Junius,
Mkuu wangu usimsome Kasheshe kufikia maamuzi pasipo wewe kufikiria kwa kichwa chako undani wa tatizo hili la Umeme.
Kwanza kabisa hapa nanukuu maneno ya Malima alivyosema.
Hata hivyo, baada ya shellukindo kusema kwamba sakata la Dowans limekwisha zikwa, Naibu waziri wa Nishati na Madini, Adama Malima aliyekuwepo katika mkutano huo aliongeza kuwa, serikali haina mpango tena wa kununua mitambo hiyo ya kufufua umeme ya Dowans, lakini endapo mtu binafsi atainunua na kuiuzia Tanesco umeme kwa sheria ya sasa itakubali.
Hapo ujuu katika maandishi menkundu inaonyesha wazi kwamba serikali yetu imeshapania kuuza mitambo hiyo kwa Tanesco. Wanaposema endapo mtu binafsi akinunua mitambo hiyo anaweza kuiuzia Tanesco Umemem ina maana gani?.. Dowans ni shrika binafsi ikiwa na maana kuna mtu binafsi aliyeinunua hiyo mitambo toka Richmond na wote hawa walitakiwa kuiuzia Tanesco Umeme..Sasa kilichoshindikana ni kipi toka mwanzo! - kwa sababu ya Ufisadi... na pili Dowans ingechukua tender kinyumwe cha sheria pasipo kutangazwa tender huru kwa wawekezaji..Leo tunapitisha sheria ya kununua mitambo hiyo hiyo chini ya maamuzi ambayo ni pinzani na sheria yetu ya manunuzi...Licha ya yote hayo tumeona shirika kama Songos wakiuponda mtambo huo kuwa ni mtumba, haifai ni chavu...leo nchi nzima tunashindwa ktk maamuzi na shirika moja dogo ambalo tumeliajiri sisi wenyewe!
Mkuu hakuna asiyejua kwamba mitambo hiyo ni mali ya MTANDAO, hii ndio fact! hao kina Lowassa na Rostam kwa hiyo jina la mtu binafsi yoyote linaweza kuwekwa kama mnunuzi na tukarudi ktk makosa yale yaliyofanyika toka mwanzo..Rostam akinunua mtambo huo wa Dowans hawezi kuandika jina lake ila atazua jina jingine la kampuni. Je, mmeshasahau kwamba ni serikali hiyo hiyo hadi leo imekataa katakata kututajia nani mwenye kumiliki shirika hilo tena walidiriki hata kusema HAWAJUI mwenye kumiliki shirika hilo, iweje leo tukanunue mitambo toka shirika ambalo viongozi wetu hawafahamu mwenyewe..Hii inaingia akilini kweli?
Pili, nakumbuka vizuri kuwa kamati ya madini na Nishati kwa maneno yake Zitto mwenyewe alisema malengo ya Tanesco kununua mitambo ile ni kuiwezesha Tanesco kuwa na mitambo yake yeynyewe badala ya kukodisha jambo ambalo limetugharimu sana kwa kipiundi kifupi toka mashirika binafsi, leo hii tunarudi ktk janga lile lile. Hivi kweli mtu unaweza pindisha sheria tukanunua mali ya wizi kwa sababu mwizi ni binadamu sio mali iliyoibiwa!
Mkuu wangu ikiwa mitambo hii ina mashaka ya Ufisadi na wahusika wake ni Rostam na Lowassa basi seriikali wala shirika haliwezi kununua mitambo hiyo hadi janga la Richmond limepatiwa ufumbuzi. Mitambo ya Dowans ni ushahidi wa kesi ya Richmond ambayo kisheria inatakiwa kuwa confiscated na mashtaka kufunguliwa mahakamani lakini tunapouza ushahidi huu ni mbinu mojawapo ya kupoteza ushahidi.
Tatu,
tatizo la Umeme kwa maelezo ya Shelukindo ni tatizo ambalo LIPO toka Kikwete anaingia madarakani yalikuwepo na ktk kiwango hicho hicho.. Tuliambiwa maelezo yote alozungumza Shelukindo, hakuna jipya na wanachi tulivaa vibwebwe pamoja na ahadi ya mvua za kisayansi na kufua umeme wa makaa ya mawe, kuboresha mabwawa yetu na mengine mengi ambayo rais mwenyewe aliwaahidi wananchi kabla hata hajakaa Ikulu..Loe hii ni miaka MINNE hakuna jipya!
Na sote tunaelewa kwamba Tender ya Richmond, Watsila na mashirika mengine zilikubaliwa kama ni tatizo lka dharura ambalo lilitakiwa haraka iwezekanavyo kwa wakati ule...Ilichukua mwaka mzima kwa Richmond kufikisha mitambo yao na haraka sana tuligundua Ubabaishaji wao na tukawasimamisha.. Toka Richmond wasimamishwe ni miaka MITATU mingine imepita wakati Tanesco na serikali wakijua kwamba hizo MW 100 ni muhimu sana iweje walishindwa muda wote huo kufidia hjizo Mw 100, ila wakazanie kununua mitambo hiyo tu kwa miaka yote mitatu?.. Hivi kweli tulishindwa kuagiza mitambo mingine au hata kuwapa hiyo Tender Watsila au shirika jingine ambalo linawauzia umeme Tanesco kwa uhalali isipokuwa Dowans pekee!..
Mkuu it's been FOUR Yrs toka tuna matatizo ya umeme kwa jiji la Dar pekee na miaka zaidi ya 20 kwa mikoa ambayo imetajwa kuwa na shida ya umeme wa dharura. Ni miaka 40 kwa nchi nzima tukiondoa wakati wa mkoloni iweje leo somo kubwa la ununuzi wa mitambo ya Dowans tena Mw100 iwe makosa makubwa ya serikali ambayo imehsindwa kuanzisha vyanzo vipya vya umeme toka mwalimu Nyerere atoke madarakani.
Hadi leo hii tunategemea vyanzo vya mwalimu Nyerere ambaye alivijenga ktk wakati mgumu sana, wakati ambao serikali iligharamia kila matumizi ya huduma za wizara na taasisi zake, leo tunashindwa kabisa kujenga vyanzo vipya wakati serikali inavuta kodi pasipo matumizi makubwa lakini wepesi kuzungumzia Dowans ambayo inaingia kinyume cha sheria.