Kumekucha!
Vilio vya kutoridhika na utendaji wa serikali ambavyo vimekuwapo kwa miaka mingi, hatimaye sasa vinasikika kila kona:
1. Zinazoitwa tozo za uzalendo,
2. Kodi zaidi zikiwamo kwenye mafuta ya vyombo vya moto,
3. Ongezea la nauli za mabasi na usafiri kwa ujumla kutokana #2,
4. Kuongezeka kwa mfumuko wa bei zaidi kwenye bidhaa na huduma zote kutokana na #2 na #3,
5. Nk
Kwa hakika havikubaliki. Serikali inabidi ijitathmini haraka na kufanya marekebisho mapema.
Kwamba posho za wabunge, Mawaziri, na vigogo wengine hazitambui tozo, kodi wala uzalendo hii nayo haikubaliki. Kwamba kuna wabunge bungeni kinyume cha sheria wakilipwa mabilioni ya pesa hili nalo haikubaliki. Kwamba kuna ufujaji wa pesa kwa mujibu CAG kuhusisha BOT, TPA, nk, haya hayakubaliki.
Kwamba kuna mashirika yanayozalisha hasara kwa taifa, nayo haikubaliki.
Nasi wahanga wa songombingo hizi za serikali, mambo ya kuweka maslahi ya vyama kichawa chawa yafike mwisho. Tuweke maslahi ya taifa mbele. Kwa pamoja tuwakemee wanaotaka kutufanya watwana katika nchi yetu wenyewe kwa kutanguliza ubinafsi wao mbele.
Hawa ni watumishi wetu wala si watawala wetu. Hawa ndiyo wanaotakiwa kutupigia sisi magoti yakiwamo pia makofi ya kutushangilia. Tunapaswa kuwafahamisha uvumilivu wetu umefika kikomo.
Kwa pamoja tunaweza.
Down na uchawa chawa uchwara wa vyama, wote !!!!!