political monger senior
JF-Expert Member
- Nov 26, 2020
- 1,827
- 5,994
AMEANDIKA ANGETILE OSIAH KATIBU WA ZAMANI WA TFF.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwani dirisha la usajili CAF limefungwa?Mchezaji ambae amepata APPROVE ya TFF na kupewa Leseni anaweza kucheza Ligi ya Ndani Wakati Mchezaji ambae Ana Leseni ya CAF anacheza Ligi zote yaani Ya ndani na Caf kwa Maana ni Lazima kuwa na Leseni ya TFF katika Usajili wa CAF.
Na ukishakuwa na Leseni ya CAF na Dirisha la Usajili kubwa la CAF likawa limefungwa huwezi kutoa Jina lolote katika List zaidi ya kuongeza iwapo hujatimiza Idadi hitajishi ya usajili na haipaswi kuzidi wachezaji 7 tu. Na ieleweke Wazi Kwa Wachezaji wa Kigeni ili kupata Leseni ya TFF ni lazima CLUB kutozidisha Wachezaji zaidi 12.
Kipindi cha mpito cha usajili kinachokuwepo baada ya Dirisha kubwa la CAF kufungwa ni kwa ajili ya kuongeza tu sio vinginevyo ndio maana unaambiwa mchezaji atacheza hatua inayofuata hii ina kupa picha kuwa tayari usajili wa msingi ulishafanyika kabla.
Kwa Mantiki hiyohiyo huwezi kutoa au kufuta Leseni ya TFF pekeyake bila kufanya hivyo hivyo katika Leseni ya CAF, Sasa Kama muda wa kufanya hivyo kwa CAF umeshapita basi pia huwezi kuondoa kwa TFF itabaki kama ilivyo.
Ili kuweza kufanya mabadiliko inapaswa kusubiria Dirisha la CAF liwe wazi wakati mwingine na uweze kufanya Transfer au Kuvunja/kusitisha mkataba au makubaliano maalum yanayomshirikisha Mchezaji husika kwa maandishi.
Itambulike kuwa kuomba ITC ya mchezaji ni jukumu la Shirikisho kwa niaba ya Club na pia ITC ni moja ya Kigezo katika kupata Leseni ya TFF/CAF ila kuwa na ITC sio usajili unaweza kuwa/kupata ITC na usifanyiwe/kuombewa usajili na Club yako mifano ipo mingi Mfano ni Yacouba anayo ITC ila hajaombewa usajili na Club yake hivyo hana Leseni ya kucheza yeyote msimu huu bali bado ana mkataba na Club yake.
PLAY FAIR, BE POSITIVE
Atacheza ndondo cupAll in all, haki huwa inacheleweshwa tu. Mwisho wa haya maigizo yote, mchezaji ataendelea na majukumu yake kama kawaida.
Tatizo ilikuwa ni usiku sana walipomsajili Kisinda. Usajili wao walikuwa wanaufanya saa 6:01 usiku, ambapo tayari ni siku mpya 🤣🤣🤣... Ningekuwa mimi ndiye kiongozi wa TFF nnae husika na usajili ningehitaji tu document ya makubaliano ya Yanga na Kambole then nayafaili basi.