Sakata la Ngorongoro; Tusioelewa vizuri tueleweshwe

music mimi

JF-Expert Member
Joined
Jun 16, 2013
Posts
485
Reaction score
876
Uelewa wangu mpaka sasa ni kwamba Ngorongoro ni hifadhi na eneo la urithi wa dunia. Ni eneo lililotengwa kwa sababu ya upekee wa binadamu ambao ni Masai wanaishi na wanyamapori uku wakifanya shughuli zao in a traditional way.

Serikali inataka kuwaondoa Wamasai wote Ngorongoro kwa sababu ya kulinda mazingira sababu kubwa ni wamasai wamekuwa wengi na wanafanya shughuli zinazoharibu mazingira ikiwemo kujenga nyumba za kisasa, kufunga kengele ng'ombe, kuwa na mifugo wengi kupitiliza, kuharibu asili ya creta nk.

Jambo nilisiloelewa mpaka sasa ndio maana nahitaji ufafanuzi.

1. Kwa nini serikali inawaondoa wamasai wote na sio kuwapunguza ili eneo libaki na ile concept yake ya binadamu kuishi na wanyama?

2. Ngorongoro na Loliondo vinaingiliana vipi? Maana ikitajwa Ngorongoro inatajwa na Loliondo, so mimi binafsi inanichanganya au vyote vinapatikana eneo moja?

3. Nimesikia kuna mwarabu anatajwa kwamba anataka kumilikishwa eneo, huyo mwarabu anamilikishwa hifadhi nzima ya Ngorongoro? Mbona ni eneo kubwa sana anataka kulifanyia nini mbali na kuwinda?

4. Nimesikia Ngorongoro kuna watu zaidi ya laki moja na mifugo zaidi ya million. Kama ni kweli ina-make sense kabisa awa watu kukaa kwenye hifadhi ni wengi sana. Ila ili kundi mbona ni kubwa sana wanaweza kweli kuliamisha kwa usafiri wa magari na kuwapa nyumba za kuishi?

Naomba wasioelewa kama Mimi tusaidiwe kupata majibu maana tunaona tu majeruhi vifo na discussion nzito. Lakini kuna vitu hatuelewi kabisa ikizingatiwa imeshaingia siasa basi inakuwa ligi ya kisiasa wengine tunashindwa kuupata ukweli.
 
Viongozi wa Afrika niwa jinga una ua raia wako kwa manufaa ya tumbo lako kwa uroho wa pesa na kuona waarabu ni muhimu Sana
 
3. Nimesikia kuna mwarabu anatajwa kwamba anataka kumilikishwa eneo, huyo mwarabu anamilikishwa hifadhi nzima ya Ngorongoro? Mbona ni eneo kubwa sana anataka kulifanyia nini mbali na kuwinda?
Shangaa kwa nini yule mzungu (Thomson?) aliyeko jirani na mwarabu hatajwi kabisa kwenye sakata hizi wakati na yeye amemegewa eneo kubwa sana huko Loliondo.
 
Nachoelewa Kuna tarafa ya loliondo ndan ya ngorongoro na kwenye tarafa Hii ndiko wamasai hawatakiwi
 
Kweli huelewi!.

Mpango wa sasa ni kuwahamisha wote au kuwapunguza, hapo ndipo hujui na hukutaka kujua!.

Alafu tofautisha Loliondo na Ngorongoro kuna watu mnashabihisha hizi sehemu mbili tofauti wakati zina issues tofauti.
 
Ngorongoro creta wamasai wanahamishwa. Maana binadamu na mifugo wamekuwa wengi, kiuhalisia wanyama wako hatarini kutoweka. Mpango wa serikali kuwahamisha umekaa vizuri kwa maslahi ya Taifa.

Loliondo ni kuweka mipaka ya Eneo ambalo litakuwa pori TENGEVU kwa kusudio endelefu la kuondoa shughuli za binadamu kama ufugaji.

Kabla ya hapo kulikuwa na rojo makazi ya muda ya wafugaji ambayo pia yamekuwa mengi na kuhatarisha usalama wa wanyama pori.
 
Ndiyo mleta mada anataka wewe unayeelewa utoe ufafanuzi. Hujaelewa nn hapo?
👇🏾Umeelewa..?
Ngorongoro creta wamasai wanahamishwa. Maana binadamu na mifugo wamekuwa wengi, kiuhalisia wanyama wako hatarini kutoweka. Mpango wa serikali kuwahamisha umekaa vizuri kwa maslahi ya Taifa.
Loliondo ni kuweka mipaka ya Eneo ambalo litakuwa pori TENGEVU kwa kusudio endelefu la kuondoa shughuli za binadamu kama ufugaji.
Kabla ya hapo kulikuwa na rojo makazi ya muda ya wafugaji ambayo pia yamekuwa mengi na kuhatarisha usalama wa wanyama pori.
 
Uelewa wangu mpaka sasa ni kwamba Ngorongoro ni hifadhi na eneo la urithi wa dunia. Ni eneo lililotengwa kwa sababu ya upekee wa binadamu ambao ni Masai wanaishi na wanyamapori uku wakifanya shughuli zao in a traditional way.

Serikali inataka kuwaondoa Wamasai wote Ngorongoro kwa sababu ya kulinda mazingira sababu kubwa ni wamasai wamekuwa wengi na wanafanya shughuli zinazoharibu mazingira ikiwemo kujenga nyumba za kisasa, kufunga kengele ng'ombe, kuwa na mifugo wengi kupitiliza, kuharibu asili ya creta nk.

Jambo nilisiloelewa mpaka sasa ndio maana nahitaji ufafanuzi.

1. Kwa nini serikali inawaondoa wamasai wote na sio kuwapunguza ili eneo libaki na ile concept yake ya binadamu kuishi na wanyama?

2. Ngorongoro na Loliondo vinaingiliana vipi? Maana ikitajwa Ngorongoro inatajwa na Loliondo, so mimi binafsi inanichanganya au vyote vinapatikana eneo moja?

3. Nimesikia kuna mwarabu anatajwa kwamba anataka kumilikishwa eneo, huyo mwarabu anamilikishwa hifadhi nzima ya Ngorongoro? Mbona ni eneo kubwa sana anataka kulifanyia nini mbali na kuwinda?

4. Nimesikia Ngorongoro kuna watu zaidi ya laki moja na mifugo zaidi ya million. Kama ni kweli ina-make sense kabisa awa watu kukaa kwenye hifadhi ni wengi sana. Ila ili kundi mbona ni kubwa sana wanaweza kweli kuliamisha kwa usafiri wa magari na kuwapa nyumba za kuishi?

Naomba wasioelewa kama Mimi tusaidiwe kupata majibu maana tunaona tu majeruhi vifo na discussion nzito. Lakini kuna vitu hatuelewi kabisa ikizingatiwa imeshaingia siasa basi inakuwa ligi ya kisiasa wengine tunashindwa kuupata ukweli.
Ni kweli huelewi na wengi hawaelewi japo wanazungumzia ishu hii.
Kabla kuzungumzia migogoro iliyopo inabidi nikueleweshe kidogo kuhusu wilaya ya Ngorongoro.
Wilaya ina tarafa tatu yaani Tarafa ya Ngorongoro ambayo Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro ipo ndani yake,Tarafa ya Sale na Tarafa ya Loliondo.
Makao makuu ya Wilaya yapo Loliondo.
Kutoka Arusha hadi Loliondo ni takribani kilometa 324.
Na kutoka Arusha hadi Mamlaka ni takribani km 140.
Hadi hapo ushajua historia kidogo na umbali uliopo baina ya Tarafa ya Loliondo na ile ya Ngorongoro.
Tarafa hizi mbili zimetenganishwa na tarafa ya Sale.
Mgogoro.
Mgogoro upo wa aina mbili.
Mosi ni kati ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro na Wamasai wanaoishi ndani ya Mamlaka.
Na hawa ndio wanaohamishwa na serikali kwenda Handeni.
Kwa hiyo ishu ya kuhamisha Wamasai kwenda Handeni inawahusu wale wa Tarafa ya Ngorongoro tu!
Mgogoro wa pili ni ule wa wananchi wa
Loliondo hasa kata za Arash,Soitsambu, Ololosokwani,Oloipiri Oloirien na maeneo dhidi ya Mwarabu wa OBC.
Km za mraba zipatazo 1500 zinamegwa kwenye maeneo wanaoishi wananchi hao kwa ajili ya ushoroba wa wanyama(kati ya Serengeti na Masai Mara huko Kenya).
Wenyeji wenyewe wanadai sio kwa ajili ya ushoroba bali ni kwa ajili ya OBC.
Mgogoro huu ni wa muda mrefu sasa.
Hao wa Loliondo wenyewe hawapelekwi Handeni kama watu wasiojua wanavyozungumza ama wanavyopotosha.
Sasa naamini umeelewa kidogo.
Nyongeza ni kuwa vurugu zilizotokea zilikuwa loliondo na sio tarafa ya Ngorongoro.
Ahsanta
 
Kweli huelewi!.

Mpango wa sasa ni kuwahamisha wote au kuwapunguza, hapo ndipo hujui na hukutaka kujua!.

Alafu tofautisha Loliondo na Ngorongoro kuna watu mnashabihisha hizi sehemu mbili tofauti wakati zina issues tofauti.
Ndiyomana kweli haelewi na ameuliza oli aelewe ni,muda wako sasa kutuelewesha kama unajuwa hili kwa mapana.
 
Kweli huelewi!.

Mpango wa sasa ni kuwahamisha wote au kuwapunguza, hapo ndipo hujui na hukutaka kujua!.

Alafu tofautisha Loliondo na Ngorongoro kuna watu mnashabihisha hizi sehemu mbili tofauti wakati zina issues tofauti.
Ndio umuel basi na sisi wengine tupate uelewa
 
Nashukuru sana kwa Elimu na ufafanuzi

hii issue imevamiwa na Wanasiasa na wanaharakati na kila mmoja anaingiza propaganda kupotosha
Ni kweli huelewi na wengi hawaelewi japo wanazungumzia ishu hii.
Kabla kuzungumzia migogoro iliyopo inabidi nikueleweshe kidogo kuhusu wilaya ya Ngorongoro.
Wilaya ina tarafa tatu yaani Tarafa ya Ngorongoro ambayo Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro ipo ndani yake,Tarafa ya Sale na Tarafa ya Loliondo.
Makao makuu ya Wilaya yapo Loliondo.
Kutoka Arusha hadi Loliondo ni takribani kilometa 324.
Na kutoka Arusha hadi Mamlaka ni takribani km 140.
Hadi hapo ushajua historia kidogo na umbali uliopo baina ya Tarafa ya Loliondo na ile ya Ngorongoro.
Tarafa hizi mbili zimetenganishwa na tarafa ya Sale.
Mgogoro.
Mgogoro upo wa aina mbili.
Mosi ni kati ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro na Wamasai wanaoishi ndani ya Mamlaka.
Na hawa ndio wanaohamishwa na serikali kwenda Handeni.
Kwa hiyo ishu ya kuhamisha Wamasai kwenda Handeni inawahusu wale wa Tarafa ya Ngorongoro tu!
Mgogoro wa pili ni ule wa wananchi wa
Loliondo hasa kata za Arash,Soitsambu, Ololosokwani,Oloipiri Oloirien na maeneo dhidi ya Mwarabu wa OBC.
Km za mraba zipatazo 1500 zinamegwa kwenye maeneo wanaoishi wananchi hao kwa ajili ya ushoroba wa wanyama(kati ya Serengeti na Masai Mara huko Kenya).
Wenyeji wenyewe wanadai sio kwa ajili ya ushoroba bali ni kwa ajili ya OBC.
Mgogoro huu ni wa muda mrefu sasa.
Hao wa Loliondo wenyewe hawapelekwi Handeni kama watu wasiojua wanavyozungumza ama wanavyopotosha.
Sasa naamini umeelewa kidogo.
Nyongeza ni kuwa vurugu zilizotokea zilikuwa loliondo na sio tarafa ya Ngorongoro.
Ahsanta
 
Nyongeza ni kuwa vurugu zilizotokea zilikuwa loliondo na sio tarafa ya Ngorongoro.
Mkuu asante kwa ufafanuzi mzuri hata mm umeniongezea kitu kichwani. Kwahiyo vurugu zinafanywa na wananchi wa tarafa ya Loliondo wakipinga uwekaji wa bikoni za ushoroba?

Lkn wale wanaohamishwa kwenda Handeni wao wako kule Ngorongoro. Na wanahama kwa hiari yao.

Sasa kwann yule mbunge wa Jimbo la Loliondo alikuwa anapotosha bungeni kuwa wananchi wake wanaondolewa kwenye ardhi ya babu zao na wamepigwa risasi wakaenda Kenya kutibiwa kwasabb wananyimwa PF3.??
 
Kinachoendelea Loliondo na Ngorongoro, Jibu Hasa tutalipata kwenye RASIMU ya WARIOBA.

Tutakapoanza kupitia MIKATABA yoote walosaini watangulizi,

KUTAPAMBAZUKA. Amen
 
Agresive na Manndasori
Inawahusu hii👇🏾...
a) Loliondo hakuna anayehamishwa, bali imewekwa mipaka kati ya kilomita za mraba 2,500 na 1,500 ambazo jumla ni kilomita za mraba 4,000.

b) Ngorongoro wanaohamishwa ni kutokana na wingi wao wa sasa, usalama wao na kukiuka masharti ya uhifadhi kwa kujenga nyumba za kudumu, kufanya kilimo na mengine mengi.
 
Back
Top Bottom