Sakata la Pierre Liquid; Shilole aomba Radhi

Sakata la Pierre Liquid; Shilole aomba Radhi

Madimba jr

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2017
Posts
1,577
Reaction score
3,146
Screenshot_20190331-144921.png
Kwa Watanzania wenzangu,

Kwanza, nikiri kwamba nimeona wengi niliowakwaza kutokana na maneno niliyoongea jana kwenye tukio liliondaliwa na rafiki yetu @jokatemwegelo (#TokomezaZiroKisarawe). Kwa kuwakwaza huko bila hata kwenda mbali kutoa maelezo yoyote, NAOMBA RADHI, MNISAMEHE SANA.

Pili, nahisi kuna namna sijaeleweka au mimi sikuweka vizuri maelezo yangu. Ninyi mnanijua vizuri, mwenzenu mimi mara nyingi sana nimeongea vitu hadharani kwa kukosea kutokana na udhaifu na uwezo wangu mdogo kwenye kujielezea (hilo mnalijua, kwamba mie mwenzenu kidogo shule sikwenda na wakati mwingine kichwa changu kinapata moto na hiyo sio sifa). Sasa naomba mniruhusu kueleza kwa ufupi nia yangu. Hoja yangu mimi ilikuwa "Kuna vitu vya msingi hamzungumzi ila vitu vya ajabu mnazungumza....." ukisikiliza ile video utasikia mstari huo. Hicho ndio kitu nlichotaka kueleza, sio kumkashifu Pierre au mtu mwingine yeyote. Iwapo Pierre ni mmoja kati ya watu waliokwazika, namuomba sana anisamehe. Lakini tuwe wa kweli, watu wengi wamewahi kusema hili (kuna vitu vya msingi havitangazwi), ila tu mimi kwa akili yangu ndogo nilishindwa kusoma mazingira na muda nikalisema jana. Nirudie tena kusema SAMAHANI.

Nimeona wengi wakirudi nyuma kutafuta matukio yangu, kutafuta nilitokea wapi hadi hapa nilipo. Niwahakikishie kwamba mimi nafahamu upendo mkubwa wa Watanzania kwangu kiasi kwamba walinibeba hata pale nilipokosea, walinivumilia katika ujinga wangu na bado wanaendelea kunivumilia, wananipenda licha ya ulewa wangu mdogo (Kingereza na mambo mengine ambayo yamegeuka utani dhidi yangu), na walinipa nafasi kujifunza, kujirekebisha na kukua hadi hapa nilipo.

Narudia tena, Nimekosea kama nilivyowahi kukosea mara nyingi, NAOMBA RADHI TENA, lakini zaidi ya yote naomba mfahamu sikuwa na nia mbaya, nilikosea tu namna ya kusema na niseme wakati gani.

Asanteni. #ChiiiiiiiiiiiiWatanzaniaMtabakiKuwaJuuuu
 
Tungekuwa Na kawaida ya kufuatilia mambo ya Msingi Hata Yeye asingekuwa Maarufu wala asingealikwa kuzungumza pale wala asingekosea, wala asingeomba radhi wala Hii thread isingeanzishwa wala Mie nisinge comment!

Yaan wao wamekuwa Maarufu kwa matendo yao ya Kipuuzi Halafu kwa roho zao mbaya wanataka wenzao wasiwe Maarufu

Leo Hii Shilole Na Amber rutty Ni Maarufu Kuliko Prof Issa Shivji Au Prof Mbwete Pamoja Na wingi wa Research zao Za kitaaluma walizoandika lakin tumechukulia poa wao roho zinawauma wenzao wakitusua
 
Teh Tanzania raha Sana...Huyu watu washaleta habari zake za kutifuliwa mtaro kwenye Fiesta Singida

Unaishi nyumba ya vioo halafu unahusudu ugomvi wa mawe ?

Ona unavyotia huruma sasa ,Maadam umeomba radhi basi wakusamehe tu

Sent using Jamii Forums mobile app
Daah,hivi ni kweli walimfanyia hivyo,naimagine maumivu anayopata mumewe

Sent using Brain
 
Tungekuwa Na kawaida ya kufuatilia mambo ya Msingi Hata Yeye asingekuwa Maarufu wala asingealikwa kuzungumza pale wala asingekosea, wala asingeomba radhi wala Hii thread isingeanzishwa wala Mie nisinge comment!

Yaan wao wamekuwa Maarufu kwa matendo yao ya Kipuuzi Halafu kwa roho zao mbaya wanataka wenzao wasiwe Maarufu

Leo Hii Shilole Na Amber rutty Ni Maarufu Kuliko Prof Issa Shivji Au Prof Mbwete Pamoja Na wingi wa Research zao Za kitaaluma walizoandika lakin tumechukulia poa wao roho zinawauma wenzao wakitusua

Ni vema kama amegundua kosa na kuomba msamaha. Ni uungwana
 
Teh Tanzania raha sana...Huyu watu washaleta habari zake za kutifuliwa mtaro kwenye Fiesta Singida

Unaishi nyumba ya vioo halafu unahusudu ugomvi wa mawe ?

Ona unavyotia huruma sasa ,Maadam umeomba radhi basi wakusamehe tu

Sent using Jamii Forums mobile app
Heee mkuu hebu tujuze vyema huyu mamalishe walimfanya nini singida?wallah akina Lissu Singida sio poa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ajifunze kusoma alama za nyakati...
lakini pili aboreshe uwezo wake wa kuona hatari.....angalia sasa watu washaanika mambo....if you live in a glass house don't throw stones....duniani tunapita hakuna mtu mkamilifu....wala mtu bora kuliko mwenzake.... mbele ya Mungu..sote tupo sawa
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] mi mambo yakimbelembele yaliisha nishinda kabisa najua kabisa kuna mtu anafile langu la fedheha siku nikiyakoroga tu anamwaga mboga, ugali na jiko anazima.. Yani hata kama kuna siku ulienda kunya kimya kimya gizani ukadhani hakuna aliyekuona nakuambia subiri siku uzingue sasa ndo utashangaaa utatajiwa hadi mavi yalikua ni rangi gani. Wahuni sio watuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi inavyosemwa kuwa 'mambo ya msingi' au 'mambo ya maana' ni kwa tafsiri ya nani na ni yepi haswa?

Hivi kwa mfano yale tunayosikia Mtu kama Zito ni ya maana ama?maana huwa nashuhudia shoruba anazopambana nazo baada tu ya kuitisha press na kuongelea deni la taifa.
 
Write your reply...akamfuate kwake Pierre akamuombe msamaha na sio blah blah hizoo!

leteni nyingine akifukuliwa mtaro plzz
 
Back
Top Bottom