CalvinKimaro
JF-Expert Member
- Sep 11, 2017
- 245
- 314
Nijuavyo ofisi ya kiongozi mkuu mstaafu ni ofisi ya umma. Yaani public office. Na kwa mujibu wa katiba yetu public office ni mali ya serikali iliyo madarakani. Haiwezekani pawe na ofisi ya umma ambayo Mtendaji mkuu wake ni mpinzani wa serikali iliyo madarakani!
Tumeshuhudia mawaziri wakuu wastaafu wawili wakiipinga serikali iliyo madarakani na bado wakaendelea kuwa watendaji wakuu wa ofisi ya umma. Ni kioja!
Tuchukulie mifano hii: ofisi ya mkuu wa Mkoa na ya mkuu wa Wilaya nazo ni ofisi za umma. Hivi itawezekana RC au DC awe mpinzani wa serikali na asalie ofisini?
Nadhani inatupaswa kuitazama upya sheria inayohusu viongozi wakuu wastaafu. Mstaafu aliyepewa ofisi ya umma akiamua kuipinga serikali basi arejeshe ofisi ya umma serikalini. Aendelee na utaratibu wake mpya.
Naomba kutoa hoja!