walichohitaji tu ilikuwa generators, sasa ilikuwaje hizi generator sizinunuliwe toka GE moja kwa moja na kuwakabidhi Tanesco?