Sakata la wanafunzi kukosa mikopo: TAHLISO yazidi kuikaba Serikali

Sakata la wanafunzi kukosa mikopo: TAHLISO yazidi kuikaba Serikali

millz

Member
Joined
Apr 12, 2013
Posts
85
Reaction score
14
HUKU ikiwa bado Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu nchini (HESLB) ikiwa inasuasua kutaja majina ya Wanafunzi wapya watakaopata Mikopo wa mwaka wa masomo 2014-2015,kutokana na bodi hiyo kusema inauwezo wa kuwapa mikopo wanafunzi 30000 tu kati ya wanafunzi 58,037 waliomba mwaka huu.


Kwa madai bodi hiyo imepewa Bajeti ndogo na serikali,Nao Jumuiya ya Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu (TAHLISO)imezidi kuibana serikali na kusema haitokubali kusikia wanafunzi wanakosa mkopo na kusema kila mwanafunzi wa anayejiunga elimu ya juu nchini anahaki kupata mgawanyo sawa wa keki ya Taifa.


Hayo yamesemwa mda huu Jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Jumuiya ya wanafunzi wa vyuo vya Elimu ya juu (TAHLISO) Musa leonard Mdede, wakati wa Mkutano na Waandishi na Habari,ambapo alisema maazimio ya Mkutano mkuu wa Tahliso uliofanyika Chuoni RUCO-Mkoani Iringa,umeitaka Serikali kwamba wanafunzi wote waliomba mkopo katika mwaka huu wamasomo wapewe wote.

“Mkutano mkuu wa TAHLISO umeazimia kwamba wanafunzi wote waliomba mkopo mwaka huu yaani wanafunzi 58,037 wapewe wote kama tu kutakuwa wamedahiliwa na tume ya vyuo vikuu kuingia Elimu ya Juu,hili jambo la dharura na tunaitaka serikali kuhakikisha kufanya hivo kwani wote ni Watanzania wanaostahili mgawanyo sawa wa Keki ya Taifa”alisema Mdee.

Mdee alizidi kusema Jumuiya hiyo imeitaka Bodi ya Mkopo kuacha kutoa Mkopo kwa ubaguzi kutokana na hivi sasa kutoa upendeleo kwa watu wenye kada ya masomo ya Sayansi na Elimu na kuzipa kisogo Taaluma nyingine kwani bodi kufanya hivyo kutalepelekea Taifa likose wasomi katika masuala mengine ikiwemo Uandishi wa habari,mambo ya Fedha na sheria.


Vilevile Jumuiya imeitaka serikali kupandisha kupandisha mara moja fedha ya kujikimu kwa mwanafunzi wa elimu ya juu toka 7500/kwa siku hadi 15000 na kusema hali ya maisha imependa huku ikizingatiwa garama za vitu viko juu tofautisha na kipindi kile cha nyuma walipopitisha kiasi hicho.


Aidha Mdee aliitaka Tume ya Vyuo Vikuu nchini TCU kusimamia misimamo yake ya mwanzo ambayo ilikuwa inavitaka vyuo Vikuu vyote nchini kutopandisha Ada ya Masomo kutokana na hivi sasa vyuo vya KCMC na St Francis kilichopo Ifakara ambapo vyuo hivyo vimekaidi walaka wa tume ya vyuo vikuu nchini iliyovita vyuo visipandishe ada za masomo.


FullHabariBlog
 
HUKU ikiwa bado Bodi ya Mikopo ya
Elimu ya Juu nchini (HESLB) ikiwa
inasuasua kutaja majina ya Wanafunzi
wapya watakaopata Mikopo wa mwaka wa
masomo 2014-2015,kutokana na bodi hiyo
kusema inauwezo wa kuwapa mikopo
wanafunzi 30000 tu kati ya wanafunzi
58,037 waliomba mwaka huu. Kwa madai
bodi hiyo imepewa Bajeti ndogo na serikali,
Nao Jumuiya ya Wanafunzi wa Vyuo
vya Elimu ya Juu (TAHLISO)imezidi kuibana
serikali na kusema haitokubali kusikia
wanafunzi wanakosa mkopo na kusema kila
mwanafunzi wa anayejiunga elimu ya juu
nchini anahaki kupata mgawanyo sawa wa
keki ya Taifa.
Hayo yamesemwa mda huu Jijini Dar es
Salaam na Mwenyekiti wa Jumuiya ya
wanafunzi wa vyuo vya Elimu ya juu
(TAHLISO) Musa leonard Mdede, wakati wa
Mkutano na Waandishi na Habari,ambapo
alisema maazimio ya Mkutano mkuu wa
Tahliso uliofanyika Chuoni RUCO-Mkoani
Iringa,umeitaka Serikali kwamba wanafunzi
wote waliomba mkopo katika mwaka huu
wamasomo wapewe wote.
“Mkutano mkuu wa TAHLISO
umeazimia kwamba wanafunzi wote
waliomba mkopo mwaka huu yaani
wanafunzi 58,037 wapewe wote kama tu
kutakuwa wamedahiliwa na tume ya vyuo
vikuu kuingia Elimu ya Juu,hili jambo la
dharura na tunaitaka serikali kuhakikisha
kufanya hivo kwani wote ni Watanzania
wanaostahili mgawanyo sawa wa Keki ya
Taifa”alisema Mdee.
Mdee alizidi kusema Jumuiya hiyo
imeitaka Bodi ya Mkopo kuacha kutoa
Mkopo kwa ubaguzi kutokana na hivi sasa
kutoa upendeleo kwa watu wenye kada ya
masomo ya Sayansi na Elimu na kuzipa
kisogo Taaluma nyingine kwani bodi
kufanya hivyo kutalepelekea Taifa likose
wasomi katika masuala mengine ikiwemo
Uandishi wa habari,mambo ya Fedha na
sheria.
Vilevile Jumuiya imeitaka serikali
kupandisha kupandisha mara moja fedha ya
kujikimu kwa mwanafunzi wa elimu ya juu
toka 7500/kwa siku hadi 15000 na kusema
hali ya maisha imependa huku ikizingatiwa
garama za vitu viko juu tofautisha na
kipindi kile cha nyuma walipopitisha kiasi
hicho.
Aidha Mdee aliitaka Tume ya Vyuo
Vikuu nchini TCU kusimamia misimamo
yake ya mwanzo ambayo ilikuwa inavitaka
vyuo Vikuu vyote nchini kutopandisha Ada
ya Masomo kutokana na hivi sasa vyuo vya
KCMC na St Francis kilichopo Ifakara
ambapo vyuo hivyo vimekaidi walaka wa
tume ya vyuo vikuu nchini iliyovita vyuo
visipandishe ada za masomo
Share 1

unafaa kuigwa!
 
Aswaaa hauwez sema elimu bora wakati wachache ndo walakeki ya taifa ni wachache
 
huo ndio uongozi bora, kupigania, kusimamia na kuhakikisha haki inatolewa kwa wote.
 
Kila mtu anastahiri mkopo weng ni watoto wakulima.halafu wote tunalipa kodi.big up endeleen kutetea masilahi ya wanyonge
 
Mkuu ameongea point sana na uu uongozi nd unatakiwa ata kwenye vitengo vingine hususan vya nchi
 
Ni kweli jamaa kaongea point
Lakini je utekelezajiii utakuwepoooooo.... kama 7500/= watu wanaitumia kwa pombe na mengine je 15000/= per day itakuwaje wakati hata ukiwa nyumbani hiyo hela kwa siku humaliziii....kumbukeni hizi hela wata tudai mwisho wa siku......thankx kiongozi lakini kwa tanzania hiii utekelezaji sio leo hiyo ni miaka 10 mbele kuja kutekelezwa lakini co leo wala kesho kama watu wanakufa mahospitalini kwa upungufu wa wauguzi,dawa,wodi,na vifaa vngne na wanaona na kusikia malalamiko lakini hayatekelezwii sembuse cc ambao wengi wao wanataka hela hiyo wakale starehe angali wanajua watokako maisha ni ya shidaaaaa


Mtu atataka atumie vitu kutoka mliman city wakati anajua kwao hajawahi vaa nguo ya dukan zaidi ya mtumbaaaa.......kaka umeongea lakini tusitegemee mabadiliko ya harakaaaaa....watu wanaandamana....wanagoma lakini mwisho wa sku utekelezaji ni F sembuse sie mtu mmoja anasimama na kuongea peke ake atasikilizwa lakini je watatekelezaaa.....kuna baadhi ya wanafunzi ukiona wanavyo tumia boom uwiiiiii unaweza ukajiuliza cjui kwann nae alipata mkopo lakini wabongo tukiambiwa ukweli tuna nuna....wabongo tunapenda kusifiwa hata vitu vya kijinga utumie vibaya boom kwenye pombe ambayo unanunua kwa 24000/= per chupa halafu tukusifie na usubili kiongozi wako aje alalamike kuwa boom halitoshiii? Daaaa inasikitish lakini ndo wabongo walivyooo......pesa ya boom uhonge halafu useme haitoshiiiii......

Ni kweliiii mkopo kila mmoja ana stahili kupewa na mkopo unavyo tolewa haupo fair....thankx bro umesikika

Next tyme jaribu kuongea na wanafunzi juu ya matumizi ya mkopo wanao pewa coz wengi wana zinguaaaa najua mganga hajigangi lakini hebu cku ongea na uwachane wanavyuo wano tumia vibaya mkopo kwenye vyombo vya habari kama ulivyo wachana hawa jamaaaa wa board ya mkopo.....nakunga mkono kwa ulicho sema lakini sarafu pia ina pande mbili.....ol da best broo
 
Hivi huwa wanapewa ama wanakopeshwa?huwa wanakuja kulipa baadae kutoka kwenye jasho la mikono yao au kodi ndizo zinazolipa?
Atakae nuna na anune kaka ila kiukweli wengi boom wanatumia vibaya hawajui kodi za watu hizoo za wasio na elimu wakipgwa na jua.kitaa hawana kazi
 
Hivi huwa wanapewa ama wanakopeshwa?huwa wanakuja kulipa baadae kutoka kwenye jasho la mikono yao au kodi ndizo zinazolipa?

Wanakopeshwa kaka kwani....lakini kwa mda ambao wanatumia wao wanatumia hovyo na wengi wao mwisho wa siku wasiajiliwe watalipaje deni na kitaa hawana kazi mwisho wa siku wanakuwa vibaka akati angetumia boom vuzuri lingeweza mtoa kaka wangapi kitaa wana hanagika kupata mkopo na mda wanapo kopeshwa hizo pesa serikali inatoa wapi kama co kodi za wana nchi
 
Mmh Nina mashaka na hiyo 15000/=/day kama inaweza kutekelezeka
 
Back
Top Bottom