Sakata la Sitti Mtemvu

Sakata la Sitti Mtemvu

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined
May 15, 2006
Posts
94,296
Reaction score
122,540
Hivi ule uchunguzi wa kama huyo binti alifanya udanganyifu kwenye nyaraka zake uliishia wapi? Ilitangazwa kuwa RITA ingefanya uchunguzi juu ya hizo tuhuma

Lakini baada ya hapo sikusikia tena kuhusu hilo jambo hususan baada ya huyo binti kuachia taji lake.Au ndo yaleyale mambo ya 'upepo' na ulishapita huo na watu (Watanzania) kama ilivyo ada yetu tushasahau kabisa.
 
Jibu la swali lako ni hiyo paragraph ya mwisho.

Kuna lingine mkuu?
 
Upepo umeishaipita mkuu
Ukiuliza utaambiwa hakuna aliyeshtaki na muhusika aliamua kuachia kwa ridhaa yake
 
Miss Tanzania ilipigwa ban kwa mwaka mmoja kutokana na hili Saga..
 
Miss Tanzania ilipigwa ban kwa mwaka mmoja kutokana na hili Saga..

Sijauliza kuhusu shindano la miss TZ.

Nimeuliza kuhusu uchunguzi kuhusu tuhuma za Sitti Mtemvu kuwa na nyaraka zinazokinzana.
 
Issue ya huyu binti sio kitu ukilinganisha na takataka na uchafu unaofanyika ktk hii nchi!!
 
Katika masakata yote makubwa umelikumbuka hilo…ingawa nalo ni tatizo lakini tungeanza kutafakari yale makubwa yaliyotikisa uchumi wa taifa.

Hata wewe unaweza ukayakumbuka hayo mengone...hujakatazwa!
 
Mkuu, yule ni mtoto wa mbunge wa ccm. Jibu liko hapo. Angekuwa mtoto wa mbunge wa chama cha upinzani, mambo yangekuwa tofauti. Hii ndio Tanzania yetu kwa sasa.
 
Tanzania tanzaniaaa nakupenda kwa moyo wote,
ikiona magazeti hayaandiki tena ,kwisha hiyo
 
Back
Top Bottom