Sumba-Wanga
JF-Expert Member
- Feb 2, 2011
- 5,353
- 1,234
Kuna tetesi niliwahi kuzisikiaga tena humu humu jamvini wakati lile jengo linaanza kujengwa kuwa ni la Rostam Aziz. Sasa yupi mwenyewe?
All in all better late than never
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kuna tetesi niliwahi kuzisikiaga tena humu humu jamvini wakati lile jengo linaanza kujengwa kuwa ni la Rostam Aziz. Sasa yupi mwenyewe?
Lazima tuelewe mfumo wetu wa ulinzi na usalama umekufa
Tangu za Mwalim kuna vijana wadogo hapa ikulu Miaka mitatu walk kuwa A'level sasa hivi wanaishi maisha anasa, statehouse sasa hivi ni ya familia pale.Othman,Zoka na wengi tu
Hata Mzee wa piga tu ndugu zake wapo kibao,Watanzania tusitegemee miujiza wengine tukihoji unaishia kwenye kisima cha maji au unapotea kabisa
Ndugu yangu GeniusBrain siwezi kukulaumu kwani inadhihilisha ni kwajinsi gani akili yako ilivyolala na ndiyo maana huwezi hata kuipa muda wa kutafakari. Ila nashukuru kwamba umesoma na umeelewa nilichoongea ndiyo maana umecomment.
Tangu sakata la ujenzi wa jengo refu la ghorofa 19 lililopo karibu na Ikulu yetu kuanza kuwa gumzo hapa nchini, binafsi nimejitafakarisha mambo mengi kichwani mwangu. kitu cha kwanza ni kwamba kabla ya jengo hilo kujengwa yalikuwepo majengo ya serikali ambayo kwa idadi kubwa yalikuwa yakikaliwa na maofisa wa juu wa serikali. ufisadi na uvivu wa kufikiri wa viongozi waliopo Ikulu ndio uliochangia maeneo hayo yatolewe kwa watu binafsi japokuwa ukweli ni kuwa hata viongozi wenyewe wa Ikulu hiyo wamo kama wabia! Majengo hayo yamekuwa yakijengwa mchana kweupe! Rais wetu na mawaziri wake hiyo ndiyo njia yao wanayoitumia asubuhi na mchana na wote wamekuwa wakiona nini kinachoendelea hapo!
Sasa iweje leo baada ya jengo hilo kukamilika ndipo ionekane kuwa limejengwa kwa makosa? Je, usalama wa Taifa kazi yao ni ipi?! Au wanadhani ni kuvaa miwani myeusi na suti tu!
Je, inamaana kama FBI wasingekuja kwa ajili ya ujio wa Obama, wasalama wetu wasingegundua athari za jengo hilo? Mbona hata watu wa kawaida ambao wanapata huduma ya chakula kwa mama ntilie pale jirani wamekuwa wakiyasema hayo, inamaana usalama wetu ulikuwa haufiki pale na kupata maoni hayo?
Na, je, kuna sababu gani ya kusema jengo libomolewe wakati linaweza kutumika kwa matumizi ya serikali na mjenzi akafidiwa pesa yake?
Kwa hili maswali yapo mengi ambayo pengine hata majibu yake hayatakuwepo.
NDIYO MAANA CHADEMA INATAKIWA ILI IJE KUPITIA UPYA MIRADI KAMA HII.