music mimi
JF-Expert Member
- Jun 16, 2013
- 485
- 876
- Thread starter
- #21
Nimekuelewa vizuri sana kiongozi.Ni kweli huelewi na wengi hawaelewi japo wanazungumzia ishu hii.
Kabla kuzungumzia migogoro iliyopo inabidi nikueleweshe kidogo kuhusu wilaya ya Ngorongoro.
Wilaya ina tarafa tatu yaani Tarafa ya Ngorongoro ambayo Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro ipo ndani yake,Tarafa ya Sale na Tarafa ya Loliondo.
Makao makuu ya Wilaya yapo Loliondo.
Kutoka Arusha hadi Loliondo ni takribani kilometa 324.
Na kutoka Arusha hadi Mamlaka ni takribani km 140.
Hadi hapo ushajua historia kidogo na umbali uliopo baina ya Tarafa ya Loliondo na ile ya Ngorongoro.
Tarafa hizi mbili zimetenganishwa na tarafa ya Sale.
Mgogoro.
Mgogoro upo wa aina mbili.
Mosi ni kati ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro na Wamasai wanaoishi ndani ya Mamlaka.
Na hawa ndio wanaohamishwa na serikali kwenda Handeni.
Kwa hiyo ishu ya kuhamisha Wamasai kwenda Handeni inawahusu wale wa Tarafa ya Ngorongoro tu!
Mgogoro wa pili ni ule wa wananchi wa
Loliondo hasa kata za Arash,Soitsambu, Ololosokwani,Oloipiri Oloirien na maeneo dhidi ya Mwarabu wa OBC.
Km za mraba zipatazo 1500 zinamegwa kwenye maeneo wanaoishi wananchi hao kwa ajili ya ushoroba wa wanyama(kati ya Serengeti na Masai Mara huko Kenya).
Wenyeji wenyewe wanadai sio kwa ajili ya ushoroba bali ni kwa ajili ya OBC.
Mgogoro huu ni wa muda mrefu sasa.
Hao wa Loliondo wenyewe hawapelekwi Handeni kama watu wasiojua wanavyozungumza ama wanavyopotosha.
Sasa naamini umeelewa kidogo.
Nyongeza ni kuwa vurugu zilizotokea zilikuwa loliondo na sio tarafa ya Ngorongoro.
Ahsanta
Naomba uniongezee kidogo, watu tunaoambiwa wanaamishwa Ngorongoro kwenye hifadhi ni kweli wanafanya shughuli za kuharibu mazingira ndani ya hifadhi na kama yes zaidi ya overgrazing wanafanya nini kingine?