Sakata la Law School: Sheria isomwe miaka 4, 'vyuo vya kata' vifungiwe

Sakata la Law School: Sheria isomwe miaka 4, 'vyuo vya kata' vifungiwe

Jaji Mfawidhi

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2016
Posts
15,835
Reaction score
23,776
Wanafunzi wazembe ambao pia ni limbukeni wa mapenzi na maisha ya Dar, wameamua kufungua kesi kushitaki chuo cha sheria kwa kufeli masomo.

RUCO[RUAHA UNIVERISTY] UDSM[MLIMANI], SAUT ni vyuo vinavyotoa DIGRII kwa miaka 4 na vilivyobaki vyote ni miaka 3 ambapo pia kile chuo cha kanisa la MARTIN LUTHER wao hata research moja inafanywa na wanafunzi wawili.

Wanafunzi anahitimu chuo cha Kanisa la Mjerumani anasoma kozi 32 wakati wa RUCO, UDSM, SAUT anasoma kozi 56; Hao wakikutana LAW SCHOOL hawawezi kuwa sawa na ndio maana mmoja anafeli mwengine anafaulu.

TCU, NACTE wafute vyuo vya miaka 3 na sheria iwe standard nchi nzima miaka 4, mmoja waende field kwa AG na unaofuata waende LAW SCHOOL.
 
Back
Top Bottom