Mkuu wangu, Nakupongeza kuwa una msimamo kwa unachokiona ni bora. Kwa mantiki hiyo hiyo sioni nina kosa kuwa na msimamo kwa ninachokiona ni bora kwa mujibu wa maoni yangu.Mpaka sasa tukiangalia maoni yetu tofauti tutagundua kuwa maoni yako ndiyo yanayoleta mada hii sasa hivi. Iwapo tungenunuwa mitambo ya Dowans na tukaingia kwenye Giza basi msimamo wangu ungekuwa ndio wenye mushkeli.
Richmond ambayo ndiyo chimbuko la matatizo yote haya ilkuwa na matatizo yake na tulishuhudia kuanguka kwa mtu mkubwa kabisda serikalini. Maoni ya kununuliwa mitambo iliyorithiwa na Dowans yalikuja katikati ya mtafaruku ulioletwa na Richmond na tayari baadhi ya Wabunge walikwishajipatia umaarufu kutokana na hilo na wengine walishapoteza nyadhifa zao kutokana na hilo. Sasa anapotokea mtu akatowa maoni tofauti na hali halisi panahitaji busara katika kuliangalia suala analolileta kinyume na mtizamo wa wengi. Busara ilihitajika kuangalia ushauri wa Wataalamu wa Tanesco na kuangalia wapi wamepata ujasiri wa kupingana na hisia za wengi?
Nasikitika hilo halikufanyika na sababu kubwa ni za kibinafsi za kutaka umaarufu. Mola anasema kuwa wanafiki siku zote hushinda kwa kipindi kifupi na baadae huzidiwa na ukweli na hilo ndilo lililotokea hapa kwetu kwani hata baada ya kufanya uchunguzi kamati ya Bunge imekiri kuwa kuna tatizo na baya zaidi wanakubali kuwa kulikuwa na kila jitihada iliyostahiki kufanywa lakini tatizo limebaki pale pale. Nini maana yake ? Kwa mie nisie na elimu naamini kuwa maana yake hapa ni kuwa wataalamu walipotoweaq pendekezo walishapima njia zote mbadala na kuona kuwa hakuna nyengine yoyote ya dharura bali kununua Dowans. Ama kwa huo msururu wa madai uliotowa nafikiri ulikuwa unajulikana na ulishatolewa ufafanuzi wa namna ya kutatua malalamiko hayo.
Hayo ni maoni yangu na nayatowa sio kwa kupendelea ufisadi bali kwa kunusuru Taifa.
Mkuu wangu nakuomba unisome vizuri na pengine wote ambao mnakubaliana na hoja hii au kupinga ni muhimu sana kusoma maeleoz yangu yafuatayo kwani inaonyesha wazi tunabishana tuuu pasipo kuelewa taratibu za kiuchumi na maendeleo.
Mkuu nitarudia tena kusema kwamba mimi sii msomi kuliko viongozi wetu tena naweza sema ni mbumbumbu ktk taaluma ya Umeme na uongozi, lakini hoja kubwa ya mjadala huu haihusiani na Utaalam isipokuwa ku Solve TATIZO la Umeme.
Hapo nyuma nimekwambia kuhusu MAHITAJI yetu ya Umeme ambayo mikakati imekwisha jengwa na serikali yetu (serikali ya Kikwete) ilipoingia Ikulu. Na katika mikakati hiyo ya MAHITAJI yetu, ambayo ipo ya muda mfupi namuda mrefu (short term/long term), huo umeme wa Richmond/ Dowans haupo ktk mipango hiyo (strategically). Nakuomba elewa hilo kwanza.
Mtambo wa Richmond/Dowans ulikubaliwa au kuletwa nchini kama mtambo wa dharura kutokana na upungufu wa umeme nchini kutokana na mabwawa yetu kutotoa umeme jambo ambalo lilisababishwa na miradi hiyo kutegemea mvua..Sawa na wewe leo hii ukanunue kibatari sokoni kutokana na umeme kukatika mara kwa mara au wananchi na wafanya biashara wanapo nunua generator zao binafsi.
Kwa hiyo basi ndio kusema kwamba mipango ya serikali kuboresha mahitaji ya umeme nchini haijapatiwa ufumbuzi hadi leo kwa muda wa miaka minne na ahadi zote alizotoa rais wetu Kikwete alipoingia madarakani ni ahadi hewa iwe kwa short term au long term isipokuwa leo hii kumewekwa ktk wakati mgumu wa kutegemea kuendesha uchumi wa nchi yetu kwa kutatua TATIZO tukitumia vibatari au generator as a short term strategy..Yaani umeme wa dharura unageuzwa kuwa ni mpoango wa muda mfupi ktk maendeleo ya mahitaji yetu ya umeme.
Ndipo napokuja na hoja yangu kubwa na ya msingi kiutalaam ktk Mahitaji.. Richmond/ Dowans wameingizwa nchini kuondoa tatizo la umemem uliopungua kutokana na mvua chache zilizonyesha wakati wa Utawala wa Mkapa, Tukaweza ku identify PROBLEM hiyo na kwa haraka tulitoa tender ili kukabiri tatizo hilo la muda..Tatizo ambalo ni nje ya hesabu ya MAHITAJIi yetu ya Umeme.
Meaning kama (mathlan) MAHITAJI yetu ya Umeme ni Mw 1500, vyanzo vyetu vya umeme vulikuwa vikifua umeme wa Mw 900 hivyo hesabu pungufu ni Mw 600 ambazo mikakati ya serikali ilikuwa imejengwa kukidhi mahitaji hayo na ya ziada kulingana na ongezeko la watu na matumizi kila mwaka.
Nitarudia kusema Dowans haikuwepo ktk hesabu hii ya upungufu wa megaWatts 600 za mahitaji yetu, isipokuwa inalenga kutatua tatizo la ambalo vyanzo vyetu vilishindwa kuzalisha zile Mw 900 kutokana na matatizo mbali mbali ikiwa ni pamoja na mvua kutonyesha. Tuseme tena mathlan vyanzo vyetu vilizalisha Mw 700 hivyo tulipatwa na tatizo pungufu la Mw 200 na ufumbuzi wa haraka ili tupate kufidia pengo hilo la Mw 200 ndipo mashirika haya yalishinikizwa kuingia mkataba kuziba pengo hilo la Mw 200.
Lakini kwa bahati nzuri mvua zilirudi kunyesha na mabwawa yetu yakajaa maji hivyo kibatari hiki cha Dowans hatukukihitaji tena..case closed...hatukihitaji tena kibatari kulingana na mipango ya serikali ya muda mfupi na mrefu KAMA ingeanza mara moja kufanya kazi..
Lakini serikali kwa Ufisadi wake wamegeuza mradi wa Dowans na mashirika mengine yaliyoingia nchini kama suluhisho la TATIZO la umeme kuwa ndio mpango wa muda mfupi ktk MAHITAJI yetu ya Umeme. Mtu kama Dr. Rashid anaelewa ukiritimba na pengine ubovu wa serikali yetu ktk kupanga na kutambua mahitaji ya nchi yetu ambayo leo hii kwa mfano wa hapo juu umefkia pengine Mw 2000 na haoni kabisa mpango wowote wa kutuwezesha kufua Mw 2000 au hata robo tatu ya mahitaji hayo. Ndipo naye anacheza na mzee kuturudishia Kibatari kwani sii kazi yake kuhakikisha nchi ina umeme ila ni kazi yake kusambaza umeme ulkiopo.
Kwa kumalizia mkuu wangu nakuomba sana fikiria kwa makini kuhusiana na hiki kibatari cha Dowans, tulikihitaji tu ikiwa umeme utakatika lakini yaonyesha wazi mwenye nyumba Kikwete na serikali yake hawana mpango wa kutuwekea Umeme ktk nyumba yetu.. na The only solution kwetu sisi kama watoto wa mzee Kikwete hatutaki kutumia kibatari, acha iwe kiza nyumba nzima hadi mzee wetu atakapo tambua kwmba Umemem ni ktk MAHITAJI ya nchi yetu ili tupate kuendelea lakini sio kutumia kibatari au mchumaa.. na kwa sababu ya Ufisadi unaoendelea. viongozi wetu watakuja fikiria kwamba sisi tumesha zoea vibatari na mishumaa, kupika kwa jiko la mkaa na kadhalika. Umeme hautawekwa na ndiyo yatakuwa maisha yetu (kimaendeleo).
Sijui kama umenipata mkuu wangu!