Sakata la Mpina na Kinachoendelea Kenya: Kila Mtanzania Anamlaumu Mwenzie

Stuxnet

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2011
Posts
13,417
Reaction score
23,310
"Kila mtanzania analaumu watanzania wengine ni wajinga hawaleti mabadiliko, na hao wanao laumiwa nao wanalaumu" - min -me

Kwa takriban juma zima sasa suala la kashfa ya sukari ime trend sana kwenye mitandao ya jamii na JF ikiwa ni moja wapo. Hatimaye sakata la sukari likiwa linaendelea likakutana na trending ya Genearation Z ambayo inapingana na Finance Bill ya Kenya ya 2024, kisha kusababisha uvunjivu wa amani na mali za Wakenya.

Machafuko yaliyotokea Kenya yamewavutia sana wanaharakati wa mabadiliko kutoka Tanzania. Kuna ambao wanatamani maandamano yangefanyika kupinga kitendo cha bunge kumuadhibu Luhaga Mpina.

Katika mitandao ya JF na Twitter (X) kila mtu analaumu kuwa Watanzania ni makondoo au waoga au maiti kwa vile hawawezi kufanya kama Gen Z ya Kenya.

Alichogundua min -me na mimi pia ni kwamba wote wanaokosoa wenzao nao wanakosolewa na wengine. Hakuna yeyote anayesema kesho ataingia barabarani kukosoa chochote.

Watanzania wanachojua ni kunyooshea vidole wengine lakini wakiitwa kwenye maandamano hawatoki. Tumeshuhudia maandamano ya CHADEMA yalivyokuwa na watu wachache

Nini KIFANYIKE?
 
Nafikiri tutumie njia ya amani kabisa ya kufanya shida zetu zitatuliwe, tofauti kabisa na maandamano yanayoonekana kwa ukanda huu wa africa ni kosa la uhaini.
 
Always sisi watanzania ni keyboard worriors, wanafiki ,wajuajii. Tuna raia mapunguani sana. Sijui tuna shida gani yaani mambo ya kijinga Huwa tunayapa mda mwingi sana huko vitu vya msingi hatufanyi tunaishia kulalamika na kulaumu Serikali
 
"Kila mtanzania analaumu watanzania wengine ni wajinga hawaleti mabadiliko, na hao wanao laumiwa nao wanalaumu" - min -me

Kwa takriban juma zima sasa suala la kashfa ya sukari ime trend sana kwenye mitandao ya jamii na JF ikiwa ni moja wapo. Hatimaye sakata la sukari likiwa linaendelea likakutana na trending ya Genearation Z ambayo inapingana na Finance Bill ya Kenya ya 2024, kisha kusababisha uvunjivu wa amani na mali za Wakenya.

Machafuko yaliyotokea Kenya yamewavutia sana wanaharakati wa mabadiliko kutoka Tanzania. Kuna ambao wanatamani maandamano yangefanyika kupinga kitendo cha bunge kumuadhibu Luhaga Mpina.

Katika mitandao ya JF na Twitter (X) kila mtu analaumu kuwa Watanzania ni makondoo au waoga au maiti kwa vile hawawezi kufanya kama Gen Z ya Kenya.

Alichogundua min -me na mimi pia ni kwamba wote wanaokosoa wenzao nao wanakosolewa na wengine. Hakuna yeyote anayesema kesho ataingia barabarani kukosoa chochote.

Watanzania wanachojua ni kunyooshea vidole wengine lakini wakiitwa kwenye maandamano hawatoki. Tumeshuhudia maandamano ya CHADEMA yalivyokuwa na watu wachache

Nini KIFANYIKE?
Maandamano yakishaitwa ya chadema tu hatuwezi kutokea, tunataka maandamano ya wananchi. Tumechoka kupigania hoja za vyama vya siasa. Tunataka kupigania hoja zetu wananchi. Wanaharakati wa wananchi kazi kwao.
 
Wafanyabishara warudi maofisini kwao, wakubaliane na kodi, wao wapandishe bidhaa basi

Maisha yakiwa magumu sana kwa mlaji wa mwisho ataamua moja, ama aitafute haki yake ya kuishi na ama akae hivyo bila kula

Kinachosumbua sana ni watu wa huku chini basi, maana wao kugandamizwa haiwapi shida, siku wakiona iko shida, wataamka
 
"Kila mtanzania analaumu watanzania wengine ni wajinga hawaleti mabadiliko, na hao wanao laumiwa nao wanalaumu" - min -me

Kwa takriban juma zima sasa suala la kashfa ya sukari ime trend sana kwenye mitandao ya jamii na JF ikiwa ni moja wapo. Hatimaye sakata la sukari likiwa linaendelea likakutana na trending ya Genearation Z ambayo inapingana na Finance Bill ya Kenya ya 2024, kisha kusababisha uvunjivu wa amani na mali za Wakenya.

Machafuko yaliyotokea Kenya yamewavutia sana wanaharakati wa mabadiliko kutoka Tanzania. Kuna ambao wanatamani maandamano yangefanyika kupinga kitendo cha bunge kumuadhibu Luhaga Mpina.

Katika mitandao ya JF na Twitter (X) kila mtu analaumu kuwa Watanzania ni makondoo au waoga au maiti kwa vile hawawezi kufanya kama Gen Z ya Kenya.

Alichogundua min -me na mimi pia ni kwamba wote wanaokosoa wenzao nao wanakosolewa na wengine. Hakuna yeyote anayesema kesho ataingia barabarani kukosoa chochote.

Watanzania wanachojua ni kunyooshea vidole wengine lakini wakiitwa kwenye maandamano hawatoki. Tumeshuhudia maandamano ya CHADEMA yalivyokuwa na watu wachache

Nini KIFANYIKE?
Ni mada iliyoshiba vizuri sana hii. Pongezi kwako mkuu 'Stuxnet' na mkuu 'min-me'.
Nitachangia mawazo nionavyo mimi hapo baadae.
Ila sikubaliani moja kwa moja na maneno yaliyotumika katika mistari hii: Nitaeleza kwa nini sikubaliani na maneno hayo.
Katika mitandao ya JF na Twitter (X) kila mtu analaumu kuwa Watanzania ni makondoo au waoga au maiti kwa vile hawawezi kufanya kama Gen Z ya Kenya.
Baadae kidogo.
 
Nafikiri tutumie njia ya amani kabisa ya kufanya shida zetu zitatuliwe, tofauti kabisa na maandamano yanayoonekana kwa ukanda huu wa africa ni kosa la uhaini.
Sasa sijui nitoe alama gani hapa. Nusu ya hoja natamani kuipa alama ya 'nzuri', lakini hiyo ya "uhaini" naikataa katakata!
 
Serikali nyingi za Africa zinaona maandamano ni kama uhaini.
 
Nafikiri tutumie njia ya amani kabisa ya kufanya shida zetu zitatuliwe, tofauti kabisa na maandamano yanayoonekana kwa ukanda huu wa africa ni kosa la uhaini.
Maandamano kama yale ya CHADEMA ya Kistaarabu ya AMANI bila kuvunjavunja Nchi na kupora na kuchoma Maduka ya Wananchi.
 
Kwa tulipo fikia sioni kama tunahitaji chama cha siasa kutuvusha , unajua matumbo yana njaa ,mda wowote mbwa anaweza tupiwa mfupa , akaacha kulinda wezi wakavunja akang'ang'ana na mifupa tu , tukapigwa tukio😁😁😁😁.
 
Kuna ukweli fulani Mkuu,lakini mimi bado nitaendelea kuamini katika Siasa za Vyama hata kama kuna dalili za Kiongozi kulambishwa kibuyu cha Asali.

Pili hao GenZ wa Kenya ni Wanaharakati wengine wametoka Vyuoni sisi hawa wa kwetu ni watu wa kudandia matukio kama sasa hivi wameacha hata KATIBA MPYA wanampamba Luhaga Mpina na kumlaani Msomali wa watu.
 
Mtu yoyote anaye simamia haki awe ccm au chadema mimi nitasimama naye
 
"Kila mtanzania analaumu watanzania wengine ni wajinga hawaleti mabadiliko
Siyo kweli. Si "kila mTanzania analaumu waTanzania wengine..." Kuna kundi kubwa sana linalonufaika na mfumo uliopo, ambalo ni kundi linalotawala chini ya CCM. Wao ndio hawataki kabisa mabadiliko ya aina yoyote nje ya CCM.
Ni hivi (na nitajaribu kueleza kwa kifupi hii hoja).Nchi yetu imekuwa chini ya chama kimoja (CCM) kwa muda mrefu sana tokea uhuru. CCM ilivyo undwa, imeenea kote hadi kwenye mtaa. CCM iliyo undwa kwa 'network' hii ilikuwa ni CCM kabambe sana, na malengo yake yalikuwa ni tofauti kabisa na haya yaliyomo ndani ya chama hicho. Licha ya mabadiliko ndani ya chama na malengo yake, lakini mfumo huu umebakia vile vile, na wengi wa wananchi, hasa huko vijijini bado wanaamini iliyo yasimamia CCM ya jana/juzi, wananchi wanagoma kubadili akili zao kuona vinginevyo.
Mbaya zaidi, CCM inawachanganya wananchi hao - chukulia CCM aliyokuwa akiiongoza Magufuli (acha ukicha wake pembeni), tazama hayo aliyokuwa akiyapigia kelele nyingi, hasa yale ya wanyonge.
CCM hiyo, siyo hii ya "Kazi iendelee" ya 'Chura Kiziwi'

Mchanganyiko maalum, au siyo? CCM yenyewe ni "Mchanganyiko maalum" huko ndani yake. Leo mama 'Chura Kiziwi' analo kundi lake huko huko ndani ya CCM; na lile kundi la CCM ya Jiwe wakabaki yatima; lakini nao wakitegemea kesho atatokea Jiwe mwingine. CCM inawapa kila kundi matumaini ya kesho. Hakuna kundi linalotaka kutia kitumbua mchanga.
Hakuna atakayetaka kutoka mbele kwenda kuandamana.

Nje ya CCM:

Nani, CHADEMA? Inalo kundi kubwa la kutosha kuwatikisa makundi yote mawili ndani ya CCM? Happana. Hawana.

Hata lile kundi lililomuunga mkono Magufuli, pamoja na kutomtaka 'Chura', hawawezi kuwaunga mkono CHADEMA, kwani kufanya hivyo ni kupoteza nafasi yao ndani ya CCM.
CCM ya "Chura Kiziwi" ilitegemea kuwavuta CHADEMA, kwani wana mambo yanayofanana katika maeneo mengi. Muungano huu huenda ume-'abort' kwa sababu mbalimbali, ambazo siwezi kuzieleza leo.

Kutokana na hali hiyo, huwezi kutegemea waTanzania walioko CHADEMA kulianzisha na kupata mafanikio, kwa sababu 'inherently' CHADEMA haijawahi hata siku moja kuingilia muundo wa CCM hadi huko mitaani na kugeuza akili za waTanzania waione CCM kuwa tofauti na walivyowahi kuiona tokea waijue.

Tayari nimekwisha andika gazeti hapa...

Enzi za Moi huko Kenya, ulisikia fyokofyoko yoyote ile toka kwa yeyote?
KANU ilipovurugwa na NARC; hali ikabadilika kabisa!

Na usisahau: Ukabila huko una mchango mkubwa sana katika hali za nchi hiyo.

Ndiyo, hata kupevuka kwao, hasa kielimu kumewafumbua macho sana.

Ndiyo, kuna viongozi wa kisiasa waliojitoa mhanga kwelikweli katika kutafuta mabadiliko huko.

Mwisho: WaTanzania ni watu majasiri sana... Wanapoelewa jambo hakuna anayeweza kuwatisha. Si kaburu, mreno wala Nduli Idd Amin.

Vuta subira kidogo, utauona ujasiri wao ulivyo, bila hata kudondosha tone la damu la mTanzania yeyote.

'Chura Kiziwi' kawapa fursa ya kuuonyesha ujasiri wao.
 
Back
Top Bottom