Sakata la Mtoto wa Rose Nungu (MunaLove), Linaumiza Sana Moyo

Sakata la Mtoto wa Rose Nungu (MunaLove), Linaumiza Sana Moyo

Hashpower7113

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2011
Posts
1,353
Reaction score
2,142
Mtoto Patrick ameshatangulia mbele za haki lakini huku nyuma, moto unawaka. Mama yake, Muna Love amesababisha kizaazaa kabla hata mwanaye hajapumzishwa kwenye nyumba yake ya milele, machozi jasho na damu vinachuruzika.

Muna anadai mtoto ni wa Casto Dickson, yule mtangazaji wa Siz Kitaa (Clouds), Casto anadai mtoto ni wake lakini upande wa pili, yupo baba halisi, Peter Zacharia ambaye anavyo vithibitisho vyote vya kisheria kwamba Patrick ni mwanaye.

Muna anataka yeye ndiye achague wapi anamzika mwanaye, Zacharia anadai yeye ndiyo baba halisi wa mtoto kwa hiyo ndiye atakayechagua wapi pa kumzika mwanaye na azikweje. Muna anasisitiza kwamba mtoto ni wake na msiba ni wake kwa hiyo yeye ndiye atakayemzika mwanaye.

Kuna misiba miwili kwa maiti ya mtoto Patrick, Muna ameweka msiba nyumbani kwake, Zacharia pia ameweka msiba nyumbani kwake. Waombolezaji wamechanganyikiwa, hawaelewi waende kwa Muna au kwa Zacharia.

Zacharia anasema mwanaye akizikwa bila ridhaa yake, yupo tayari hata kufuata sheria ili mwanaye akafukuliwe na azikwe anapopataka yeye, kwa sababu yeye ndiye baba halisi. Anavyo vithibitisho, kikiwemo cheti cha ndoa na Muna na anaeleza kwamba hajawahi kumuacha mkewe huyo, ile yeye ndiye aliyekimbia nyumbani kwao, mtoto akiwa na miaka mitatu.

Nini hatma ya malaika Patric ambaye maskini ya Mungu hana hatia katika hili? Maiti yake inagombewa na kuna hatari akizikwa kabla ya hizi tofauti hazijapatiwa ufumbuzi, mwili wake utafukuliwa na kuzikwa upya.

Yajayo yanahuzunisha sana!


Habari zaidi, soma=>TANZIA: Mtoto wa Munalove Patrick Peter Zacharia Komu almaarufu Partsmartboy Afariki dunia
 
Aisee kwa sisi wachaga hatuwezi kukubali mtoto wetu akazikwe na mama. Huyu muna ni tapeli wa mapenzi na pesa, mtoto ni mali ya baba. Na tutahakikisha tunampeleka moshi tukampumzishe mtoto wetu
Kazi kwelikweli, mnamtesa marehemu
 
wanaume ifike wakati tukubali kulea watoto tunaoletewa kwa kuwa hawa wanawake washaamua hivyo na ikifika wanawang'ang'ania basi tuwabe zawadi na hasa pale inapotokea mzazi mwenzio hakukuhusisha kwa matunzo au hakukwambia ukweli toka mwanzo.
tukumbuke kuwa tuna mbegu nyingi tumezitupa bila sababu hivyo isiwe dili kivile kama mtu kang'ang'ania mtoto wake na hasa katika atua za msiba.
vinginevyo mtoto kama ni wako ipo siku atarudi tu.
 
Hakuna marehemu anayeteswa. Huu mwili umesha kuwa mfu haujui lolote yanayoendea ni upuuzi tu wa walioshindwana katika ndoa na umalaya!
Hata mfu anatakiwa kuheshimiwa mkuu, ndiyo maana tunawastiri wafu kwenye nyumba zao za milele Mkuu
 
zoefu unaonyesha watoto wa namna hii huwa hawana furaha siku zote na hasa wakiwa hawajui asili yao sahihi. tunajidanganya kwa kuwapa baba wengine lakini nafsi zao huwa zinaelewa wapi walikotoka na zinawaletea maumivu ya ndani makubwa mno kupita kiasi.
matokeo yake huwa na roho ya kisasi na kujikataa na wengine kuishia kuwa malaya na wakati mwingine huwa wanaweza kujiua.
lakini pia wapo ambao hubadilika na kuwa na upendo mkubwa kwa jamii kwa kuwa ndio wanaoiamini.
hivyo wakinamama acheni hii mchezo.
 
Back
Top Bottom