philltaya
Member
- Sep 5, 2015
- 53
- 11
Mkuu wa wilaya ya Mvomero nashukuru kwa kulifuatilia swala hilo la ukatili alilofanyiwa mama Fatuma Hasani Diawi, lakini katika swala hilo polisi wanataka kujenga kitu mpaka sasa, baada ya kulifikisha hilo swala mahakamani, wanamtaarifu mlalamikaji kuwa taarifa zote atapata kutoka kwa mtendaji wa kijiji sasa je hii ni sheria mpya au ndiyo mwongozo wa kipolisi, au mtendaji ni hakimu?
Kwa namna hii mkiwakumbatia wafugaji wananchi wataendelea kuteseka polisi kazi yenu ni kukamata mtuhumiwa kumuhoji na kumfikisha panapo stahili baada ya kujiridhisha na kuviachia vyombo vingine vifanye kazi. Ombi mkuu wa wilaya tafadhali fuatilia mpaka mwisho swala la huyu mama ili aweze pata haki, maana inaonekana kama polisi wanataka kucheza na maisha ya watu. Wasitumie mwanya wa huyo mama kutokujua cha kufanya na kumdhulumu haki yake, watendaji wa vijiji timizeni majukumu yenu hacheni ubabaishaji juu ya maisha ya watu.
Pia nikuombe mkuu wa wilaya kwa kazi hiyo hiyo ambayo umeifanya Doma tafadhari fika Menge/Vianzi.