Sakata la kutoridhika na utendaji wa serikali

Sakata la kutoridhika na utendaji wa serikali

Sauti yetu wanaisikia lakini hawaisikilizi, ni kama kelele za chura...hazimzuii tembo kunywa maji. Wananchi ndio tunatakiwa kutambua kuwa sisi ndio wenyenchi, hapo ndio unaweza kutegemea mabadiliko !

Wanazozisikia ni kelele. Wanapaswa kuisikia kauli yetu.

Kuna tofauti kati ya sauti na kauli.

Kauli ya watu ni kauli ya Mungu.
 
Tozo ziko pale pale hakuna kitakachobadilika,watu wa serikali wanashindwa nini kutoka na kutetea hili?
 
Tozo ziko pale pale hakuna kitakachobadilika,watu wa serikali wanashindwa nini kutoka na kutetea hili?

Wenye kuamua tozo kubaki au kuondoka ni sisi bila kujali nani kutoka wapi anasema nini.
 
Uzalendo wa kulazimisha,uzalendo wa kulipia kodi
 
Wacha tushughulukiwe ili akili itukae vzr,wabunge wanadai mishahara yao ipande wkt watumishi wa serikali wako tabani bin hoi
 
Kumekucha!

Vilio vya kutoridhika na utendaji wa serikali ambavyo vimekuwapo kwa miaka mingi, hatimaye sasa vinasikika kila kona:

1. Zinazoitwa tozo za uzalendo,
2. Kodi zaidi zikiwamo kwenye mafuta ya vyombo vya moto,
3. Ongezea la nauli za mabasi na usafiri kwa ujumla kutokana #2,
4. Kuongezeka kwa mfumuko wa bei zaidi kwenye bidhaa na huduma zote kutokana na #2 na #3,
5. Nk

Kwa hakika havikubaliki. Serikali inabidi ijitathmini haraka na kufanya marekebisho mapema.

Kwamba posho za wabunge, Mawaziri, na vigogo wengine hazitambui tozo, kodi wala uzalendo hii nayo haikubaliki. Kwamba kuna wabunge bungeni kinyume cha sheria wakilipwa mabilioni ya pesa hili nalo haikubaliki. Kwamba kuna ufujaji wa pesa kwa mujibu CAG kuhusisha BOT, TPA, nk, haya hayakubaliki.

Kwamba kuna mashirika yanayozalisha hasara kwa taifa, nayo haikubaliki.

Nasi wahanga wa songombingo hizi za serikali, mambo ya kuweka maslahi ya vyama kichawa chawa yafike mwisho. Tuweke maslahi ya taifa mbele. Kwa pamoja tuwakemee wanaotaka kutufanya watwana katika nchi yetu wenyewe kwa kutanguliza ubinafsi wao mbele.

Hawa ni watumishi wetu wala si watawala wetu. Hawa ndiyo wanaotakiwa kutupigia sisi magoti yakiwamo pia makofi ya kutushangilia. Tunapaswa kuwafahamisha uvumilivu wetu umefika kikomo.

Kwa pamoja tunaweza.

Down na uchawa chawa uchwara wa vyama, wote !!!!!
JWTZ sijui wanasubiri nini kuweka pembeni hii serikali ya ccm
 
JWTZ sijui wanasubiri nini kuweka pembeni hii serikali ya ccm
JWTZ hawafanyi kazi hizo. Kazi hizo ni zetu sisi wenye nchi. Hiyo ikiwa hatua ya mwisho kabisa baada ya jitihada zote za kuhitaji busara kutamalaki kuwa zimeshindikana.

Au nasema uongo ndugu yangu?
 
Wacha tushughulukiwe ili akili itukae vzr,wabunge wanadai mishahara yao ipande wkt watumishi wa serikali wako tabani bin hoi

Kabla ya chakula kuwiva, yataka kutokota vilivyo kwanza.

Acha waendelee kuuchochea moto.
 
Kuna watu wanamshauri huyu bibi vibaya ilimradi tu marehemu aonekane alikuwa anayaweza na asiposhtuka mapema, stori itajirudia.
Bibi anaweza kurembua tu,na kula urojo huku akiskiliza taarabu asili ya bi kidude
 
JWTZ hawafanyi kazi hizo. Kazi hizo ni zetu sisi wenye nchi. Hiyo ikiwa hatua ya mwisho kabisa baada ya jitihada zote za kuhitaji busara kutamalaki kuwa zimeshindikana.

Au nasema uongo ndugu yangu?
Mkuu njia za kiraia zimeshaprove failure, mara ngapi peaceful demonstration zinapigwa bit na form failure mambosasa? Mroto?
Hakuna raia atakayenyanyua mguu kudemonstrate nchii hii ambapo hawa mbwa wa kijani wamegeuza jeshi letu la polisi kama mbwa wa mama yao, tutavumilia tu utawala wa kijeshi ili hao mbwa wa kijani waonje chungu ya kuwa nje ya madaraka, wameshaifanya nchi kama shamba la bibi yao
 
Ninakusoma lakini kwetu tatizo limekuwa ni kwenye uchawa uchwara wa kutanguliza uvyama mbele huku tukifa na tai shingoni.

Panapo nia tuweke uchawa uchwara wa vyama pembeni, mbona mambo yatakwenda tutakavyo?

Nchi ni yetu sisi. Wao waliyo nayo ni dhamana tu. Hawawezi kutufanya sisi kuwa watwana nchini mwetu.

Uamuzi ni wetu mkuu Afande Tanzania.
 
Mtanikumbuka kwa mazuri na kwa mabaya by Hayati Magufuli

Sasa hivi tuko vizuri zaidi kuliko wakati mwingine kabla:

1. Corona tunaongea lugha moja hata jingalao yuko nasi.
2. Hali kadhalika kwenye wizi BOT, TPA, na ripoti za CAG tuko pamoja.
3. Wasiojulikana wameufyata.
4. Uchawa uchwara umetambulika si dili tena.
5. Nk

Mungu atupe nini tena?
 
Huyu mama ni muislamu lakini ana Bariki kodi ya dhuluma kuwaumiza watu wake,anaua ajira na uchumi.
 
Back
Top Bottom