Sakata la maslahi ya Wabunge na hekaya ya Hilda Newton

Sakata la maslahi ya Wabunge na hekaya ya Hilda Newton

Kitakachoshusha thamani ya shilingi siyo hiyo miradi bali wingi wa shilingi zatakazokuwa kwenye mzunguko bila kuwa proportional na mwenendo wa uchumi. Wabunge akishaanza kujipangia kuwa wapewe pesa nyingi, viongozi wa serikali nao wakaanza hizo zinazoitwa semina endekezi zenye per diem kubwa kubwa ambazo zinaishia kwenye mzunguko, ndipo hapo thamani ya shilingi itakapoanza kuporomoka.
As long as they don't print money then wingi wa shilingi ni ule ule. Labda mgawanyiko wake utabadilika. Zikiwa mtaani ziko less likely kutumiwa kununua forex kuliko zikiwa kwa wachache. Hao wachache huwa wanahamishia kwenye akaunti zao nje.
 
Mheshimiwa Kichuguu,

Nafahamu wewe ni mtu mwenye michango mizuri sana huku kwa siku nyingi. I have nothing but respect for you. Ila hili la shilingi kushuka kwa kasi sasa nadhani umekosea. Ni sahihi kwamba miradi ya SGR, madaraja, ujenzi wa meli na kadhalika itachukua forex nyingi, lakini miradi ya LNG na bomba la mafuta italeta nchini forex nyingi pia. Miaka michache ijayo shilingi itapanda, na sio kushuka. Wekeza tu dola zako Bongo sasa. I am in the same boat.
Niko na mixed feelings for both of you, the policies are still blurred to surfice predictability
 
Mitano tena kwa wabunge wa ccm...wakumbuke hawakufuatwa wagombee waliomba wenyewe kama haitoshi wapishe wasiombe tena
 
Point yangu ni kuwa kupitia tight monetary policy hali ya kuwa na circulation kubwa haitakuwepo. Mi muda mrefu watumishi wa serikali hawajaongezwa mishahara lakini bei za bidhaa zimekuwa zinapanda. Watu wakipewa imcrements zao sidhani kama circulation ya pesa itakuwa kubwa. Tukumbuke kipindi cha Raisi Mwinyi, Mkapa na Kikwete...
Kipindi cha JK ndio kipindi tulichokuwa tunashuhudia unga ukifika hadi 2,500 kwa kilo na mchele 3,500 kwa kilo.

Je kwa Magu uliwahi kuona hali kama hiyo zaidi ya sukari?
 
Wangetafuta namna ya kuwadhibiti hawa waropokaji.

Hii ni namna nyingine ya kusema hawamuogopi aliyepo madarakani....maana sidhani kama angethubutu kuropoka hivi mbele ya Magufuli.
 
Kipindi cha JK ndio kipindi tulichokuwa tunashuhudia unga ukifika hadi 2,500 kwa kilo na mchele 3,500 kwa kilo.

Je kwa Magu uliwahi kuona hali kama hiyo zaidi ya sukari?
Kipindi cha Magufuli nyama ilifikia kilo moja elfu kumi. Sukari ikapanda.

Huwezi ficha madhaifu kwa kutafuta madhaifu ya mtu mwingine. Atakuja mtu hapa atahama mada ya vyakula na kuanza kuongelea deni la taifa.

Kila uongozi una madhaifu. Ni kuyatafuta tu.
 
Yani unaongelea nyama kufika elfu 10 tena msimu wa sikukuu?

Ongelea kupanda kwa unga na mchele hapo hata bibi yako kule kijijini lazima akione cha moto
 
Yani unaongelea nyama kufika elfu 10 tena msimu wa sikukuu?

Ongelea kupanda kwa unga na mchele hapo hata bibi yako kule kijijini lazima akione cha moto
Bibi yangu tena?
 
Kipindi cha JK ndio kipindi tulichokuwa tunashuhudia unga ukifika hadi 2,500 kwa kilo na mchele 3,500 kwa kilo.

Je kwa Magu uliwahi kuona hali kama hiyo zaidi ya sukari?
Acha uongo wewe dada, kikwete Hadi anaondoka madarakani 2015, bei ya unga wa sembe kwa Kg ilikuwa 600/=✓
sukari kg ilikuwa Tsh. 1000-1200/=
mchele kg ilikuwa haizidi TSH 1000,

Alivyoingia dikteta ndio kila kitu kikawa juu, sukari ilifika bei hadi elf tano, unga pia ,mchele alkadhalika,
Mwendazake Hana la kukumbukwa kweny utawala wake, labda kutekwa watu, kupigwa risasi 38 Lissu Kama wanaua tembo, kuminya uhuru wa habar na kupashana habari, etc
 
Tunaohoji hadi Kuwashangaa Wabunge kudai nyongeza ya Mshahara tumeshajiuliza Swali ni lini Mshahara umewahi Kumtosha Mwanadamu?...
Wapunguze kujali matumbo yao na wachangie kodi kabla ya kudai kuongezwa mshahara.Hiyo misaada wanayotoa mfano mbunge mmoja wa ifakara aliwahi kutoa mbuzi wawili na kreti kumi za soda kwenye shule moja ya sekondari.
 
Acha uongo wewe dada, kikwete Hadi anaondoka madarakani 2015, bei ya unga wa sembe kwa Kg ilikuwa 600/=✓
sukari kg ilikuwa Tsh. 1000-1200/
Nani dada sasa!

Usiwe jinga!

Ni katika kipindi cha JK pekee bidhaa muhimu kama unga uliwahi kufika 2,500 na mchele 3,500

Magu kakuta unga unauzwa kati ya 1000 na 1200, nyuzi zake ziko humu!

Hiyo bei yako ya 600 ni ya wakati JK anachukua madaraka!
 
Izo bei labda zilikuwa kwenu Rwanda, me nna duka la vyakula nnachokuambia nna ushaidi nacho kijana
Wewe una shida sana!

Muulize huyo shemeji yako ambae ndio huwa ananunua bidhaa wewe kazi yako ni kula tu huwezi kujua.
 
Tunaohoji hadi Kuwashangaa Wabunge kudai nyongeza ya Mshahara tumeshajiuliza Swali ni lini Mshahara umewahi Kumtosha Mwanadamu?

Kuna Shirika moja la Ndege ( hapa hapa EAC Kwetu ) Marubani wake kila Mwezi wanalipwa USD 8000 ( Hela ambayo ukiichenji kwa Shilingi yetu inazidi hata ya Wabunge ) huku Posho zao kila wakiruka ( wakipaa ) ni USD 200 lakini bado walitishia Kugoma ili waongezewe.

Huko nyuma nami GENTAMYCINE nilikuwa ni Muumini wa 'Kukurupuka Kudemka' hasa Kushangaa Wabunge wakitaka Kuongezeka Mishahara yao ili nilivyokaa Siku moja na Mbunge fulani na akanichambulia jinsi Pesa zao zinavyotumika na kuishia kwa Kuwasaidia Wananchi ambao 24/7 huwapelekea Shida zao mbalimbali kiukweli wakidai hiyo nyongeza ni halali ( haki ) yao.

Tatizo Kubwa nililoligundua humu Mtandaoni ( Mitandaoni ) ni kwamba kumekuwa na 'Kautamaduni' ambako naona kana Ushamba na Upumbavu mwingi ambapo Watu tumekuwa 'tunahemka' kwa Hisia zetu tu za Itikadi ya Vyama vyetu vya Kisiasa pamoja na Chuki kwa Bunge lenye Wabunge wengi wa CCM na Serikali yake pia ila hatutaki Kujishughulisha kutumia Akili zaidi ya Kutafakari na Kuchambua jambo.

Nimalizie tu kwa Kuwauliza je, nyie mnaopinga Wabunge Kuongezewa Mshahara au hata Watu wa Kada zingine Kupandishiwa Mishahara nyie mngekuwa ndiyo Wabunge au Watu hao mngekuja humu Mitandaoni na Kukataa kuwa isipandishwe?

Ifike muda tupunguze Nongwa na Wivu.

Kama mshahara uliokuwa haiwatoshi kwanini walipora uchaguzi ili wawe wabunge? Na kipi kinachowafanya waendelee kubaki kwenye ubunge walioupata kwa wizi ,wakati hata mshahara hautoshi? Inawezekana kweli mshahara ni mdogo, lakini huo mshahara mdogo ndio uhalisia wa umasikini wa nchi yetu.
 
Wangetafuta namna ya kuwadhibiti hawa waropokaji.

Hii ni namna nyingine ya kusema hawamuogopi aliyepo madarakani....maana sidhani kama angethubutu kuropoka hivi mbele ya Magufuli.
Naona unaturopokea. Kwenye kutetea haki ni lazima kusema bila woga. Ni freedom of speech.

Bootlicking is a vicious vice. Nyerere angekuwa anawaza kwamba kuwakosoa viongozi ni kosa kama unavyodhani wewe tungechelewa kupata uhuru.
 
Wamajiwekea 3.8M kwenye salary slip ili kukwepa makato ya kodi.

Kwenye hiyo 3.8M wamejiwekea miposho posho na allowance kibao isiyo na makato yoyote mpaka kitu inaenda mpaka 12M kwa mwezi.

Kubwa kuliko yote ni wao kupewa mafao ya zaidi ya Tsh 250M ndani ya miaka 5 tu bila yao kuchangia chochote kwenye mfkina Silinde na Lijualikali walivyo kuwa

Wamajiwekea 3.8M kwenye salary slip ili kukwepa makato ya kodi.

Kwenye hiyo 3.8M wamejiwekea miposho posho na allowance kibao isiyo na makato yoyote mpaka kitu inaenda mpaka 12M kwa mwezi.

Kubwa kuliko yote ni wao kupewa mafao ya zaidi ya Tsh 250M ndani ya miaka 5 tu bila yao kuchangia chochote kwenye mfuko.
Nikikumbuka kina Silinde na Lijualikali walivyo kuwa wanalialia, sasa mtu umelipwa 10 million per month for 5 years plus 250 million mafao
 
Tusimbeze Huyo mbunge aliyetoa maoni yake tukahisi ni yeye tu kajifikiria kichwani akaja na maoni ya kuongezwa mshahara, huenda ni agenda ya wengi lakini imeletwa na Nicodemas kama kupima upepo hivi ili baadae waikomalie kwa pamoja ipitishwe na mishahara kuongezwa .
 
Back
Top Bottom