Sakata la kijana aliyechoma picha ya Rais kutoweka lawaibua polisi

jjackline

Senior Member
Joined
Jul 25, 2024
Posts
111
Reaction score
274

Baada ya siku kadhaa tangu Mwananchi kuripoti kuhusiana na taarifa za kutoweka kijana, Shadrack Chaula (24) aliyetuhumiwa kuchoma picha ya Rais Samia Suluhu Hassan, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Benjamini Kuzaga amevunja ukimya.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana Agosti 8,2024, Kamanda Kugaza amekiri kuwepo kwa tukio la kutoweka kwa kijana Shadrack huku akiomba wananchi kutoa ushiriano.

'Taarifa ya Kuzaga imeeleza kuwa baba mzazi wa Shadrack, Yusufu Chaula (56) alitoa taarifa ya kutoweka kijana wake Agosti 2, mwaka huu akiwa katika shughuli zake katika Kijiji cha Ntokela Kata ya Ndato Wilaya ya Rungwe.

Soma Pia:

- Baba Chaula: Polisi niambieni mwanangu kama yu hai tu basi inatosha, nahisi roho yangu inashindwa kuvumilia haya maumivu

- Aliyehukumiwa kwenda jela miaka 2 kwa kuchoma picha ya Rais amechukuliwa na watu wasiyojulika, mpaka sasa hajulikani alipo

"Jeshi la Polisi lilipokea taarifa kwa sasa wako katika uchunguzi kujua watu waliomchukua na kuomba wananchi kutoa ushirikiano ili aweze kupatikana” imesema taarifa hiyo.
Shadrack hapo awali alihukumiwa kulipa faini ya Sh5 milioni au kifungo cha miaka miwili jela baada ya kukiri kosa la kuchoma picha ya Rais.

Snapinsta.app_454626329_485735320739063_3117030171575085562_n_1080.jpg
 
Katika siasa kuna machakaramu na vichaa.
Huko Marekani mtu kamkosakosa Trump.
Nchi zenye demokrasia pevu mwanasiasa kutupiwa yai viza kitu cha kawaida.
Lakini yote yachukuliwe kwa uzito wake.
Kuna kijana Mbeya alichoma picha ya Rais Samia, akahukumiwa kifungo au faini ya milioni 5.
Wassmaria wakiona huyu nimtu asiyejielewa wakamhurumia na kampeni ikapigwa faini ikalipwa.

Tetesi ambazo hajijathibithishwa ni kwamba huyo kijana alipotea na haijulikani kama yuko hai au mfu.
Swala la kumpoteza huyo kujana haliisaidii CCM.wala mama Samia.
Sana sana litaibua chuki dhidi ya utawala.
Mimi ni kada wa CCM lakini kama kuna kitu kinaweza kuwaunganisha tena kwa nguvu kubwa wananchi wa mkoa wa Mbeya ni msombolezo ya kifo cha dhuluma.
Hili lichukuliwe kama angalizo tu na ni vema serikali ikaliweka sawa.
 
Uhai wa binadamu ndio kitu muhimu kuliko yote na Katiba ya Nchi imeliweka bayana. Kila Kiongozi anayeapa cha kwanza ni kulinda uhai. Sasa sijui huu utekaji umelenga kulinda vipi uhai?
 
Katika siasa kuna machakaramu na vichaa.
Huko Marekani mtu kamkosakosa Trump.
Nchi zenye demokrasia pevu mwanasiasa kutupiwa yai viza kitu cha kawaida.
Lakini yote yachukuliwe kwa uzito wake.
Kuna kijana Mbeya alichoma picha ya Rais Samia, akahukumiwa kifungo au faini ya milioni 5.
Wassmaria wakiona huyu nimtu asiyejielewa wakamhurumia na kampeni ikapigwa faini ikalipwa.

Tetesi ambazo hajijathibithishwa ni kwamba huyo kijana alipotea na haijulikani kama yuko hai au mfu.
Swala la kumpoteza huyo kujana haliisaidii CCM.wala mama Samia.
Sana sana litaibua chuki dhidi ya utawala.
Mimi ni kada wa CCM lakini kama kuna kitu kinaweza kuwaunganisha tena kwa nguvu kubwa wananchi wa mkoa wa Mbeya ni msombolezo ya kifo cha dhuluma.
Hili lichukuliwe kama angalizo tu na ni vema serikali ikaliweka sawa.
Nyie makada ongeeni na wenzenu uko.
Kinachosikitisha zaidi huyu kijana ndo anaweza akawakapotea mazima hivyo..mtu anapotea serikali inashindwa mtafuta..sasa watu wanalipa kodi za nini??
Inasikitisha sana....hizi katiba za kikoloni zinasumbua sana
 
RPC KUZAGA, damu ya mtu haipotei bure mtakufa wooote familia zenu zile hasara kiss kumtetea MAMA ABDUL ambaye yupo zake Chamwino au Magogoni ANAKULA BATA. HAO waking wakiweka tego mnaondoka wote. Huyo mtoto Hana hatia faini alishalipa mnataka kumuua kwa FAIDA gani?!
 
Back
Top Bottom