Sakata la Spika Ndugai; CCM imeonesha kiwango cha chini cha Uongozi

JF Member

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2014
Posts
7,914
Reaction score
10,793
CCM kama chama kikongwe na kilichodumu kwa mda wa miaka, ni chama kinachoaminika kuwa na uongozi imara na makini.

Binafsi nimeshangaa kuona namna gani umeshindwa kushugulikia swala la Spika na Rais. Maswala haya ni ya mihimili miwili, Spika anatakiwa alindwe kwa nguvu na kama anavyolindwa Rais na JM kwa maana ya mihimiri mitatu kama ilivyo katika katiba yetu.

Kwa niliyoyaona kwa macho na masikio yangu nimeanza kufikilia kwamba hii nchi haina viongozi mathubuti wa kushugulika na mambo magumu na mazito. Viongozi waliopo wengi wanaangalia masirahi yao binafsi.

Swala la CCM kuruhusu vijana kumtukana sipika kisa tu katoa maoni kinzani ni kuonesha umma kwamba CCM haijapevuka; bado ni changa mno. Zile ngonjera nilitegemea kuziona ACT wazalendo kwa maana viongozi wengi ni wapya kwenye changamoto kubwakubwa ila sio CCM.

CCM kimeonesha udhaifu kwenye kusimamia masirahi ya UMMA kwa maana ya muhimiri ya Bunge. Kwa sasa ni ngumu sana kuwaaminisha watu kwamba kuna mihimiri mitatu kwa maana watu wameshaona.

Sote tunajua Ndugai alikuwa na uadui na upinzani kwa jinsi alivyowafanyia lakini hii haikuwa na maana CCM wangeruhusu kelele za upinzani ziwatoe kwenye reli. CCM wamecheza ngoma ya upinzani na sasa mjiandae kueleza umma kwamba mihimiri iko mingapi.

Nashawishika kusema kwamba CCM iko kwenye denial stage. Ndio maana haina uwezo tena wa kufanya upembuzi yakinifu.

Asanteni, tukutane 2025.
 
Mkuu hongera sana kwa kujitahidi kuongelea kutokupevuka kwa viongozi wengi wa CCM.

Kwa kuongezea ni kwamba CCM wamedhihisha kuwa maslahi ya chama chao ni muhimu kuliko maslahi ya taifa. Kadhalika, hawajali kabisa kuhusu maslahi ya Nchi yetu.

Pili, wameonesha uzumbukuku wao mkubwa sana kwa kutokujua maana ya mihimili mikuu mitatu na ni kwa namna gani inafanya kazi. Kwa akili zao ndogo wameona kuwa Ayubu kamkosea Rais wakati Ayubu alikuwa anatumia vizuri haki yake ya kikatiba kuhoji na kukosoa mhilimili mwingine wa serikali.

Tatu, sakata hili limedhihirisha chuki na unafiki mkubwa sana katika chama chao kwa kuruhusu vijana wa CCM kutoa matusi, kejeli na lugha za ajabu ajabu kwa Ayubu bila Kuzingatia kwamba alichokifanya kilikuwa kinaruhusiwa kisheria na alikosoa na kutoa maoni kwa kuzingatia mipaka yake kama kiongozi mkuu wa mhimili wa Bunge.

Mwisho, wameonesha uwezo ndogo sana walionao siyo tu katika kuongoza bali hata katika kufikiria na kuchakata mambo mbalimbali kiufasaha bila kuwa na hisia zozote.
 
Kidumu chama cha Mapinduzi

Polepole bado anaamini anaweza kutingisha chama

Ukiona Ndugu wanageukana na kupigana mapanga bila ya huruma jitathmini wee Mhamiaji haramu ukijichanganya si wanagawana hadi bandama lako

Wachawi wame update software yao sasa hivi sio radi tu hadi Corona unarushiwa
 
Back
Top Bottom