Sakata la Kashfa ya Richmond: The Facts

Asha Abdala - Nikukumbushe kidogo uliyokuwa umesema hapa barazani miezi michache iliyopita:

Jamani weeeh DUA. CCM wamenikatisha tamaa kipindi cha miezi michache iliyopita. Nimefanya uamuzi kama wa Mkandara na Kitila. Sasa ama zao ama zangu, naombeni mniamini. Niko tayari kukubiliana na Richmonduli, naombeni silaha. Ripoti nimeiona, kama ni hiyo ya PPRA nimezungumza na mjumbe mmoja wa kamati wamesema wameshaipitia tayari. Mi nataka vitu tofauti, nikasimame moja kwa moja kama shahidi. Nilikuwa namwamini handsome JK na braza Lowassa. Wamenisaliti. Nisameheni jamani.

Asha
 

Pole sana dada, kwa mawazo yako ulidhani hapa JF wana ushahidi wowote???

Subiri, watu wata-discuss vitu vingine kabisa... mambo mengi yaliyo jadiliwa ni mfano report ya PPRA... etc.. ambayo tume ya bunge inayo mkononi... sasa leta lingine kama unalo...
 

You have just mentioned it, in bold above! for more clarification contact Dr. Slaa a member of parliament (CHADEMA) main initiator and support of the motion!
 
 
Hivi si wange review tu utaratibu mzima uliotumika kwenye kutoa hiyo tender toka siku ya kwanza mpaka mwisho na kisha ndio wanawaita wahusika wote waliohusika. Kama kungelikuwa na ushahidi toka kwa watu wengine hiyo ni bonus lakini kwa kupitia tena records zilizopo kungetosha kuwafanya waelewe nini kilitokea. Wanatuzunga tu hawa jamaa, hakuna jipya hapa!

 
Ambacho sijaelewa ni kitu kimoja ambacho ni hiki, hivi wananchi wa kawaida walitarajiwa wakatoe ushahidi gani kwenye hili jambo? Hebu nisaidie mwenzenu, mimi sielewi, maana hata mimi nikiambiwa leo nikatoe ushahidi sioni ushahidi nitautoa zaidi ya kusema kwamba umeme haukuwepo kwa kipindi kadhaa na kwamba ile kampuni haikukamilisha kazi yake kama ilivyo kwenye mktaba au kama tulivyotangaziwa na viongozi wetu. Hivi kweli mwananchi wa kawaidia atakuwa na ushahidi wa this high level of corruption?

It would appear to me that this committee's methodology of gathering their information is flawed and therefore their results are likely to be flawed. As such, we should not expect much from this committee, they are already preparing grounds for dismissing the corruption allegations as baseless just like what TAKU.. did!
 
Jamani! sasa wao wanataka waletewe tu ushahidi, si wakafanye researh ndiyo maana walipwa mihela kibao ya per diem ili watumie akili zao! Kama kazi yao ingekuwa kuandika ushahidi wangepewa kazi ya kuwa sekretari! Waache utani!
Waje hapa JF wazombe ushahidi wote tulioupata kuhusu Richmond investments na wahindi koko ambao ni owners wake. By the way nimeona sasa kuna Richmond tours, wanatamba mjini na basi lao na magari yao ya kukodisha wameandika kwa herufi kubwa RICHMOND! Sasa wanashindwa nini, wanashindwa ku-add two and two together!? Wasipoteze hela za wananchi bure!
 
Kwa kweli hii inachosha!
kamati ya Richmond...take the PPRA report halafu mu i edit palipoandikwa PPRA andika Richmond committee.
At least that will make it a good report.

Maanake hamueleweki...sisi tuwape nyie info? Tulikuwepo? kwa kuanzia muanze na waliokuwepo....
Sasa mlikubali kazi gani msiyoweza kuitekeleza? si mnazo TOR?
 
Kitila, hawa watu wanachanganya siasa na realities on the ground. There's no need to hurt yourself further... The system is flawed and wanakamati pia wako corrupted. They know how to work on this issue, but wanajaribu kwachezea watu akili kijingajinga. They know kwamba hakuna yeyote atakayewabana hata kama wakiandika pumba in their final report, maana wanafahamu kwamba anayepaswa kuwabana naye ukimfatilia kwa karibu utakubaliana nami kua huwa anatoa conflicting statements kila mara.

How could the mwananchi wa kawaida come up with that evidence? They know where to get such evidence, but they continue making us "wadanganyika"... You can predict what kind of utumbo will come out at the end... I guess they'll come up na report inayofanana na ile ya PCCB... Haya ni mazingaombwe tu...
 
Swali! Hivi katika kamati hii ni akina nani kutoka vyama vya upinzani wamo? Maana kamati nazo nyingi siku hizi!
 
Tatizo kubwa la kamati hii ni kuwa watu wamepewa muda mrefu sana kuharibu, kuficha na kutengeneza ushahidi. Kamati hii ilitakiwa kuundwa wakati ule ule au mara tu baada ya RDC kushindwa kutimiza masharti yake. Sasa mmewapa watu mwaka mzima kujiandaa kwa hili wanatarajia nini?

Wengine tuliandika maswali ambayo majibu yake tuliyadokeza mwaka mmoja na ushee uliopita, sasa tufanye nini kingine? Mimi nawaombea tu chochote walichonacho watuambie.. ili msije kushangazwa na matokeo... mkijua hili, wenzenu wanajua lile.
 

Kitila,

Niliyasema haya siku ile hii kamati imeundwa hapa JF watu wakaniita chizi. Hii kamati na huyo Mwakyembe ilikuwa dead on arrival the second tu imeundwa.

Kila kitu kilikuwa wazi kuwa hii kamati iliundwa kupoteza pesa na muda wa watu na kisha kusema the obvious kuwa tumekaa na kusubiri watu walete ushahidi na hakuna aliyeleta kwa hiyo hii Richmonduli ni halali!.

One down, one to go..........
 
watanzania sasa tumegundua janja ya CCM wengi chadema waliposema kamati ya madini ni zuga tu na wakamshauri Zitto ajitoe waliwaita wabinafsi leo mnaanza kugundua kuwa CCM ni wasanii sio? hakika mwaka huu Mungu anawapa kila kitu LIVE tuone kama mtabisha tena hoja zikiwekwa na watu makini!!!

mfano richmond ilikuwa imuhoji na waziri mkuu maana alihusika leo waziri mkuu amepanag na rais kikwete huyo katimkia VIENA-Austria nani atabisha kuwa hakuwa na shughuli za kitaifa? changa la macho hilo, mimi nawahakikishia spika SITTA yumo na ten percent ndio pesa alizojengea nyumba yake kwani hamjui hili? nani atoe ushahidi wa kittoto kwa mwakyembe? sisi sio majuha CCM wahuni tu!!!!!
 

Hivi ni jana ama Desemba 15, 2007?
 
Dr. Mwakyembe with a Ph.D in Legal Jurisprudence has proven himself how a person can be corrupted by politics,anajua wananchi hawajawahi kuaccess hizo confidential info. za huo utumbo wa Richmond na eti anataka wananchi wakatoe ushahidi!What sheer hipocrisy.Hii ni kutengeneza kinga mapema kwamba wanajua wanatengeneza utumbo,majibu yakitoka na wadanganyika kutoridhika waseme,"Sisi tulikaa pale Karimjee siku zote tukisubiri ushahidi hakuna hata mtu mmoja aliyejitokez kuleta,sasa tufanye miujiza?",wakati wanapaswa kwenda kufukunyua kila makabrasha ingawa ushaihidi wenyewe ulikiwsha haribiwa siku nyingi kabla.Kingine kwa nini tu wasimfuate Lowassa na kumwambia "Mkuu rudisha angalau hata nusu ya hela za Richmond tuwafute machozi wadanganyika!"
 
Hii ndio Tanzania na serikali yetu ya CCM. Ndio maana niliwapa pongezi CCM kwa ushindi wao dhidi ya upinzani kwenye thread ile nyingine.

Katika hizi kamati jamaa walicheza kama Pele. Nilipondea hizi kamati siku ya kwanza zimeundwa watu wakaniita chizi hapa. CCM walitumia the best trick out there ya kuchukua momentum kutoka kwa wapinzani kwa kuunda hizi kamati.

Na kuhakikisha kuwa wana-control spinning, wakamchagua Mwakyembe kuwa Mwenyekiti hapa, na memba kwenye ile ya Madini. The guy ni spin master na smart. Ona vile anavyotumia maneno yake kwa ufundi na uangalifu mkubwa:


Good job CCM, job well done! kwa hili mmepata ushindi wa kisiasa kwa sasa na mnastahili pongezi!

Poor Tanzania!
 
Invisible,

KUna nini mbona umeiondoa ile thread nyingine? bahati mimi nilishanyonya copy yangu.
 
Invisible,

KUna nini mbona umeiondoa ile thread nyingine? bahati mimi nilishanyonya copy yangu.

Oh, nilitaka tu waipate wachache. Walopata wamepata. Zaidi ni baadae; nadhani inatosha kwa sasa. Uko makini mkuu!
 

Ahsante sana Kitila, hata mimi nawashangaa hawa jamaa, hivi wanategemea mwananchi wa kawaida akawaambie nini kuhusiana na huu mkataba!? Hizi info atazipata wapi? 😕
Hapa jamaa wamechemsha ile mbaya kweli ukistaajabu ya Mussa utaona ya firauni. Nina wasi wasi hata ile kamati ya madini 'itakosa ushirikiano' na hatimaye kuja na ripoti isiyo na chochote maana kwa maoni yangi ni lazima waonyeshwe mikataba ambayo mpaka sasa imefanywa siri, vinginevyo itakuwa ni kazi bure.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…