Sakata la Kashfa ya Richmond: The Facts

fanya hima kidogo niupate kabla hata Kaimu Rais hajarudi,EL anakutafuta sana coz kuna mtu wa PMO kaniambia anataka kujua unafananaje?

heheheheheee Mwambie mwanakijiji anafanana na mwanakijiji. Mwanakijiji wawekee ile picha yako hapa ile umevaa shati lilochanika ukiwa unachuma bangi shamabi ili wakuone.
 
Richmond contract leaked

THISDAY REPORTER



Source: ThisDay
 
Mambo ya serikali ya awamu ya nne ... mkataba unasainiwa usiku, sijui wanatumia nguvu za giza??? Mwaka huu tutaona na kusikia mengi na huu ni mwanzo tu. Ndanda Kosovo njoo au mtume Nguba akanushe kwamba mkataba wa Richmond uliovuja ni fake au tumia sheria ya TAKUKURU kuzuia kuongelea mkataba wa Richmond.

Halafu Hoseah pamoja na kuwa mwanasheria mahiri aliyebobea anasema Richmond ilikuwa swafi! Hivi akisoma hii news atajionaje? Kwanini asijiuzulu? Nitamshangaa sana kama atakaa kimya bila kusema lolote vinginevyo itabidi tuombe hiyo report yake iliyosafisha dili la Richmonduli na kusema mambo ni swafi na kumbe ni uozo mtupu!!!!! Halafu bado wanataka tuendelee kuwa na imani na PCCB!
 
huyu DK.Ringo Tenga atakuwa naye ni fisadi tu kama Mkono,angalia amekuwa akitetea wahujumu uchumi.Rejea kesi ya Prof Mahalu,Tunataka kujua je alilipwa sh. ngapi?na inavyoonekana yeye ndiye alidraft contract hiyo akishilikiana na Wezi wengine wa Wizra ya Nishati na Madini!!

sitaki kuamini nchi yetu ina watu mazuzu,
sitaki kuamini wana wa watanzania wanawapenda sana sisiemu,
Sitaki kuamini kwamba Mafisai haawawezi kug'oka,
sitaki kuamini Kikwete haona kinachofanyika,

Mungu Naomba unisaidie sababu natamani kuwachoma moto mafisadi wote kabla haujawachukua!
 
Yeyote aliye na contacts za Mchambuzi Maasai Worrier-Morani the Quiter naomba anipatie maana sasa tunamhitaji zaidi kuliko kipindi kile alipoanza premature campaign ya kutuambia EL ndiyo next presida!
 
Yeyote aliye na contacts za Mchambuzi Maasai Worrier-Morani the Quiter naomba anipatie maana sasa tunamhitaji zaidi kuliko kipindi kile alipoanza premature campaign ya kutuambia EL ndiyo next presida!

Mtumie kwenye e mail yake naamini anaweza kupata. Inawezekana pia yupo humu lakini kwa jina lingine mwanangu.
 
Sasa serikali ilipomlipa Dowans 19.5bn shillings ililipa kwa misingi ipi wakati hicho kipengere hapo juu kiko wazi kabisa. Halafu huyo Richmondulian ndio bado anapeta tu? sio ajabu anatetea mkataba mwingine bomu wa Buzwagi maana anafahamu his ass is dirty.
 
This is terriblle, Toka Muungwana ameingia madarakani issue za ajabu zimetokea.

Hii nchi yetu inaenda wapi, Upole wetu waTZ unatupeleka pabaya. We need to rise kutetea maslahi ya nchi yetu na watu wake. Siamini kama kweli nchi yetu ni maskini kiasi hiki kiasi cha kubaki ombaomba.
 
Unajua lazima tukubali kuwa pamoja na uozo unaofanyika, Muungwana anaonekana ni mtu ambaye kwa kiasi fulani anaheshimu uhuru wa media. Kama ungekuwa ni utawala wa Ben nadhani gazeti kama This Day lingekuwa limefutwa, au kama angekuwa ni kiongozi mwingiine tungesikia kuwa waandishi wa This day wamepotea, wamepewa scholarships kwenda kusoma au wamekufa.
Hata hivyo sidhani kama sasa ndio issue ndio zinatokea, zilikuwepo toka enzi za Mwinyi, Mkapa lakini kipindi hicho kutishia waandishi wa habari kulikuwa kukubwa kuliko sasa hivi.
Hata hivyo mwamko na uwezo wa wabongo unazidi kuwa mkubwa tofauti na miaka kumi iliyopita
 
Nadhani mchambuzi karudi tena JF kaa Demu?
tena anatumia jina linaloanzia na J.
kipindi hiki hakuna siri katika serikali hii ndio maana madudu mengi yameanza kuanikwa wazi..nasikia kipindi cha mkapa,alikuwa anatumia intranet na washirika wake wa karibu(kina Yona,Kigoda,na Mjomba Sumaye)na alikuwa anawaamini asilimia mia.mambo yote alikuwa anayaweka humo ndani na wanadiscuss nini cha kufanya(kwa kifupi mkapa anendesha mambo yake kisanyansi,na ukimugeuka tu anajua..ndio maana ilikuwa ni vigumu kujua alichokuwa anafanya katika PANGO LA WANYAN'GANYI.na inasemekana mpaka sasa antumi intranet hiyo na washirika wake..hizi kashfa za kiwira hawezi kuzijibu sababu anajua hamna ushahidi wa kutosha zaidi ya kujua kuna mkataba na kampuni yake na Yona.

you will neva see Mkapa pale Maelezo akijibu tuhuma hizi,wewe hauoni hata katika vikao vya CC-sisisemu analikwa ila hauzulii?

serikali ya Jk kila mtu ni mpishi,kila mtu anweza kujua nchini kunafanyika nini..But it is good now tunaweza kujua nchi inaliwa na kwanini hatutakiwi kuwachagua mafisadi kuongoza nchi.
 
Dr. Tenga!!! Kazi ipo. ni Rafiki mkubwa wa Dito, Dito rafiki mkubwa na wakaribu wa Kingwendu,

so what do you expect
 
Dr. Tenga!!! Kazi ipo. ni Rafiki mkubwa wa Dito, Dito rafiki mkubwa na wakaribu wa Kingwendu,

so what do you expect
yaani uhuni mtupu,ndio maana kipindi kile cha uchaguzi wa Nec watu walisema kingendu Muhuni..Si nini hiki,Ditto anawatusi watu tu kwa sababu anjua hawezi kufanywa chochote..na kwa habari za uhakika zitto anatumia Gani La Serikali..sas sijui kwa madaraka yapi aliyonay?utawal gani huu ulio bora na wa kisheria?
 

Usidanganyike ndugu yangu, hapa mkwere yuko njia panda MCC wako mbele kupambana na ufisadi ili mkopo wao usipotee bure, na baadhi ya vyombo vya habari vinanufaika na ruzuku hii ya MCC Mkwere akitia mkono ahadi zake zote zitakuwa hewa kwani hawa mabwana watafreeze kila kitu.

Mwenye mahojiano ya balozi wa marekani na gazeti la Tanzania daima ayaweke hapa mtaelewa kwa undani chungu na utamu ya misaada.

pitia hii document uone goals za MCC
 

Attachments

na kwa habari za uhakika zitto anatumia Gani La Serikali..sas sijui kwa madaraka yapi aliyonay?utawal gani huu ulio bora na wa kisheria?

ni ditoo na si zitto,hawa jamaa ni wachawi sana mpaka nimeteleza
 

Hivi mnyonge mnyongeni haki yake mpeni!!!

Mambo ambayo yametokea na kusababishwa directly na Awamu ya nne japo kwa 75% ni:- mengine ni taarifa tunazozipata kwa kuwa watu wanakuwa huru zaidi, mfano wa mambo yaliyoongelewa kwenye maadhimisho ya nyerere watu wengi wamethubutu kuongea mambo ambayo walikuwa hawawezi,,,tena wengine wasomi wazuri sana....

1. Richmond Saga, ambalo ni matokeo ya pressure ya matatizo ya umeme na ukame, tatizo ambalo alirithi, nakumbuka akina Jenerali Ulimwengu walivyokuwa wanaipressure serikali itangaze hali ya hatari, ili taratibu za Procurement zifuatwe ili kupata suluhisho la umeme haraka.

2. Buzwagi, ambapo tatizo ni sheria yenu ya madini, mpaka sasa hakuna aliyesema amekosea kifungu gani cha sheria..., other than kwamba London hotelini, etc etc..

3. Nikumbusheni...


Mengine ni ya kurithi tu!!! sasa kwa kuwa yanatokea kipindi chake na watu ni wasahaulifu basi kila kitu kimetokea kutoka kwa Awamu ya nne...

Ukiniuliza naona awamu ya nne imesababisha watu(individual, taasis, NGOs) etc kuwa na huru kujadili mambo ya kitaifa na kwa uwazi zaidi hili ni jambo jema kwa serikali....


Awamu ya nne iliweka wazir marosoroso ya Auditor General reports kwa mahesabu ya serikali kwa ajili ya wananchi wafahamu na viongozi husika wafuatilie.

Jamaa wamebadilisha sheria ya rushwa,,, na sasa sio sheria ya bribery bali ya corruptions,,, hii imesababisha at least hata kwenye CCM watu wamekemewa au imeonekana sio jambo tena la kawaida...

Takrima is out!

Naomba kuendelea kuelemishwa maana nadhani kama ni Ben abebe mzigo wako na kama ni Jakaya pia abebe mzigo wake!
 
Zitto mara kwa mara huwa anatumia gari la serikali, maana kuna wakati huwa amewahi Kukaimu nafasi ya Kiongozi wa Upinzani Bungeni ama akiwa katika majukumu yake ya Ukatibu wa Upinzani Bungeni ambao wana gari (STJ) na dereva wa serikali. Lakini pia kwa nafasi yake Mbunge ni kiongozi wa serikali. Sasa Ditto ana nafasi gani? Inawezekana ana "Kazi maalumu".

Lakini jamani Kama Ditto anatumia gari ama hatumii, lisitushughulishe, kwanza ni kiongozi ambaye pamoja na 'makeke' yake anathubutu kukemea UFISADI, na ndio maana kuna wanaoshangilia sana kupata kwake "AJALI" ya kuua dereva wa daladala. Mwisho tusipoteze muda kujadili Ditto tukasahau "RICHMOND"... Nimeona niwahi ili tusikubali kubadilishwa mwelekeo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…