Martin B
New Member
- Mar 31, 2024
- 1
- 0
U can pay for it...if ur in a such a hurryMkuu kwema? Weka hata vipande 10 pls umeniacha na arosto Kali sana
Ñ on the other side u'll be supporting our buddy ....#vizuri vina gharama😁#
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
U can pay for it...if ur in a such a hurryMkuu kwema? Weka hata vipande 10 pls umeniacha na arosto Kali sana
Ndo mnunue sasa sio kuanza kunipopoa huku [emoji28]U can pay for it...if ur in a such a hurry
Ñ on the other side u'll be supporting our buddy ....#vizuri vina gharama[emoji16]#
Tunanunua njia ipiNdo mnunue sasa sio kuanza kunipopoa huku [emoji28]
Kuna namba za WhatsApp kwenye kila episode ninayo tuma. Unaweza ukanicheki WhatsApp au unaweza ukalipia kupitia hizo namba kisha ukaja WhatsApp nikakutumia.
Tunaendelea kimyaSIMULIZI: ELECTION SAGA (MONEY IN BLOOD)
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
UKURASA WA SABA
Wakati huo kwenye hoteli moja kubwa sana mapema ya asubuhi hiyo walikuwa wanaonekana watu wawili ambao hawakuhitaji maelezo mengi kuweza kujieleza kwamba wao walikuwa kwenye penzi zito sana. Mwanaume alivaa bukta tu huku mwanamke pia akiwa ndani ya bikini tu, walikuwa wanapata chai huku wakiwa wanapeana mahaba ya wazi wazi.
“Mpenzi ni lini utafika nyumbani kwa ajili ya kujitambulisha?” ilikuwa sauti ya mwanamke akiongea kwa mahaba ya wazi wazi kwani hata macho yake yalikuwa yakiongea jambo hilo. Alikuwa ni Patrina Apson Limo ambaye alikuwa binti mkubwa wa mwana siasa na tajiri Apson Limo.
“Mzee wako kwa sasa anajiandaa na mambo ya uchaguzi, sioni kama ni muda sahihi sana, hili likipita tu mimi nakuja kwenu na kukuvisha pete kabisa inabaki harusi tu” Ni lugha safi ambayo aliipata kutoka kwa mwanaume ambaye alikuwa akimpenda sana.
“Basi usije ukanidanganya maana nitajisikia vibaya sana kwa sababu mimi nakupenda sana” aliongea akiwa na furaha sana Patrina lakini wakati huo huo simu ya mwanaume huyo ilianza kuita, alivyo angalia namba hiyo ya mpigaji, alitoka haraka sana hilo eneo na kwenda nje kabisa ya kile chumba.
“Ndiyo baba”
“Mpango ukikamilika tu niambie nilitekeleze hilo haraka sana maana hata muda huu nipo naye hotelini”
“Sawa baba” mwanaume huyo aliikata simu yake na kurudi ndani akisingizia kwamba alikuwa naongea na simu ya biashara zake binafsi, na mwanamke huyo kwa sababu alikuwa akimuamini sana basi hakuona kama ilikuwa ni busara sana kuanza kubishana naye, uwepo tu wa mwanaume huyo ulikuwa unamridhisha sana asijue mwenzake alikuwa na mipango ipi juu yake maana hata dakika hizo hizo alitoka kumwongelea ikionekana wazi kwamba kuna mpango mzito sana ambao ulikuwa unaandaliwa kwa ajili yake yeye.
Majira ya usiku wa mapema Mr Apson Limo alikuwa na familia yake nyumbani kama ilivyokuwa kawaida yake, alichagua kuwa baba bora wa familia yake na kuyabeba majukumu vile inavyo takikana. Akiwa hapo sebuleni majira hayo anacheza na mwanae wa mwisho alimuona moja kati ya walinzi wake wa getini anakuja kwa spidi sana akiwa anahema kama mtu ambaye alijaa hofu sana ndani yake, alimgeukia na kumwangalia kwa macho ya kumuuliza kuhusu kile ambacho kilikuwa kinaendelea.
“Bosi kuna watu wamekuja na gari za Ikulu nje hapo, sasa sijui kama niwaruhusu waingie?” swali la huyo mlinzi wake lilimshtua sana, alishangaa gari za ikulu zinatafuta nini kwake wakati hakuwa hata na miadi nao? Hakupata jibu hivyo ikamlazimu yeye mwenyewe kuweza kutoka ili kujua kwamba watu hao walikuwa wanahitaji kitu gani hasa mpaka wamfuate nyumbani kwake.
Alitoka akiwa na wasiwasi sana kwenye nafsi yake hata geti hilo alienda kulifungua yeye mwenyewe ndipo alipo kutana kweli na gari hizo za Ikulu tatu zikiwa zimesimamishwa nje ya nyumba yake huku wanaume waliokuwa waamevaa suti nyeusi wakiwa wamezizunguka gari hizo.
“Mheshimiwa tunaomba utusamehe sana kwa kuja kwako bila taarifa ila ni maagizo kutoka juu hivyo hatukuwa na namna zaidi ya kuyatekeleza” aliongea mwanaume mmoja ambaye alionekana kuwa kiongozi wa wengine huku akiwa anaguna kidogo kumpa nafasi mheshimiwa kuweza kuwajibu kwa maana walimuona kama bado alikuwa kwenye mshangao sana.
“Hii yote inamaanisha nini?”
“Ni maagizo ya mheshimiwa raisi anakuhitaji Ikulu kwa sasa, amesema kwamba ana mazungumzo marefu na nyeti sana na wewe” alijibu mwanaume huyo
“Mhhhhhh kwahiyo raisi anahisi kwamba nafasi yake inamfanya kumpata kila ambaye anamhitaji na kwa muda ambao anautaka yeye?”
“Sidhani kama ni hivyo mheshimiwa ila ni bora kubali wito ukatae maneno, itakuwa kama dharau sana kumkatalia mkubwa wa nchi kwa kukualika Ikulu”
“Sawa nakuja” aliongea kwa hasira sana huku akielekea ndani, bila shaka alienda kumuaga mkewe ambaye alimsindikiza kwa wasiwasi sana wakati wa kutoka na Mr Apson Limo akapanda kwenye gari ili kuweza kufika huko Ikulu”
Ndani ya nusu saa gari hizo zilikuwa zinaingia Ikulu bila wasiwasi huku mr Limo akiwa ana hasira sana na alipanga kumpa makavu raisi wake lakini ni kama hata aliyekuwa amepanga kumpa makavu yake alikuwa amejipanga juu ya hilo.
“Akili ni kitu bora zaidi kwa mwanadamu na siku zote watu wenye akili huwa hawakurupuki wala kutanguliza hasira mbele kwa kuamini kwamba kila lililopo mbele yao linaweza kuwa na umuhimu mkubwa sana kwao. Ni jambo jema sana kama umekubali kuja kuongea na mimi, karibu sana mr Apson Limo” mheshimiwa huyo aliongea huku akiwa anampa mkono mwanaume ambaye macho yake yaliingia kwenye ofisi hiyo kwa hasira sana lakini kwa maneno ambayo alipewa aliamua kuwa mpole mwenyewe naye akaishia kumsalimia kiongozi wake kisha akaketi ili kumsikiliza kuhusu kile ambacho alikuwa amemuitia usiku huo.
“Nimeukubali wito wako kwa sababu wewe ni mheshimiwa raisi na napaswa kukusikiliza kama kiongozi wangu japo hili ni baya sana kwa sehemu mbili. Sehemu ya kwanza kistaarabu ulitakiwa kunipigia simu na kunitaarifu mapema maana hata mimi nina ratiba zangu za kifamilia na kikazi, sio ustaarabu kwa sababu ni raisi basi unajiamulia kila linalo kuja mbele yako. Lakini jambo la pili usiyatumie madaraka vibaya mheshimiwa, kumbuka hata kabla ya kuingia hapa wewe pia ulikuwa raia wa kawaida tu mtaani, sasa unapo anza kutumia nguvu kama hivi sio sawa. Walicho kifanya vijana wako ni kama uvamizi tu nyumbani kwangu huku wakiamini kwamba kwa sababu wewe ni raisi basi wapo sahihi kwa kila jambo ila sio kweli” alimpa vidonge vyake mheshimiwa kama alivyokuwa amekusudia tangu mwanzo. Boniphace Walawalaa alitabasamu ila kwa uchungu, kuwa raisi alihisi kwamba yeye yupo juu ya kila kitu sasa inapotokea mtu ndani ya nchi yake anataka kumchukulia kawaida alikuwa anajihisi kutokamilika kama raisi ila aliamua kumezea kwanza maana huyo mtu ilikuwa ni karata mhimu sana kwake kuweza kuichanga vyema.
“Mr Apson Limo najua nimekukosea wewe na familia yako ila kuna muda ukiwa kiongozi hauna budi kufanya maamuzi magumu hata kama hayata wafurahisha wale ambao wanayapokea. Kuwa kiongozi ni moja ya jukumu kubwa sana japo wanasema kwamba kiongozi anapaswa kuwasikiliza wale ambao anawaongoza lakini sio kila muda kwani ukisema umsikilize kila mtu basi mtachelewa sana kufikia maamuzi ya mwisho kitu ambacho kitapelekea kuchelewa sana kuweza kufanikiwa au kuendelea” mheshimiwa raisi aligeuka kuwa kama mwanafalsafa kuanzia mbali kumrubuni mtu huyo.
“Mheshimiwa mke wangu atakuwa na wasiwasi sana kwa jinsi nilivyo ondoka nyumbani, nitafurahi sana kama utaenda moja kwa moja kwenye pointi yako ya msingi kwani kwa kipindi tulichopo hata wananchi wakijua mimi na wewe tunakutana italeta picha mbaya sana kwetu sote wawili wakihisi kwamba labda kuna mambo ambayo tunakubaliana au tunayapanga pamoja kitu ambacho sitaki kukifanya kwani wananchi wangu wananiamini sana” hakuhitaji ngonjera za bwana huyo hivyo alimwambia aende kwenye pointi ya msingi moja kwa moja.
“Ok nahitaji uiachie hiyo nafasi ambayo wewe upo na tutamuweka mtu mwingine hapo” raisi alizungumza huku akiwa amemkazia macho asiwe hata na tone la wasiwasi kwa upande wake.
“Unaweza ukanipa sababu ya msingi ya wewe kuniambia maneno kama hayo?” Mr Apson Limo hakushangazwa sana na kauli hiyo kwa sababu hata mr Mafupa alikutana naye na kumuomba kitu kama hicho, ilikuwa ni kawaida sana hayo mambo kutokea kwenye siasa.
“Nahitaji kuendelea kubaki Ikulu bado ndiyo maana sitaki upinzani wowote kutoka kwako kwa sababu mr Mafupa hana shida yule ni wa chama changu hivyo tutamalizana ndani ya chama ila wewe ndiye wa mhimu maana upo kwenye chama kingine tofauti kabisa na wananchi wanakuamini sana. Nina imani kama ukiwa upande wangu basi kauli yako moja tu inatosha kuwafanya wananchi wote wanao kuamini wakaweza kunipigia kura mimi kisha nitakupa nafasi yoyote ambayo wewe utaitaka” aliendelea kushusha sera zake mheshimiwa raisi.
“Umesema utanipa nafasi yoyote ile?”
“Ndiyo”
“Unaweza kuniachia Ikulu?”
“Whaaaaat?”
“Nisikilize mheshimiwa, mimi sio wale watu ambao wanarubunika kwa maneno au kwa pesa, nimebahatika kuwa na kila kitu kwenye maisha yangu ila kitu pekee ambacho ninatamani kwa sasa ni kuwalipa mema wananchi wangu ambao wana imani kubwa sana na mimi. Nchi haina miundombinu ya kuridhisha kila mwaka mnawapiga porojo tu huku mkizinufaisha familia zenu na matumbo yenu kwa kuiba mali nyingi za serikali na kuzihifadhi kwenye mabenki ya nje. Kuna watoto mpaka leo hawana hata madarasa ya kusomea, kuna watoto hawana hata walimu wa kuwafundisha na walimu kibao wapo mtaani hawana ajira mkisingizia kwamba uchumi wa nchi sio mzuri, watoto wanakosa elimu bora, vijijini wananchi hawapati huduma za kijamii zaidi ya kujisaidia wenyewe, kuna vijiji vingi havina hata umeme, vijiji vingi havina huduma za afya tunaishia kupoteza wamama wanao jifungua na watoto kila mwaka huku nyie mkiishia tu kupiga picha kwenye maeneo yenye hali nzuri mkiyatumia kwenye kampeni. Unahitaji niwe chini yako tukaendelee kufanya ufisadi kwa pamoja niwaache wananchi wangu wakiwa wanataabika namna hiyo bado? Mheshimiwa kuna maisha ambayo baadhi ya watu wanayaishi ndani ya nchi hii hata watu wa nje huko wakijua watatucheka sana na kutushangaa kwamba raisi huwa unafanya kazi gani labda. Hivyo kiufupi ni kwamba siwezi kufanya hicho unacho kitaka, siwezi kuwasaliti wananchi wangu na sidhani kama nitakuja kukubali wito wako tena kama ndio huu ujinga ambao umeniitia hapa” aliongea kwa ukali sana na kumwambia ukweli raisi huyo. Alikuwa ni mzuri tu wa ahadi na visingizio vingi sana ila kiuhalisia kwenye nchi yake wananchi wengi sana walikuwa na maisha magumu mno.
Alimchana ukweli kwamba zama hizi hazikuwa za watoto kukosa madarasa wala sehemu za kusomea, hazikuwa zama za nchi kushindwa kutekeleza huduma za kijamii wakati viongozi wanatanua kwa kuishi maisha mazuri isivyokuwa kawaida kwenye nchi yao. Mheshimiwa raisi mpaka wakati huo ndita zilikuwa zimejichora vibaya sana kwenye paji lake la uso, ukweli ambao unaumiza huwa ni kisu kikali sana kwa mtu mwenye jeraha la namna hiyo.
Wakati huo mr Apson Limo alikuwa amenyanyuka na kuanza kutoka hapo bila hata kuaga lakini alisimama baada ya meza kugongwa kwa nguvu sana na mheshimiwa raisi ikamfanya asimame;
“Naona umeanza kunikosea heshima, unasahau kwamba unaongea na nani na uko wapi wakati huu! Unajua nina uwezo wa kukufanya usifike kwako mpuuzi wewe? Unawaongelea wananchi gani wa kuwapigania? Wananchi ambao hata hawajielewi hawa, wananchi ambao kila wakati wanawaza ujinga tu na hakuna jambo la maana lolote lile ambalo wanaliwaza? Nilikuwa nakuona mtu wa maana sana ila kumbe naongea na moja kati ya watu wajinga sana kuwahi kutokea duniani mpuuzi mkubwa wewe” mheshimiwa maneno yale yalimuuma sana kiasi kwamba hakuweza kabisa kuyavumilia ndiyo maana aliongea kwa ukali sana na kumtisha mr Apson Limo. Mr Apson Limo alitabasamu na kurudi kisha akainamia kwenye hiyo meza ya mheshimiwa akiwa anamwangalia usoni.
Unatamani kujua kwamba mr Apson Limo alimwambia nini mheshimiwa raisi baada ya hapo? Ukurasa wa saba naweka nukta hapa, panapo majaaliwa tukutane wakati ujao.
Febiani Babuya.
Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app