Sakata la Wazee EAC: Litaisha lini?

Wengine wanaonekana vijana???!!! haielekei kama wote hawa walikuwa kazini miaka 30 iliyopita!

Mkuu hao wengine ni warithi wa marehemu baba zao ama babu zao waliokuwa wakifanya kazi EAC, ndo wandai badala ya hao waliokufa ama wengine ni wazee sana kufatilia madai yao!!

Ushi
 

Ndugu yangu YournameisMINE, unajua unachokisema au unasema unachokijua. Hivi unajua kwanini hawa wastaafu wanainuka kudai haki zao leo na si miaka mitatu baada ya kuvunjika kwa shirikisho. Hivi vitu haviji tu kutoka hamna mahali. Vina sababu zake. Kwa kukusaidia nenda tena kapitie madesa yako ya historia ya uchumi wa nchi hii.

Hivi unaweza kumdai mdeni wako aliefilisika na unajua kwamba amefilisika!!

Kwa kuongezea hapo, nilikuwa naamaanisha MWALIMU NYERERE!!!!. Haihitaji digrii kujua kuwa mwalimu alikuwa binadamu. Kuna wakati alifanya vitu sivyo ndivyo. Lakini kwa hili la wazee si la kumnyooshea kidole mwalimu hata kidogo. Ni uhuni tu wa hawa jamaa!!!.
 


.........much as I hate to admit it, you have a very big POINT there, mkuu!
 
Picha wazee walikuwa barabarani leo asubuhi !








Nimesaidia kuziweka zionekane. Ukishazi-upload una-copy link, halafu unatumia "insert Image" japo source ni JamiiForums.




.
 



....and you have an even BIGGER POINT, mkuu! I LOVE JF!
 
Wengine wanaonekana vijana???!!! haielekei kama wote hawa walikuwa kazini miaka 30 iliyopita!

wazee wao nafikiri watakua hawajiwezi au walisha aga dunia kwaio watakua wanawakilisha

by the way sizani mtu asubuhi yote ile uende tu kufunga barabara bila sababu yoyote labda uwe na upungufu wa akili.

leo msg nafikiri imewafikia ipasavyo serikali
 
This is an embarrasment!Ninaungana na Gembe kwamba JK is a one term president!Hivi huyu mtu ana masikio kweli?Haoni watu wameshachoka kabisa?Na bado serikali isipotoa tamko lao kuhusiana na ada za wanafunzi nao wanagoma!Jana waaandishi wa habari leo wazee kesho nani?Is this country on the verge of collapsing and being termed as a failed state?
Sijui tunakoelekea kwa kweli!
 

i think we have an ceremonial president
 
wamekoma, hao wazee so ndo namba wani wapiga kampeni za ccm kwamba ndo chama chao cha zamani? sasa mbona selikali wanayoipenda imewasaliti, wakione cha moto kidogo. vijana tunaposema waachane na icho chama wao huwa wanafikiri tunawapoteza. ni funzo kwao kwa uchaguzi wa 2010. poleni kidogo tu lakini.
 

Wazee wamekuwa wastaarabu vya kutosha. Kama sikosei pesa zao zilitolewa tangu 1984 ni miaka 24 sasa tangu pesa zitolewe. Na wameanza kudai pesa zao kwa kutumia njia za kistaarabu bila kuwaathiri wasiohusika na kama binadamu inafika wakati wanaona ni bora watafute njia mbadala ndiyo watasikilizwa. Kikwete haoni kama kuna umuhimu wa kukutana na wazee hao, anadhani kwa kukaa kimya tatizo la wazee hao litakwisha kimya kimya. Kuna faida gani basi ya kuwa na kiongozi wa nchi ambaye hayuko tayari kutafuta uvumbuzi wa matatizo yanayowakbili wananchi wake!? Kama nchi imemshinda ni bora aachie ngazi kuliko kuendeleza usanii.
 
.


TATIZO LA EAC LILIANZA NA MCHONGA...HUO NDIO UKWELI.

You nail it bro,

I think it will be better if we could put like this. UFISADI uliaanza zamani sana hata kabla ya Mkapa sema watanzania wengi walikuwa hawajasoma na pia magazeti yalikuwa hayako huru sababu yalikuwa yamejaa jukwaa la wahariri lile kla zamani ambalo serilai inalitambua.

Jukwaa hili jipya ni kiboko,Absalom Kibanda unatisha mdogo wangu..Keep it up,Najua ulimpa sana heko Mkulu Jk kipindi cha 2005 kabala haujamfahamu.

Pesa za Wastaafu zililiwa kipindi cha mchongo na wizarani hazipo,ila busara inatakiwa itumike kwa rais kutoa pesa katika mfuko wa rais,una pesa nyingi sana ..

toka mwezi uliopita wastaafu na maandamano,Yes am tired with this issues,Rais wangu naomba uchukue hatua hata kama awewe ni bubu mtendaji?
 

Hilo swali lako mkubwa limenifurahisha sana, tena sana!Ikulu siyo mahali pa kukaa na kula kuku kwa mrija, pale ndio makao makuu ya matatizo yote ya Watanzania! Kama mtu anakimbilia pale akidhani kwamba kwenda kula starehe, matokeo yake ndio hayo sasa!! Kila kukicha maandamano!
 
mimi kinachonisikitisha ni kwamba utasikia rais anataka kuongea na wazee wazee hao hao ndo watakwenda na kupiga makofi na nyimbo za kumsfia kwa sana. Pamoja na hilo inasikitisha sana kuon vingozi wetu wanashindwa kushughulikia suala hili la wazee wetu kwa ufanisi mpaka yanatokea haya yote. Kwakweli hata vyombo vya usalama nilidhani vingepaswa kuheshimu hawa wazee wetu , inasikitisha san kuona viongozi wetu wanakosa heshima na huruma
 
baba, hilo ni funzo kwao, siku ingine watakiona icho chama chao cha mafisadi sumu.
 
Jamani hawa wazee pesa zao zilitumika kupigana vita ya kagera na uingereza iliahidi kulipia pesa hizo mpaka leo hazijalipwa
 
Jamani hawa wazee pesa zao zilitumika kupigana vita ya kagera na uingereza iliahidi kulipia pesa hizo mpaka leo hazijalipwa

ina maana pesa ya wastaafu ililipwa kwa ajili ya vita??
 

ukiangalia vitu kama hivyo mabadiliko hayatatokea, ni kupunguza kero lakini cha msingi ni kafanikiwa katika malengo
 


Mwana wa Mungu, sikuungi mkono katika hili.
Sio kweli kuwa wazee ndio wanaishikia wanaopenda ccm tu, bali hata vijana kwa ujumla mmekuwa wagumu mno wa kufikiri.

Takwimu zinaonyesha kuwa karibia asilimia 49% ya watanzania ni umri wa miaka 0-17, 33% ni umri wa miaka 18-44, wakati wazee wa umri wa 45-100 ni sawa na 18%.

Kwa taarifa zaidi vijana kati ya miaka 18-34 ni takribani 23%, wakati watu wa umri 35 na zaidi ni 28%, sasa hapa unaonaje.

Sasa kuwasingizia wazee wakati vijana mmekuwa wagumu wa kubadilika ni makosa, ona jinsi wazee wanavyoonyesha uweza wa kudai haki zao, mie nawaunga mkono. Bado kama vijana wangekuwa wakweli, hali isingekuwa hii tunayoiona leo.
 



Kwanza nakiri kwamba nimepatwa na jazba, lakini hio haibadilishi kitu, msimamo wangu hautabadilika jazba itakaposhuka. Chanzo cha jazba yangu ni jazba iliyojionesha kwenye post yako ya awali. 🙂


Naelewa unachosema, sioni tatizo kuuingiza uongozi wa Nyerere kwenye hili. Hata hivyo ulimtetea JK bila kujua unafanya hivyo. Halafu uchaguzi wa mtu uliyeamua kum-quote ndio ulileta balaa, maana Lighondi alikuwa akizungumzia kitu muhimu sana ambacho uongozi wa sasa kwa uzembe na ubinafsi umethubutu kupuuzia.


Maneno ya Lighondi hapa.





Nimekuelewa.




.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…