Sakata la Kashfa ya Richmond: The Facts

Sakata la Kashfa ya Richmond: The Facts

mzee ES............

unajua it seems as the days goes on JF inazidi kupata umaarufu.nafikiri ni good news kuwa MUUNGWANA anapita humu na kuona mwenyewe.vipi kuhusu VP dr shein?duh naona jamaaa yupo kool sana yule.
 
Nafikiri kama kweli muungwana anapitia hapa basi naathihirishe usemi aliousema katika hotuba ya kuzindua bunge kuwa anamsimamo katika masuala ya msingi,akipumzisha watu kama sita na kuendelea hapo ndio ataona waliobaki watawajibika ipasavyo kwani kwa sasa ni kiburi ndio kinawasumbua kwasababu wanajua hakuna wa kuwawajibisha.
 
Naona tunapoteza muda mwingi kuzungumzia mtu mmoja tuu katika hiyo kamati Dr. Mwakyembe , lakini kama kamati sio mtu mmoja ! What about the rest wana qualification gani ? Kwa sababu kuwa mbunge tuu aitoshi kushiriki katika hii kamati ambayo itakuwa inadeal na masuala ya nyeti ya kisheria.

Pili kwa nini spika anawachagulia upinzani mtu wa kuwepo kwenye hiyo kamati ? mimi nadhani ingekuwa vyema kama watu wa upinzani wangeachagua mtu wanayeona anawafaa wao !
 
mbona unacopy na kupaste kila sehemu wewe ??

tyshayaona maswali yako ! nilipofanya hivyo, uliita flooding sasa hii nayo naona ni EL NINO !!

Kuna kuna kitu wana Jambo Forum mnanifurahisha ni njisi mnavyomchunia huyu mjinga na mawazo yake potofu ya kuangamiza malaki ya watanzania.
 
Mwakyembe supported ujinga wa CCM kuua watu kule Zanzibar and he went far by suggesting treason kwa uongozi wa CUF.Sasa leo nashangaa kwamba yeye anatakiwa kila mahali hivi hakuna watu zaidi humo Bungeni ?
 
Je Kamati hii ina nguvu gani?

a. Je inayonguvu ya kuita mashahidi na ushahidi(subpoena power)
b. Je inayo nguvu ya kuapisha mashahidi kusema kweli, na kweli tupu under penalty of perjury?
c. Je inayonguvu ya kutoa kinga (immunity power)?

Kama haina nguvu mojawapo ya hizo hapo juu, basi Kamati hii ni mazingaombwe mengine. Ili iweze kufunua yaliyomo kwenye sakata la Richmond it should have all the three powers.
 
Viongozi wetu wa Tanzania wanachekesha sana. Na mara nyingine waweza kufikiria kuwa wanafannya maamuzi bila kufikiria.
Kuundwa kwa kamati teule ya Mh. Spika Sitta ni kitu kizuri. Kati ya wanakamati ni Mhe. Harrison Mwakyembe mbunge wa CCM
Kamati hii inatakiwa kuoa mapendekezo yake mara moja.

Rais J.K. naye kaunda kamati ya kuptia mikataba ya madini. KAti ya wanakamati ni Mh. Harrison Mwakyembe mbubge wa CCM. Kamati hii inatakiwa kutoa mapendekezo yake ndani ya miezi mitatu.

Swali! Mh. mwakyembe atafanyaje kazi katika kamati mbili hizi kwa wakati mmoja?
Je hii ni dalili ya kuwa maamuzi MAZITO yenye maslahi yanafanywa bila ya kufikiria
Je Tanzania hakuna watu wenye uzoefu wa akina Mwakyembe pale mlimani kitivo cha sheria au kwa vile siyo mwenzao?

Je Uteuzi wa Mh. Zitto Kabwe kama mwanakamati , ni kuwa kwa wale watanzania wenye "AKILI" ni kuwa ni kumaliza nguvu mbunge huyo. Je iwaje afanye kazi wakati amesimamishwa na shughuli za Bunge?
Je Kwa vile Tanzania tunaanza kukomaa kisiasa. Mh. Kabwe anaweza kukataa uteuzi huo wa kuwa ndani ya kamati ili apate nafasi nzuri ya kutadhmini yatakayopendekezwa na kamati hiyo?

Kwa kweli tanzania kunaunafiki mkubwa sana.

Hapa ninataka kuzungumzia Kampuni ya serikali na Jeshi inaiwa MEREMETA

Hii kampuni, kutikana na marangumkilema iliundwa kwa maslahi ya watu 6. Ninamajina yao, siku za kuzaliwa, Anwani zao, nafasi zao katika serikali, jina na anwani ya wakili wao huko London, Account details za waheshimiwa wote 6. Pia nina minutes za kikao kilichokaa kuifunga hii kampuni baada ya kuandamwa sana na kuonekana kuwa iliundwa ili kuwaibia watanzania

Nitawapeni hint kidogo kuwa ninaifahamu hii issue hata kuliko anavyoifahamu Mkurugenzi wa PCCB bwana Hosea. Hapa sibabaishi!

Mmoja ya watu hao 6 ni Vicent Fred Mrisho, Date of Birth 28/09/1947, Nationality ni Mtanzania, Occupation Civil servant. Address yake ni 136 Migombani street...Mikocheni.. Dar es salaam Akisema hausiki na MEREMETA, basi na huyu naye atabisha?

Lt. General Gideon Fundi Sayore DOB 10/02/1945
Kazi ni army officer etc etc

Pili, Tansort Vyanzo vyetu vya habari tunao ushaidi wa kutosha ambao hata Bunge tukufu na kamati yake iliyoteuliwa ilishindwa kupata vielelezo hivyo ilipotembelea ofisi hizo miaka ya nyuma huko London. Ukweli wa Tansort na ni kwa kiasi ganitanzania tumekuwa tukidanganywa up kwa file analo marangumkilema.
Kwa ruhusa ya jambo forum nitaiweka bayana mambo tote haya kwa maslahi ya watanzania.

Mimi mtiifu wa serikali ya Jamhuri ya Muungano na mtiifu kwa rais Jakaya Kikwete na Bunge lako Tukufu, marangumkilema
 
Kuna kuna kitu wana Jambo Forum mnanifurahisha ni njisi mnavyomchunia huyu mjinga na mawazo yake potofu ya kuangamiza malaki ya watanzania.

hata mie napenda sana hiyo kitu ! mbaya zaidi na wewe umechangia ! teh teh !
 
Do, marangumkilema haya ni makubwa! Ama kweli JK na serikali yake hii iko kazi. tunasubiri Ernest and Young wamalize kazi yao ya Bank Kuu, na endapo vitufulani fulani havitatolewa bayana, then tutaweka ukweli kwa watanzania. Mimi Msukumamkurya
 
marangumkilema umejifunga kamba mwenyewe ! ndio ubaya huo wa kutumia mawe mawili kaka !
 
Kamati inaundwa na wabunge, wa ccm na upinzani.
Jamani naomba mnipe shule.Hivi inapoundwa kamati kuna sheria inayosema ni lazima watoke CCM na upinzani? Kwanini wasitoke upinzani tu?Amabao ndo walionyeshwa kutoridhika
 
This piece is dedicated to Mwafrika wa kike...
Monday, October 1, 2007
SAKATA LA ZITTO:

Karamagi amuingiza Kikwete

Serikali yazidi kuanikwa

· Karamagi alisaini mkataba akiwa peke yake
· Ajaribu kumwingiza Rais Kikwete
· Masilingi, Mwakyembe, wambana mbavu
· Mudhihiri alalamika, "Ninatumiwa lakini…"

Na Saed Kubenea

SAKATA la Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi la kusainia mkataba wa madini nje ya nchi, liliibua mtafaruku mkubwa ndani ya Kamati ya Wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), MwanaHALISI limeelezwa.
Wabunge wengi waliopata fursa ya kuchangia, walimbana Karamagi aeleze hasa kilichotokea kuhusiana na kusaini mkataba.
Kikao cha wabunge wa CCM kilifanyika siku mbili baada ya Bunge kumsimamisha Zitto Kabwe kuhudhuria mikutano ya Bunge hadi Januari mwakani. Kabwe ni mbunge wa Kigoma Kaskazini.
Taarifa kutoka ndani ya kikao zinasema alipoanza kujieleza, Karamagi alionekana kama anayetaka kumhusisha Rais Kikwete, lakini ghafla akakaa kimya.
Hiyo ilikuwa baada ya kuulizwa iwapo Rais Kikwete alikuwa anajua jambo hilo. Hata hivyo baadhi ya wabunge walishikilia kutaka kujua nafasi ya rais katika sakata hilo.
MwanaHALISI limeambiwa kuwa awali, Karamagi alikieleza kikao kuwa alimuanga Rais Kikwete kwamba anakwenda kukutana na wamiliki wa kampuni hiyo.
Hapo ndipo palizua kasheshe. Wabunge walihoji, mara hii kwa kutoa macho, "Je rais alijuajie kama Karamagi alikuwa anakwenda kusaini mkataba wakati alimuanga anakwenda kukutana tu na wamiliki?"
Taarifa zinasema alikuwa ni, Dk. Harisson Mwakyembe, mbunge wa Kyera na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Biashara na Uwekezaji, aliyesimama na kumtaka Waziri Karamagi kusema ukweli juu ya sakata zima lilivyokuwa.
Gazeti hili limedokezwa kwamba Mwakyembe alisema mbele yawabunge wenzake kuwa Karamagi hajawahi kuiambia kamati yake juu ya kusaini mkataba na yeye, Karamagi hakuzungumzia suala hilo hata katika bajeti ya wizara yake.
"Nje tumelimaliza. Ndani atueleze ilikuwaje? Mimi ni Makamu Mwenyekiti (Kamati ya Bunge ya Biashara na Uwekezaji). Ndani ya kamati yetu hatujui hili. Hajatueleza," amenukuliwa Mwakyembe akisema.
Taarifa zinasema Mwakyembe alihoji hata uamuzi wa kusainia mkataba huo hotelini badala ya ubalozini.
Alisema hata kama mkataba huo ulisainiwa hotelini kwa bahati mbaya, lakini mbona kuna taarifa kwamba hakukuwa na hata ofisa mmoja wa ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza, wakati wa utiaji saini.
Chanzo chetu cha habari kinasema kauli ya Mwakyembe ilitanguliwa na malalamimiko ya Mudhihir Mudhihir, mbunge wa Mchinga, ambaye alimlalamikia Karamagi akisema, "Si mtu mwenye shukurani."
"Mheshimiwa mwenyekiti, mimi nimekuwa kinga kwa muda mrefu. Nimekuwa nikilinda chama chetu. Lakini hakuna shukurani. Huu ni uungwana kweli," alisema mtoa habari akimnukuu Mudhihir.
Chanzo chetu cha habari kinasema Mudhihir alilalama, "Nimechoka kutumika. Huyu Bwana Karamagi kabla ya sijasimama bungeni kumtetea, alikuwa ananipigia simu mara kadhaa na hata kunitembelea nyumbani kwangu.
"Lakini sasa hata nikimpigia simu hapokei. Jamani huu ni uungwana?" aliuliza Mudhihir.
Ni Mudhihir aliyewasilisha hoja ya kumbana Zitto hadi bunge kufikia uamuzi wa kumsimamisha vikao vya bunge hadi Januari mwakani kwa madai ya "kusema uwongo" dhidi ya Karamagi.
Zitto atakuwa akipata nusu mshahara kwa mwezi kwa kipindi chote.
Taarifa za ndani ya kikao cha wabunge wa CCM zinasema, aliyepinga adhabu ya Zitto waziwazi, ni Wilson Masilingi, Mbunge wa Muleba Kusini. Alisema adhabu iliyotolewa haikuwa sahihi.
Masilingi alitoa msimamo huo baada ya makubaliano ya kikao kuwa iundwe "tume" ambayo itapita kwenye vyombo vya habari kutetea hoja ya bunge ya kumfungia Zitto.
MwanaHALISI inazo habari kwamba tume hiyo iliundwa na tayari imeanza kazi. Tume iko chini ya uenyekiti wa Naibu Spika, Anna Makinda.
Habari zinasema wajumbe wengine ni, Wilson Masilingi, Manju Msabya (Kigoma Kusini), Adam Malima (Mkuranga) na Mudhihir Mudhiri (Mchinga).
Hata hivyo, kwa mujibu wa habari hizo, Masilingi alisema kazi ya kuzuia moto wa wananchi itakuwa ngumu kutokana na suala zima kutawaliwa na utata.
"Mheshimiwa Mwenyekiti, mkataba wenyewe siujui. Yanayozungumzwa yana wingu zito. Nikiulizwa na waandishi wa habari je, umewahi kuuona huo mkataba unaoutetea, nitasemaje?" alisema mtoa habari akimnukuu Masilingi.
Aliongeza, "Suala limekwenda katika hali ya usiri. Hakuna uwazi, hakuna tunachokijua. Ni usiri juu ya usiri."
Masilingi ambaye kitaaluma ni mwanasheria aliwahi pia kuwa Waziri wa Utawala Bora, katika serikali ya Benjamin Mkapa.
Akionyesha kupinga adhabu dhidi ya Zitto, Masilingi alisema, "Kwanza, kilichokuwa mbele ya Bunge ilikuwa ni hoja ya kuunda kamati teule ya Bunge ya kuchunguza mkataba huu. Huwezi kuamua hoja juu ya hoja."
"Hapa ilikuwa ama kuunda kamati teule au kuliachia suala hili. Lakini badala ya kupiga kura kukata uamuzi wa kuunda kamati, tunapiga kura kumfungia mbunge. Hili si sahihi," amenukuliwa Masilingi akinasihi wenzake kistaarabu.
Taarifa toka kikaoni zinasema mbunge wa Kahama ambako ndiko uliko mradi huo, James Lembeli, alililamika kwamba hajawahi kuelezwa na Karamagi juu ya kuwapo kwa mradi huo.
Wapo pia baadhi ya wabunge walioonyesha mashaka yao juu ya busara iliyotumika.
Wengi walihoji iwapo suala la mfanyabiashara Reginald Mengi na mbunge wa Mkuranga, Adam Malima liliudiwa tume ya bunge, kwa nini hili limeshindwa kuundiwa tume.
Wachunguzi wa mambo wanasema ni uamuzi wa Kamati ya CCM wa kuunda tume ndio ulisababisha Katibu wa Bunge Damian Foka, kutoa taarifa kwa vyombo vya habari akizuia wananchi na asasi za kijamii kulalamikia maamuzi ya bunge juu ya Zitto.
Lakini kilichowaacha hoi wajumbe wengi, yalikuwa ni majibu ya Karamagi kwa madai ya Mudhihir.
Karamagi alisema ameshindwa kupokea simu za Mudhihir kwa kuwa amebanwa na kazi za kuandaa nyaraka za kikao cha Baraza la Mawaziri, mtoa habari amelieleza gazeti hili.
Majibu haya, hata hivyo, hayakuwafurahisha wabunge wengi. Mmoja wao amenukuliwa akisema "Ni kawaida ya baadhi ya mawaziri kujitia kiburi na hata kubadilisha simu."
Zitto aliwasilisha hoja binafsi bungeni akitaka Bunge liunde kamati teule kuchunguza hatua ya waziri Karamagi kusainia mkataba nje ya nchi.
Katika majibu yake bungeni, Karamagi alidai kwamba serikali isingeweza kuacha nafasi ya kusaini mkataba ipotee, ikiwa na maana kwamba wawekezaji huenda wangebadilisha mawazo.
Hoja hiyo, badala ya kuzima moto iliuwasha na kuibua maswali mengine mengi.
Je, ni serikali iliyowaomba wawekezaji hawa kuja nchini na sasa wanaweka masharti kuwa watawekeza tu ikiwa mkataba utasainiwa kabla ya mwisho wa Machi?
Lakini si wawekezaji wenyewe ni Barrick Gold Mines ambao wapo nchini tayari?
Je, si walikuwa wanajua kuwa serikali inapitia upya taratibu za mikataba? Je, walitaka waingie mkataba mpya kwa utaratibu wa zamani?
Je, hata hii juhudi ya serikali "kuwashawishi" wawekezaji hawa kubadilisha vipengele kadhaa vya mikataba hiyo, si itagonga mwamba?
Kwa nini ripoti ya mazingira haikutiliwa maanani? Je, iwapo ikigundulika baadaye kuwa mradi huo ni hatari kwa mazingira, serikali itajinasua vipi kama siyo kwa gharama kubwa au kushindwa hata kuchukua hatua yoyote?
Je, kwa nini Karamagi hakuweza kutoa taarifa yoyote kwa Kamati ya Buge ya Biashara na Uwekezaji juu ya mradi huo tangu Februari iliposaini mkataba hadi alipobanwa mbavu?
MwanaHALISI linaendelea kufuatilia mfumuko wa taarifa juu ya suala hili nyeti.
 
Tuliofuatilia sakata hili tunafahamu fika JK na EL walikuwa wanalifahamu hili ndio sababu Karamagi bado anakula kuku tu lakini tutafika, ukweli wote utatokea tena sio mbali waswahili walisema 'subira huvuta kheri'.
 
Gazeti hili limedokezwa kwamba Mwakyembe alisema mbele yawabunge wenzake kuwa Karamagi hajawahi kuiambia kamati yake juu ya kusaini mkataba na yeye, Karamagi hakuzungumzia suala hilo hata katika bajeti ya wizara yake.
“Nje tumelimaliza. Ndani atueleze ilikuwaje? Mimi ni Makamu Mwenyekiti (Kamati ya Bunge ya Biashara na Uwekezaji). Ndani ya kamati yetu hatujui hili. Hajatueleza,” amenukuliwa Mwakyembe akisema.
Taarifa zinasema Mwakyembe alihoji hata uamuzi wa kusainia mkataba huo hotelini badala ya ubalozini.
Alisema hata kama mkataba huo ulisainiwa hotelini kwa bahati mbaya, lakini mbona kuna taarifa kwamba hakukuwa na hata ofisa mmoja wa ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza, wakati wa utiaji saini.

Ukweli ni kwamba huenda hawa wamezichukua hizi info hapa na kuzifanyia-modification tu ndogo ndogo, maana tuliyasema haya siku ya pili tu Zitto, aliposimamishwa bunge, kweli JF mbele zaidi, lakini still this is very interesting story!

JF idumu!
 
Mzee, nilipokuwa na confirm habari za kuvunja baraza nyumbani yaani watu wanauliza "imeripotiwa JF?".. maana watu walikuwa nusura waende online.. bahati nzuri source nyingine ya uhakika zaidi ikaniambia "not yet". Na hapa sasa nimejifunza we need to protect the forum nadhani its about time nichukue rungu langu...
 
Karamagi welcomes Richmond probe
SOSTHENES MWITA in Dodoma
Daily News; Thursday,November 15, 2007 @00:02

THE Minister for Energy and Minerals, Mr Nazir Karamagi, has promised to co-operate fully with the parliamentary select committee named to investigate the award of a power supply tender to Richmond Development Corporation in 2005.

Mr Karamagi was responding to charged interventions by MPs during the debate on a report on the controversial contract by the House Committee on Investment and Trade on Tuesday evening.

The minister told a hushed House that the government had nothing to hide.

“I will give the probe team all documents involving floating of the tender and the consequent signing of the contract agreement.”

“The whole truth will come out,” Mr Karamagi said. At this juncture, Mr Christopher Ole-Sendeka (Simanjiro – CCM) cut him short demanding to know why he refused to give the Contract Agreement to the parliamentary committee. Mr Karamagi said the committee chaired by Mr William Shellukindo, did not file a formal request.

“No one informed me that the committee needed the documents,” he said.

Debating Mr Shellukindo’s report earlier, Ms Mhonga Said Ruhwanya (Special Seat – Chadema) demanded to know the names of the top executives in Richmond.

She also wanted to know the name of “this influential culprit in government who swayed the modalities of floating the tender.”

Ms Ruhwanya said she was baffled that the company (Richmond) that had failed to implement a fuel pipeline project (from Dar es Salaam to Mwanza) had “yet again won the trust of government” and was offered another lucrative contract.

Dr Wilbrod Peter Slaa (Karatu – Chadema) read a section of a report he said was by the Public Procurement Regulatory Authority (PPRA) saying, “The contract between Tanesco and Richmond was signed at night under strange circumstances.”

The report further said “Tanesco did not even know the agent who drew the contract agreement.”

The US firm failed to install power generators within the agreed time when Tanzania was facing acute shortage of electricity.

The project was later taken over by Dowans Holdings of the United Arab Emirates.

The National Assembly voted overwhelmingly on Tuesday evening to form a probe team, which was immediately named by House Speaker Samwel Sitta.

It comprises Dr Harrison Mwakyembe (Kyela – CCM); Engineer Stella Manyanya (Special Seat – CCM); Mr Herbert James Mntangi (Muheza – CCM); Mr Mohamed Juma Mnyaa (Mkanyageni – CUF) and Mr Lucas Selelii (Nzega – CCM).

The Speaker advised the team members to pick their chairperson and start work as soon as possible.

He gave the team no mandate to touch IPTL and Dowans Holdings in their enquiry. “Concentrate on the Richmond contract,” he instructed, adding:

“We want to know the people who form Richmond. Unearth all that transpired before Richmond was awarded the contract.

We also want to know if procurement procedures were respected and if Richmond got illegal support from government officials.”
 
Bandugu wa JF

najua ni vigumu kutambua nani ataweka mada gani hapa JF..............wachache tuliokuwepo tangu bcs, TEF then JF tumeweza kuiweka hii forum yetu ktk hali ilipo hivi sasa...........hivyo basi tusikubali kuona watu wachache wakishusha hadhi ya JF................hapa nafikiria ni jinsi ganiya kupambana na MAFISADI wa JF............nilipenda the way Mwafrika wa Kike alivyopambana na waliokuwa wanajitahidi kuipondea JF...................tujifunze toka kwa Mwafrika wa kike tupambane na MAFISADI wa JF
 
THE Minister for Energy and Minerals, Mr Nazir Karamagi, has promised to co-operate fully with the parliamentary select committee named to investigate the award of a power supply tender to Richmond Development Corporation in 2005.

Mr Karamagi was responding to charged interventions by MPs during the debate on a report on the controversial contract by the House Committee on Investment and Trade on Tuesday evening.

The minister told a hushed House that the government had nothing to hide.

“I will give the probe team all documents involving floating of the tender and the consequent signing of the contract agreement.”

“The whole truth will come out,” Mr Karamagi said. At this juncture, Mr Christopher Ole-Sendeka (Simanjiro – CCM) cut him short demanding to know why he refused to give the Contract Agreement to the parliamentary committee. Mr Karamagi said the committee chaired by Mr William Shellukindo, did not file a formal request.

“No one informed me that the committee needed the documents,” he said.

Debating Mr Shellukindo’s report earlier, Ms Mhonga Said Ruhwanya (Special Seat – Chadema) demanded to know the names of the top executives in Richmond.

She also wanted to know the name of “this influential culprit in government who swayed the modalities of floating the tender.”

Ms Ruhwanya said she was baffled that the company (Richmond) that had failed to implement a fuel pipeline project (from Dar es Salaam to Mwanza) had “yet again won the trust of government” and was offered another lucrative contract.

Dr Wilbrod Peter Slaa (Karatu – Chadema) read a section of a report he said was by the Public Procurement Regulatory Authority (PPRA) saying, “The contract between Tanesco and Richmond was signed at night under strange circumstances.”

The report further said “Tanesco did not even know the agent who drew the contract agreement.”

The US firm failed to install power generators within the agreed time when Tanzania was facing acute shortage of electricity.

The project was later taken over by Dowans Holdings of the United Arab Emirates.

The National Assembly voted overwhelmingly on Tuesday evening to form a probe team, which was immediately named by House Speaker Samwel Sitta.

It comprises Dr Harrison Mwakyembe (Kyela – CCM); Engineer Stella Manyanya (Special Seat – CCM); Mr Herbert James Mntangi (Muheza – CCM); Mr Mohamed Juma Mnyaa (Mkanyageni – CUF) and Mr Lucas Selelii (Nzega – CCM).

The Speaker advised the team members to pick their chairperson and start work as soon as possible.

He gave the team no mandate to touch IPTL and Dowans Holdings in their enquiry. “Concentrate on the Richmond contract,” he instructed, adding:

“We want to know the people who form Richmond. Unearth all that transpired before Richmond was awarded the contract.

We also want to know if procurement procedures were respected
and if Richmond got illegal support from government officials.”

Source: Daily News
 
Back
Top Bottom