Elections 2010 Sakata la mauaji ya Dereva wa CCM Maswa na hatima ya Shibuda

Elections 2010 Sakata la mauaji ya Dereva wa CCM Maswa na hatima ya Shibuda

Kwanini

Senior Member
Joined
Sep 25, 2010
Posts
121
Reaction score
1
"Nimeingia Maswa na kukutana vurugu za kisiasa kati ya CCM na CHADEMA,vurugu hizo zimepelekea watu kadhaa kujeruhiwa na dereva aliekuwa anaendesha gari la kampeni la CCM kuuawa na wafuasi wa Chadema."(Thaddeus Musembi anatuhabarisha lisaa limoja lililopita).
 
Kwanini, sema vizuri hiyo taarifa yako!! kwanini wamemuua na kipi kinaendelea saizi? Tupe habari zaidi maana hawa jamaa kwa fitina ndo zao, wanajaribu kila mbinu ili waaminiwe. mwenye detail zaidi atupe.
 
‎"Nimeingia Maswa na kukutana vurugu za kisiasa kati ya CCM na CHADEMA,vurugu hizo zimepelekea watu kadhaa kujeruhiwa na dereva aliekuwa anaendesha gari la kampeni la CCM kuuawa na wafuasi wa Chadema."(Thaddeus Musembi anatuhabarisha lisaa limoja lililopita).

Na kama ni taarifa ya uzushi na wewe upelekwe mahakamani kama yule kiongozi wa wastaafu wa africa mashariki
 
This is murder case,justice must take its position!
 
‎"Nimeingia Maswa na kukutana vurugu za kisiasa kati ya CCM na CHADEMA,vurugu hizo zimepelekea watu kadhaa kujeruhiwa na dereva aliekuwa anaendesha gari la kampeni la CCM kuuawa na wafuasi wa Chadema."(Thaddeus Musembi anatuhabarisha lisaa limoja lililopita).[/QUOTE

MH KAMA KWELI HII MBAYA SANA!
 
nimeongea mgombea wa chadema, john shibuda sasa hivi, yuko kituo cha polisi, amesema nimpigie baada ya dakika 5!.
 
Nilimpata tena Shibuda, amethibitisha tukio, ni dereva wa mgombea wa CCM, hakuthibitisha kifo maana kifo huthibitishwa na daktari, ila yeye alikamatwa na amelala mahabusu, wakati tukiendelea kuongea, simu ilikatika!
 
Hii kweli ni tofauti na ile ya mbowe kupigwa kuumizwa kisha kupelekwa usa kupitia pretoria! Nahisi Kuna njama za makusudi zinafanywa ili kuipotezea credibility Jf kuwa major source of reliable information!
Mpaka iwe comfirmed kwanza!
 
Baada ya matishio ya kumwagika kwa damu Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, hatimaye jana damu imemwagika kweli huko Maswa ambapo dereva wa gari la mgombea wa CCM jimboni humo, ameuwawaw na wananchi wenye hasira.

Nimezungumza na Mgombea wa Chadema, John Magalle Shibuda, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, japo hakuthibisha maafa, bali ametoa upande wake wa story kuwa yeye akiwa Jukwani kwenye kampeni zake, akatuma gari lake la matangazo kutangulia kijiji kinachofuata.

Gari hilo likiwa njiani, lilivamiwa na gari la mgombea wa CCM wakitaka kuligonga ndipo likalikwepa na ikawa ndio salama yao, gari lile la mgombea wa CCM nalo likasisima, watu wakashuka na kuanza kuwashabulia hao kwenye gari la Chadema.

Kwa mujibu wa Shibuda, vijana wake wakapiga mayowe ya kuvamiwa, wanakijiji wakajitiokeza kuwasaidia ndipo waliotembeza hicho kichapo kwa dereva huyo.

Kwa vile Shibuda ni interested party, upande wake wa story lazima upatiwe balance ya upande wa pili wa CCM na hatimaye kuthibitishwa na authorities za Jeshi la polisi.

Naendelea kufuatilia upande wa pili na uthibitisho wa polisi, pia nafanya juhudi za kumtafuta mpiganaji Fredirick Katulanda ambaye siku zote husimama wima bila kuegemea upande wowote.

Update 1.

Nimefanikiwa kumpata mpiganaji Fredirick Katulanda, kwanza amenithibitishia ni kweli damu imemwagika kwa kifo kimetokea kweli.
Pia ni kweli John Shibuda, jana amelala mahabusu, leo ameachiliwa kwa dhamana ndogo na kurejea mikonani mwa polisi mpaka sasa.
Amenithibitishia kuwa polisi wamethibitisha tukio hilo.

Vesion ya CCM kwa mujibu wa Katulanda, gari la mgombea wa CCM na la Mgombea wa Chadema yalipishana, Gari Chadema wameshuka 'kuchimba dawa' gari la CCM wakajipitia zao (naasume walizomeana), baada ya kupita mtu mmoja kwenye gari ya CCM akadondosha kofia, hivyo gari la CCM likasimama mbele, aliyedondosha kofia akarudi nyuma kuifuata, ndipo wafuasi wa Chadema wakamdaka na kumtembezea kichapo, wenzao kuona hivyo wakarudi kumsaidia ndipo wakavamiwa na wafuasi wa Chadema na ndipo ikafuatiav piga nikupige iliyosababisho kifo cha dereva.

Katika hatua nyingine, Katulanda ameendelea kupasha kuwa Mgombea wa CCM kwa jimbo hilo, anatafutwa na polisi kwa kosa la kumshambulia OCD wa Maswa. RPC amesema tukio la kifo ni tukio jingine, na hilo la shumbulio kwa OCD ni tukio jingine na hayana uhusiano.

Bado nafuatilia taarifa rasmi toka kwa RPC Mwanza.

Update 2
Hili ni andiko la Katulanda kwa hisani ya wanabidii.

Jeshi la Polisi limemkamata mgombea wa Chadema John Shibuda kutokana
na afuasi wake kudaiwa kumpiga mpaka kufa dreva wa gari la mgombea wa
CCM Robert Simon Kisena wote wa jimbo la Maswa Magharibi.

Tunafualia zaidi kwani habari zineeleza kuwa mbali na shibuda watu
wengine 10 wanashikiliwa na polisi huku ikielezwa kuwa mgombea wa CCM
naye anasakwa na polisi kwa kumpiga OCD wa kituo cha Maswa akimtuhumu
kuwapendelea wapinzani ambao anadai kuwa wamemuua dreva wake.

Tunaendelea.
 
Tunashukuru pasco kwa hii update! Hali inavyonesha mwaka huu watu hawana hofu wakiwa provoked wanajibu! Haya tusubiri habari kamili aliyeiripoti kasema upo kwenye scene sasa mbona anaripoti kama tetesi!
 
Back
Top Bottom