Sakata la uchaguzi: Pesa kwenye damu

Sakata la uchaguzi: Pesa kwenye damu

SIMULIZI: ELECTION SAGA (MONEY IN BLOOD)
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+

UKURASA WA THELATHINI NA NANE
Ndani ya dakika kumi baada ya yeye kuondoka, kuna msafara wa gari sita uliingia hapo, alikuwa mr Mafupa mwenyewe akiwa ameongozana na mwanae Remsi hivyo walichelewa kidogo sana kufika hilo eneo hali ambayo iliwafanya wapishane na mtu ambaye walikuwa wamemfuata.

Walikuwa kwenye mwendo mkali sana ili kuweza kuwahi ndani kujua kipi ambacho kilikuwa kimejiri humo lakini walicho fanikiwa kukiona yalikuwa ni mauaji tu tena mwanaume mmoja akiwa amekatwa kichwa chake kikahifadhiwa pembeni na kiwili wili chake. Waliwahi mpaka ndani ya chumba ambacho walikuwa wamemhifadhi Patrina, chumba kilikuwa kitupu bila mtu yeyote yule, walichoka sana.

Mr Mafupa aliitoa simu yake haraka mno na kuipiga mahali ambako ilionekana wazi kwamba ni kwa mr Oscar.
“Nakuja hapo sasa hivi” aliongea akiwa anahema kwa nguvu sana kichwa chake kikionekana kuvurugika moja kwa moja, hayo mambo kama yangeweza kufika kwa waandishi wa habari yangemharibia kila kitu ambacho alikuwa amekitengenza kwa muda mrefu sana na hakuwa tayari kabisa jambo hilo kuweza kutokea ndani ya nchi yake hata kama ingekuwa kwa kumwaga damu za watu kiasi gani. Aliondoka hilo eneo haraka sana akiwa kama mtu ambaye alivurugwa na ni kweli hayo mambo yalianza kumvuruga haswa.

Hakukuwa na muda wa kupoteza tena, usiku huo huo ambao Tommy alikuwa ametoka Kurasini alipitiliza moja kwa moja mpaka mhimbili kwenda kukabidhi kichwa hicho ambapo alisisitiza sana kwamba kichwa hicho kilitakiwa kuunganishwa pamoja na mwili wa mdogo wake ili uandaliwe kwa ajili mazishi maana hicho ndicho kitu pekee ambacho kilikuwa kinasubiriwa na familia, ingekuwa aibu kubwa sana kuweza kukizika kiwili wili pekee bila kichwa chake.

Baada ya kuhakikisha ametimiza hilo jukumu, alisogea mpaka kwenye wodi ambayo baba yake alikuwa amelazwa, alimwangalia sana baba yake pale kitandani ambapo alikuwepo, alikuwa anajihisi kuwa na hatia sana kwa kushindwa kuweza kuilinda familia yake.
“Nimewapa binti zako wote baba, wanao nimewarudisha” aliongea kwa hisia sana akiwa anaamini kwamba mzee huyo hakuwa akimsikia kabisa kisha akatoka humo ndani kwani alikuwa na kazi ya kumpeleka dada yake nyumbani. Lakini wakati ametoka humo ndani mwanaume huyo ambaye alikuwa amelala hapo kitandani, hakuwa na uwezo hata wa kuchezesha vidole vyake lakini machozi yalionekana yakishuka kwenye mashavu yake kitu kilichokuwa kinaashiria kwamba alikuwa anasikia kila kilichokuwa kinaendelea humo ndani.

Safari ya Tommy iliishia nyumbani kwao ambapo nje ya geti la nyumbani kwao alifanikiwa kumkuta daktari binafsi wa familia akiwa anamsubiria hapo ikiwa ni maagizo yake na hakutaka mtu huyo aiingie ndani kabla ya yeye kufika ndani ya hilo eneo. Waliongozana pamoja mwanaume akiwa amembeba dada yake kwenye mikono yake.

Baada ya geti hilo kufunguliwa, alimuona mama yake mzazi akiwa amekaa karibu na zilipo ngazi za kupandishia kwenye jengo hilo la kifahari. Muda ulikuwa umeenda sana hivyo ni wazi kwamba mama huyo sababu kubwa ya kukaa hapo alikuwa anamsubiri mwanae huyo arudi ili wawe na mazngumzo marefu sana lakini baada ya kumuona Tommy akiwa amembea dada yake alijikuta anatoa machozi na kumshika mtoto wake wa kike huyo ambapo ililazimika kupelekwa ndani kisha dakatari akaachwa aweze kuifanya kazi yake ambayo ilikuwa imemleta.

“Alikuwa amechomwa sindano za madawa ambayo yangemfanya alale kwa masaa kumi na nane ila nimemchoma sindano nyingine ambayo itamfanya asubuhi awe ameamka na atakuwa sawa hakuna kitu kibaya sana kwenye mwili wake ila anatakiwa kupatiwa muda mrefu zaidi wa kuweza kupumzika na asiwe karibu na vitu ambavyo vinaweza kumpatia msongo wa mawazo inaweza kumletea matatizo makubwa sana kwenye akili yake” daktari alitoa maelezo akiwa anamkabidhi Tommy dawa ambayo dada yake huyo alitakiwa kuitumia baada ya kuamka kisha yeye akatoka humo ndani kuelekea kwake.

Licha ya mama kuwa na furaha kubwa sana mwanae wa kike kuweza kupatikana na moyo wake kuonekana kutulia kwa kiasi kikubwa lakini alikuwa na wasiwasi mkubwa sana kwenye nafsi yake na ndiyo sababu kubwa haswa ambayo ilikuwa imemfanya aweze kumsubiria mwanae wakati wote huo ili aweze kufika hapo waweze kuongea kwa marefu zaidi juu ya yale ambayo yalikuwa yanaendelea.

“Nataka uniambie wewe ni nani na kila kitu ambacho kipo kwenye maisha yako. Kama unaniheshimu mimi kama mwanamke niliye kuzaa basi usije ukathubutu kunidanganya kama ulivyo nidanganya kwa miaka yote hii ambayo mimi sikuwa nakujua kabisa wewe, uliondoka tofauti na umerudi ukiwa mtu mwingine kabisa. Nahitaji uniambie kwamba wewe ni nani?” lilikuwa ni jambo la hatari sana mama yake mzazi ambaye alimzaa alikuwa amuuliza kwamba yeye ni nani. Mama alikuwa hamuamini tena mwanae huyo kwa sababu alihisi wanaishi na kiumbe ambacho hata wao hawakuwa wanakijua kwamba kipoje na kilikuwa kinafanya kazi zipi hasa kwenye maisha yake. Tommy alijisikia vibaya sana kupata maneno kama hayo kutoka kwa mama yake mzazi lakini njia pekee ambayo alikuwa nayo ya kuweza kufanya mama huyo amuelewe ilikuwa ni kumweleza ukweli wa maisha yake halisi ambayo alikuwa anayaficha sana.

“Mimi ni jasusi mama”
“Samahani, unamaanisha nini kusema hivyo?”
“Mimi ni mpelelezi wa siri kutoka ndani ya idara ya usalama wa taifa wa nchi ya Uingereza” mama huyo alibakia ameinamia chini akiwa hana hata la kusema maana alichoka sana kuyasikia hayo maelezo kutoka kwa mtoto ambaye alikuwa amemlea mwenyewe na kumtoa kwenye tumbo lake. Basi Tommy hakuwa na namna zaidi ya kuanza kumweleza mama yake ukweli wa mambo ulivyokuwa.

“Mimi kule wananijua kama T1 ikiwa na maana ya target namba moja kwa sababu kwenye huo mpango ambao ulinifanya mimi kuingia huko, mimi ndiye nilikuwa mtu wa mhimu zaidi kuliko mtu yeyote yule”
“Kwa mara ya kwanza tangu naenda kujiunga na masomo yangu ya elimu ya juu huko nchini Uingereza sikuwahi kabisa kuyajua haya mambo wala kufikiria kwamba siku moja na mimi nitakuwa mtu wa namna hii mpaka pale ambapo nilifanikiwa kukutana na mwanamke mmoja ambae anaitwa Harper”

“Baada ya kufika ndani ya kile chuo kila kitu kilikuwa kugeni sana kwangu, sikuwahi kumzoea mtu yeyote yule kwa sababu nilikuwa mtu mwenye aibu sana mama kama ulivyokuwa umeniambia mwanzo kitu ambacho kilifanya nihisi kwamba kila kitu kilikuwa kigeni na kigumu sana kwangu kwa sababu ya upweke wangu na nyie mlikuwa mbali sana na mimi. Ule upweke wangu ndio ambao ulimvuta mwanamke mmoja kuja karibu yangu mimi, mwanamke ambaye nilihisi kwamba alikuwa amekuja kwangu kwa sababu ya kuona kama mwanaume ninaye mfaa mama, mwanamke ambaye naweza kusema kwamba ndiye amekuja kuwa chanzo cha kila ambacho unakiona kinatokea kwenye maisha yangu”

“Ni mwanamke mrembo sana ambaye aliwahi kuniambia ana asili ya nchi ya Tanzania na Uingereza japo kwa baadae nilikuja kugundua kwamba alinidanganya pakubwa sana baada ya kujua kwamba alikuwa na asili ya Kiisyopia na kiingereza. Yule mwanamke alinifanya nisijihisi mpweke tena kwenye maisha yangu, akanifaya nikawa na furaha sana na kuyaona maisha ya kule yalikuwa mazuri sana na kwa mara ya kwanza nikajikuta naenza kuipenda nchi ambayo haikuwa nyumbani kwa sababu tu nilimpenda sana mwanamke yule”

“Nilimpenda kana kwamba ilifikia hatua nikawa namuamini sana, nikamuaonyesha mpaka kwangu nilipokuwa nakaa kwa sababu niliona kwamba ni mwanamke ambaye baada ya kumaliza masomo huenda ningekuja kuoana naye na kumtambulisha kwenu ila sikuwahi kuwa sahihi mama. Wanamwita H2 ikiwa na maana ya Honey Trap, mtego wa mapenzi ndio ambao huwa anautumia kushinda vita zake na anaitumia namba mbili kwa sababu baada ya mimi yeye ndiye ambaye ulikuwa mpango wa pili kwenye kulikamilisha hilo jambo ambalo walitarajia mimi ndiye niweze kulifanya”

“Yule mwanamke alikuja kwangu baada ya kugundua kwamba nina uwezo mkubwa sana kichwani hivyo walikuwa wanahitaji kukamilisha kuteketeleza mipango yao ya kuweza kuja kuishika dunia kwenye mikono yao kwa kutumia akili yangu hivyo ili kujua kila kitu kuhusu mimi wakalazimika kumtumia mwanamke huyo ambaye aliifanya hiyo kazi na baada ya kuona amepata kila ambacho alikuwa anakitaka kwangu ndipo siku moja alinijia na baadhi ya wakubwa wake wa kazi na kuniambia ukweli kwamba yeye alikuwa nani na lengo ambalo lilikuwa limewaleta pale”

“Waliniambia kwamba wanahitaji kukitengeneza kirusi pamoja na dawa yake na kirusi hicho walikuwa wanahitaji kukitumia kujilinda wao dhidi ya maadui zao na kwamba kingekuja kutumika kwenye kazi zingine za kisayansi hapo baadae kwenye nchi yao hususani kwa wasomi ambao walikuwa wanaendelea kuzalishwa kwenye mavyuo mbali mbali ndani ya nchi ya Uingereza. Mimi niligoma kabisa jambo hilo ndipo wakanisisitiza kwamba hawakuwa na lengo baya na kirusi hicho ambacho kingetengenezwa lakini bado niligoma kabisa kushiriki kwenye jambo la hatari sana namna hiyo”

“Baada ya kuona nimegoma, walinipa taarifa zote kuhusu familia yangu na wakanipa chaguo kwamba nitaamua mimi kama nahitaji familia yangu iachwe hai basi sina budi kuweza kukubali kazi yao lakini kama nikigoma basi nyie wote mngekuwa mmekufa muda mrefu sana. Hawakuishia hapo tu wakaniambia kwamba hata nchi yangu ingeingia kwenye machafuko makubwa sana ambayo yangefanya maisha ya watu wengi sana kuweza kupotea bila kusahau kuwekewa vikwazo vikali sana vya kiuchumi kwenye masoko ya kimataifa hali ambayo pia ingeifanya nchi yetu iingie kwenye umaskini mkubwa sana ambao ungekuwa ni mgumu hata kuweza kuulezea kwa lugha ya kawaida”


“Hivyo sikuwa na nguvu ya kuweza kukataa tena hilo ombi lao nikakubali kuifanya kazi yao kwa kuongeza sharti moja. Kwanza nilitaka wasije wakayafanya hayo ambayo waliyaorodhesha halafu ndipo nikahitaji na mimi wanitengeneze niwe binadamu hatari sana kwa sababu nilijua hayo mambo yanaweza kuja kuharibika baadae angalau wakati yanaharibika niwe na uwezo wa kuilinda familia yangu lakini pia niwe na uwezo wa kuilinda nchi yangu”

“Waliniambia ombi langu ni rahisi sana kulitekeleza ila kuna sheria zao na misingi yao, kama nikihitaji waweze kulifanya hilo zoezi maana yake nitatakiwa kuwa memba halisi wa shirika lao la kijasusi la MI6 kwani wasingeweza kunitengeneza mtu ambaye sikuwa mmoja wao kwani kama kazi ambayo nilikuwa naifanya ningelipwa hivyo ya gharama za kutengenezwa zilikuwa zinatoka kwa wale tu ambao wanakuwa ni miongoni mwao. Kulingana na unyeti wa tukio husika nikakubali na rasmi nikaapishwa kujiunga na shirika la kijasusi la nchi ya Uingereza kwa makubaliano kwamba nitakapo kamilisha kazi yao basi wataniruhusu niendelee na maisha yangu ya kawaida huku wakiniahidi kuilinda familia yangu kwa muda wote ambao ningekuwa mbali isipokuwa mwezi mmoja kabla ya mimi kurudi tulikubaliana waondoke kabisa na waache kuwa karibu na familia yangu maana nilitaka wakati narudi nisikute alama zao zozote kwani tungekuwa tumemalizana”

Ukurasa wa thelathini na nane nauhitimisha hapa, panapo majaaliwa tukutane wakati ujao.

Wasalaam,

Febiani Babuya.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
SIMULIZI: ELECTION SAGA (MONEY IN BLOOD)
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+

UKURASA WA THELATHINI NA TISA
“Walinilipa pesa nyingi sana mimi kuweza kufanya ile kazi mpaka kuna muda nikawa naogopa sana lakini sikuwa na namna, nilitengeneza kirusi kimoja hatari sana kuwahi kutokea kwenye historia ya maisha ya mwanadamu bila kusahau na dawa yake pia niliitengeneza huku nikiendelea kula mafunzo makali sana na masomo nikiwa naendelea kumalizia. Baada ya kukamilisha kukitengeneza walinipelekwa kwenye mafunzo kwenye nchi ya China kisha nilimalizia huko Tirana Albania ambako kulikuwa na kambi yao ya siri. Baada ya hapo nilikuja kuwa binadamu mkatili sana mama kwani nimeyachukua maisha ya watu wengi sana hususani kwenye kazi ambazo walikuwa wakinituma kuzifanya kwa makubaliano maalumu na malipo maalumu ila nikiwa chini ya shirika lao la kijasusi ikiwa ni kama sehemu ya mkataba kukamilisha kile ambacho tulikubaliana ili waweze kuniacha niendelee na maisha yangu mwengine ya kawaida. Lakini jambo ambalo sikuwahi kulijua ni kwamba kumbe walikuwa wamepanga kuweza kuniua pale tu ambapo ningefanikiwa kuweza kumaliza kazi zao na baada ya hapo wakawa wamechukua sehemu ya ubongo wangu ili waje kuupandikiza kwa watu wengine wakiamini kwamba nao watakuwa na uwezo mkubwa kama mimi hivyo watalisaidia taifa lao kwa hapo baadae hata mimi nisipokuwepo ndiyo maana hawakuona umuhimu wangu tena kw sababu waliamini kwamba wanaenda kutengeneza watu wao ambao wangekuja kuwa na uwezo sawa na wangu tu”

“Jambo la kuniua lilikuja kushindikana baada ya kile kirusi kuibiwa na kuingia kwenye kundi la kigaidi kutoka huko Afghanstan hivyo wakaogopa kwamba kama wakiniua inaweza kutokea wakawa wanahitaji kutengeneza kingine au kutafuta dawa wakashindwa maana vijana wao bado wanasoma, hiyo ndiyo nafasi pekee ambayo ilinifanya mimi nikaachwa salama. Lakini kwa bahati mbaya sana hicho kirusi kimekuja kudondokea ndani ya nchi ya Tanzania”

“Gaidi huyo baada ya kufanikiwa kukipata alikimbia nacho na kuja Tanzania ambako aliamini kwamba itakuwa ni sehemu salama kwake na akipata sehemu ya kuweza kukitunza kirusi hicho itakuwa vizuri zaidi hivyo akaamua kukutana na raisi wa nchi ya Tanzania na kufanya nae makubaliano kwamba kiongozi huyo aweze kukihifadhi huku wakitafuta mteja kutoka nchi kubwa wa kuweza kukinunua kirusi hicho ambacho wanaamini kwamba kitawapa utajiri mkubwa sana isivyo kawaida. Hivyo mpaka hivi ninavyo ongea kirusi hicho inasemekana kwamba kimehifadhiwa Ikulu na huyo gaidi ambaye ndiye alikuja na kirusi hicho analindwa na mheshimiwa raisi”

“Kwahiyo mimi nikiwa kwenye mipango ya kuweza kurudi huku nilikuwa namalizana kabisa na MI6 na ndipo nikawa nimepata habari mbaya sana huku nyumbani ambazo zimesababishwa na sakata la uchaguzi baada ya kupigiwa simu na baba niweze kurudi. Hiyo ndiyo stori ya maisha yangu kwa upande ambao haunifahamu mama yangu, naomba unisamehe sana mwanao kuwa namna hii ambavyo nimekuwa” mwanaume hakuona haja ya kuendelea kumficha mama yake mzazi ilibidi ampe ukweli wa mambo na namna ulivyo kuanzia maisha yake ya huko ambako alikuwa mpaka alipokuwa amefikia siku hiyo.

Mama yake alimsikiliza mwanae huyo kwa utulivu wa hali ya juu sana, hakuwa na jambo la kuweza kufanya kwa sababu huyo alikuwa ni mwanae na alikuwa akimpenda sana na ndiye pekee alikuwa wa kiume kwenye familia yake. Alinyanyuka na kwenda kumkumbatia mwanae kwa uchungu sana, ilikuwa ni mara yake ya kwanza kabisa anapata nafasi ya kumjua mwanae, mwanaume ambaye waliamini kwamba hakuwa na uwezo wa kuushika hata mwiko akafanikiwa kusonga ugali kwa namna alivyo ondoka akiwa mlaini ndiye huyo kwa wakati huo alikuwa anazikata shingo za watu kirahisi mithili ya nyanya sokoni.

“Asante kwa kurudi ukiwa salama mwanangu, namshukuru Mungu kwa kukufanya uendelee kuwa mzima. Nahitaji kumuona huyo mwanamke”
“Sawa mama nitamleta”
“Fanya kile ambacho utaona kwamba ni sahihi kwako na kwa familia”
“Nimekuelewa mama” mama huyo hakutaka kuongea sana licha ya kusikia mengi sana ambayo yalikuwa nyuma ya maisha ya siri ya mwanae. Baada ya kuongea hayo machache ya kumpa ruhusa kichaa huyo alizungushe rungu kwa namna ambavyo angeona kwamba inamfaa, mama huyo alikuwa amechoka sana hivyo akawa anahitaji kwenda kulala maana muda ulikuwa umeenda sana na ulikuwa ni usiku wa manane mno.

Lakini kabla ya kupiga hatua hata mbili walisikia breki za magari zikiwa zinasimama nje ya jengo hilo huku mlinzi akija kwa nguvu na kutoa taarifa kwamba gari hizo zilikuwa za serikali na kuna kiongozi ambaye alikuwa anahitaji sana kuweza kuongea na Tommy. Mwanaume alitoa amri mtu huyo afunguliwe na ndipo alipo ingia mkurugenzi wa idara ya usalama wa taifa akiwa ameongozana na kijana wake Nickson waweza kumuita Matiasi Ndugu.

Tommy hakushangazwa sana na ujio wa kiongozi huyo ila aliye shangaa sana jambo hilo alikuwa ni mama yake mzazi na Tommy maana ilikuwa ni ghafla sana. Huyo kiongozi alikuwa ni rafiki yake mkubwa sana hivyo kuja na vijana wake hapo ilimaanisha kwamba walikuja kikazi na sio kirafiki kama ilivyokuwa siku zote. Kiongozi huyo alimpa heshima mama huyo na kuomba awapishe kidogo maana walitakiwa kuwa na mazungumzo ya kiume kidogo ambapo walienda mpaka nyuma ya jumba hilo la kifahari ambako kulikuwa na sehemu nzuri ya kupumzikia.

Masaa kadhaa nyuma
Niick kipigo ambacho alikipata kilimfanya siku nzima aweze kumfikiria sana yule mwaaume na kushindwa kabisa kuelewa kwamba alikuwa ni mtu wa namna gani na huo uwezo aliutolea wapi. Alipigwa akawa hana hata namna ya kuweza kujitetea tena ilibakia tu mtu huyo kufanya maamuzi kama angetaka hata kumuua asingeweza kujitetea kabisa lakini mwanaume huyo alimwacha hai huku akimpa onyo kwamba iwe mara ya kwanza na ya mwisho yay eye kuweza kumfuatilia na alitakiwa kumpa taarifa kiongozi wake kwamba mtu huyo alikuwa anahitaji sana kuweza kukutana naye.

Nick alikumbuka vyema kile ambacho alikiona kule posta kichwa kikawa kama bado hakielewi kimtafsiri vipi Tommy, pia alikuja kushtushwa na yale mauaji ambayo mtu huyo aliweza kuyafanya kule Mikocheni akakamilisha hesabu za kwamba huyo mtu hakuwa binadamu wa kawaida kama ambavyo huenda alikuwa anaonekana kwenye macho ya watu wengi. Alifunga hesabu za kuanza kumuogopa mwanaume huyo baada ya yeye mwenyewe kuweza kuingia kwenye kumi na nane zake kitu ambacho kilimfanya abakie anahesbu dakika za kuwa hai lakini Mungu alikuwa upande wake siku hiyo baada ya kuweza kupewa siku nyingine ya kuendelea kuwa hai.

Siku nzima majira ya mchana alishinda ndani akiwa anauguza maumivu yake maeneo hayo ya Msasani. Majira ya usiku wa mapema aliwasiliana na kiongozi wake na kumwambia kwamba alikuwa na taarifa za mhimu sana za kuweza kuziwasilisha kwake ili kiongozi huyo aone kwamba angefanya nini juu ya jambo hilo.

Ndani ya eneo la Ubungo Plaza ndipo mahali ambapo walikutana usiku huo mzee huyo akiwa kama moja ya wafanya biashara, alifika kwenye eneo hilo akiwa na walinzi wa kutosha ambao nao ungewaona ungehisi kwamba walikuwa na shughuli zao hilo eneo ila walikuwa hapo kuhakikisha kwamba kiongozi huyo anakuwa salama kwa masaa ishirini na manne.

Nick baada ya kufika hilo eneo kama utaratibu ulivyokuwa alisimama mlangoni ambapo alikakuguliwa kila sehemu ya mwili wake na silaha zake aliziacha hapo kisha akaingia huko ndani kuongea na bosi wake.
“Una jambo gani la maana mpaka unanileta huku na usiku wote huu?” mzee huyo aliongea akiwa anaikagua kalamu yake mkononi, Nick aliinama kutoa heshima kisha akaliweka koo lake vizuri ili atoe kilichokuwa kwenye moyo wake.
“Ni kuhusu mtoto wa kiume wa Apson Limo”
“Kafanyaje?”
“Ulisikia yale mauaji ya Posta?”
“Ndiyo”
“Na Mikocheni pia?”
“Ndiyo”
“Ni yeye ameyafanya yale yote?” mzee huyo hakuongea jambo lolote bali aligeuka kuweza kumwangalia Nick kwa umakini sana akiwa kama mtu ambaye hakuamini kile ambacho kilikuwa kinaongelewa pale.
“Una maanisha nini kusema hivyo?”
“Yule mtu ni binadamu hatari sana na muuaji mkatili zaidi mimi kuwahi kumuona kwenye maisha yangu tangu nizaliwe”
“Inawezekana vipi yeye kuwa hivi?” Nick hakuongea alivua shati yake ambayo ilikuwa imenyooshwa vizuri sana, kwenye mbavu yake moja palikuwa pamebonyea, alivyo hakikisha bosi wake amepaona vizuri akaendelea;
“Haya majeraha ni yeye alinipatia kwenye mwili wangu”
“Nick are you serious?”
“Ndiyo bosi, wakati namfuatilia nadhani kuna kosa kubwa ambalo nililifanya la kuweza kudondosha picha yangu. Sasa jana wakati nikiwa narudi sehemu ambayo nilikuwa nimepanga nilihisi kama kuna mtu ananifautilia hivyo nikahitaji kuchepuka sehemu nyingine ambayo ingenifanya niwe salama na asijue kwamba nimeenda wapi ila kwa bahati mbaya sana nilimkuta ananisubiria mbele yangu” Nick aliongea huku akiwa anasikitika sana
“Baada ya hapo niligundua kwamba hakuwa amekuja kirafiki sana ndipo tulipo anza kupigana lakini kitu cha ajabu ni kwamba kwake nilikuwa kama mtoto mdogo maana alinipiga mpaka nikawa sina hata uwezo wa kufanya lolote hivyo kama angekuwa anahitaji kuniua basi angeniua kiwepesi sana pale”
“Mhhhhhhh Nick wewe ni miongoni mwa watu ambao wana mafunzo ya juu sana kwenye tasnia ya upiganaji sasa unaniambiaje kwamba alikupiga ukawa hauna hata nafasi ya kujitetea?”
“Mkuu mimi hilo halikunishangaza sana ila kilicho nishangaza ni kwamba anajua historia nzima ya maisha yangu mpaka jina langu la kuzaliwa na baadhi ya taarifa zangu za siri ikiwemo ile ya kumuua yule shushushu mwenzangu ambaye aliwahi kutembea na mchumba wangu”
“Hili haliwezekani Nick, kivipi mtu azipate taarifa zako ambazo mimi pekee ndiye ambaye nina uwezo wa kuzifikia?”
“Inaonekana yule ni jasusi kutoka kwenye taifa lenye nguvu kubwa sana ambalo linaweza kupata taarifa hata za siri za kiusalama kwa kutumia vifaa vyenye uwezo mkubwa”
“Yule ni mtanzania inakuwaje awe jasusi kutoka ndani ya nchi nyingine?”
“Mkuu hata mimi nimechanganyikiwa sana, zile taarifa zangu watu ambao wana uwezo wa kuzipata ni watu ambao wanatuzidi nguvu za kiutendaji wa idara hizi za usalama wa taifa kwani huko ndiko wanaweza kuchakata taarifa hizi sasa kama hayupo huko unahisi alizipatia wapi? Kuna haja kubwa sana ya kuweza kumtambua haraka sana kwamba huyu mtu ni nani kwani kwa nilivyo muona tu anaonekana ni mtu mwenye kisasi kizito sana ndani yake na alikuwa anamtafuta dada yake na kichwa cha mdogo wake hivyo anaweza kuendelea kufanya mauaji ya kutisha ambayo huenda yataliweka taifa kwenye hali ya hatari mno jambo ambalo kwa kipindi hiki cha uchaguzi litafanya nchi iingie kwenye machafuko makubwa. Inabidi tumzuie haraka”

39 inafika mwisho.

Wasalaam.

Febiani Babuya.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
SIMULIZI: ELECTION SAGA (MONEY IN BLOOD)
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+

UKURASA WA AROBAINI
“Niletee mkoba wangu nje hapo” mzee huyo aliongea akiwa kama amechanganyikiwa, mtu ambaye alimtuma kijana wake aweze kumlinda ndiye huyo ambaye alitaka kumuua kijana huyo huku akidai kwamba kijana huyo alikuwa dhaifu sana kiasi kwamba hakuwa na uwezo wa kumlinda mtu mwingine bali alitakiwa kujilinda yeye kwanza.

Ndani ya muda mfupi Nick alirudi na mkoba wa mzee huyo ambao ndani yake kulikuwa na mashine kubwa mithili ya simu ya kisasa. Mzee huyo aliiwasha na kuandika jina la Tommy lote hapo ili waweze kupata taarifa za maisha ya mtu huyo kuanzia siku anazaliwa mpaka siku ambayo alikuwa anarudi ndani ya nchi ya Tanzania baada ya kusikia kwamba baba yake alipata matatizo pamoja na mdogo wake kuweza kuuawa.

Hakukuwa na ukakasi wowote ule kwenye taarifa zake kwani zilionekana kuwa za kawaida tu
“Kuna jambo halipo sawa hapa, naanza kuyaamini maneno yako”
“Wapi mkuu?”
“Baada ya kwenda nje ya nchi hakuna taarifa yoyote ile zaidi ya taarifa tu kwamba alikuwa anaenda kusoma ndani ya taifa la Uingereza”
“Kwahiyo tunafanyaje mkuu? Nadhani ni vyema kama tukimkamata tumhoji”
“Hapana, inaweza kuwa hatari sana kwani kama anayafanya haya na ni mtu wa namna hii basi huenda nyuma yake kuna watu na kama tukikurupuka basi tunaweza kusababisha madhara makubwa zaidi hata ya tunavyo fikiria hivyo njia ya pekee hapa ni kuweza kuongea naye kama alivyo hitaji. Beba kila kitu tunakwenda nyumbani kwao saivi” baada ya muda mrefu sana wa kukaa ndani ya chumba hicho wakiwa wanazichakata taarifa za mtu huyo walitoka ili kuweza kuwahi nyumbani kwa Apson Limo ili wakafanye mazungumzo na mtoto wake huyo huenda wangefikia mwafaka wa mambo ambayo yalianza kutokea kwa siri sana.

“Najua utakuwa umesha nifahamu kwamba mimi ni nani baada ya kuniona na huyu kijana wangu ambaye bila shaka ulimpa maagizo kwamba unahitaji kuweza kuonana na mimi?” mkurugenzi aliongea akiwa anafungua kifungo kwenye koti lake baada ya kuketi ili kufanya mazungumzo na Tommy akiwa sambamba na kijana wake Matiasi Ndugu waweza kumuita Nick.
“Ndiyo mzee”
“Kwanza nikupe pole sana kwa matatizo ambayo yameweza kukutokea wewe na familia yako lakini pia kwa ambayo mnayapitia kama familia kwani yanahitaji moyo ili kuweza kuyastahimili yote”
“Asante sana kwa hilo”
“Lengo la mimi kuja usiku huu hapa ni baada ya kupitia marejeo ya video zetu za siri ambazo unafanya mauaji ya kikatili sana namna ile ambayo kiukweli yamenisikitisha sana kwa sababu ni jambo la hatari mno. Ilitakiwa ukamatwe usiku huu huu wa leo lakini sijaona kama ni sahihi kufanya hivi kwa sababu mimi na mama yako tuna historia ndefu sana hivyo kwangu huwa namchukulia kama dada na sikuona ni jambo la busara kama nikikurupuka kabla ya kuweza kuja kuongea na wewe kwanza” mzee huyo kuhusu video alikuwa amedanganya ila ilikuwa ni moja kati ya njia za kuweza kumshinda adui yake hivyo hakuwa na namna zaidi ya kuitumia. Aliendelea;

“Kuja kwangu hapa, nahitaji mimi na wewe tuweze kufahamiana zaidi ili tuone kama naweza kukusaidia juu ya mambo ambayo bila wazi yatakuwa yanakusumbua sana ila hili ni kwa ajili ya taifa pia kwani haya mambo kama tukiruhusu yaendelee kutokea basi tutakuwa tunaliweka taifa letu kwenye hali ya hatari sana.”
“Unataka kunifahamu kwamba mimi ni nani?”
“Ndiyo”
“Mhhh mzee sioni kama ni jambo la busara sana, naona ni mapema sana”
“Hapana kijana wangu, kwa namna nilivyo kufuatilia najua kabisa kwamba wewe ni moja kati ya watu ambao wanafanya kazi na idara fulani ambayo huenda ni kwa siri sana hivyo mimi nahitaji nijue ni idara ipi ili tuangalie namna ya kuliweka taifa salama kwani nina imani kwamba hata wewe sidhani kama unatamani taifa hili liweze kuingia kwenye machafuko”
“Kabla ya kukujibu hicho unacho kihitaji nataka kwanza kujua nyie kama chombo ambacho ndicho mnahakikisha taifa lipo salama ni kwamba hamjui kinacho tokea nchini au mnajua na mnaamua kupuuza?”
“Mimi najua kila kitu kijana wangu”
“Sasa mbona umekaa tu haufanyi jambo lolote?”
“Mhhhhh sidhani kama nimekaa tu sifanyi lolote ila nchi yetu mifumo ya uendeshaji imekaa sehemu mbaya sana, siwezi kukwambia kila taarifa ila unatakiwa kujua kwamba hakuna jambo kubwa ambalo linaweza kufanyika ndani ya nchi bila ruhusa ya raisi hata kama tuna ushahidi nalo. Huenda sio tu namna uongozi wetu ulivyo ila hata katiba inamlinda yeye kufanya hivyo kwahiyo hadi kisheria anakuwa yupo sahihi na huwezi kushindana naye”
“Unamaanisha kwamba raisi ndiye mtu ambaye anakwamisha nyie kufanya maamuzi”
“Uko sahihi kabisa”
“Sasa wewe una mpango gani?”
“Nimekutafuta ili nifanye kazi na wewe bila mheshimiwa kuweza kutambua lolote lile”
“Unataka kufanya kazi na mimi?”
“Ndiyo”
“Kivipi mzee?”
“Ndiyo maana nataka tutambuane kwanza”
“Unaweza ukanipa taarifa zote ambazo labda zisijui?”
“Zipi?”
“Kuhusu wahusika wakuu wa hili tukio”
“Kwamba hujui kama Remsi ndiye ambaye alikuwa nyuma ya kila kitu?”
“Hilo nalitambua lakini sioni kama kijana kama yule anaweza kuwa anafanya haya mambo bila ya kuwa na mtu mzito ambaye anamlinda nyuma yake”
“Yeah upo sahihi”
“Kwahiyo ni nani?”
“Mr Mafupa”
“Kwanini?”
“Yule ni baba yake mzazi na yule bwana mdogo”
“Ohhhh shiiit! Kwahiyo ndiyo maana walimtumia dada yangu kwa sababu walikuwa wanahitaji kushinda kwenye siasa kwa kumuangusha baba yangu kwa staili kama hiyo”
“Yeah”
“Mwingine nani?”
“Huku mbele mambo ni mazito sana tunako elekea lakini kwa sababu tumeahidi kupeana ushirikiano acha nikwambie ukweli bwana mdogo ila hakikisha unaniambia pia ambacho nimekijia hapa”
“Huyo mr Mafupa anafanya kazi chini ya mtu kwa makubaliano maalumu japo yeye anamtumia mwanae kuweza kukamilisha mambo yake ambayo anayahitaji hususani kutimiza malengo yake ya kisiasa”
“Nataka jina la huyo mtu”
“Mr Oscar”
“Ndo nani?”
“Waziri mkuu wa zamani”
“Inawezekanaje?”
“Hii ni siri kubwa sana ambayo tumeipata kupitia baadhi ya vijana wetu ambao wanafanya nao kazi kwa ukaribu sana. Huyu bwana wakati akiwa kiongozi kuna mali ambazo aliwahi kujichumia kwa njia ambazo hazikuwa za halali hivyo tulifanikiwa kumtia nguvuni baada ya kuwasilisha ushahidi kwenye vyombo husika ambapo alipokonywa mali zake nyingi sana kwa kesi ya kuhujumu uchumi. Lakini alikuwa amefanikiwa kutengeneza mizizi mirefu sana ambayo imemfanya kuwa na watu wengi sana kwenye mifumo ya nchi hivyo anadaiwa kuwa moja kati ya viongozi wenye ushawishi mkubwa sana ndani ya chama chake lakini pia ni kiongozi mwenye nguvu kubwa sana”

“Sasa wakati wanaingia kwenye hili sakata la uchaguzi baada ya kuona kwamba baba yako ana nguvu kubwa sana ndani ya taifa hili na anapendwa kuliko mtu yeyote yule ndipo mr Mafupa alipo mtafuta mtu huyo kuweza kumuomba msaada wa kusaidiwa ili aweze kushinda kwenye uchaguzi wa sasa. Mtu huyu anadaiwa kwamba alikubali kumsaidia ila kwa masharti makubwa mawili, sharti la kwanza ni kwamba mr Mafupa ahakikishe anamrudishia mali zake zote ambazo zilibinafsishwa na hili mr Mafupa aliliahidi mwenyewe lakini jambo la pili ni kwamba ahakikishe anafanya kazi chini yake, kwa maana hiyo kama mr Mafupa ataingia Ikulu nchi itakuwa chini ya Mr Oscar jambo ambalo linaweza kuja kuwa hatari sana kwa upande wa nchi kwa ujumla”

“Yeye alikubali kumsaidia kwa kudili na mheshimiwa raisi ambaye amekubali kuyaachia madaraka na akawa amemuachia baba yako mr Mafupa mwenyewe amalizane naye na ndipo hapo yalipo anza kutokea haya mambo yote ambapo pia inasemekana kwamba kuna kikao cha siri sana ambacho kilikuwa kinaendelea siku chache kati ya raisi na mr Oscar na baada ya muda mchache raisi ameonekana kukubali kuachia kiti na kuanza kumpigia chapuo mr Mafupa aweze kuingia Ikulu.”

“Tunajaribu sana kufuatilia kwa ukaribu ili tuweze kujua walikuwa wameingia makubaliano yapi hasa mpaka raisi akubali kuiachia Ikulu kirahisi sana namna hii maana imeleta mshtuko mkubwa na huenda taifa linaweza kuingia kwenye hatari kubwa hivyo tumekuwa na kazi kubwa ya kuwafuatilia watu hawa watatu ambao wanaonekana kuwa makini sana kwa kila hatu ambayo wanaipiga” mkurugenzi aliamua kumpa siri nzima namna mchezo ulivyo kijana huyo ili aweze kumuamini kwani kweye moja kati ya njia za kuweza kumfanya mtu afunguke kuhusu mambo ambayo huenda kwake ni ya siri sana inatakiwa kwanza umpe imani kwamba wewe unamuamini sana na ndiyo maana umekuwa tayari mpaka kumpatia siri zako za ndani sana ambazo huenda zilikuwa ni kwa ajili ya watu ambao unawaamini isivyo kawaida.

Tommy alihema kwa nguvu sana kwa sababu alihisi anapambana na mtu mmoja kwenye huo uwanja wa vita ambao ramsi alikuwa ameuingia lakini kumbe kulikuwa na kundi kubwa sana la watu ambao walikuwa ni wazito sana, alitakiwa kuwafuatilia kwa umakini sana.
“Kwahiyo huenda hata mheshimiwa anahusika sio?”
“Sina jibu la moja kwa moja kuhusu hili ila simwamini sana mheshimiwa raisi kwa sababu ni mtu ambaye anayatanguliza sana maslahi yake mbele kuliko maslahi ya nchi kitu ambacho kimenifanya mimi kuwa na hisia naye mbaya sana. Unajua changamoto kubwa ni kwamba hakuna mtu ambaye anaruhusiwa kumfuatilia raisi hata mimi sina hiyo ruhusa hivyo haijalishi kwamba nina ushahidi kiasi gani wa madudu ambayo anayafanya katiba inazuia mimi kumfanya lolote lile kwani kiitifaki yeye ni bosi wangu. Kwahiyo kukujibu ni kwamba simwamini kabisa ila sina ushahidi wowote wa kutosha juu yake kuhusu haya ambayo yanaendelea japo huenda kuna mkono wake pia” aliongezea maelezo hayo mzee huyo huku Nick akiwa anawasikiliza kwa umakini sana wataalamu wawili hao wakiwa wanaongea mambo mazito sana huku akiwa na hamu kubwa ya kumuona Tommy akifunguka ukweli wa maisha yake.
UKURASA wa 40 narush shilingi.

Wasalaam,

Febiani Babuya
 
SIMULIZI: ELECTION SAGA (MONEY IN BLOOD)
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+

UKURASA WA AROBAINI NA MOJA

“Mimi sipaswi kukuamini kabisa wewe hata kama umenipa baadhi ya taarifa za mhimu wakati huu maana nina uhakika umenipa taarifa ambazo umeona hata nikizijua hazitakuwa na madhara yoyote yale ila nitakupa ufafanuzi mdogo sana kuhusu maisha yangu, nakupa taarifa chache kuhusu mimi na hizo taarifa kama mkizitumia vyema zitawasaidia sana lakini kama mkishindwa kuzitumia vizuri basi huenda mkapata madhara makubwa tofauti na unavyoweza ukafikiria” mwanaume aliongea na kutulia kidogo kisha akaendelea tena.

“Mpo sahihi kwa hisia zenu za kuhisi kwamba nilikuwa nafanya kazi chini ya moja kati ya mashirika ya kijasusi, mimi natokea kwenye shirika la MI6 ambalo naweza kusema hatupo wote kwa sasa japo wao wanadai bado mimi ni mtu wao. Ni stori ndefu sana ila mimi nitakupa baadhi ya taarifa zangu kwa ufupi kwa namna ambayo naona inafaa nyie kuweza kuzipata na kuzijua na ambazo hazitakuwa na madhara kwa upande wangu na kwenu pia” Tommy aliongea kwa sauti yake nzito huku akiwa anampa taarifa ambazo aliona zinafaa kuwapa watu hao kuanzia siku anaingia ndani ya taifa la Uingereza mpaka siku hiyo ambayo alikuwa nao mbele yao. Walichoka wote wawili kwani mawazo ya nick yalikuwa sahihi sana kuhusu kumshtukia mtu huyo.

“Sikujua kwamba ndani ya nchi yetu tunaishi na kiumbe hatari sana namna hii” mkurugenzi aliongea akionyesha wazi maskitiko makubwa sana ya kuweza kushindwa kulitambua jambo hilo mapema.
“Hivyo ndivyo wanadamu wanavyo ishi, viumbe hatari huwa havijulikani siku zote na ukifanikiwa kuvijua basi siku zako zinakuwa zinahesabika ili siri iendelee kutunzwa. Mimi hapa nimewaambia mkiwa wawili tu hivyo kama hili jambo likijulikana mahali popote najua watu wa kudili nao ni nyie wawili” Tommy aliongea kuonyesha msisitizo mkali sana juu ya hilo jambo ambalo aliwapa ukweli wake.

“Samahani nimeona umegusia swala la kirusi hapo bado sijakuelewa” Nick alilazimika kuulizwa kwa mara ya kwanza baada ya kuyasikiliza maongezi hayo kwa umakini mkubwa sana. Tommy alimgeukia kijana huyo akamwangalia kwa umakini sana kisha akayarudishia macho yake kwa mkurugenzi na kusikitika pakubwa mno.

“Kirusi hatari zaidi hapa duniani kipo ndani ya nchi yenu na vyombo vya usalama hamjui hata kidogo? Gaidi wa kundi la ISIS yupo ndani ya nchi aliingia na hata akiamua kutoka anatoka muda wowote na bado watu wenye mamlaka ya kulilinda taifa hamna hata taarifa moja? Hili ni jambo la hatari sana kwa nchi kwa sababu kama huyo mmoja ameingia unahisi kwa mwaka wanaingia magaidi wangapi na kutoka bila kujulikana? Vipi kama maeneo ya mhimu kama Kariakoo yakivamiwa mnajua watapotea watu wangapi wasiokuwa na hatia yoyote? Hili ni jambo ambalo binafsi mnapaswa sana kujitafakari hususani wewe mkurugenzi kwa sababu itaonekana hakuna kazi ya maana ambayo mnaifanya zaidi ya kula kodi za wananchi tu” mwanaume alimpasulia bosi huyo ukweli, mzee huyo alibakia akiwa anameza mate kwa shida sana kwa sababu aliambiwa ukweli mtupu, ulikuwa ni uzembe mkubwa sana kwao kuruhusu mambo kama hayo kutokea na huku wakiwa hawana taarifa.
“Nahitaji msaada wako Thomas”
“Msaada wangu?”
“Ndiyo”
“Kivipi labda?”
“Nahitaji kuhakikisha hiki kirusi ambacho unakisemea kinapatikana na huyu gaidi tunamtia kwenye mikono yetu kwa sababu hatujui ana malengo gani haswa na kirusi hiki ambacho umekitaja hapa”
“Kiongozi, nafikiri kwenu jambo la kumjua gaidi au kukipata kirusi sidhani kama ni la mhimu sana kwa sasa kwanza kwa sababu hamuwezi kukipata lakini jambo la pili ni mhimu kujua lengo kubwa la hicho kirusi ni nini kabla ya kuanza kumtafuta mhusika kwani mnaweza mkafanikiwa kumpata na kumuua mkipenda lakini tatizo likabaki pale pale maana nina uhakika hamjui kwamba kama huyo gaidi yupo pekeyake au na wenzake wengine ambao huenda hawatambuliki” Tommy aliongeza

“Una maanisha nini kusema kwamba hatuwezi kukipata?”
“Kwa sababu kipo kwa bosi wako”
“Una maanisha raisi?”
“Ndiyo”
“Hili haliwezekani”
“Unahisi ni jambo gani haliwezekani hapa duniani inapo wekwa pesa mbele ya watu?”
“Mhhhh kivipi raisi ajiingize kwenye uharamia mkubwa kama huu na wewe hizi taarifa umezijuaje?”
“Kwa sababu mimi ndiye ambaye nilikitengeneza hicho kirusi”
“Whaaaaaaaat?” Nick na bosi wake walijikuta wote wakiuliza kwa mshangao mkubwa sana hivyo mwanaume akawapa historia ya namna alivyo fanikiwa kukitengeneza kirusi hicho mpaka kikafanikiwa kuja kufika ndani ya nchi ya Tanzania na mheshimiwa raisi akawa amekihifadhi Ikulu sehemu ambayo waliamini kwamba hakuna mtu ambaye alikuwa anaweza kukifikia.

“Na leo usiku ndio muda ambao raisi anaenda kukutana na gaidi huyo kwa ajili ya makubaliano ya mwisho kabisa ya kuweza kufanya biashara ya hicho kirusi ambacho kinadaiwa kwamba kinaweza kuuzwa ndani ya falme za kiarabu huko kwa pesa nyingi sana”
“Wanakutania wapi?”
“Kwa taarifa ambayo nimetumiwa muda mfupi inasemekana kwamba wanakutana ndani ya hoteli ya Johari Rotana ambapo majira ya usiku huu wa manane hakuna mtu ambaye anaruhusiwa kuwepo eneo lile yaani limekodiwa lote kwa najili tu ya watu hao kukutania hapo”
“Saa ngapi itakuwa?” Tommy hakujibu kwanza bali aliitazama saa yake ambayo ilikuwa inasoma ni saa saba na nusu usiku.
“Kwa maongezi yake anadaiwa kwamba muda ambao alikubaliana na mtu wake ilikuwa ni saa saba kamili usiku”
“Kwahiyo tumesha chelewa?”
“Ulitaka kufanya nini?”
“Nilitaka nikipate kirusi hicho pamoja na huyo mtu”
“Unamaanisha unahitaji kumvamia raisi?”
“Yeah naweza kutuma watu ambao hawajulikani pale wakamkamate huyo mwanaume ambaye ndiye mwenye hicho kirusi pamoja na kirusi chenyewe au nikaenda mimi mwenyewe na vijana wangu”
“Unahisi kwamba unaweza kukipata kwa kufanya jambo la hatari sana namna hiyo?”
“Kama ningwahi ningekipata nina uhakika, siwezi kukaa na kuangalia jambo la hatari namna hii linafanyika ndani ya nchi yangu na nikawa naangalia tu ilikuwa ni lazima nifanye jambo”
“Kumbuka hiki kirusi kinatafutwa na watu wengi sana”
“Hakuna mtu mwingine ambaye anaweza kukipata zaidi yangu”
“Unajua watu ambao niliwatengenezea walinilipa shingapi mpaka wakiache kijinga tu hivyo?”
“Hilo mimi sijali nataka kukipata”
“Unataka kushindana na taifa la Uingereza?”
“Hii ni nchi yangu na hata siku wakija basi hawawezi kuingia bila ruhusa yangu” Tommy alimwangalia sana mzee huyo na kusikitika sana
“Hao ambao unataka kushindana nao ndio watu ambao wana taarifa za kutosha kuhusu kila jambo ambalo linakihusu kirusi hicho. Ni watu ambao wapo ndani ya nchi hii kwa kazi hiyo kwa miaka mitatu halafu wewe unataka kushindana nao?”
“Unamaanisha majasusi wa kiingereza wapo ndani ya nchi hii kwa sababu ya hiyo kazi?”
“Wana watu mpaka ndani ya Ikulu hivyo kuwa makini sana na hesabu zako ambazo unazipiga. Licha ya kuwasiliana kwamba ni saa saba lakini watu hawa huwa wanawasiliana kwa njia ya siri ambayo hata kama kuna mtu atafanikiwa kuyasikiliza maongezi yao hawezi kuelewa. Kwenye kila muda ambao wanautaja basi wanaongeza masaa mawili mbele ndipo wanakutana maana yake kama amesema saa saba usiku basi ujue wanakutana saa tisa usiku hivyo kazi kwako kama unahitaji kukutana nao. Mnaweza kuondoka kwa sasa mama yangu atakuwa na wasiwasi sana na mimi nimechoka nahitaji niweze kulala” Tommy aliona watu hao kama hawana mpango wa kuondoka basi alilazimika kuwafukuza kiaina.

“Kabla sijaondoka, naweza kujua kwamba una mpango gani labda?”
“Hawa wote ambao umenitajia hapa sina muda wa kupoteza nao bali nawaua wote”
“Hapana usifanye hivyo, kuna jambo ambalo naomba unisaidie hapa”
“Unataka kusemaje kiongozi?”
“Hawa watu naomba usiwaue haraka sana namna hii kwa sababu kila mmoja wao atatusaidia sana kukamilisha ushahidi endapo hili la leo litashindikana hivyo nakuomba sana uwape muda kwanza wa kuishi ili tukamilishe kazi ambayo italeta mabadiliko makubwa sana hata kwa maraisi ambao watakuwa wanafuata huko mbele. Najua una hasira nao sana kwa yale ambayo waliyaleta kwenye familia yako ina nahisi ni salama zaidi kama tukiumaliza huu umoja ambao unaonekana kutengenezwa wote kwa ujumla na kutusaidia kukipata kirusi hicho”

“Mimi sifanyi kazi na nyie sasa kwanini unahisi kwamba naweza kuwasaidia nyie?”
“Kwa sababu wewe ni mtanzania Tommy, wewe ni mzaliwa wa nchi hii, kama ulivyo eleza kwamba ulikubali kukitengeneza kirusi hicho ili kuikoa nchi kuwekewa vikwazo vya kiuchumi lakini pia kuzuia machafuko ya kisiasa hivyo hivyo pia najua hauwezi ukaiacha nchi ya mama yako inaingia kwenye machafuko ambayo yatasababisha maisha ya watanzania wengi wasio na hatia kuweza kupotea kizembe sana” Mzee huyo aliongea kinyonge sana huku akiwa amesimama kujiandaa kutoweka eneo hilo. Tommy alimwangalia sana mzee huyo tena kwa umakini mkubwa sana.

“Mimi sijali sana kuhusu hicho kirusi ila nitawapa muda mfupi sana muweze kukamilisha jambo lenu ila kwa sharti moja”
“Nakusikiliza”
“Nahitaji kwanza nimuue yule kijana Remsi kwa sababu mbili. Kwanza kwa alicho mfanyia dada yangu lakini jambo la pili ni kwamba nimefanikiwa kukipata kichwa cha mdogo wangu hivyo jesho tutafanya mazishi yake. Siwezi kumzika mdogo wangu huku mtu ambaye amemuua anakula maisha na kubadilisha wanawake akituona kwamba sisi ni washenzi sana, hilo siwezi kuliruhusu kabisa huyo anatakiwa kufa kesho kwa gharama yoyote ile. Lakini pia kuna masharti mawili madogo” mwanaume alikuwa anaongea kwa msisitizo mkali mno kiasi kwamba alikuwa anamaanisha sana kile ambacho alikuwa anakisema.

“La kwanza hakikisha kesho DCI anazungumza na vyombo vya habari na kutengua kauli yake kuhusu baba yangu tena aombe msamaha hadharani nitakuwa nimemsahe ila kama hatafanya hivyo basi hataimaliza siku ya kesho atakufa na makubaliano yangu na wewe yatakuwa yameishia hapo. Lakini la pili ni kwamba kuanzia sasa sitaki kuja kuona wala kusikia kwamba kuna vijana wako ambao wananifuatilia mimi au familia yangu. Kama ukifanikisha hayo masharti ambayo kwa ujumla wake yanakuwa matatu basi naweza kusema ombi lako litakuwa limekubaliwa lakini kama utaenda kinyume na haya ambayo nimekwambia hapa basi utashuhudia mambo ambayo yatakufanya wewe mwenyewe utamani kuweza kuihama nchi yako” mwanaume aliongezea ujazo pale ambapo alikuwa anahisi hapakujaa vizuri.

41 NISEME bye bye.

Wasalaam,

Febiani Babuya.
 
SIMULIZI: ELECTION SAGA (MONEY IN BLOOD)
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+

UKURASA WA KWANZA
Ndani ya ofisi moja kubwa sana, alikuwa anaonekana tajiri mmoja ambaye bila shaka umri wake ulikuwa umeenda kiasi cha kutosha. Mzee huyo mwenye kitambi cha wastani ambacho kiliashiria ukwasi ambao alikuwa nao, alikuwa ameketi kwenye meza yake ghorofa ya juu zaidi ndani ya ofisi yake hiyo.

Meza yake upande wa mbele ilikuwa imeandikwa CHAIRMAN kwa maandishi makubwa kisha likafuatia jina lake ambao lilisomeka kama Apson Limo, bila shaka yeye ndiye ambaye alikuwa mmliki wa hizo ofisi kama sio kampuni kwa namna ilivyokuwa inaonekana humo ndani. Ofisi ilikuwa imepambwa kwa vitu vya gharama sana huku ukutani kukiwa na picha kubwa mbili ambazo zilionekana kwa usahihi sana.

Kulikuwa na picha moja ya kawaida ya muasisi wa taifa la Tanzania hayati Julius Kambarage Nyerere lakini pia upande wake wa juu palikuwa na picha kubwa sana ambayo bila shaka ilikuwa ni ya familia. Kwenye picha hiyo alikuwa anaonekana yeye, mama mmoja ambaye bila shaka alikuwa ni mkewe lakini pia walikuwa wanaonekana watoto watano ambapo kati ya hao watoto watano, mmoja tu pekee ndiye alikuwa ni mtoto wa kiume kati yao. Ni picha ambayo ilikuwa inaonyesha namna familia hiyo ilivyokuwa kwenye furaha kubwa sana maana wote walikuwa ndani ya tabasamu zito mno ambalo usingeweza hata kujisumbua kulielezea kwani mtu angeiona tu picha hiyo angeelewa ni kwa namna gani familia hiyo ilikuwa kwenye hiyo furaha kubwa.

Upande wa mkono wa kulia mwa ofisi hiyo ukutani, kulikuwa na maneno makubwa ambayo yalikuwa yanang’aa sana yakiwa yapo chini ya nembo ya kampuni hiyo yakiwa yanasomeka LIMO INVESTMENTS. Ofisi hiyo kubwa ilikuwa pia imenakshiwa kwa vito vya thamani sana ikiwemo na samani za kutosha huku ikiwa na sehemu nzuri sana ya wageni kuweza kukaa na sehemu ya kufanyia mazungumzo ambayo yangekuwa ya mhimu na kumfanya mhusika aongee na tajiri huyo moja kwa moja.

Mzee huyo akiwa ametulia kwenye hilo eneo anaangalia kwa umakini sana jina la kampuni yake ukutani na kuwaza namna alivyoweza kutoka mbali na kampun hiyo mpaka ikaja kusimama vyema na kuwa moja kati ya makampuni makubwa sana nchini, simu yake ya mezani ilimshtua kutoka kwenye mawazo baada ya kuanza kupiga kelele kwa nguvu, akaipokea.

“Mruhusu aingie” ni kauli moja tu ambayo aliitamka bila shaka aliipokea simu ya ugeni kutoka kwa katibu wake ambaye alimpa ruhusa kuweza kumruhusu mtu ambaye alikuwa amefika hapo. Ndani ya muda mfupi mlango ulifunguliwa, aliingia mwanaume mmoja ambaye naye umri ulikuwa umemtupa mkono kidogo akiwa ndani ya suti ya gharama mno na fimbo yake mkononi bila shaka.

“Karibu sana Mr Mafupa” alimkaribisha mgeni wake huku akiwa ananyanyuka kwenye kiti chake na kumpa mtu huyo mkono na ilionekana kwamba walikuwa wakijuana sana.

“Nadhani sio waafrika wote ambao hawajastaarabika, kuna watu mpo safi sana na huo ndio utamaduni wetu waafrika bwana lazima tusalimiane kwanza hata kama hatupo sawa” Mr Mafupa alijibu naye huku akiwa anaukutanisha mkono wake na mheshimiwa Apson Limo.

“Ujinga wa mtu mmoja usiujumlishe kwa waafrika wote, sio kawaida sana wewe kuja hapa, nilivyo ipata taarifa kwamba unahitaji kuniona nilishtuka kidogo kwamba kwanini usingesubiri sehemu nyingine nje na hapa tukakutana ila nikaamua kukubali kwa sababu nilijua huenda una shida ya mhimu sana” mr Apson aliongea akiwa anaketi baada ya kuhakikisha pia mgeni wake ameketi chini kwa ajili ya mazungumzo.

“Mhhhh sehemu yoyote ile inafaa kwa mazungumzo hususani kwa wanasiasa na wafanya biashara kama mimi na wewe, vipi mwanao alisharudi kutoka masomoni? Maana ni muda sana naskia yupo nje ya nchi”

“Sio muda anarudi nadhani kwa sasa amemaliza masomo yake”

“Kwahiyo anakuja kumsaidia baba yake kwenye mambo ya kampeni? Maana ndiye mtoto wa pekee wa kiume uliye naye”

“Ni vizuri kama ungeenda moja kwa moja kwenye maada ambayo imekuleta hapa sidhani kama mambo ya familia yangu yanakuhusu sana au yana umuhimu kwa hapa tulipo”

“Sawa ila yanaweza kuwa na umuhimu mkubwa sana kwa hapo baadae ndiyo maana nakuuliza usidharau sana. Lengo la mimi kuja mpaka hapa kwenye ofisi yako kuna makubaliano ambayo nahitaji tuyafanye mimi na wewe. Ni makubaliano ya mhimu sana ambayo yanakubidi wewe ufanye maamuzi ya kiume, narudia tena ni ya mhimu sana mr Apson”

“Nenda moja kwa moja kwenye hoja ya msingi acha kuzunguka mr Mafupa”

“Nahitaji ujitoe kwenye mbio za kugombea uraisi”

“Hahahaha Mr Mafupa nadhani uliko toka umelewa sio? Hivi unajua hata kuja hapa nimekukubalia tu kwa sababu nakuheshimu sana, huu muda mimi na wewe ni wapinzani sidhani kama ni sahihi kukutana kutana kirahisi sana namna hii maana wananchi wakijua wanaweza kuanza kuwaza mambo mabaya, nadhani kama hauna jambo la mhimu la kuongea na mimi ni vizuri zaidi kama utanyanyuka na kutoka nje ya ofisi yangu kisha usije ukarudi tena hapa maana nitafanya kama sijawahi kukufahamu”

“Najua mr Apson, najua kwamba ndani yako kuna moto unawaka sana hususani pale ambapo unakuwa unaiwaza ile Ikulu, unawaza namna watu wanavyo yasimulia maisha ya pale ukiwa kama ndiye kiongozi mkuu maana hata baadhi ya vikao vingi na mialiko mikubwa ulikuwa unaipata ila nimekuja kukuomba kistaarabu sana achia hiyo nafasi na awekwe mtu ambaye ni dhaifu na hawezi kuniyumbisha kwa sababu mimi nahitaji kuingia pale Ikulu kisha kuna makubaliano ambayo mimi na wewe tutaingia hata nikiingia Ikulu utakuwa kama mkono wangu wa kulia”

“Makubaliano yapi hayo Mr Mafupa ambayo unahisi yatanishawishi mimi kukubali kuwasaliti wananchi wangu ambao wameniamini na kuniruhusu mimi kuingia Ikulu na kuahidi kunipa kura zao za ndiyo na kwa sababu ipi hasa?”

“Kuna mpango ambao nimeuandaa, sababu tutatengeneza ugonjwa feki na kudai kwamba utakuwa nje ya nchi hospitali kwa mwaka mzima ambapo uchaguzi utakuwa umekamilika na hauwezi kuchaguliwa mtu ambaye upo hospitali hivyo watatakiwa kusubiri mpaka upone. Mwaka ukiisha mimi nitakuwa tayari Ikulu na wewe nitakuteua uwe makamu wangu kwa kuwaahidi wananchi kwamba utaingia Ikulu kama wanavyo hitaji kwenye uchaguzi ambao unafuata huku wakihisi kwamba hakuna tatizo baina yetu ni upendo tu umetawala ndiyo maana nimekupa nafasi kubwa ya umakamu wa raisi na hayo mambo inabidi uyathibitishe wewe mwenyewe kwenye vyombo vya habari. Ukikubali tu kutoka kwenye hiyo nafasi, utaingiziwa bilioni mia moja kwenye akaunti yako maana mimi najua namna ya kuzirudisha nikiingia Ikulu kisha tutaingia mikataba ya kibiashara mimi na wewe ambayo itatusaidia kutengeneza pesa kadri tutakavyo na kutufanya kuwa miongoni mwa watu matajiri sana hapa Afrika”

“Kwahiyo unahisi bilioni mia moja na hiyo mikataba ndiyo itanifanya mimi niuze uzalendo wangu na kuwasaliti wananchi wangu na kuuza utu wangu? Mr Mafupa tangu unatoka kwako ulitakiwa kuwaza kwa umakini aina ya mtu ambaye unaenda kuongea nae. Kwahiyo umeona kwamba mimi nina njaa sana na unaweza kuninunua kwa hiyo pesa? Umekosea sana, nitafanya kama hili hujaliongea naomba utoke kwenye ofisi yangu”

“Koh, koh, Mr Apson mimi huwa ni mara chache sana kumuomba mtu jambo ambalo naweza kulifanya hata kwa lazima bila mapenzi yake, mpaka nakuja kukuomba hapa ni kwa sababu nimeamua kukuheshimu kama rafiki tu japo hatujawahi kuwa karibu. Mimi Ikulu naingia kwa gharama yoyote ile na haujui kwanini naihitaji sana ile Ikulu. Hivi umewaza labda kwamba kwanini nimekubali kuingia kwenye kinyang’anyiro na mheshimiwa raisi ambaye yupo madarakani wakati nipo naye chama kimoja? Ungejua hayo basi hiyo nafasi ungeiachia mwenyewe bila kulazimishwa. Unaongelea uzalendo kwenye nchi hii ambayo wananchi wakipewa hata noti moja tu wanauza utu wao? Uzalendo upi labda ambao unakufanya ujione wewe ndiye ulizaliwa kwa ajili ya hii nchi? Jambo la msingi zaidi ambalo wewe unapaswa kuliwaza sana kabla ya kufanya maamuzi yoyote yale ni familia ndugu yangu. Nitajisikia vibaya sana kama itafikia hatua ya kunilazimu niingie mpaka upande wa familia wakati una nafasi ya kufanya maamuzi sahihi, una wanao ambao ni waz…….”

“Stooop! mjinga wewe, una jeuri gani ya kuiongelea familia yangu mbele yangu kirahisi sana namna hiyo? Nitakupiga risasi nikuzike humu humu ndani kwangu. Nisije nikakusikia tena ukiwa unaitaja familia yangu kirahisi sana namna hiyo, mimi siyo kama wewe ambaye unashinda na hao wanawake ambao unawabadilisha kila siku kama nguo kwenye makasino. Tena ukija kutaja neno familia kwangu basi nitakuua hapo hapo” alikuwa amesimama mr Apson akiwa ameitoa bastola yake amemnyooshea mwanaume mwenzake huyo ambaye alionekana kwamba alikuwa ni mgombea mwenzake kwenye nafasi ya uraisi wa nchi ya Tanzania. Mwenzake huyo baada ya kushindwa kumshawishi aliamua kuitumia familia kama ngao ya kumdhoofisha na ndiyo sababu ya mr Apson kumnyooshea bastola mr Mafupa kwani kwake familia ndilo lilikuwa jicho lake aliipenda mno. Mr Mafupa alijikohoza kidogo na kumfungukia;

“Huo uwezo wa wewe kunipiga risasi mimi hauna kwa sababu watu wameniona naingia hapa hivyo nisipo toka lazima wewe ndiye utakuwa mhusika namba moja na kesho tu asubuhi magazeti na vyombo vya habari vitaandika kwamba umemuua mgombea mwenzako ili uingie Ikulu, unadhani nani atakuamini tena? Nani atatamani kukupigia kura tena wakati wewe ni muuaji na una tamaa ya madaraka? Hahahaha utakuwa unaisubiria jela wakati huo na familia yako haitakuwa na msaada wowote ule hivyo huo ubavu hauna wa kuiacha familia yako maana unaipenda mno, mpaka hapo nipo salama na hauwezi kunifanya lolote” alitulia kidogo kuacha maneno yamuingie vyema mr Apson kisha akaendelea.

“Mimi nimekuomba kistaarabu lakini umeishia kunidharau, unajua kuna maongezi ya wanaume yanatakiwa kufanywa kiume hata maamuzi yake yanatakiwa kwenda kiume pia na hivyo ndivyo siasa inavyotakiwa kuwa lakini kwa sababu hautaki kwenda kistaarabu basi mimi nitakuonyesha namna sahihi ya kuweza kuyafanya maamuzi magumu ukiwa hauna namna na huenda kwa wakati huo hautakuwa na namna zaidi ya kutoa kilio. Likumbuke neno familia kwenye kichwa chako mr Apson na ujue tu kwamba nitarudi na kwa sasa sitarudi kukubembeleza bali nitarudi na kukufanya ulie huku ukija mwenyewe mbele yangu kunipigia magoti na kuniomba kwamba umekubali masharti yangu ila huenda utakuwa umechelewa tayari”

“Out” aliongea kwa sauti kali yenye uchungu sana baada ya mr Mafupa kumaliza kujigamba mbele yake na kuitishia familia yake huku akiwa anaikoki bastola yake, mr Mafupa alitabasamu na kutoka humo ndani kwa dharau kubwa mno.

Mr Apson alipigiza bastola yake chini kwa hasira sana huku akiwa anahema kwa nguvu mno, aligeukia ukutani na kuangalia picha ya familia yake ambayo ilikuwa kwenye tabasamu zuri sana, moyo wake ulizidi kumuenda mbio isivyo kawaida. Alikusanya begi lake na kutoka haraka sana humo ndani, alitaka kuwahi nyumbani kwanza aione familia yake maana vile vitisho ambavyo alipewa pale alihisi huenda familia yake ilikuwa kwenye matatizo huku akiwa anaendelea kumpigia simu mkewe ambaye naye hakuwa akipokea basi alizidisha wasiwasi sana kwenye nafsi yake, siasa ilianza kumtokea puani mapema sana.

Ukurasa wa kwanza naweka nukta hapa. Niseme tu karibu sana tuweza kujumuika kwa pamoja ndani ya simulizi hii ili tuweze kujua kwamba imetuandalia nimi haswa ndani yake. Unataka kujua hilo salata la uchaguzi linahusiana vipi na hizo pesa kwenye damu? Basi usibanduke twende sawa.

Kwenye kalamu nipo mwenyewe, mwapenda kuniita Bux the storyteller lakini jina langu waweza kuniita;

FEBIANI BABUYA.

Wasalaam.View attachment 2818483

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
Weka PDF ya kitabu chote hapa. Mambo ya itaendelea kesho watu tunakaa tunakusubiri kama YOGA hatutaki.
 
SIMULIZI: ELECTION SAGA (MONEY IN BLOOD)
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+

UKURASA WA AROBAINI NA MBILI
“Deal Tommy” mzee huyo aliongea kisha wakapeana mikono na akaanza kutoka humo ndani ambapo alikuwa ameahidi kwamba alikuwa anatakiwa kwenda kumkamata gaidi ambaye usiku huo alikuwa na kikao kizito sana na mheshimiwa raisi. Mkurugenzi na kijana wake Nick waliondoka ndani ya eneo hilo bila hata kufanya mazungumzo na rafiki yake wa siku nyingi sana ambaye alikuwa ni mama mzazi wa Tommy kwa sababu alikuwa anawahi eneo ambalo aliamini kwamba angefanikiwa kumnasa gaidi aliyefanikiwa kuingia na kirusi ndani ya nchi ya Tanzania bila hata wao kuwa na taarifa.


Usiku wa kutisha.
Majira ya saa tisa usiku ndani ya eneo ambapo inapatikana moja kati ya hoteli kubwa sana na ya kifahari mno, ni hoteli ambayo pesa zako unazihesabu kwa mikono huwezi kushinda hapo kwani gharama yake ni ada za watoto shuleni, inaitwa Johari Rotana. Ndani ye eneo hilo umeme ulikatika ghafla sana jambo ambalo huenda lilikuwa la ajabu sana ndani ya sehemu kama hiyo umeme kuweza kukatika kirahisi sana namna hiyo kwani ni jambo ambalo halikuwa la kawaida kabisa.

Baada ya umeme huo kuweza kukatika, yalionekana magari ya kifahari sana kumi yakiwa na namba za Ikulu yakiongozana ndani ya eneo hilo ambapo geti lilifunguliwa na gari hizo zikaingizwa sehemu maalumu ambayo hata mtu angeingia humo ndani basi asingeweza kukubali kwamba humo ndani kulihifadhiwa gari nyingi za kifahari.

Ndani ya gari moja ambayo ilizungukwa na wanaume wengi sana ambao walionekana kuwa wa kazi isivyo kawaida ailishuka Boniphace Walawala akiwa kwenye suti yake nzito sana ambayo iliushika vyema mwili wake na kumpendeza sana. Baada ya mheshimiwa huyo kushuka walisogea mpeka mbele na kuingia kwenye lifti huku akiwa na walinzi wa kutosha.
“Mgeni alishafika bila shaka”
“Ndiyo mkuu”
“Hakikisha hakuna uzembe wala ujinga wowote ambao unafanyika ambao unaweza kupelekea jambo lolote lile la kijinga kuweza kufanyika au hata mgeni wetu kuweza kupatwa na tatizo lolote lile” alikuwa akiongea na kijana wake wa kazi ambaye bila shaka alikuwa ndiye mlinzi wake mkuu, mwanaume ambaye alikuwa na mwili wa miraba minne haswa.

“Sawa mkuu” alijibu kwa unyenyekevu mno kwani huyo ndiye mtu ambaye alikuwa akimpa uhakika wa kusihi vizuri kwa mshahara mnono ambao alikuwa anampatia. Baada ya kushuka kwenye lifti alikuwa anakiangalia chumba ambacho kilikuwa juu kabisa ya ghorofa hilo mbele yake. Waliingia walinzi wa kutosha kwanza ambapo walifanya uchunguzi wa kutosha ili kuhakikisha kwamba kiongozi wao anakuwa salama kwa namna yoyote ile.

Baada ya muda mfupi waliweza kutoka nje huku wakimpa ruhusa kiongozi huyo kuweza kuingia ndani ya chumba hicho ambapo alitakiwa kuingia akiwa mwenyewe kwani mazungumzo ambayo yangeendelea huko yalikuwa ya siri sana.

Nusu saa ilipita tangu mheshimiwa aweze kuingia humo ndani lakini ghafla sana zilisikika kelele upande wa nje kitu ambacho kilizua taharuki sana na kuleta wasiwasi, hivyo walinzi walijipanga kwenye mlango wa chumba hicho ambapo mlinzi mkuu wa mheshimiwa aliingia ndani kabisa ya chumba hicho lakini raisi hakuonekana kuwa na wasiwasi wowote ule licha ya mambo yote hayo kuweza kuendelea ndani ya jengo hilo. Walinzi wengine walishuka huko chini ili kuweza kuona kwamba ni kipi kilikuwa kinaendelea usiku huo lakini walirudi wakiwa wameongozana na mwanaume ambaye umri ulienda akiwa kwenye suti nzito sana.

Wengi walikuwa wanamfahamu sana hivyo waliishia kuinama kumpatia heshima yake kwani alikuwa ni mkurugenzi wa usalama wa taifa na vijana wote hao ambao walikuwa wanamlinda raisi kabla ya kupewa kazi hiyo walipita kwenye mikono yake hivyo kwao bado alikuwa ni bosi ndiyo maana hakuweza kabisa kugushwa na mtu yeyote yule. Basi ikabidi taarifa iweze kutolewa mapema sana kuhusu uwepo wake ambapo raisi alimruhusu kuingia humo ndani.

Mkurugezi Lingson Mfwomi aliingia kwa pupa sana ndani ya chumba hicho huku akiwa anangaza kila upande kuona kama kuna jambo jipya angeweza kuligundua. Hakuona jambo lolote jipya zaidi ya kuona briefcase ya mheshimiwa pamoja na mwanamke mrembo sana ambaye alikuwa amekaa upande wa pili wa mheshimiwa raisi wakionekana wamekaa kimahaba sana.
“Heshima yako kiongozi” aliongea akiwa anajifuta jasho kwa sababu alihisi kumkosea sana mheshimiwa kwani alichokuwa anategemea kukiona kilikuwa ni tofauti sana na kile ambacho alikutana nacho.
“Hivi ndivyo kazi yako inavyokutaka kuhakikisha unanifuatilia mpaka kwenye mambo yangu binafsi bwana Lingson?” mheshimiwa aliongea kwa sauti ya ukali sana kitu ambacho kilimfanya mzee huyo achezeshe midomo yake ka kuhitaji kuongea jambo lakini aliishia kumwangalia kwa umakini sana yule mrembo ambaye alikuwa mbele ya mheshimiwa hivyo rahisi akaamua kumpa taarifa kijana wake kwamba amtoe mwanamke huyo.
“Mpeleke bibie kwenye hoteli ambayo amefikia nitafanya naye mazungumzo baadae” amri yake ilitekelezwa haraka sana na mlinzi wake huyo.
“Mheshimiwa naomba unisamehe sana kwa kuingilia starehe yako kwa sababu jukumu langu mimi la kwanza ni kuhakikisha kwamba nakulinda kwa masaa ishirini na manne hivyo baada ya kupata taarifa kwamba umetoka usiku huu nimeogopa sana kwa sababu ni jambo la hatari sana raisi wa nchi kutoka bila taarifa tena muda kama huu wa usiku, sikuwa na imani sana ndiyo maana nikaamua kufika mpaka hapa ili kuhakikisha kama kuna usalama wa kutosha” kiitifaki alichokuwa amekiongea kilikuwa ni sahihi sana lakini huenda kwa mheshimiwa hakikuwa sawa licha ya kwamba ambacho alikiongea ndio ulikua ukweli wenyewe.

Mheshimiwa kwenye macho yake ilionekana hasira ya waziwazi sana lakini asingeitumia hasira maeneo kama hayo ingefanya afikirike vibaya na kuonekana kwamba hakuwa raisi ambaye alikuwa anayajua vyema majukumu yake ya kazi.
“Usijali Lingson, nimefurahishwa sana na jambo hili la wewe kuonyesha kwamba unamjali raisi wa nchi yako na upo tayari hata kuweza kuyatoa maisha yako ili kuhakikisha tu kwamba anakuwa salama. Nadhani wewe ni moja kati ya viongozi bora sana mimi kuwahi kuwateua kwenye utawala wangu”
“Asante sana mheshimiwa”
“Umewezaje kujua kwamba nipo hapa?”
“Umesahau mheshimiwa kwamba kwenye mwili wako una vifaa maalumu ambavyo hata ukipotea inakuwa rahisi sana kuweza kukupata popote pale?” raisi alionekana kutikisa kichwa kukubali jambo hilo.
“Ni muda mrefu sana nashinda ofisini hivyo leo niliona ni vyema sana kuweza kupata muda wa kufurahi ndani ya eneo hili lakini asante pia kwa kujali uwepo wangu hapa”
“Ndiyo kazi yangu mheshimiwa”
“Umefikia wapi kwenye ile kazi yangu?”
“Nimewafuatilia kwa umakini sana familia ile lakini hawaonekani kuwa na jambo lolote lile ndani yao zaidi ya kuzidiwa na hofu kubwa juu ya mambo ambayo yametokea siku kadhaa hizi”
“Na yule bwana mdogo wa kiume?”
“Yule ni kijana wa kawaida sana mheshimiwa ambaye hana tatizo lolote lile hivyo sijaona haja ya kuendelea kumfuatilia sana maana tumechimbua taarifa zake zote na inasemekana kwamba baada ya mambo ya msiba kukamilika anaweza kukaa wiki chache tu na kuondoka nchini kwani anaona kama nchi hii haimfai asije akauliwa na yeye” mkurugenzi alionekana kabisa anampa mheshimiwa taarifa za uongo kwa sababu ambazo alikuwa nazo mwenyewe.
“Siasa ukiiendea kichwa kichwa ni mbaya sana na ndicho ambacho kimemponza Apson, alikuwa ni moja kati ya watu wabinafsi sana kuwahi kutokea kwenye nchi hii. Ubinafsi ni jambo baya sana kwenye kundi la watu wengi kwa sababu badala ya kupendwa unajikuta unaanza kuchukiwa na wale watu ambao ulipaswa kula nao wewe ukaleta ulafi wa kuweka umimi. Yule mzee maisha yake ameyaharibu yeye mwenyewe” mheshimiwa aliongea huku akiwa anatoka ndani ya hicho chumba ambapo waliondoka hilo eneo wote pamoja na mkurugenzi wa usalama wa taifa ambaye alikuwa makini sana kuweza kutazama kila sehemu kama labda angeweza kumuona mtu wa tofauti ambaye Tommy alimwambia kwamba angekuwa na kikao na mheshimiwa raisi lakini hakuambulia kitu chochote mpaka akaanza kuhisi kwamba huenda Tommy alikuwa anataka kumgombanisha na kiongozi wake.



Lakini wakati ule yule mrembo anatoka mle ndani, mita miambili kutoka ilipo ile hoteli alionekana mtu ambaye alikuwa kwenye mavazi meusi akiwa juu ya ghorofa lingine akiwa na jicho ya mwewe akiangalia umbali huo kwa umakini sana mpaka alipo muona mwanamke yule akiwa anashuka ndani ya jengo lile akiwa na walinzi wa kutosha naye alifunga kila kitu chake na kubeba begi lake mgongoni akaanza kushuka chini kabisa mwa jengo hilo akionekana wazi kwamba likuwa anataka kumuwahi mwanamke huyo.

Licha ya kuwa na mavazi meusi kila sehemu ya mwili wake bado mwonekano wake alionekana kuwa mwanamke mtu huyo. Baada ya kufika chini kabisa ya hilo jengo ambalo alikuwepo aliiwasha tablet yake mkononi ikiwa inaonyesha mjongeo wa magari ambayo bila shaka alikuwa ametega vifaa vya mawasiliano kwenye moja kati ya gari hizo ambazo zilikuwa kwenye msafara huo ambao alikuwa anauangalia wakati huo. Alikuwa makini sana kisha akapanda kwenye pikipiki yake na kuanza kuelekea usawa wa huo msafara ambao alionekana kuufuatilia kwa umakini sana wakati.

Kutokana na mwendo mkali ambao alikuwa nao alienda kuukuta msafara huo maeneo ya chuo cha CBE ambapo aliupita na kwenda kusimamisha pikipiki yake katikati ya barabara kitu ambacho kilipelekea msafara huo kusimama na wakashuka wanaume ambao walikuwa na silaha nzito sana kwenye mikono yao. Mwanaume mmoja alisogea kwenye hilo eneo lakini hakufanikiwa kuona mtu kitu ambacho kilimfanya atoe taarifa kwa wenzake kuongeza umakini kwani mtu huyo alionekana kwamba alijificha mahali baada ya kuitelekeza pikipiki yake hapo.

Mwanaume huyo ambaye alikuwa anaendelea kuikagua pikipiki hiyo alishuka chini taratibu akiwa ameishika shingo yake baada ya risasi kuitoboa vibaya sana hiyo shingo. Hali hiyo ilifanya wanaume ambao walikuwa hapo waongeze umakini na kulizunguka gari ambalo alionekana kuwepo mgeni wao ambaye bila shaka walipaswa kuhakikisha kwamba anakuwa salama wakati wote. Walinzi wote ambao walikuwa wamelizunguka gari hilo alikuwa anashuka mmoja mmoja chini kwani hawakuwa wakimuona mdunguaji aliyekuwa anawashambulia zaidi ya kuona mtu mmoja mmoja akiwa anashuka chini huku mitaa ikiwa imetulia isivyo kawaida.

42 Inafika mwisho.

Wasalaam

Febiani Babuya.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
SIMULIZI: ELECTION SAGA (MONEY IN BLOOD)
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+

UKURASA WA AROBAINI NA TATU
Baada ya dakika sita eneo lilibakia kimya sana huku akiwa amebakia mwanaume mmoja tu nje ya gari hiyo lakini kitu cha kushangaza mtu ambaye alikuwa ndani ya gari hiyo alikuwa ni yule mwanamke ambaye alikuwa na mheshimiwa raisi muda mchache ambao ulikuwa umepita akiwa amekaa na mlinzi mmoja ambaye alikuwa na asili ya kiarabu akiwa kwenye suti yake bila hofu. Mlinzi ambaye alikuwa amebakia nje ya eneo hilo aliona kuna mtu anakuja upande wake wakati akiwa anampa amri ya kusimama mtu huyo alikirusha kisu chake ambacho kilikita sehemu ya moyo wa mwanaume huyo kisha akamsogelea na kumchinja.

Alifungua mlango kwa pupa lakini alirudishwa na teke kali sana ambalo lilimrushia mbali isivyo kawaida huku akijibamiza kwenye kuta za chuo hicho cha biashara. Alishuka mwanaume ambaye alikuwa ndani ya gari hiyo pamoja na mwanamke ambaye alionekana kwa mara ya mwisho akiwa na mheshimiwa raisi.
“Kill her” ndiyo kauli ambayo ilitoka kwa mwanamke huyo na kitu cha kushangaza sana ni kwamba ilikuwa sauti ya kiume kabisa na wala haikuwa ya kike kama ilivyokuwa inaonekana. Mwanamke huyo alivua mawigi na kila urembo ambao ulikuwa kwenye mwili wake akabakia na vest tu pamoja na pensi fupi. Alikuwa ni mtu wa kazi haswa tena mwanaume ambaye alikuwa na asili ya kiarabu bila shaka.

Mwanaume yule ambaye alipewa amri ya kuweza kuua hakuwa na muda wa kupoteza tena zaidi ya kumshambulia mwanamke ambaye sura yake ilifunikwa mbele yake. Alikuwa yupo fasta sana kwani urushaji wake wa mateke mazito haukuwa ukipimika hususani kwa mtu ambaye mwili wake ulikuwa mzito sana kuweza kukabiliana na vitu ambavyo vinakuja haraka.

Mwanamke yule alijikuta anapokea mashambulizi makali sana tena ya ghafla isivyokuwa kawaida lakini hakuwa mnyonge kabisa kwani alijizungusha kwa mateke mengi ambapo yalitua kwenye kifua cha mwanaume huyo ambaye alienda kujibamiza kwenye gari moja mpaka ikabonyea lakini alisimama kama vile hakuna kilichokuwa kinatokea huku yule mwanaume ambaye ndiye alionekana kuwa mlengwa akiiwasha sigara yake bila hofu na kuendelea kuivuta akiwa anamuona mlinzi wake anashambuliana na mwanamke huyo.

Ngumi kali sana zilikuwa zinapigwa kati ya mwanamke yule mvamizi pamoja na mlinzi wa mtu huyo, ngumi ambazo zilidumu kwa dakika tano wakiwa wanapokezana mashambulizi kitu ambacho bila shaka mwanaume yule aliona kama wanampotezea muda. Aliingalia saa yake yake ya mkononi na kuona ni muda ambao watu wataanza kuingia ndani ya eneo hilo kufanya biashara hivyo inaweza kuleta tafrani sana alipaswa kupotea hilo eneo haraka sana iwezekanavyo. Wakati yule mwanamke akiwa anakuja kwa sataili ya nge ili kumshambulia yule bodyguard alikutanishwa na teke zito sana la shingo kutoka kwenye miguu ambayo ilivalishwa sendo ya yule mwanaume ambaye alikuwa kwenye kipensi chake.

Miguu ilikomaa sana kiasi kwamba kama mwanamke huyo hakuwa mtu wa kazi basi huenda shingo yake ingeweza kuvunjika muda ule ule baada ya kushambuliwa, alikuwa anatua vibaya kwenye ukuta lakini alifikia miguu na kudondoka chini lakini wakati huo mwanaume yule alizamisha mkono wake kwenye kiuno cha bodyguard wake na kuitoa bastola yake na kushambulia alipo mwanamke yule pale ukutani.

Alianza kukwepa risasi zile na kuamua kurukia ndani ya ukuta wa chuo hicho huku akiwa ameshikilia eneo la bega lake ambalo bila shaka kuna risasi ambayo ilikuwa imepenya hapo. Mwanaume huyo alikuwa anamfuata kwa kasi hakutaka kuacha ushahidi hivyo wakati anauparamia ukuta huo ili aweze kummaliza mwanamke huyo ambaye alidondokea kwa ndani alisikia sauti kali ya mtu akiwa anampa amri ya kusimama kama alivyokuwa.

Amri hiyo ilitoka kwa mlinzi wa chuo hicho ambaye alikuwa amelala usingizi, risasi za mdunguaji ambazo hazikuwa zikipiga makelele hazikumshtua kabisa kwamba hilo eneo kuna hatari kubwa inatokea lakini pia hata yale mapambano pale hakuyasikia kabisa kutokana na kupata muda mchache sana wa kupumzika kwani usiku alikuwa chuo na mchana alitakiwa kuingia mtaani kupambana na mtaa. Hivyo ule mlio wa sauti ya risasi ambazo alizipiga mwanaume yule ndizo ambazo zilimshtua na kumuamsha ndipo naye akaamka na kumuona mwanaume huyo akiwa na bastola kwnye mkono wake huku akionekana kwamba kuna mtu ambaye alikuwa anamshambulia wakati huo. zile kelele zake za kumsimamisha mwanaume huyo zilimfanya kuchukia sana kwani mlinzi huyo ndiye ambaye alifanya mwanamke huyo afanikiwe kupotea hilo eneo alijua kabisa kwa muda huo asingeweza kabisa kumpata. Mwanaume huyo aligeuka kwa hasira sana ambapo alimmininia mlinzi huyo risasi mbili ambazo zilikuwa zimebakia ndani ya bastola hiyo na kuingia kwenye gari ambapo aliondoka na mlinzi wake kwa kasi sana.

Ni kweli kama asingekuwa mlinzi huyo yule mwanamke ambaye mtu huyo alikuwa anamfuatilia huenda angekufa kwani alikuwa amejibanza tu ndani ya ukuta ndani ya fensi hiyo kiasi kwamba kama mwanaume huyo angeingia ndani tu basi alikuwa anamuona mbele yake moja kwa moja na huenda angemuua hivyo kifo cha mlinzi kikawa usalama wa mwanamke huyo. Baada ya kuhakikisha kwamba watu hao wametoweka hata yeye hakutakiwa kabisa kuzubaa ndani ya hilo eneo kwani alijua polisi wangefika hapo muda wowowte ule kuanzia wakati huo.

Alimsogelea mlinzi huku na yeye akiwa anavuja damu kwenye bega lake kwa risasi ambayo alikuwa amepigwa, mlinzi huyo alikuwa amekufa tayari, alisikitika sana na kupanda kwenye pikipiki yake na kutoweka kwa kasi kubwa sana ndani ya eneo hilo ambapo muda mchache tu baada ya yeye kuondoka vilisikika ving’ora vya polisi vikiwa vinaelekea ndani ya lile eneo.

Baada ya kufika mbali na lile eneo mwanamke yule alikivua kile kitambaa chake usoni ili aweze kupumua vizuri maana hata hali yake haikuwa nzuri sana. Sura haikuwa ngeni kabisa, alikuwa ni Harper Campbell mwanamke ambaye alikuwa ni bosi wa kampuni kubwa ya bima ya kiingereza ya British Insurance Company na asubuhi yake alipaswa kuwepo ofisini lakini pia hiyo haikuwa kazi yake tu, kazi yake kubwa ni hiyo ambayo alitoka kuyatimiza majukumu yake kwa wakati huo ya ujasusi ambapo alikuwa anamsakama gaidi ambaye alikuwa anakimiliki kirusi ambacho alimkabidhi mheshimiwa raisi.

Gaidi huyo alienda lile eneo kwa kujipamba kama mwanamke mrembo sana kitu ambacho kilimuingiza mkenge mkurugenzi wa usalama wa taifa hivyo watu hao walifanikiwa kufanya kikao chao kama kilivyopangwa lakini Harper alikuwa ameishtukia hiyo ishu mapema sana kwani alikuwa na watu wake ndani ya Ikulu ambao walikuwa wakimpenyezea nyepesi nyepesi kwa kila ambacho kilikuwa kinafanyika na ndiyo sababu ambayo ilimfanya yeye amtambue kabisa mwanaume huyo kwamba ndiye alikuwa gaidi mwenyewe kitu ambacho alikuwa sahihi sana.

Baada ya kutoka eneo hilo mheshimiwa raisi aliagana na mkurugenzi wa usalama wa taifa kisha yeye akaingia chumbani kwake kwa ajili ya mapumziko lakini akiwa hapo alitabasamu sana kwani kikao kilienda vyema. Aliyakumbuka mazungumzo yake na mtu wake baada ya kukutana ndani ya hoteli ile ya kifahari.
“Habari yako mr Abbas” mheshimiwa alimsalimia mwanamke huyo ambaye alikuwa mbele yake ndani ya chumba hicho ambacho ndicho walikuwa wanafanyia mikutano yao. Lugha ambayo ilikuwa inatumika kilikuwa ni kiingereza ambacho kilikuwa rafiki kwa kila mmoja.
“Salama mheshimiwa, habari ya siku ngapi hizi?”
“Nzuri kabisa, umeridhika na huduma ambazo unapewa na watu wangu?”
“Ndiyo mheshimiwa, kwakweli wako vizuri sana na hiyo imenifanya niipende sana nchi hii”
“Vizuri sana sasa twende moja kwa moja kwenye kitu ambacho kimetuleta hapa saivi. Ule mzigo upo kama tulivyo kubaliana lakini naona kwamba watu ambao wanaweza wakafika bei nzuri ni waarabu na nimewasiliana na moja kati ya wafanya biashara kutoka ndani ya falme za kiarabu anakuja wiki ijayo ili kuweza kuangalia mzigo unafanyaje kazi kama anaweza akaridhika nao ameahidi kutoa pesa nyingi sana”
“Wazo lako sio baya sana mheshimiwa ila hakikisha unakuwa makini sana kwa kila hatua ambayo unapiga kama unavyojua kwamba kile ni kirusi hatari sana hivyo huenda kuna watu wanakifuatilia kwa siri sana bila hata sisi kujua, mwisho wa siku tunaweza kuhisi tupo salama lakini kumbe kuna mambo mengi sana ambayo yanaendelea”
“Yes, nalielewa hilo ndiyo maana hata mazingira ya kukutana yanakuwa namna hii, najua kabisa kutakuwa na watu ambao wanatufuatilia lakini nitahakikisha hakuna kitu watakipata na yeyote ambaye atajulikana kwenye hili basi moja kwa moja namuua ili kulinda hii biashara yetu iweze kufanyika kwa amani kabisa”

“Ndiyo maana najivunia sana kufanya kazi na wewe, nina imani hiyo wiki ijayo biashara inaweza kukamilika hivyo mimi nitatakiwa kuondoka haraka sana na utatakiwa unisafirishe kwa siri mpaka eneo ambalo nitaenda kuyaanza maisha yangu mengine huko”
“Hilo halina shida sana kwani wewe umepanga kwenda kwenye nchi gani labda baada ya hii biashara kukamilika? Maana najua kwamba utakuwa na pesa nyingi sana”
“Nawaza kwenda kujificha huko Australia ndani ya jiji la Canberra nadhani hakuna mtu ataweza kujua kwamba mimi nipo huko”
“Mimi nitahakikisha nakusafirisha mpaka huko bila kukaguliwa na mtu yeyote yule maana utatumia ndege yangu”
“Huoni kama itakuwa ni hatari sana mheshimiwa kusafiri na ndege yako ifike kule halafu wewe wasikuone?”
“Hapana hilo jambo lipo ndani ya uwezo wangu, nina watu wengi sana ambao nafahamiana nao hivyo mpaka nakwambia hivyo basi ujue ni suala dogo sana mbele yangu”
“Nitashukuru kwa hilo na nina imani kwamba biashara itafanyika kama tulivyo ipanga ila kwa masharti ya kwamba watu hao hata kama watakitumia kirusi hicho vibaya basi wahakikishe kisije kikadhuru na nchi zetu”
“Naelewa hilo nipo makini nalo sana. Labda kuna jambo lingine la mhimu ambalo unalihitaji kutoka kwangu?”
“Ndiyo mheshimiwa, nahitaji kuanzia siku ya kesho uniongezee ulinzi wa kutosha maana sina imani sana na maisha yangu nahisi kabisa kwamba kuna watu wananifuatilia sana”
“Ondoa shaka kesho kuna makomando wataanza kukupatia ulinzi hivyo nina imani hakuna mtu ambaye atafanikiwa kuweza kukugusa au kukufuatilia tena baada ya hapo maana atakuwa anatafuta ni kifo”
“Shukrani mheshimiwa” walipeana mikono baada ya kufikia makubaliano yao na kikao chao kikawa kimeishia hapo. Wakati bwana huyo Abbas akihitaji kunyanyuka akiwa kwenye hayo mavazi ya kike ndio muda ambao mkurugenzi wa usalama wa taifa alikuwa anaingia hapo ndani hivyo alifika wakati kikao hicho kikiwa kimeisha tayari hakufanikiwa kupata jambo lolote lile zaidi ya kuhisi kwamba Tommy huenda alimpa taarifa ambazo hazikuwa sahihi.

43 Inafika mwisho.

Wasalaam,

Febiani Babuya.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
SIMULIZI: ELECTION SAGA (MONEY IN BLOOD)
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+

UKURASA WA AROBAINI NA NNE
Mheshimiwa alitabasamu baada ya kukumbuka jambo hilo lakini akiwa anahitaji kulala baada ya kuhakikisha kila kitu kipo sawa ndipo alipo pokea simu kutoka kwa mtu wake ambaye muda mchache uliokuwa umepita alitoka kufanya naye kikao, ni simu ambayo iliumaliza usingizi wake kabisa licha ya kuwa kwenye uchovu mkali sana alijikuta anaaamka mheshimiwa.
“Kuna tatizo mr Abbas?”
“Ndiyo mheshimiwa”
“Lipi hilo?”
“Nimevamiwa”
“Whaaat?”
“Ndiyo, walinzi wote ambao umenipa wameuawa na mdunguaji ambaye baadae alijitokeza akionekana kabisa kwamba alikuwa anahitaji kunipata mimi lakini tumemdhibiti mimi na bodyguard wangu”
“Ohhhh shiiiit! Kwahiyo mpo naye huyo mtu kwa sasa?”
“Hapana amefanikiwa kukimbia ila tayari nimemjeruhi kwenye mwili wake nadhani ni eneo la begani kwa chini kidogo ana jeraha hivyo unaweza ukaingiza watu wako mtaani na hospitalini waweze kufanya msako wa kumtafuta”
“Hilo halina shaka sana, vipi umefanikiwa kumfahamu au kumuona hata sura yake labda?”
“Hapana kwa sababu alikuwa amejifunika ila ni mwanamke”
“Mwanamke?”
“Ndiyo”
“Mchana wa leo makomando watakuwa wamefika hapo halafu kuna watu nitawaingiza mtaani ili kuweza kumtafuta mtu ambaye anaweza akawa analeta mashaka kwamba anatufuatilia kwa ukaribu sana. Kikao kilikuwa ni cha siri sana sasa mtu huyo amezipataje taarifa?”
“Sioni kama wazo lako ni sahihi sana”
“Kivipi?”
“Hautakiwi kuwaleta makomando”
“Kwanini?”
“Hao wapo chini ya mkuu wa majeshi mheshimiwa hivyo hatuwezi kuwaamini moja kwa moja kwa sababu wale wanamheshimu sana mkuu wa majeshi kuliko wewe ila wanakuogopa wewe sana kuliko yeye. Mtu ambaye anakuheshimu sana yupo radhi kufanya lolote kwa ajili yako hata kukwambia zile siri ambazo ni za hatari sana tofauti na mtu ambaye anakuogopa kwani yeye anafanya unafiki tu ili uamini kwamba yupo na wewe wakati kiuhalisia anaweza asiwe na wewe na siku yoyote ile anaweza kukuletea majanga makubwa sana”

“Nimekuelewa vyema, nina watu wangu wa siri sana nadhani hawa watafaa nikiwaleta huko ili kuhakikisha upo salama na lile eneo ambalo unakaa kwa sasa inatakiwa uondoke haraka sana kabla hatujachelewa tusije tukaharibu mambo dakika za jioni”

“Sawa mheshimiwa” simu ikawa imekatwa ambayo iliumaliza kabisa usingizi wa mheshimiw raisi. Mawazo yake yalienda mbali zaidi na kuwaza kwamba ni mwanamke gani huyo ambaye alikuwa anaanza kuingia kwenye biashara yake, ni mwaamke gani huyo ambaye alifanikiwa kuuvamia msafara kama ule na kufanikiwa kuwaua watu wake kiwepesi sana namna hiyo? Hakuelewa aamini kipi au kichwa chake kifanye maamuzi yapi kwa wakati huo kwani aliona kama mambo yanaenda haraka sana isivyokuwa kawaida.


Usiku huo huo wa siku hiyo mr Mafupa baada ya kushuhudia mambo ya kutisha sana kule Kurasini na namna wale watu walivyokuwa wameuawa kikatili akiwepo yule mmoja ambaye kichwa chake kilikuwa kimekatwa hakuona haja ya kusubiri tena zaidi zaidi alimpa taarifa mr Oscar kwamba alihitaji kuonana naye usiku huo kwani alikuwa na mazungumzo naye huku akionekana kabisa kama mtu ambaye alikuwa amechanganyikiwa haswa.

Safari ya dakika thelathini tu ilimfikisha mbele ya jumba kubwa sana la mr Oscar ambalo lilifunguliwa na aliye ruhusiwa kuingia ni yeye tu pekeyake huku walinzi wake wote wakibakia nje kabisa ya jengo hilo. Alinyoosha moja kwa moja mpaka kwenye chumba ambacho aliambiwa kwamba mtu huyo alikuwa anamsubiri baada ya kukaguliwa na kutokutwa na silaha yoyote ile kwenye mwili wake. Baada ya kufika mle ndani hakuongea jambo lolote lile zaidi ya kufungua friji na kuchukua pombe kali sana ambayo aliikuta humo, aliinywa bila kupumzika kwa mkupuo mpaka alipo ifikisha nusu ndipo aliitua chini.

Macho yake yalikuwa yanatoa machozi kwa ukali wa hiyo pommbe ambayo alikuwa ameibugia kwa wingi sana. Alihema kwa nguvu sana huku akiwa anajipapasa kwa umakini sana kwenye mwili wake na kuitoa simu ambayo baadae alikuja kukumbuka kwamba aliidumbukiza kwenye mfuko wake wa koti. Hakuongea jambo bali aliiweka video ambayo alijitumia kutoka kwenye simu ya Kaoneka na kumuwekea kigogo huyo ambaye hakuwa na shaka akawa anaiangalia kwa umakini sana huku mr Mafupa akiwa anaendelea kushusha pombe yake kwa hasira kali sana.

Baada ya kumaliza kuiangalia video hiyo mr Oscar aliunyanyua uso wake na kumwangalia kwa umakini sana mr Mafupa ambaye alikuwa amechanganyikiwa ili kuonyesha kama labda alikuwa na jambo la kuongea lakini alionekana kuwa mbali sana kwenye mawazo.
“Hii video ni ya lini?” aliamua kuyafungua maongezi hayo.
“Naweza kusema ni asubuhi ya leo kama bado haijafika saa sita kwenye saa yako ila kama ni siku nyingine basi naweza kusema ni asubuhi ya jana” aliongea mithili ya mtu ambaye hata hakuwa na habari kabisa na muda.
“Na huyu aliye uawa hapa ni nani?”
“Huyo ni moja kati ya walinzi wakubwa sana wa mwanangu”
“Mwanao ana ulinzi wa kutosha?”
“Sina imani, kwa mara ya kwanza nimejikuta naanza kuogopa sana kwa haya ambayo yametokea”
“Kuna lingine zaidi ya hili lililo tokea?”
“Ndiyo, ndiyo lipo”
“Lipi hilo?”
“Si unakumbuka nilikwambia kwamba nimeingia kwenye ile familia kupitia yule binti wa Apson Limo ambaye alikuwa ameingia kwenye mtego wa kijana wangu?”
“Ndiyo nakumbuka vizuri”
“Sasa yule binti alikuwa ametekwa na kuhifadhiwa eneo la siri sana lakini mpaka hivi ninavyo ongea hayupo”
“Kaenda wapi?”
“Nadhani huyo ndiye kamchukua”
“Kitu gani ambacho kimekuwa ni cha tofauti kwenye hilo tukio?”
“Mauaji”
“Unamaanisha nini?”
“Kila sehemu ambayo mtu huyo anahusika anamkata mtu mmoja kichwa na kukiweka pembeni na mwili”
“Si na wewe ndivyo ulivyo mfanyia binti wa Apson Limo?”
“Ndiyo ila sikujua kama tunaweza kufikia huku”
“Unapo amua kufanya jambo la hatari kama lile ambalo ulilifanya basi unatakiwa kuwa tayari kwa matokeo yoyote yale ambayo yanakuja kutokea. Nilikwambia mapema kwamba usipende kudharau sana vitu ambavyo unakuwa hauna taarifa navyo za kutosha lakini ukasema kwamba kwako hakuna tatizo yule ni kijana wa kawaida sana na unaweza ukalimaliza swala lake bila nguvu, leo tena unakuja hapa unaniambia kwamba umeanza kuogopa?”
“Naogopa sana maisha ya mwanangu yanaweza kuwa hatarini sana nawaza kuiteketeza ile familia nzima”
“Usije ukafanya huo ujinga”
“Una maanisha nini? Niendelee kumwangalia mtu ambaye anahatarisha maisha yangu na ya familia yangu akiwa anaishi anavyohitaji yeye?”
“Yeah kuna muda siasa inakutaka uwe hivyo kwa sababu kama ukikurupuka unaweza ukajikuta unaharibu kila kitu ambacho umekipigania kwa muda mrefu sana kwenye maisha yako”
“Bado sijakuelewa”
“Nina uhakika huwezi kunielewa ila swali langu ni kwamba huyu kijana ni nani hasa na huu uwezo kaupatia wapi, una taarifa zake labda?”
“Nimetafuta kila sehemu lakini hakuna taarifa yake yoyote yenye ukakasi kwenye historia nzima ya maisha yake mpaka inafika sehemu naanza kuhisi kwamba labda kuna mtu mwingine tu ambaye alikuwa amevaa kinyago chake ndiye anayatimiza haya”

“Usiwe mvivu sana wa kufikiri kiasi hicho, nafikiri niliwahi kukwambia kwamba kuna watu ambao unatakiwa kuwaweka kwenye mkono wako, watu wenye nguvu kama mkurugenzi wa usalama wa taifa pamoja na mkuu wa majeshi ila naona kama unadimba dimba tu huu ndio muda ambao wangekusaidia sana kwenye kuweza kulimaliza hili. Angalia sana kwa sababu kama yakikutokea puani kumbuka mimi sihusiki kwenye hili”
“Nahitaji msaada wako”
“Upi”
“Kwanza ulinzi kwangu halafu pili nahitaji kuhakikisha kwamba huyu bwana mdogo ni yeye au sio yeye. Kwaiyo nataka tuandae mtego ili akiingia kwenye huo mtego basi moja kwa moja tuweze kummaliza hapo hapo biashara yake inakuwa inaisha mshenzi huyo”
“Sasa hapo mimi unataka nikusaidiaje?”
“Nahitaji unipe watu baadhi wa kuendelea kunilinda lakini pia uniandalie huo mtego ambao unaweza ukafanya tukamjua kwamba ndiye mhusika au vipi na baada ya hapo tumuue” mheshimiwa huyo alimwangalia sana mr Mafupa kisha akatikisa kichwa kuonyesha kwamba alikuwa amelikubali ombi lake.
“Mtego ufanyikie hospitali”
“Una maanisha nini?”
“Baba yake si kalazwa pale?”
“Ndiyo”
“Basi tutafute watu wavamie pale na kama kweli atakuwa na huo uwezo ambao wewe unataka kuuthibitisha basi ataudhihirisha wazi kwani hatakuwa tayari kumuona baba yake akiwa anaingia kwenye matatizo lazima ataamua kumtetea na hapo ndipo tutawaulia wote yeye na baba yake mzazi”

44 sina la ziada tukutane tena wakati ujao.

Wasalaam,

Febiani Babuya.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom