Katika hali isiyokuwa ya kawaida Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, ambayo huko nyuma ilikuwa mbogo katika masuala ya utendaji wa Tanesco, jana ilikuwa kama kondoo wakati ikipokea taarifa za Serikali kuhusu hali halisi ya uzalishaji wa umeme nchini.
Extracts kutoka gazeti la Tanzania Daima la jumanne Tarehe 13 Oktoba 2009 "Siri Yafichuka Umeme Tatizo Sugu :
Extract 1
"Kikao cha pamoja kati ya Serikali, Shirika la Ugavi (Tanesco), na Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, kimebaini kwamba ufumbuzi wa kudumu wa tatizo la mgawo wa umeme nchini utapatikana baada ya muda mrefu.
Ukweli huo mchungu kuhusu mgawo wa nishati hiyo unaoweza kuendelea kulikabili taifa mara kwa mara ulibainishwa jana wakati pande hizo tatu zilipozungumza na wanahabari muda mfupi baada ya kikao chao."
Extract 2
"Akizungumza katika mkutano huo wa pamoja, Mwenyekiti wa Kamati ya nishati na Madini ya Bunge, William Shellukindo (CCM) alikiri kwamba, uchunguzi uliofanywa na wajumbe watatu wa kamati hiyo waliotembelea mabwawa ya kuzalisha umeme ya Kihansi, Hale na Pangani umebainisha kwamba, mgao huo haujasababishwa kwa namna yeyote na vitendo vya hujuma."
Extract 3
"Pamoja na kukiri kwamba, kikao chao kilibaini kuwa, tatizo la umeme litaendelea kulisumbua taifa kwa kipindi kirefu zaidi, Shellukindo alisema suala la kuitaka serikali kununua mitambo ya Dowans halikuwa sehemu za ajenda walizozijadili.
Hata hivyo, baada ya shellukindo kusema kwamba sakata la Dowans limekwisha zikwa, Naibu waziri wa Nishati na Madini, Adama Malima aliyekuwepo katika mkutano huo aliongeza kuwa, serikali haina mpango tena wa kununua mitambo hiyo ya kufufua umeme ya Dowans, lakini endapo mtu binafsi atainunua na kuiuzia Tanesco umeme kwa sheria ya sasa itakubali.
Katika hilo, Malima alisema kwa sheria ya sasa, Tanesco ina uwezo wa kununua umeme kutoka katika makampuni na taasisi binafsi ili iweze kukidhi mahitaji yake ya kuhakikisha kuwa nishati hiyo inakuwepo wakati wote nchini."
Extract 4
"Kwa upande wake, akizungumzia sababu sababu zilizolifikisha taifa hapa lilipo sasa, Shellukindo alibainisha kuwa, mgawo wa sasa unatokana na upungufu wa megawati 72 ambao kamati yake iliridhika na sababu za kitaalamu kutoka serikalini na Tanesco."
Extract 5
"(Shellukindo) aliishauri serikali kupitia Sheria ya Manunuzi ya mwaka 2004, kuona namna ya kuondoa urasimu uliopo ili usiathiri manunuzi ya mitambo miwili itakayozalisha umeme wa jumla ya megawati 160, katika miji ya Dar es Salaam na Mwanza.
Wakati Shellukindo akitoa rai hiyo, kumbukumbu zinaonyesha kuwa, miongoni mwa sababu ambazo zilisababisha Bunge kuitia msukosuko serikali, wakati wa sakata la Richmond mwaka jana ni uamuzi wake wa kuamua kutumia utaratibu uliokuwa ukijaribu kukwepa ukiritimba wa sheria ya manunuzi."
Extract 6
"Katika hali ambayo haikutarajiwa katika mkutano huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Dk idris Rashid, alishindwa kujibu maswali ya waandishi wa habari waliomtaka kutoa ufafanuzi wa kauli zake alozitowa machi mwaka huu kuwa serikali isiponunua mitambo ya Dowans, nchi nitaingia gizanimwishoni mwa mwaka na wananchi wasimlaumu kwa hilo.
Baada ya kuulizwa swali hilo, Dk. rashid alisita kujibu na kunyamaza kimya, hatua aliyowafanyawaandishi kumshinikiza kuelezea suala hilo.
Hata hivyo, Naibu Waziri Malima aliingilia kati kwa kujibu kuwa alifanya utabiri wa nyota ulioegemea katika utaalamu wa kisayansi na ambao matokeo yake yamethibitisha kwamba alikuwa sahihi.
"Mkurugenzi alituandikia mwezi Februari mwaka huu akitoa mapendekezo ya kitaalamu kuwa serikalini tusipochukua hatua za haraka, nchi inaweza kuingia gizani mwishoni mwa mwaka kutokana na uwezekano wa kutokea ukame na tumeona" alisema Malima."
Alisema wazi kuwa wataalamu wa masual ya umemewaliliona tatizo hili mapemana kutoa ushauri wao wa kitaalamu, hivyo serikali ilipaswa kuzingatia.
Extract 7
"Mapema mwaka huu, dhamira ya serikali kupitia Tanesco kutaka kununua mitambo ya Dowans, iliibua mjadala mkali miongoni mwa watanzania, huku wakionyesha shaka kuhusu ununuzi huo."