Hapo hakuna uhusiano wowote kati ya kugombea ubunge na mauaji,mauaji ni kosa la jinai,linashughulikiwa kijinai,mambo ya kugombea ni masuala ya sheria za uchaguzi,tume ndo inaweza kumtoa asigombea kama amevunja sheria za uchaguzi.Kimazingira hakuna ushahidi kuwa amevunja sheria ya uchaguzi,kwanza alikuwa jukwaani wakati tukio linatokea.Pili kama taarifa zilivyosema wafuasi wa chadema walikuwa wanaelekea kwenye eneo la mkutano wa kampeni utakaofuata ndipo wakakutana na wafuasi wa ccm ambao haikujulikana walikuwa wanaelekea wapi.Kwa hiyo ukiangalia hapo unaona kuwa chadema hawakuwafuata ccm,bali ccm waliwafuata chadema,chukulia wamekutana kama ilivyosemwa,inakuwaje kofia isidondoke sehemu yoyote ile isipokuwa pale ambapo chadema wapo?Hii inaonesha kuwa ccm wamekuwa na tabia y uchokozi halafu wanakimbilia polisi maana wanajua polisi wameshapewa maelekezo na wakuu wa chama.
Kwa kuangalia mfululizo wa matukio ya ghasia yaliyotokea mpaka hivi sasa utagundua ccm wanatoa vijisababu tu ilimradi kujikosha wakati wanaingilia mikutano na misafara ya chadema waziwazi.Polisi nao wanawaacha tu wakijua fika ni nini kitatokea.Sasa mzaa mzaa hutumbuka usaha,walizoea mambo yataishia watu kujeruhiwa,lakini sasa ni maafa.
CCM wanafanya vibaya mno kuwatumia vijana kama chambo,sasa ona mtu anapoteza maisha halafu wao wanaona ni mchezo mzuri na kutake advantage,Ifikie hatua vijana wa ccm wakatae kuwa chambo kwani ni maisha yao na wakifa hakuna atakayewakumbuka.
Kesi iende mahakamani,hakuna atakayejitoa kwani mtuhumiwa wa mauaji hajitoi kugombea bali hupelekwa mahakamani,kama ingekuwa ni kujitoa kugombea basi Chenge asingekuwa anagombea.