Pre GE2025 Sakata la Makonda na Gambo Zitto amchana Gambo kuhudhuria vikao asifikiri kuna kupita bila kupingwa kama 2020

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

The Supreme Conqueror

JF-Expert Member
Joined
Feb 13, 2017
Posts
458
Reaction score
1,280
Kiongozi Mstaafu wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, amesema vikao vya Kamati ya Fedha na Mipango vya Manispaa, Baraza la Madiwani na Baraza la Ushauri Mkoa (RCC) ni vikao vya kisheria hivyo utetezi wa Mbunge wa Arusha Mjini Mrisho Gambo wa kutohudhuria vikao hivyo hauna mashiko.

Kupitia ukurasa wake wa X, Zitto ame-nukuu habari yenye utetezi wa Gambo akisema “Lakini Mrisho, vikao vya Kamati ya Fedha na Mipango vya Manispaa, Baraza la Madiwani na Baraza la Ushauri Mkoa (RCC) ni vikao vya kisheria, Wabunge wengi haswa wa siku hizi mnadharau sana vikao vya chini na matokeo yake hamfanyi kazi ya uwakilishi vizuri, huu utetezi wako sio”

Zitto amejibu pia hoja ya Mdau wa Mtandao huo aliyeandika Wabunge wengi wanajisahau kutokana na kupita bila kupingwa maana wanaamini Chama dola kitawabeba na laiti kungekuwa na ushindani wa kweli kwenye sanduku la kura wasingekuwa Wazembe........... Zitto akaandika “Sio kujisahau, Wabunge wengi wanadharau vikao vya chini, nilipokuwa Mbunge moja ya vikao nilikuwa nahakikisha sikosi ni RCC, hiki ni kikao ambacho kinakupa sura ya maendeleo ya Mkoa mzima, kuna nyakati kikao kizima nilikuwa Mbunge pekee yangu kati ya Wabunge 8 wa Mkoa”

Utetezi wa Gambo umekuja baada ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Makonda hapo jana kumtaka Gambo kuachana na siasa za uchonganishi na badala yake ahudhurie vikao vya mipango ngazi ya Halmashauri na vya ngazi ya Mkoa ili kujadili pamoja kuhusu changamoto na suluhu za masuala mbalimbali yanayohusu Mkoa wa Arusha.

Katika utetezi wake kuhusu sakata hilo la jana, Mbunge Mrisho Gambo leo ameibuka na kusema “Mimi sio Mfanyakazi wa Serikali, mimi ni Mwakilishi wa Wananchi, mimi ni Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mtu ambaye anaweza kutoa taarifa na rekodi kwamba sihudhurii vikao kwa mujibu wa sheria ni Bunge na sidhani kama yeye kwa nafasi yake ni sehemu ya Bunge”
 
Huyu mstaafu anasikika sana kwaniaba ya chama kuliko aliyeko madarakani
 
Kuna watu wanamchukulia Makonda kama mpenda sifa lakini ukichunguza kwa ndani wakati mwingine yupo sahihi halafu nimeshawauliza wanagenzi 3 mbona huyu Makonda ana sauti ya Mamlaka hii nguvu anaitoa wapi? Sikujibiwa bila shaka kuna namna
 
Ulipowauliza wakajibu nini
 
Gambo kajikanyaga sana kwa utetezi aliotoa ni bora angekaa kimya tu.
 
Kuna watu wanamchukulia Makonda kama mpenda sifa lakini ukichunguza kwa ndani wakati mwingine yupo sahihi halafu nimeshawauliza wanagenzi 3 mbona huyu Makonda ana sauti ya Mamlaka hii nguvu anaitoa wapi? Sikujibiwa bila shaka kuna namna
Makonda amepikwa akapikika huko Gamboshi amemezeshwa kikoromo cha Simba.
 
Kwamba hatujui jimbo lile hata mtoto pendwa analitaka?
 
Hata Mimi nimesikitika sana gambo kumjibu angetulia tu na upepo ukapita. Hiki alichofanya ni kumpa kiki tu makonda kwani haya mambo ya majibizano na kutunishiana misuli huwa anayapenda sana. Gambo alisahau hili, 'dont argue with fools, they will drag you down to their level and beat you with experience'. Gambo kaharibu sana, angetulia tu.
 
Kwani Gambo nae si walewale. Level 1 na level 2.
 
Back
Top Bottom