Sakata la Wazee EAC: Litaisha lini?

na hiyo dhamana ay pesa???

dhamana gani tena? mimi nasema hakuna haja ya kuwapeleka mahakamani hao wazee, kinachotakiwa ni kuwsalipa tu kwani ni pesa ngapi? hao wazee hawawezi kutulia mpaka wamepata chao.
 
"Hivi kwa uzembe huu wa UWT(TISS) kushindwa kuliona hili mapema kuna mtu atawajibika?"

Hawakuona mawe yaliyojipanga barabarani chunya itakua kuwasuspect vikongwe?....
 

YuonameisMINE ama mwaka 1977 ulikuwa hujazaliwa au unatawaliwa na chuki isiyo kifani na Mwalimu Nyerere.

Jumuiya ilikufa mwaka 1977 na zoezi la ugawaji mali za jumuiya lilichukua miaka saba na fedha za wastaafu zililipwa benki kuu ya Tanzania mwaka 1984. Zoezi la kuwalipa wahusika, baada ya uhakiki, lilitakiwa lianze mwaka 1985 wakati Mwalimu hayuko madarakani. Kati ya mwaka 1985 mpaka 1990 ilikuwa ni vigumu sana kulalamika na ukasikika kwa sababu ya monopoly ya vyombo vya habari. Hata hivyo mwaka 1991 ndio vilio vya hawa wazee vilianza kusikika kupitia magazeti binafsi kama Family Mirror. Kiongozi wa kwanza wa serikali chini ya Raisi Mwinyi kutamka kwa mbwembwe kuwa serikali haitawalipa hata wakipiga kelele nama gani alikuwa ni Mzee Cigwiyemwisi John Malecela, Waziri Mkuu na Makamu wa kwanza wa Rais. Huyo Malecela pia ndiye kabla ya hapo alikuwa balozi wetu Uingereza mwaka 1985 wakati "crown Agents" wanatoa hundi ya malipo haya kwa serikali ya Tanzania. Hizo fedha kwa pauni za kiingereza zililipwa moja kwa moja Benki kuu ya Tanzania.

EAC ilikuwa ni jumuiya ya kimataifa na ilikuwa na bunge lake, service commission yake, pensions fund yake na saving scheme yake. Makato ya pension yalitunzwa Uingereza kwa agents wa EAC waliojulikakna kama "crown agents". Mkataba wa EAC ulisema kuwa ikitokea jumuiya ikavunjika waajiriwa wake walipwe fedha zao kwanza ndio mengine yafuate, period. Pia waliainisha namna ya kulipa hizo kulingana na thamani halisi ya dola na riba ya asilimia 7%. Pia kumbuka kuwa baada ya kukalia hizi pesa kwa muda mrefu, serikali iliwahi kutamka kuwa madai yamekuwa makubwa kuzidi uwezo wa serikali - swali ni kwa nini hawakulipa mapema ? Hata kama kulikuwepo na matatizo ya kifedha nchini je serikali ilikuwa na haki gani kutumia fedha ambazo hazikuwa za serikali na kama walikopa ni kwa makubaliano yapi. Ukweli ni kuwa huu ulikuwa wizi wa kiwango cha kutisha kinachozidi hata hiki cha EPA.

Hawa hawakuwa wafanyakazi wa serikali na hizo fedha hazikuwa za serikali. Ni kama vile wewe unaaminiwa unapewa fedha umfikishie mag3, halafu wewe unaamua kuzitumia bila idhini yangu je, wewe siyo mwizi ? Kwa mfano mwingine karani wa fedha anapewa mshahara awalipe wafanyakazi, yeye anaamua kuzitumia je, si atakuwa ameiba ? Ni serikali iliyowaibia hawa wazee fedha zao na hivyo serikali inawajibika iwe ya Mwinyi, Mkapa au Kikwete si hoja. Mimi hili swali nalielewa vizuri sana kwa sababu nimekula miaka (lol). Kuna wakati hata wafadhili walikuwa tayari kuisaidia serikali kwa kuikopesha fedha iwalipe hao wastaafu kupunguza fedheha mradi tu serikali ieleze ilitumiaje hizo fedha. Kwa kuwa fedha zenyewe zilitumika kiajabu ajabu na katika mazingira yasiyoeleweka, serikali ilishindwa kufanya hivyo na hapo kuonyesha wazi kuwa fedha zilihujumiwa.

Katika kujaribu kujikosha kuna wakati serikali ilitoa malipo ya kati Tshs. 100.00 hadi 500,000.00 kwa kandika hundi katika kile kilichoonekana kama matusi kwa wastaafu. Serikali siyo tu imewaibia wananchi wake bali imekaidi hata amri ya mahakama kwa kutotekeleza makubaliano yaliyofikiwa. Madai ya wastaafu yamewatajirisha wezi serikalini na kinachonisikitisha ni ukimya wa bunge letu kwenye jambo hili. Wezi hawa wanatakiwa waache usanii na wazee wapewe haki yao ambayo haitapotea hata kama itadaiwa na vitukuu wao. Kwamba wabunge wanapigana vikumbo na hao wazee huko wizarani wakifuatilia posho zao bila chembe ya huruma kwao ni dalili ya uozo ndani ya nchi na ishara ya kupotea kwa maadili. Inasikitisha.

Kabla ya Raisi Mkapa kuondoka madarakani mwaka 2005 alitamka kwamba atahakikisha hamwachii mrithi wake hili deni ambalo lilikuwa limefikia karibu shilingi bilioni 450. Fedha zilitengwa na Waziri wa fedha Mramba alitangaza bungeni kuwa hawa wazee wangelipwa kwa awamu. Awamu ya kwanza wangelipwa bilioni 110 chini ya robo ya madai yao na wangeendelea kulipwa mpaka deni liishe. Hizo fedha zilizotengwa ziko wapi na nani aulizwe kama si serikali ya Kikwete ? Ajabu ni kuwa hizi fedha hazijalipwa hadi leo na wabunge wako kimya kama vile hawakuwa bungeni wakati huo na hivyo wazee kujikuta yatima kwenye nchi yao. Serikali haiwajali, bunge liko kimya na maamuzi ya mahakama yanadharauliwa - sasa nani asingelala barabarani ?
 
Dozi ya JF imenitosha kwa leo, mniwie radhi - I'm going home.
I need time alone to contemplate calmly on a number of things.
Bye bye now!




.
 

Huyu dogo Yourname alikuwa bado yuko kwenye nepi na bado alikuwa ananyonya.....na ndio maana hana appreciation yoyote kwa Nyerere....
 
Hivi CCM ambacho ni chama kilichoiongoza Serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania kwa miaka yote huku Mwenyekiti wake wa chama akiwa rais au rais mstaafu ilikuwa na maamuzi yeyote ya kuweza kuwasaidia hawa Wazee kulipwa mafao yao?

Inaonekana kuna wengi hapa wanajitahidi kumuondoa Nyerere katika kuhusika kwake kuwanyima haki zao wazee wetu waliokuwa wafanyakazi wa EAC. Mimi nina maswali yafuatayo.

1)Je Nyerere aling'atuka lini uenyekiti wa CCM?

2)Je Nyerere hakuwa na influence ndani ya Chama na Serikali baada ya yeye kung'atuka Urais? Na kutokana na hiyo influence yake, alifanya nini kuhakikisha anatetea haki za hawa wazee na hatimaye kulipwa Mafao yao.

3)Je mnakubaliana nami kwamba marais wote waliopita na hata wa sasa wanahusika katika kuwanyima haki zao hawa wazee. Tena kutokana na jumuiya hii kuwepo wakati wa utawala wa Mwalimu Nyerere, nadhani yeye ndio mhusika nambari moja katika kuwanyima haki hawa wazee.

Sidhani ni busara kwa wengi kujitahidi kumsafisha Mwalimu Nyerere katika udhalimu huu wa haki za wafanyakazi wa iliyokuwa EAC, yeye ni mhusika nambari moja ambaye ameshiriki kwa kiasi kikubwa kuwanyima haki hawa wazee.
 

Nyundo inatumika kutuponda kichwani tukilalamika na kudai haki zetu na jembe linatumika kutukata miguu ya kiuchumi ili tusiweze kusogea mbele matokeo yake hali ya maisha ya mtanzania ni "KILA KUKICHA BORA JANA" na wale wenye angalau kidogo basi wanabakia palepale miaka nenda rudi,hiyo ndiyo nadhani correct interpretation ya jembe na nyundo kwa sasa tofauti na ilivyokusudiwa.
 

Jiulize tu, walikuwa na ubavu wa kumgusa?utapata jibu
 

Kama tumefikia kukusanya kodi mpaka zaidi TShs billioni 300(soma - Sunday Observer hapa) kwa mwezi sidhani kama kulipa kulipa TShs billioni 450 kwa awamu ya miezi 5 mpaka 12 inashindikana. Kinachokosekana ni utashi, uaminifu na roho ya huruma na kinyume chake watu wana roho mbaya, wivu na husuda hasa hapo serikalini.

Nadhani wengi wa watumishi serikalini wanaangalia na kuona wao kwa miaka yao ya kazi serikalini wengine mpaka 30 au 40 hawapati hela kama hiyo hao wazee wanapata baada ya kufanya kazi miaka 10 kwenye jumuia pamoja na interest yake.
 
Ok tukubaliane; Nyerere ndiyo chanzo cha haya matatizo ya wazee. Tukubaliane kuwa kutolipwa kwao kumetokana na roho mbaya, choyo na udhalimu wa Nyerere. Tukubaliane pia kuwa kama Nyerere asingeiingiza nchi kwenye Jumuiya ya Afrika ya Mashariki tusingekuwa na tatizo hili leo hii. Sasa tumekubaliana hayo na kuweka lawama panapostahili, how does that resolve the plight of these people.

Tumfukue Nyerere kaburini na kumrudisha Ikulu ili afanye maamuzi? Tumuombe Mr. Q aturudishe kwenye muda (time warp) ili Nyerere afanye maamuzi ya mwaka 1980? Tufanye nini ili Nyerere atusaidie kutatua tatizo la wazee wetu hawa baada ya kugundua kuwa yeye ndiye mhusika mkubwa?
 
..sasa hilo ni tatizo la nani!? na nini unajaribu kutuambia hapo? kwamba alikuwa dikteta au sio?? hilo ndio tatizo, braza...kwahiyo huyu "mswahili" wanamburuza kwa kuwa yeye si Nyerere au ni nini hasa?

Tufanye nini ili Marehemu Nyerere mhusika mkubwa na nambari moja wa matatizo ya wazee hawa aje kutatua matatizo yao? Twende tukahani kwenye kaburi lake au tulifukue na kumuweka tena Ikulu ili tupate ufunuo wa kushughulia matatizo yote ambayo yalianzia chini ya utawala wake? Baada ya kuhakikisha tumembesha marehemu mzigo wa matatizo yetu yote kwa usahihi kabisa na lawama zote kuziweka juu ya kaburi lake afanye nini kutoka huko ahera madukani kutusaidia na tatizo la hawa wazee? Unataka hawa wazee waende Butiama kulia kwenye kaburi la Nyerere kwa kuwawekea roho ngumu na kula mali zao?
 

Lakini ni Nyerere huyo huyo ndiye aliyewaambia IKULU si maala pa kukimbilia ni mzigo.....sasa nadhani waheshimiwa wanaanza kuyaona. Kifupi mimi sioni sababu ya hawa wazee kutolipwa, serikali ipunguze au kubana matumizi kwa mwaka mmoja. Wakiweza kwa mwezi kubana TShs billioni 40 mpaka 50 kwa miezi kumi na mbili wanalipa hili deni la hawa wazee.

Mkapa kuna wakati alimua kuwa tunalipa deni letu la nje ingawa alipingwa hata na Nyerere lakini aliamua kukaza buti matokeo yake baadaye madeni mengi yalisamehewa na Tanzania ikaanza kupata mikopo. Kinachohitajika ni boldness ya Rais kama kiongozi wa nchi kuchukua maamuzi mazito na machungu wakati mwingine, afuatilie kwa dhati kuwa matumizi yanabana na hawa wazee wanalipwa kutokana na savings za serikali itakapobana matumizi. Nadhani hili linawezekana.
 

Asante YournameisMINE
Lakini nafikiri kuna kitu hukukielewa katika maelezo yangu. Kwanza nia yangu haikuwa kumtetea Nyerere bali kuelezea mtiririko wa sakata lenyewe. Pili kwa huo umri uliyoutaja ni wazi kuwa iliyokuwa EAC hukuijua na historia yake hukuijua.

1. Mgawanyo wa mali ya defunct EAC ulisimamiwa na World Bank na uliendeshwa na mtaalamu wa benki hiyo aliyejulikana kama Dr. V. Umbritch.
2. Uhakiki wa mali kwa nchi zote tatu, Kenya Uganda na Tazania, haukuwa kazi ndogo kama unavyofikiria na ulijumuisha mashirika na idara zote za jumuiya kwa kuzingatia assets na liabilities zote za jumuiya nje na ndani ya Afrika Mashariki na hasa Ulaya.
3. Viongozi wakuu wa nchi hizi tatu walikabidhiwa report mwaka 1984 na baada ya kuikubali walitakiwa waweke saini zao. Report ilikuwa kubwa na ndefu na ilihitaji muda kusoma na kupitia kila kipengele. Kama sikosei nafikiri ilikua na kurasa zisizopungua mia nne.
4. Baada ya hapo hesabu za malipo zilifanywa na hundi moja kutolewa kwa kila nchi kulipa raia wake waliohusika. Uhakiki wa wadai ulifanyika na mwaka 1987 ulikuwa uwe mwanzo wa malipo.
5. Kwa sababu zisizoeleweka serikali ya Mwinyi haikuweza kutekeleza hilo na wadai pamoja na kulalamika kimya kimya hawakuwa na namna nyingine ya kusikika kwa kuwa hakuna gazeti wala redio iliyoweza kutoa habari hizo. Juhudi zao za kukutana na kuandamana zilidhibitiwa vilivyo na FFU ambao wakati huo walikuwa wamepata zana za kisasa za kusambaratisha mkusanyiko wowote.
6. Baada ya kusikia wenzao wa nchi zingine wanalipwa ndio wakazidi kupaza sauti na mwaka 1991 madai yao yaliweza kuchapishwa kwenye vyombo vya habari vya binafsi kama Family Mirror. Ni wakati huo serikali iliweza kutoa tamko kupitia kwa waziri mkuu.
7. Ingawa sikumbuki vizuri kuna wakati walijaribu kumwona Mwalimu ambaye wakati huo ailshastaafu hata uenyekiti wa CCM na inasemekana alistushwa sana kusikia hawajalipwa.
9. Wakati jumuiya ikingali hai, Jakaya Kikwete aliwahi kuwa kwenye baraza la Mawaziri wa EAC na anaelewa vizuri sana hili jambo hivyo ukimya wake unashangaza kweli.
10. Ukimya wa wabunge, waandishi, watetea haki za binadamu na makundi mbali mbali kwenye hili swala ndio unaowasukuma hawa wazee kujiuliza maswali ambayo majibu yake ni kitendawili na kuamua kulala barabarani.
 

Ahsante sana Mag3 kwa maelezo yako mazuri.

Mimi swali langu kwako ni kivipi Mwalimu Nyerere nae asilaumiwe kwenye hili suala la kuwanyima haki zao hawa wafanyakazi wa iliyokuwa jumuiya ya EAC Kama marais wengine waliomfuata?

Je kutokana na hiyo tetesi ya hao wazee kumuona Mwalimu Nyerere na yeye kushtushwa kwa kutolipwa kwa hawa wazee, ni uamuzi gani aliouchukua kuhakikisha hawa wazee wanalipwa huku ikijulikana kabisa yeye katika mwaka huo wa 1987 alikuwa na influence kubwa sana serikalini na kama sikosei alikuwa bado mwenyekiti wa CCM.
 


Geeque, kiwango gani cha lawama Nyerere apatiwe?

a. Jumuiya imevunjika
b. Kaanzisha mchakato wa kufuatilia mali na madeni ya EAC
c. Mchakato ukamalizika
d. Pesa zikawa tayari kabla yeye hajaondoka
e. Alipoondoka 1985 mchakato ulikwisha na fedha zilikuwa zianze kutolewa ndani ya miezi michache.
f. Wenzetu Uganda na Kenya wakaanza kuwalipa watu wao
g. Fedha zetu zikawa tayari 1987
h. Nyerere alishang'atuka na Rais alikuwa mwingine, baraza jingine na viongozi wengine waliotakiwa kutekeleza kitu kilishokwisha amuliwa.
i. Mwinyi hakutoa zile fedha ambazo Nyerere alisimamia mchakato wake toka mwanzo hadi anaondoka madarakani hakukuwa na malalamiko ya waliowahi kuwa watumishi wa EAC.
j. Ni baada ya Mwinyi kushindwa kutekeleza na kugawa fedha ilivyokuwa ndio minong'ono ilipoanza
k. akaja na Mkapa ni yale yale
l. Na sasa Kikwete ni yale yale.


Sasa Nyerere kosa lake ni kutokuwa na influence? Kama yeye mwenyewe alioneshwa kushangazwa kuwa fedha ambazo alijua tayari zipo na hazijagawiwa ilivyopaswa huoni kuwa ndio sababu ya yeye katika ile miaka ya tisini kuhoji sana mambo ya Ikulu? Aliposema kuwa "Ikulu kunanuka rushwa" yawezekana alikuwa anajua mengi kweli ambayo alijaribu kuyafuatilia (kuweka influence). Yawezekana alijaribu kufanya influence ya mambo lakini hatimaye alijua kuwa he was out of the loop?

Inawezekana alikuwa na influence lakini hakuwa Rais. Hakuwa na uwezo wa mambo mengi sana ndani ya serikali influence yake ilikuwa zaidi ndani ya chama. Na utakumbuka aliamua pia kuachia Uenyekiti wa chama kule Kizota na ninadhani ni mwaka huo huo 1987 au ilikuwa 1990 ile?

Lakini Mwinyi si bado yupo hai kwanini yeye hauulizwi kuhusu sababu zilizomfanya asiwalipe wale wazee na kama Nyerere alijaribu kumshawishi kwa namna yoyote ile.. Malecela yupo hai, na wengine waliokuwepo bado wapo kwanini hawa hatuwaulizi walihusika vipi kuhusu malipo ya wazee hawa?
 
Man...I'm tired of hearing Nyerere this...Nyerere that.....can you people get over him? Geeeez!!! The man is dead and he ain't coming back. Get over him....
 
Man...I'm tired of hearing Nyerere this...Nyerere that.....can you people get over him? Geeeez!!! The man is dead and he ain't coming back. Get over him....

Umesema kweli Nyani,

Nadhani watu/viongozi wasipomtoa Nyerere vichwani mwao na kuanza kufikiria kwamba wao ndio wenye dhamana na taifa hili kwa sasa tutaendelea tu kuwa wa mwisho kwa kila kitu. Viongozi wanatakiwe waanze kufikiria kuhusu solution za matatizo sio ....kila siku Nyerere Nyerere Nyerere kama njia ya kukwepea lawama.
 
tatizo langu lipo palepale kwamba, "waajiliwa wa EAC walipaswa kulipwa kwanza incase jumuia inavunjika." Hayo ni maneno yako msee, sasa kama ndivyo hivyo kwanini hilo lisiwe la kwanza na badala yake limekuwa la mwisho?

Sijui kama umemnukuu vizuri au umeelewa vibaya lakini utaweza vipi kuwalipa watu mafao wakati jumuiya bado iko hai? Yaani unamlipa mtu kabla jumuiya haijavunjika na ulijua itavunjika au just in case inavunjika?

Kama Nyerere alikuwa muadilifu, mpenda maslahi ya watu wake na kumweka nje ya hii mess (kilawama) ilitakiwa asimamie utekelezaji wa waajiliwa kulipwa kwanza kabla ya hayo mengine.

Kasimamia hadi cheki imetolewa mwaka 1987; ulitaka apangishe mstari pale msasani na kuanza kuwalipa kutoka mfuko wake?


Nyerere keshakufa, na tatizo bado lipo, what DO WE DO NOW? Kuendelea kumlilia Nyerere hakutatui tatizo ama kunatatua? Toa pendekezo leo hii serikali iliyoko madarakani sasa ifanye nini kutatua tatizo la wazee hawa? Hutaki kufanya hivyo unataka tumbebeshe lawama Nyerere, tayari tumembebesha.

Hakuwa mwadilifu,
Hakulifuatilia suala hili
Alitakiwa kufanya hivi hakufanya
bla bla bla..

Now we are here, right now, what do we do?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…