Hili ni lazima litolewe ufafanuzi wa kutosha. Nilikwisha andika na ninarudia tena kuwa CHADEMA wawe waangalifu na hujuma za kijasusi zinazofanywa na CCM dhidi yao.
Hii ni mipango ya kitaalam sana ya kijasusi ambapo wana CCM wanaotumwa kuanzisha vurugu hawajui kuwa wanatumwa kama mbuzi wa kafara. Wao wauawe, CCM ipate 'public sympathy' halafu wanachi waichukie CHADEMA na kuiona ni chama cha magwanda kinachoashiria vurugu na sasa zinathibitika.
Tangu shirika la kijasusi la nchi fulani kubwa lichukue tenda ya kusaidia JK aingie madarakani suala hili limeendelea kujitokeza na cha ajabu limetokea hata maeneo ambayo vurugu huwa si jambo la kawaida.
Hivi leo hii mimi nikute watu wako kwenye mkutano wa CCM halafu nipite katikati ya huo mkutano na mavazi ya CHADEMA au nikipepea bendera ya CHADEMA nakuwa natafuta kitu gani. Majasusi hawa wanajua kitu kinaitwa 'mob psychology'. Wanaelewa akilianzisha mmoja basi akili ya mtu mmoja inagawanyika na idadi ya mob yaani mfano 1/100,000. kisha 'fraction' hii ndio hufanya maamuzi, kupiga, kuvunja mbavu n.k.
Naona taratibu baada ya CCM kujua kwa uhakika kuwa wamepoteza uchaguzi huu, wanaanza kuleta mbinu za Burkina faso, Ivory Coast, Sierra Leone, Somalia na Sudan.
'Provoke them, let them seem dangerous to rule, destroy their public image, gain public sympathy'.
CCM hata mkiishiwa sera, tafadhali msimwage damu zetu na kusingizia CHADEMA. Hawa green guard na wengineo mlio nao wanayoyafanya ni sawa na suicide bombing.
Mfano kama green guard wangekuja kunivamia mimi, nisingekubali kupoteza maisha au afya yangu kwa kuwatazama tu, ningeweza kupiga mtu risasi ya kichwa, lakini mimi ndio ningeonekana muuaji.
Please please CCM huku mnakoenda sasa ni usengeni!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!