Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,184
SAKATA LA MAWAKILI BINAFSI: Wanasheria wa Serikali watupa lawama kwa AG
Monday, 27 December 2010 08:48 James Magai
BAADHI ya wanasheria waliowekewa pingamizi na serikali wasisajiliwe kuwa mawakili binafsi, wamelalamikia kuwa kitendo ni uonevu mkubwa. Wanasheria 50 waliwekewa pingamizi na serikali wakati wa sherehe za 42 za usajili wa mawakili wapya zilizofanyika Desemba 17, mwaka huu, viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
Waliozuiwa ni watumishi wa umma wanaofanya shughuli za kisheria chini ya ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) na walioko kwenye mashirika, taasisi na wakala mbalimbali wa serikali.
Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali (DAG), George Masaju, alilieleza Mwananchi kuwa wanasheria hao wamewekewa pingamizi hilo kwa sababu walikiuka sheria Namba 4 ya mwaka 2005 ya Ofisi ya AG.
Masaju alisema kwa mujibu wa sheria hiyo na kanuni zake za mwaka 2006, wakili wa serikali, ofisa wa sheria au mtumishi yeyote anayefanya shughuli za kisheria kwenye shirika, taasisi au wakala wa serikali ni kinyume cha sheria kuwa wakili wa kujitegemea.
Alisema kitendo walichofanya waombaji hao ambao ni watumishi wa umma, ni ukiukaji sheria hiyo na kanuni zake hususan kifungu cha 8 (2) cha kanuni.
Alisema kwa mujibu wa kifungu hicho, wakili wa serikali, mwanasheria au ofisa yeyote anayefanya shughuli za kisheria, haruhusiwi kufanya shughuli za uwakili binafsi.
Hata hivyo, wakizungumza na Mwananchi mwishoni mwa wiki iliyopita, baadhi ya wanasheria hao waliowekewe pingamizi walisema kitendo walichofanyiwa ni uonevu na kwamba, walifanyiwa kwa nia mbaya.
Walalamikaji hao ambao hawakutaka kutajwa, pia walimtupia lawama Jaji Mkuu, Augustino Ramadhan, ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Elimu ya Sheria kwa kukubaliana na pingamizi hiyo na kuwaengua kwenye orodha ya waombaji waliosajiliwa siku hiyo.
Mawakili hao walidai kuwa, hata serikali ilijua pingamizi lao halikuwa na msingi na kwamba, ndio maana walivizia na kulitoa dakika za mwisho wakati wakisubiri kusajiliwa na kukabidhiwa vyeti.
Walidai kuwa, wakati wakifanyiwa usaili mbele ya baraza hilo, AG au mwakilishi wake alikuwepo maana yeye ni mjumbe muhimu ambaye asipokuwepo yeye au mwakilishi wake hakuna usaili unaofanyika.
Tulimaliza usaili Septemba mwaka huu, lakini la ajabu serikali inakuja kutuwekea pingamizi siku ya usajili, sasa muda wote huo ilikuwa wapi? alihoji mmoja wamawakili hao.
Kuhusu maelezo ya DAG kuwa, hatua hiyo ni kinyume cha sheria, mlalamikaji huyo alisema kinachozuiliwa na sheria hiyo ni kufanya shughuli za uwakili binafsi sio kusajiliwa na kutambuliwa na Chama cha Wanasheria nchini (TLS).