Brazakaka,
Sidhani kama umri wangu au nimezaliwa lini ni nyeti ktk huu mjadala! lakini kama itasaidia basi mie umri wangu ni kati ya miaka 28-32....
Chuki sina na bwana Nyerere na hata ikitokea siku nimekutana nae mbele za haki, basi mie nitamueleza yalo alotuachia na li chama lake bovu aliloliasisi..
Umetoa maelezo mengi mazuri na marefu, lakini kimsingi umejichanganya sana na mwisho wa siku bila kujijua umekuja upande wangu ktk hii debate....kwamba monster hapa ni serikali ya awamu ya kwanza chini ya Nyerere na baada ya hapo wamekuwa wanapokezana vijiti!! Kusema sehemu umeandika, "mkataba wa EAC ulisema kuwa ikitokea jumuia ikavunjika, basi waajiriwa wake walipwe fedha zao kwanza ndio mengine yafuate, period." Mwisho wa kunukuu....sasa kama hivyo ndivyo kwanini wao waliamua kutofuta hicho kipengele na badala yake wakatumia miaka saba kugawana mali na malipo ya hawa vikongwe yakawa mwisho?? kosa la nani kama sio mkuu wa nchi wa wakati huo ambae ni Mchonga (mungu amrehemu)!!.
Kisha kuna sehemu umeuliza swali, "kwanini hawakulipa mapema."?? Kwa mawazo yako tokana na kipengele nilicho quote hapo juu unadhani lawama za kutolipa mapema ni za nani?? wote tunajua kuwa deni likikaa muda mrefu riba ina pile na hivyo kuongezeka, njia rahisi na lengo hasa la kusema waajiriwa walipwe kwanza ilikuwa ni ku-avoid hiyo mess...lakini ni awamu ya kwanza iliyoruhusu hiyo delay na kufika hapa tulipo leo.
Maana ya kutomwachia mrithi wako deni ni kwamba unakuwa umelipa kabla ya kuondoka!! vinginevyo kiswahili labda pia sijui siku hizi, hizi story za kusema, "oooh simwachi mrithi wangu deni" halafu baadae unasema nilimwachia fedha alipe ni usanii mwingine! Pia, hakuna ushahidi kwamba Mkapa aliacha fwedha za kulipwa hawa wazee.......ktk hili sakata lawama nyingi zaidi ni kwa awamu ya kwanza, pili, tatu na kidogo sana kwa awamu ya nne! Nionacho mimi, hii finger pointing ikome, kilichobaki tuje na jinsi ya kuwalipa hawa wazee fwedha zao...lakini story za kupaka matope wa wa awamu ya nne kusema kwamba wao ndio waliovunja EAC siwezi kukubaliana nalo.
Mkini-label kuwa namtetea Kikwete pouwa tu......lakini mie sizimii CCM wala Chadema, napenda kusema kweli!!.
njioni njema....
Asante YournameisMINE
Lakini nafikiri kuna kitu hukukielewa katika maelezo yangu. Kwanza nia yangu haikuwa kumtetea Nyerere bali kuelezea mtiririko wa sakata lenyewe. Pili kwa huo umri uliyoutaja ni wazi kuwa iliyokuwa EAC hukuijua na historia yake hukuijua.
1. Mgawanyo wa mali ya defunct EAC ulisimamiwa na World Bank na uliendeshwa na mtaalamu wa benki hiyo aliyejulikana kama Dr. V. Umbritch.
2. Uhakiki wa mali kwa nchi zote tatu, Kenya Uganda na Tazania, haukuwa kazi ndogo kama unavyofikiria na ulijumuisha mashirika na idara zote za jumuiya kwa kuzingatia
assets na liabilities zote za jumuiya nje na ndani ya Afrika Mashariki na hasa Ulaya.
3. Viongozi wakuu wa nchi hizi tatu walikabidhiwa report mwaka
1984 na baada ya kuikubali walitakiwa waweke saini zao. Report ilikuwa kubwa na ndefu na ilihitaji muda kusoma na kupitia kila kipengele. Kama sikosei nafikiri ilikua na kurasa zisizopungua mia nne.
4. Baada ya hapo hesabu za malipo zilifanywa na hundi moja kutolewa kwa kila nchi kulipa raia wake waliohusika. Uhakiki wa wadai ulifanyika na
mwaka 1987 ulikuwa uwe mwanzo wa malipo.
5. Kwa sababu zisizoeleweka serikali ya Mwinyi haikuweza kutekeleza hilo na wadai pamoja na kulalamika kimya kimya hawakuwa na namna nyingine ya kusikika kwa kuwa hakuna gazeti wala redio iliyoweza kutoa habari hizo. Juhudi zao za kukutana na kuandamana zilidhibitiwa vilivyo na FFU ambao wakati huo walikuwa wamepata zana za kisasa za kusambaratisha mkusanyiko wowote.
6. Baada ya kusikia wenzao wa nchi zingine wanalipwa ndio wakazidi kupaza sauti na
mwaka 1991 madai yao yaliweza kuchapishwa kwenye vyombo vya habari vya binafsi kama Family Mirror. Ni wakati huo serikali iliweza kutoa tamko kupitia kwa waziri mkuu.
7. Ingawa sikumbuki vizuri kuna wakati walijaribu kumwona Mwalimu ambaye wakati huo ailshastaafu hata uenyekiti wa CCM na inasemekana alistushwa sana kusikia hawajalipwa.
9. Wakati jumuiya ikingali hai, Jakaya Kikwete aliwahi kuwa kwenye baraza la Mawaziri wa EAC na anaelewa vizuri sana hili jambo hivyo ukimya wake unashangaza kweli.
10. Ukimya wa wabunge, waandishi, watetea haki za binadamu na makundi mbali mbali kwenye hili swala ndio unaowasukuma hawa wazee kujiuliza maswali ambayo majibu yake ni kitendawili na kuamua kulala barabarani.