Sakata la Mwabukusi , mahakama kuu yaipiga stop tena kamati ya maadili ya mawakili

Sakata la Mwabukusi , mahakama kuu yaipiga stop tena kamati ya maadili ya mawakili

carbohydates

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2026
Posts
260
Reaction score
607
Mahakamani Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu Dodoma, kwa mara nyingine tena leo, Jumatatu Oktoba 19.2026 imetoa amri dhidi ya Kamati ya Taifa ya Maadili ya Mawakili kusitisha usikilizwaji wa shauri lililofunguliwa kwenye Kamati hiyo dhidi ya Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) Wakili Boniface Mwabukusi

Amri hiyo ya Mahakama Kuu, imetolewa na jopo la Majaji watatu (3) wakiongozwa na Jaji Amir Mruma, ambapo Kamati ya Taifa ya Maadili ya Mawakili imetakiwa kusubiri hadi pale Mahakama Kuu itakapotoa uamuzi wa shauri la Kikatiba lililofunguliwa, ambalo pamoja na mambo mengine linapinga mchakato wa kumuondolea UWAKILI Rais wa TLS Wakili Boniface Mwabukusi, mchakato ambao unaendelea mbele ya Kamati hiyo lililoletwa na Wakili Chacha Mwita Nashon

Jopo la Mawakili linalomtetea Wakili Mwabukusi kwenye mashauri hayo linaongozwa na Wakili Mwandamizi Mpale Mpoki, ambapo baada ya uamuzi huo Mawakili hao wa utetezi wameeleza matumaini yao kwa Kamati ya Taifa ya Maadili ya Mawakili kuzingatia kile kilichoamuliwa na Mahakama Kuu kama msingi wa kuheshimu Utawala wa Sheria.

Hii ni mara ya pili kwa Mahakama Kuu kutoa amri ya aina hiyo kuhusu shauri hilohilo linamomkabili Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) Wakili Boniface Mwabukusi.

Kupitia shauri lililopo kwenye Kamati ya Taifa ya Maadili ya Mawakili, Wakili Mwita 'anataka' Wakili Mwabukusi avuliwe UWAKILI wake kutokana na kile anachodai kuwa amekiuka Kanuni za Mawakili kutokana na kauli zake alizowahi kuzitoa siku za nyuma kuhusu mwenendo wa kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Tundu Lissu ambaye pia ni Rais wa zamani wa TLS

Endapo, Wakili Mwabukusi atakutwa na hatia kwenye Kamati hiyo na kuvuliwa UWAKILI, maana yake moja kwa moja atakuwa anakosa sifa ya kuendelea kuwa Rais wa TLS.
Chanzo : Royal tv

Mahakamani Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu Dodoma, kwa mara nyingine tena leo, Jumatatu Oktoba 19..webp
​
 
Wanaohubiri wenzo waheshiklmu utawala wa sheria wao ndio wanaukanyaga
 
Back
Top Bottom