Sakata la Wapenzi wa Diamon kurusha chupa stejini

Sakata la Wapenzi wa Diamon kurusha chupa stejini

Hating too much,

Nadhani hayo uliyoyaorodhesha ndiyo yanayowatofautisha wewe na yeye, yaani wewe una elimu na usimamizi mzuri na ndio maana upo hapo ulipo na yeye hana ndio maana yupo hapo alipo.

Busara ni kusubiri kumsikia na yeye anachosema badala ya kukimbilia kuhukumu kwa maelezo ya upande mmoja.

Nijuavyo mimi kila kizuri kina gharama, utamuelewa vipi mtu atakayekuja kwako na kukwambia anauza range rover evoque mpya kwa tsh milioni mbili ?.....kama ni mtu mzima na una akili timamu basi kitu cha kwanza utakachoweza kufanya ni kumuomba arudie alichosema, then nadhani kuepusha shari utajiondokea.....nadhani shughuli yake umeiona hapo kwenye video.

Na iwapo kuna alichokosea basi bado hata wewe unaweza kutoa ushauri afanye nini next time....nionavyo mimi bado ana nafasi ya kutafuta ushauri kwa waliomtangulia, na wazoefu wa mambo ya burudani iwapo kama alizengua.....sidhani kama kuna tatizo kuuuuuuuubwa hapa.

ukweli una sifa ya kuwasha - source miss strong

yani we FYATU mwenzio anaambiwa ukweli na anashauriwa lakini wewe unasema anachukiwa.huu ndio ukweli na kama umemsoma mwandishi huyo kwa utulivu utagundua kuwa amejaribu kuhakikisha diamond anaonekana mbaya na mjinga,kigeugeu,anajikweza kupitiliza.

hebu tueleze kama hayo aliyo yadai diamond yalikuwa ndani ya makubaliano au mkataba wa show, pengine waandaji walihamua kutimiza matakwa yake ili wasiwakwaze mashabiki.

Mwandishi amewafumba macho kwa kumpamba mwishoni lakini lengi lilikuwa ni kimshitaki diamond kwa mashabiki wake na wafanya biashara ya muziki.

Ni wazi kuna tatizo kwa diamond na hili swala linahitaji ufafanuzi maana habari hiyo si nzuri kwa biashara yake.
 
Last edited by a moderator:
hakika Nguruvi3. ni wazi hii habari kama watu waneisoma vyema ni wazi inamchafua diamond maana mwandishi ameonesha diamond ni mtu wa kulinga na ni mtu wa kwenda kinyume na makubaliano na anaye jikweza kupita kiasi.

Ni kweli kwenye hili inabidi meneja au diamond mwenyewe anatakiwa atoe ufafanuzi maana mwandishi ameonesha kuwa diamond ni mwanamuziki kigeugeu na asiye jua nini maana ya makubaliano, na huyu mwandishi amemuharibia japo mwisho kampamba lakini dhima yake ilikuwa kuonesha jinsi diamomd alivyo na ujinga.

Na hili swala litamuharibia na wengi wanaweza kufurahi kuwa kapambwa kumbe ukisoma kwa makini utagundua mwandishi anajaribu kumpaka matope.

Kwa swala hili ni vyema wakatolea ufafanuzi maana litamwalibia biashara kabisa.

Diamond amepata nafasi asijaribu kuichezea.
Sasa tukiwapa maarifa wanasema eti ni haters!!
Nina hakika Diamond haiingi huku lakini wapo watu wake wa karibu, waende na kumsadia maana naona anguko lake(siombei) lakini kwa uzoefu tuliona nao habari kama hizi si nzuri.

Fikiria mwandishi anaanza na presidential suite na private jet halafu mwisho anamalizia Diamond alikonga hata hivyo. Hapa kuna damage kubwa sana kwa Diamond.

Mkuu Pasco nadhani huwa anakutana na vijana katika mihangaiko yake ya mkate labda anaweza kutusadia kumnong'oneza kama akipata fursa
 
Last edited by a moderator:
hebu twambie heaven on desert kama alicho kiomba diamond kilikuwa ndani ya mkataba au lah.
unajua kwa nini mwamdishi amemuita diva?
Diva ina maana nyingi, yaweza kuwa ndava, mtemi, kichwa ngumu n.k. Ukiitwa diva kwa jambo jema haijambo, lakini unachelewa ndege, unaomba usafiri wa anga na chumba anacholala museveni halafu mtu anasema wewe ni ndava au kichwa ngumu hapo lipo tatizo
 
Mkuu Pasco nadhani huwa anakutana na vijana katika mihangaiko yake ya mkate labda anaweza kutusadia kumnong'oneza kama akipata fursa
Nilikutana naye Dodoma kwenye event fulani , yeye akiwa entertainer, mimi nikiwa digital produce. Fungu Nile 2quote lilikataliwa likapigwa panga hadi half, kwa kisingizio cha tight budget!. Nilipopata upenyo nikaidukuzi overall budget, nikaona fungi lake, ni mkwanja mnene! 6mara 4 ya kafungu nilichokatiwa mimi nikilinganisha na anachofanya na kukubaliwa, na ninachofanya mimi, niliishia kushangaa tuu na kukubali watu wana bahati zao!.

Dogo ana behave ki MJ,MJ hadi dressing, hajui kusalimia!, atasikiliza?!. Aliingia wakati JK anahutubia, watu walimshangilia kuliko hata rais!.Mimi nilimpenda Diamond yule humble and down to earth aliyeimba Mbagala huku rangi yake ikiwa ni maji ya kunde na sio huyu cheupe, bishoo na big super star nadhani kwa sasa ndiye #1 top bongo celeb baada ya Wema!.

Nikukutana nae tena nitamshauri, ila kiukweli ni mmoja wa hastily climbers!, usually have a sudden fall!.
P.
 
huyo mwandish kapotosha..its true kuwa diamond popote aendapo na team yake huwa ni lazima alale hotel yenye hadhi ya 5 star kulingan na eneo husika.but hiyo ishu ya mombasa hakuchelewa kwa sababu hizo walizoandika but alizinguana na waandaaji baada ya wao kutaka wamlipe nusu ya pesa iliyobaki (zaid ya dolla 7000 )baada ya show na diamond halipagwai nusu nusu hivo kuepuka dhuruma.so akakomaa mpaka wakamlipa pesa iliyobaki ndiyo akapanda stejin akiwa amechelewa na ahow alipiga vizuri tu...na diamond ni mtu asiependa masihara or mtu kuonyesha dharau kwa kazi yake..coz music kwake ni biashara..hakuna anaependa ahalibiwe biashara yake na ni mara nying tu alishakataa show za mamilion coz za ubabaishaji ka hivyo
#WCB
 
ukweli una sifa ya kuwasha - source miss strong

yani we FYATU mwenzio anaambiwa ukweli na anashauriwa lakini wewe unasema anachukiwa.huu ndio ukweli na kama umemsoma mwandishi huyo kwa utulivu utagundua kuwa amejaribu kuhakikisha diamond anaonekana mbaya na mjinga,kigeugeu,anajikweza kupitiliza.

hebu tueleze kama hayo aliyo yadai diamond yalikuwa ndani ya makubaliano au mkataba wa show, pengine waandaji walihamua kutimiza matakwa yake ili wasiwakwaze mashabiki.

Mwandishi amewafumba macho kwa kumpamba mwishoni lakini lengi lilikuwa ni kimshitaki diamond kwa mashabiki wake na wafanya biashara ya muziki.

Ni wazi kuna tatizo kwa diamond na hili swala linahitaji ufafanuzi maana habari hiyo si nzuri kwa biashara yake.

Nasisitiza kwenye maelezo yangu kuwa twahitaji kusikia utetezi wa Diamond, hayo ni maelezo ya upande mmoja ambayo hayatoshi kumuhukumu.
 
Nilikutana naye Dodoma kwenye event fulani , yeye akiwa entertainer, mimi nikiwa digital produce. Fungu Nile 2quote lilikataliwa likapigwa panga hadi half, kwa kisingizio cha tight budget!. Nilipopata upenyo nikaidukuzi overall budget, nikaona fungi lake, ni mkwanja mnene! 6mara 4 ya kafungu nilichokatiwa mimi nikilinganisha na anachofanya na kukubaliwa, na ninachofanya mimi, niliishia kushangaa tuu na kukubali watu wana bahati zao!.

Dogo ana behave ki MJ,MJ hadi dressing, hajui kusalimia!, atasikiliza?!. Aliingia wakati JK anahutubia, watu walimshangilia kuliko hata rais!.Mimi nilimpenda Diamond yule humble and down to earth aliyeimba Mbagala huku rangi yake ikiwa ni maji ya kunde na sio huyu cheupe, bishoo na big super star nadhani kwa sasa ndiye #1 top bongo celeb baada ya Wema!.

Nikukutana nae tena nitamshauri, ila kiukweli ni mmoja wa hastily climbers!, usually have a sudden fall!.
P.

ni vyema ukampa ushauri asije akajiponza
 
I love how the article was written!! Fack Diamond!!
 
Back
Top Bottom