Sakata la maslahi ya Wabunge na hekaya ya Hilda Newton

Tutajie na majina Yao tujifunze kutoka kwao . Mbona majina hamyataji

Sent from my CPH1937 using JamiiForums mobile app
 
Kwanini wanakuwa wabinafsi kabla ya kuwapigania Wafanyakazi kama Walimu, Madaktari, Manesi ambao wengi wao hawafikii hata robo ya mishahara yao wajitangulize wao ambao wanaishi maisha mazuri kabisa kutokana na mishahara na marupurupu manono? Mshahara wa milioni 12 kwa mwezi, posho ya shilingi 340,000 Kwa siku na kiinua mgongo cha zaidi ya milioni 300 kila baada ya miaka mitano?
 
Yani unaongelea nyama kufika elfu 10 tena msimu wa sikukuu?

Ongelea kupanda kwa unga na mchele hapo hata bibi yako kule kijijini lazima akione cha moto
Mbona sukari na mafuta ya kupikia yalipanda mpaka basi?
Kila awamu na vimbwanga vyake.
 
Wanaoweza kupigania maslahi ya wengine ni viongozi wa huko ulaya ila sio hawa wakwetu. Sio wazungu wote wanaakili sana ila wapo wachache smart wanaopambania nchi kwa manufaa ya wote.
 
Natamani ifike mahali tuwe na wabunge 26 tu nchi nzima na hapo kutakuwa na ushindani wa dhati kwa anayetaka kuwa mbunge lazima aoneshe deliverables, kama wakuu wa mikoa wapo kazini kila siku na wanaweza kupitia wilaya zao zote, inakuwaje wabunge wanatumitaa 20 miaka mitano inakwisha hawajamaliza kuzungukia hata halimashauri moja!!!?
 
Huyo bwana ni kama namjua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…