Imbombo Ngafu!! Hii ngoma bado mbichi.. Afe kipa, afe beki!
Leo kupitia 255 ya Clouds FM, Nay wa Mitego amenukuliwa akitoa yake ya moyoni kuhusiana na ngoma ya 'Freedom' inayogombaniwa kati ya Mr. Blue na 'Sugu' ambae ameshaifanyia video na kunyofoa vocals za Mr Blue.
Nay anasema;
''Blue angekuwa ni mshikaji wangu ningemshauri na yeye amtoe Sugu halafu kama inawezekana aniweke mimi kwenye chorus halafu tuharibu hali ya hewa tutajuana huko mbele ya safari, halafu kama ni hela ya kuifanyia Video ngoma hii mimi nitalipa hata kwa GodFather au Hanscana‘:- Nay wa Mitego.
Tuwepo!