Update One.
Nimefanikiwa kumpata mpiganaji Fredirick Katulanda, kwanza amenithibitishia ni kweli damu imemwagika kwa kifo kimetokea kweli.
Pia ni kweli John Shibuda, jana amelala mahabusu, leo ameachiliwa kwa dhamana ndogo na kurejea mikonani mwa polisi mpaka sasa.
Amenithibitishia kuwa polisi wamethibitisha tukio hilo.
Vesion ya CCM kwa mujibu wa Katulanda, gari la mgombea wa CCM na la Mgombea wa Chadema yalipishana, Gari Chadema wameshuka 'kuchimba dawa' gari la CCM wakajipitia zao (naasume walizomeana), baada ya kupita mtu mmoja kwenye gari ya CCM akadondosha kofia, hivyo gari la CCM likasimama mbele, aliyedondosha kofia akarudi nyuma kuifuata, ndipo wafuasi wa Chadema wakamdaka na kumtembezea kichapo, wenzao kuona hivyo wakarudi kumsaidia ndipo wakavamiwa na wafuasi wa Chadema na ndipo ikafuatiav piga nikupige iliyosababisho kifo cha dereva.
Katika hatua nyingine, Katulanda ameendelea kupasha kuwa Mgombea wa CCM kwa jimbo hilo, anatafutwa na polisi kwa kosa la kumshambulia OCD wa Maswa. RPC amesema tukio la kifo ni tukio jingine, na hilo la shumbulio kwa OCD ni tukio jingine na hayana uhusiano.
Bado nafuatilia taarifa rasmi toka kwa RPC Mwanza.
Tunaendelea.