Sakata la Kashfa ya Richmond: The Facts

Sakata la Kashfa ya Richmond: The Facts

Hawakuona kitu? Are you sure? Inawezekana walisema kuwa hawakuona kitu lakini mazingira yanaonesha kuwa waliona kitu, ila hawakusema. Lakini kweli wewe na akili zako can you trust PCCB?

Kweli kabisa kijana.
Kuna suala PCCB wanaficha, aidha kwa shinikizo ama wameonywa kuwa wa "shut Up, or else". Kuna mambo mengine huwa hayaonekani katika darubini za PCCB, yanaonekana kwa darubini maalum za wanajamii wenye uchungu na pesa zao.
PCCB inaripoti kwa raisi, sasa kama raisi ni mhusika wa hio issue unadhani watafurukuta na kusema kuna madudu katika mkataba? Thubutu!
Ila, Time will Tell.
 
SHELUKINDO AMETOA HOJA KWA KUSEMA:

Kwa kuwa suala la tatizo la umeme ni la kitaifa na inapofikia njia mbadala kutafuta umeme wa dharura lazima iwe ya uhakika, kwa kuwa kampuni ya Richmond ilipewa na kushindwa kufanya kazi hiyo, na kwa kuwa suala zima la Richmond limezua maswali mengi ambayo yanahitaji majibu, hivyo Bunge liunde kamati teule kuchunguza

Kamati itakavyotumia vigezo pana zaidi kuliko vya TAKUKURU…. Naomba kutoa hoja

WAMEPIGA KURA NA WALIOAFIKI WAMESHINDA KWA KUSEMA NDIYOOOOOOOOOOO

BUNGE LIMEAMUA KUUNDWA KW AKAMATI TEULE KUCHUNGUZA ZABUNI YA KAMPUNI YA RICHMOND NA TANESCO...
 
Spika kasema hivyi

"Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limeamua kwamba iundwe kamati teule ya kuchunguza mchakato mzima za zabuni ya Richmound Development Cooperation"

Spika amewateua wajumbe wa kamati hii.
  1. Harison George Mwakiembe
  2. Eng. Stella Martin Manyanya
  3. Mohamed Habib Mnyaa (Kutoka kambi ya upinzani na ni waziri kivuli wa Nishati na madini)
  4. Lucas Lumambo
  5. Habat James Mtangi
Kwenye kikao chao cha kwanza, Hao wajumbe watachagua mwenywekiti wao.

Spika amewataka hao wajumbe washulikie haya mambo.
  1. Kwanza ni kubainisha RDC ni kinanani, na ni kampuni ya shughuli zipi na kupima uwezo wake kupatiwa zabuni ya kuleta nchini na kujenga mtambo wa umeme wa megawalt 100.
  2. Kutathmini mchakato mzima wa jinsi zabuni walioshinda RDC ilivyoshuhulikiwa kwanzia kamati ya zabuni hadi mwisho ili kujiridhisha sheria, taratibu, miiko na maadili yanayotawala zabuni za aina hiyo zilifuatwa au vipi
  3. Kutathmini Mkataba kati ya RDC na TANESCO, ili kujiridhisha kuhusu uhalali na masharti ya mkataba huo ukizingatia gharama na masharti mengine yakilinganishwa na masharti yaliyomo katika mikataba hiyo hiyo iliyofikiwa na tanesco na serikali
  4. Kubainisha huduma na misaada mbalimbali waliopewa Richmound kama vile kufunguliwa letter of credit nk.. na kupima uhahahli wa hatua hizo
  5. Kuziangalia na kuzitolea maoni taarifa za takukuru, PPRA na taarifa zingine zilizoangalia utaratibu wa zabuni ya RDC
  6. Kuangalia mambo mengine yeyote yanayohusika na mchakato wa RDC, ili kutoa mapendekezo taratibu za zabuni kwa siku sijazo kwa maslai ya taifa letu
RDC - Richmound Development Cooperation
 
SPIKA AKASEMA:

KWA MAMLAKA NILIYOPEWA;;; WAJUMBE WA KAMATI TEULE WATATEULIWA NA SPIKA NA WATATEUA MWENYEKITI

KWA MAMLAKA HAYO NIMEWATEUA

Dr Harison Mwakyembe, Stella Manyanya, Mohamed Mnyaa, CUF na Lucas Selelii, Hubert Mntangi

Hadidu za rejea zifuatavyo, isije kuingizwa mambo mengine ya Dowans, IPTL na kadhalika…. Kanuni haziruhusu….

Hadidu za rejea,

1-Kwanza ni kina nani?
2-Mchakato wa zabuni ili kujiridisha
3-Kutthmini mkataba Richmond na Tanesco
4-Kubainisha huduma na misaada mbalimbali waliyopewa Richmond na kupima uhalali
5-Kuziangalia na kuzitolea taarifa za TAKUKURU NA PPRA
Kuangalia mambo mengine yoyote yanaoyohusiana na RICHMOND
 
MWakyembe anaonekana katika kamati zote mbili ya Richmond na ile ya Madini... bye 4 now
 
SHELUKINDO AMETOA HOJA KWA KUSEMA:

Kwa kuwa suala la tatizo la umeme ni la kitaifa na inapofikia njia mbadala kutafuta umeme wa dharura lazima iwe ya uhakika, kwa kuwa kampuni ya Richmond ilipewa na kushindwa kufanya kazi hiyo, na kwa kuwa suala zima la Richmond limezua maswali mengi ambayo yanahitaji majibu, hivyo Bunge liunde kamati teule kuchunguza

Kamati itakavyotumia vigezo pana zaidi kuliko vya TAKUKURU…. Naomba kutoa hoja

WAMEPIGA KURA NA WALIOAFIKI WAMESHINDA KWA KUSEMA NDIYOOOOOOOOOOO

BUNGE LIMEAMUA KUUNDWA KW AKAMATI TEULE KUCHUNGUZA ZABUNI YA KAMPUNI YA RICHMOND NA TANESCO...

Namnukuu HALISI
 
Wajumbe naambiwa ni Mwakyembe,Lukas Selelii,Mnyaa wa CUF,.....NASUBIRI SIMU KUJUA MWINGINE WAKO WATANO.

Swali inakuwaje mwakyembe kuwa kote ama spika hana taarifa za uteuzi wa rais?
 
Mwafrika wa Kike, kwa taarifa yako Dr Mwakyembe pamoja na kuwa CCM, lakini ana msimamo kama vile yuko upinzani; hataki ku-entertain ufisadi unaondelea ndani ya serikali ya CCM ... kwa inaonekana JK anataka kufanya kweli this time!

Huyu Dr Mwakyembe ninamjua vyema na ninaweza kutoa opinion yangu kuwa ni mbovu tu amekuwa akisapoti ufisadi na wizi wa ccm kinafiki underground.

Alikuwa wapi wakati kina Shivji na wasomi wengine wakichambua mikataba ya madini na suala la kufukuzwa zitto bungeni. This guy amekuwa ndio source ya magazeti ya mwizi na mkoloni Rostam Aziz kwa kutoa vigezo vya kisheria ambavyo vinapindishwa ili kutetea serikali.

Mwakyembe hafai kabisa na kuwamo kwake kwenye hii kamati ni ushahidi tosha kuwa huu ni usanii Kikwete anacheza hapa.
 
Admin. Nisaidie kuhamisha nimechemsha kuingiza hoja za RICHMOND humu.
 
MWakyembe anaonekana katika kamati zote mbili ya Richmond na ile ya Madini... bye 4 now

Mwakyembe ndio Kazi yake huko ccm.

Kutetea ufisadi ndani kwa ndani. Ni spinner mzuri na utamuona sana akiwekwa kwenye kamati nyingi zenye utata wa kisheria kwa sababu jamaa anasaidia sana kufunika mambo ya uovu wa ccm huko bungeni na kwenye ubishi mwingi wa kisheria nchini.

yeye ndio amekuwa anafanya kina Karamagi kusema publicly kuwa katika mkataba wa Buzwagi hakuna sheria yoyote iliyovunjwa!
 
I wonder, ndiyo kusema hakuna watu wengine zaidi ya mwakyembe,maana yupo kwenye tume mbili at the same time.Mimi sijajua viongozi wa kitanzania wana matatizo gani kichwani!?they are not seriuos all times.
 
Spika kasema hivyi

"Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limeamua kwamba iundwe kamati teule ya kuchunguza mchakato mzima za zabuni ya Richmound Development Cooperation"

Spika amewateua wajumbe wa kamati hii.
  1. Harison George Mwakiembe

    [[/I]


  1. Hivi hakuna wabunge wengine wanaojua kuandika Ripoti zaidi ya huyu bwana? Kutakuwa na kitu hapa
 
Hivi hakuna wabunge wengine wanaojua kuandika Ripoti zaidi ya huyu bwana? Kutakuwa na kitu hapa

Huyu Mwakyembe ndiye spin master wa serikali kwenye mikataba hii kwa hiyo lazima wamuweke ili awasaidie jamaa zake. Ukweli ni kuwa jamaa ni smart kwa hiyo tegemea bonge la spin toka kwa huyu bwana!
 
Mbona hawa kazi yao ni rahizi waje tu hapa JF wadownload nondooooz na kucompile.. Tatizo ni kwamba lazima ieditiwe na kiranja mkuu??? EL
 
Huyu Mwakyembe ndiye spin master wa serikali kwenye mikataba hii kwa hiyo lazima wamuweke ili awasaidie jamaa zake. Ukweli ni kuwa jamaa ni smart kwa hiyo tegemea bonge la spin toka kwa huyu bwana!

Kwa watu wanaomfahamu Dr. Mwakyembe watakubaliana nami kuwa huyu jamaa amekuwa mwiba mchungu sana kwa vigogo wa CCM. Rejea mzozo wa Mwakipesile na Tume ya Kinana kule Kyela. Kuhusu jina lake l´kuonekana mara mbili binafsi nachukulia kama kipimo kwa Mh. Sita kujisahihisha na kujirudi, kwani kwa kuwa yeye mwenyewe ni rebel by nature (ukiondoa udhaifu wake uliojitokeza mara katika kadhia ya Kabwe), anahitaji watu wa kariba ya kina Mwakyembe kwa ajili ya kuiweka serikali sawasawa. Tatizo naloliona wengi wanaangalia ulaji na sio unyeti na utendaji wa mtu, tubadilike.
 
Nondo za JF zinafanya kazi. Bandugu mkomeni nyani giladi mchana kweupe kabla giza halijaingia.
 
Back
Top Bottom