Tatizo credibility ya Esther ndogo sana kutokana na historia yake.Ni mwanafunzi mtukutu(kaingia na kibomu,ame dare kunyoa kiduku shule strict,yaani ni yule mwanafunzi anayeenjoy kuwajaribu walimu/ kusumbua walimu/ hana nidhamu!!)
Maswali ninayojiuliza:
1.Kama ni mwanafunzi mzuri ilikuwaje yuko bwenini muda wa kuwa madarasani!(eti alichelewa kwenda kuchukua chakula sijui...kwann awe nyuma ya ratiba ya shule!)
2. Tukio la kudisappear disapper na baadaye kutoroka lilitokea baada ya kukutwa na kibomu kwenye mtihani(kwa mujibu wa maelezo ya wiki zilee),mwalimu Jimmy anaingiaje hapo?
3.Iweje isemwe aliokotwa na muuza mkaa.Mbona muuza mkaa baada ya kumuokota mtu hakumpeleka polisi au hata kwa viongozi wa kijiji au mtaa au kitongoji?Na kama binti alitoroka ili kujiokoa na unyanyasaji wa mwl Jimmy au shule kwa ujumla kwanini hakwenda nyumbani kwao au hata kwa ndugu ikiwa wazazi ni wakali?Si alikuwa anaokoa maisha/ usalama wake?sasa kwanini asiende sehemu sahihi baada ya ku escape shule? If at all!!
4 Kwa kawaida mashuleni na hasa boarding walimu wa nidhamu huchukiwa sana( ni utoto tu lakini ukikua unagundua walimu wale walikuwa na mchango sana kutufanya tuwe bora), na kweli wengi ni wafuatiliaji.Na kwa za tabia Esther tulizoambiwa watz,ni wazi kwa vyovyote alikuwa subject wa mwalimu wa nidhamu mara kwa mara.Hivyo isije ikawa anatumia mwanya huu kujikosha kwa kumuangushia msala mwalimu wa nidhamu.
5.Ile sentensi ya barua ya Esther kuwa sijui mwl jimmy alimfanya awe na maisha magumu shule iangaliwe kwa upana.Huenda maisha magumu kwa huyu binti ilikuwa ni kule kufuatiliwa kinidhamu.
Potentially haka kabinti ni manipulative.Suala hili litazamwe vizuri wanajamii.